Hey
,Weekend kwangu ipo poa sana,Natumaini hata yako imetulia,kinyume na hapo jipe moyo siku hazifanani na pia hazigandi...
Leo shangazi nimeona niongee hili suala kidogo la kudate na mwanaume aliye kwenye ndoa,ninaongea kwa experience yangu na kwa experience ya kuangalia mahusiano ya wengine...Jamani,kina dada hii kitu mimi ilishanishinda sijui wenzangu mnawezaje kuwa happy na mahusiano ya namna hiyo,yaani ukute huu muda dada uko zako hotel happily na married man sijawahi enjoy,nishajaribu kudate nao mara kadhaa ila mara nyingi nimekuwa nikiangukia pua sifiki mbali yaani kuna vitu ambavyo nashindwa kuroll nao,mfano
1.UONGO,
Jamani hao viumbe ni waongo Shetani akasome,utasikia mwingine anasema hampendi kabisa huyo mwanamke kwanza alilazimishwa kumuoa,mwingine utasikia kwanza silali nae chumba kimoja mpe miezi sita utamuona huyoo anampeleka mkewe clinic
,ukisikia hizo mambo za design hivo sister,Don't buy it!
2.UNAFIKI
Hao jamaa achana nao,kuna wale wanafiki uko nao ila kila muda utasikia wife this,wife that,yaani anajifanya anampeeeeendaaaaa unabaki kushangaa kama unampenda mbona unamcheat?nikishasikia tu mume wa mtu kaanza wife sijui nini nini,hilo penzi linanishinda kabisaa,Inakata sana stimu
3.UMBEA
kuna wale wasengenya wake zao oooohooo usiombe ukutane nao anamuanika mkewe unabaki kushangaa,huyu kama mkewe aliyemtolea hadi mahali hivi mimi sasa si ndio atanipiga na picha hapo ni ndukiiii
NUKSI
Ukiwa nao hao mambo hayaendi kabisa kuna namna tu unakuwa unakwama,sijui maombi ya wake zao yanaweka kizuizi,au ni vile mi mwenyewe nakuwaga napata kauoga na ka guilty utasikia kale ka kamstari ka Ebr 13 :4 " ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi"kanakuwa kananijiajia tu bila sababu za msingi
KUFICHWAFICHWA.
Yaani unakuwa kama heroine,huku bado upangiwe muda wa kumpigia simu,utasikia "Baby ndio nimefika home usinipigie,usiku mwema ,nakupenda sana🙄🙄🙄"Whaaaaat?
Anyway yako mengi,sijui wenzangu mnawezaje,ila kupanga ni kuchagua ,maana unaweza kudhani uko kwenye mahusiano unakataa watu wema kumbe uko single..wake up weekend njemaaa