Kero za Wabara (Tanganyika) wakiwa Zanzibar

Kero za Wabara (Tanganyika) wakiwa Zanzibar

Ikiwa wewe umezaliwa Tanganyika basi ukifika hapa kisiwani jiandae na kero zifuatazo.

1. Kudaiwa leseni ya udereva Zanzibar (hata kama unayo ya huko kwenu).

2. Kukosa Uhuru wa kutumia kilevi hadharani.

3. Kukosa fursa ya kumiliki ARDHI.

4. Bullying "name calling" (kuitwa CHOGO).

5. Uhuru wa kuabudu mashakani (ref. Uchomaji Moto nyumba za ibada)

NB: ukifika Zanzibar epuka wahuni wanaojificha kwa kuvaa kanzu.
Unification for strategic security that's the main reason. Wakikataa niite Mrundi nipo pale nasubiria wakatae
 
Lakini wazungu wana nunua ardhi sana uko mashamba Paje, Jambiani, Michamvi kote uko wazanzibari wana uza aridhi kwa wazungu, Wazanzibari wasikuizi wana wapenda sana Wazungu kuliko waarabu sijui kwanini yana wadiriki kuwa uzia mpaka maeneo ya makaburi ya ukoo, baada ya miaka 30 wazanzibari watakuwa wapagani

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
😳😳😳
 
Ila wao wakija huku wanataka Kila fursa. Ni ngumu sana ata ukiwa mtu wa bara kuajiriwa zanzibar
Huku ni Tanzania wazanzibari wanahaki kamili, ila nyie waTanganyika hamnahaki yotote Zanzibar. Na hiyo ndio faida ya kulazimisha Muungano.
 
Huu Muungano ni janga na si kero.

Kero ni neno dhaifu unapouzungumzia Muungano.Mkeo au mwanao anaweza kukukera na bado akawa mkeo na mwanao.

Kero kwa hakika maana yake halisi ni vitu au mambo madogo madogo mfano ukienda kukata ticket unavamiwa na wapiga debe kumi hiyo ni kero.

Kero unaweza kwenda dukani kununua soda ya Tsh 700 unatoa note ya Tsh 10,000 muuza duka anatumia dakika 10 kukutafutia Tsh 9,300 hiyo ni kero.

Kero ni pale Msukuma ambaye haenda shule (Secondary) sasa ni Dr Msukuma.

Kero ni maudhi madogo madogo ambayo unaweza kumudu kuyavumilia na maisha yakaendelea.

Neno sahihi unapozungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Janga.

Hili neno kero limeletwa na CCM ili kutupumbaza waTanganyika tuone matatizo ya Muungano na mambo madogo madogo.

Ngongo kwasasa Kibanda maiti.
Nitapita kukusabahi natokea huku mchamba wima
 
Raisi wa zanzibari ili bidi awe ni kama waziri tu..mambo ya kua na rais wao nao ni ujuha tu
 
Elimu kubwa tulioyonayo tunashindwa kutengeneza nchi mmoja.
 
Wakati huo kuna hadi mawaziri wa SM ya Zanzibar wana ardhi bara!
 
Back
Top Bottom