Hii kesi ikiendelea ni aibu kwa serikali na ikifutwa na DPP ni aibu kwa serikali. Aibu haikwepeki kwa serikali kwa njia yoyote ile, yani kunyoa au kusuka hawapendezi.
Pili, swala la Police kuwateka na kuwatesa Makomandoo wa JWTZ, ambao wana Mahakama, Mahabusu na Police wao (Military Police MP, Martial Courts, Martial Lock Ups) zao pindi wanapotenda kosa. Police walipata baraka kutoka wapi??? Kwa CDF Mabeyo au IGP Sirro au Rais???
Tatu, swala la usalama wa washtakiwa na mashahidi kwa hatua ya hii kesi ilipofikia, hatua gani zimechukuliwa kuwa hakikishia wana usalama huko mahabusu walipo hifadhiwa na pindi wanapo safirishwa kwenda mahakamani??? Tumeona wakisafirishwa kwa gari bovu lililogoma kuwaka mahakamani, je ikitokea msafara wao nje ya mahakama au barabarani kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumiminiwa mzigo wa risasi ili kuficha aibu, hilo jambo litachukua taswira gani mbele ya dunia???
Swali la kizushi;
CDF wetu angekua ndio yule mwamba wa Guinea, bwana Kanali Mamady Doumbouya angekubaliana na mwenendo huu wa kulinajisi jeshi la nchi kwa kuwateka Makomandoo na kuwafanya waliofanywa (Kupigwa, Kuteswa na Kuchomwa bisibisi za makalioni)???[emoji38][emoji38][emoji38]