Kero za kudate mume wa mtu

Kero za kudate mume wa mtu

Unaongea culture za kizungu'nini?

Waafrika mila na desturi zetu ni mitala.

Ukiachana na mambo ya uhawara, je wewe mitala halali hauwezi oleka?

Nauliza, mtu aje kakupenda analia kabisa na mahari anaenda toa, hauwezi mkubalia kwa sababu tu eti kaoa wakati mila zetu zinaruhusu?

Embu funguka na hili ili niutathimini msimamo wako mdada.
Sijaongelea mitaala bro...nimeongelea mume wa mtu,yaani kuwa kimada.
 
Sasa kwa nini tuongee uongo madam, demand inapungua kwa wanawake kadri umri unavyokata. At 35+ ni mwendo wa kushare tu, ibahatike mtu akutane na 50s au 60s aliye mgane, otherwise ni maumivu, hao 40s tu wanataka vitoto vya afumbili(ukiniondoa mimi🤣)
Mgane fresh japo nae hana jema,ukipika pilau anaanza kulifananisha na la marehemu mkewe,....hivi Legend ina maana kweli hamna late 40z ambao ni ma senior bachelor kweli?
 
Sema maisha yanashangaza kuna Dada mmoja alikuwa mrembo Sana alikuwa Jirani yangu

Kafanya sana mambo ya kuwa mchipuko kala Sana hela za maziwa ya watoto kavunja Sana ndoa

Ila Leo anapokea malipo ya karma

Kaolewa na Shekh mmoja Ila huyo anamuumiza balaa anamfumania kila siku

Ukiachana na hilo mwanae sasa amekuwa upinde anachezewa hatari.

So sometimes what goes around comes around.
This is Very sad story
 
Sijaongelea mitaala bro...nimeongelea mume wa mtu,yaani kuwa kimada.
Hilo nililiona halina mashiko ndonikaisongesha mada kwenye mitala, vyote lakini si vinapikika chungu kimoja kihisia?

Uhawara huo ulioongelea mara nyingi huwa umelenga manufaa kwa pande zote.

Sasa hauwezi ku 'deep in' kihisia kwa sababu unaelewa dhahiri kuwa mtu huyo uliyenaye ni mpita njia.

Lakini kwa terms of maslahi, mbona mnainjoi na kuburudika tyuu?

Tatizo tulilonalo wengi, kila tuonjapo asali tunataka kuchonga na mzinga, mwisho wa siku ni maumivu ya kichwa na moyo.
 
Hey
,Weekend kwangu ipo poa sana,Natumaini hata yako imetulia,kinyume na hapo jipe moyo siku hazifanani na pia hazigandi...
Leo shangazi nimeona niongee hili suala kidogo la kudate na mwanaume aliye kwenye ndoa,ninaongea kwa experience yangu na kwa experience ya kuangalia mahusiano ya wengine...Jamani,kina dada hii kitu mimi ilishanishinda sijui wenzangu mnawezaje kuwa happy na mahusiano ya namna hiyo,yaani ukute huu muda dada uko zako hotel happily na married man sijawahi enjoy,nishajaribu kudate nao mara kadhaa ila mara nyingi nimekuwa nikiangukia pua sifiki mbali yaani kuna vitu ambavyo nashindwa kuroll nao,mfano
1.UONGO,
Jamani hao viumbe ni waongo Shetani akasome,utasikia mwingine anasema hampendi kabisa huyo mwanamke kwanza alilazimishwa kumuoa,mwingine utasikia kwanza silali nae chumba kimoja mpe miezi sita utamuona huyoo anampeleka mkewe clinic
,ukisikia hizo mambo za design hivo sister,Don't buy it!

2.UNAFIKI
Hao jamaa achana nao,kuna wale wanafiki uko nao ila kila muda utasikia wife this,wife that,yaani anajifanya anampeeeeendaaaaa unabaki kushangaa kama unampenda mbona unamcheat?nikishasikia tu mume wa mtu kaanza wife sijui nini nini,hilo penzi linanishinda kabisaa,Inakata sana stimu

3.UMBEA
kuna wale wasengenya wake zao oooohooo usiombe ukutane nao anamuanika mkewe unabaki kushangaa,huyu kama mkewe aliyemtolea hadi mahali hivi mimi sasa si ndio atanipiga na picha hapo ni ndukiiii

NUKSI
Ukiwa nao hao mambo hayaendi kabisa kuna namna tu unakuwa unakwama,sijui maombi ya wake zao yanaweka kizuizi,au ni vile mi mwenyewe nakuwaga napata kauoga na ka guilty utasikia kale ka kamstari ka Ebr 13 :4 " ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi"kanakuwa kananijiajia tu bila sababu za msingi

KUFICHWAFICHWA.
Yaani unakuwa kama heroine,huku bado upangiwe muda wa kumpigia simu,utasikia "Baby ndio nimefika home usinipigie,usiku mwema ,nakupenda sana🙄🙄🙄"Whaaaaat?

Anyway yako mengi,sijui wenzangu mnawezaje,ila kupanga ni kuchagua ,maana unaweza kudhani uko kwenye mahusiano unakataa watu wema kumbe uko single..wake up weekend njemaaa
Kuna Ile ya kushushwa kwenye Gari mkewe akipiga video call...watu wanaodate Na waume za wary hawaenjoy
 
Back
Top Bottom