Kesi dhidi ya Mbowe: Ushahidi wa Luteni Denis Urio ni muhimu sana

Kesi dhidi ya Mbowe: Ushahidi wa Luteni Denis Urio ni muhimu sana

Kesi hii ilipikwa mno hadi ikaungua! palipo na uongo wa kishetani Mola huweka njia ya ukweli ili kumuumbua shetani!
 
Adamoo na mwenzake walienda morogoro kabla ya kuanza safari ya Moshi - Je walikwenda kumwona nani? kwa kusudi lipi? Je yawezekana akawa Luteni Urio na hapo ndipo tatizo likaanziapo?
Mini nafikiri hivyo.
 
Ndugu zangu!

Kwa wale tunaofuatilia kwa ukaribu hii kesi pendwa, tutakumbuka maelezo muhimu kutoka kwa mashahidi wa pande zote mbili.

Kwenye kesi ya msingi, tulisikia ushahidi wa ACP Kingai akimtaja Luteni Denis Urio kuwa alitumika kama mtego kwa sharti la kuripoti kila hatua.

Kwa maelezo yake, Urio alihusika 'kumtafutia' Mbowe wasaidizi aliowahitaji. Ikawa hivyo.

Hapa tulitegemea kuwa Urio 'amemchoma' kwa kuripoti mipango yake inayoitwa ya ugaidi.

Lakini kwenye ushahidi wa kesi ndogo uliotolewa na Komandoo Ling’wenya (mtuhumiwa), yeye kamtaja Urio kuwepo kwenye moja ya mahabusu za hao wanaoitwa magaidi na amemshuhudia akipitia mateso kama hao wengine.

Hii inatupa mwelekeo gani? Kwanini mtu aliyetajwa kufanikisha ukamatwaji wa magaidi naye anakula kichapo?

Urio yupo upande gani?

Japo si mmoja wa mashahidi katika hii kesi ya msingi, lakini sasa ni rasmi ameingizwa na itabidi apande kizimbani.

Ushahidi wake unaweza kutusogeza hatua nyingi kuelekea kuufahamu ukweli, tunamhitaji Luteni Denis Urio kizimbani bila kukosa.

Ncha Kali.[emoji1614][emoji276]
Kuna mchezo mchafu unatengenezwa wa kumfunga Mbowe
 
Ni nadra sana kuona mtu kama Luteni wa Jeshi aliyeko kazini anateswa hovyo hovyo na hawa ma copro wa Police - nafikiri mama arudishe hadhi ya jeshi letu hili haraka mno - kesi ya Mh. Mbowe imeonyesha wazi wazi.

Kama Mwanajeshi kakiuka basi kuna mamlaka ya kijeshi yamchukulie hatua lakini si kumtoka kambini na kuteswa na raia wakakamavu. Hata leo hii wananchi wakiwaona JWTZ wanapita kwa mazoezi husimama kushangilia huku kina mama kupiga vigelegele - JWTZ ni jeshi letu wananchi lipewe hadhi yake.

Awamu ya tano kuna mambo imefanya hayakuwa sawa kwenye hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
 
Ndo mnavyojidanganya hapo ufipa? Kweli mmekosa akili nyie watu!

Inaelekea una umri mdogo sana! Uliza komando Tamimu alifanywaje na vyombo vya dola mwaka 1981 baada ya kuongoza jaribio la kutaka kumpindua nyerere?

Tanzania kwenye kudeal na wahalifu haijalishi wewe Nani wanakupa dozi tu!
Hio ilikuwa zamani subiri muda utasema, utopolo wa akina kingai na mahita mtaaga public, hii dharau na aibu haipiti bure.
 
Ni nadra sana kuona mtu kama Luteni wa Jeshi aliyeko kazini anateswa hovyo hovyo na hawa ma copro wa Police - nafikiri mama arudishe hadhi ya jeshi letu hili haraka mno - kesi ya Mh. Mbowe imeonyesha wazi wazi.

Kama Mwanajeshi kakiuka basi kuna mamlaka ya kijeshi yamchukulie hatua lakini si kumtoka kambini na kuteswa na raia wakakamavu. Hata leo hii wananchi wakiwaona JWTZ wanapita kwa mazoezi husimama kushangilia huku kina mama kupiga vigelegele - JWTZ ni jeshi letu wananchi lipewe hadhi yake.

Awamu ya tano kuna mambo imefanya hayakuwa sawa kwenye hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Hii ishu imesukwa na TISI kwa kushirikiriana machoko wa polisi na Magufuli aliwakatalia huu upuuzi, sasa wamempa huu utopolo Samia, hii vita wajipange watakufa wengi mno, tujipe muda within 12 months mtajionea wenyewe.
 
Tatizo lenu mnajiona nchini ni ya kwenu zaidi kuliko wengine.
Mnajiona vyombo vya ulinzi na usalama hasa PT ni vya kwenu zaidi kuliko vya wananchi!
Kwa taarifa yako usiishi zamani... Zama zimebadilika! 1981 hadi leo ni 40 years.
Hii kesi ina mashahidi wengi ambao si raia wa kawaida. Na Ukweli unafahamika!
We jidanganye!

NB: mnaiogopa Bavicha hadi mnafanya makosa obvious! Wengine ni free radicals!
Kuwa na Mashahidi wengi sana kwa upande wa serikali ni very risk sana,tena mnoooo hasa kwa kesi ya kupikwa.Just imagine tayari serikali imeshaleta mashahidi watatu na wote ushahidi umeshatofautiana tofautiana baina yao,Je,mpaka wakifika shahidi wa 23 unategemea nn kitatokea 🤣 🤣 🤣
 
Hii kesi ikiendelea ni aibu kwa serikali na ikifutwa na DPP ni aibu kwa serikali. Aibu haikwepeki kwa serikali kwa njia yoyote ile, yani kunyoa au kusuka hawapendezi.

Pili, swala la Police kuwateka na kuwatesa Makomandoo wa JWTZ, ambao wana Mahakama, Mahabusu na Police wao (Military Police MP, Martial Courts, Martial Lock Ups) zao pindi wanapotenda kosa. Police walipata baraka kutoka wapi??? Kwa CDF Mabeyo au IGP Sirro au Rais???.

NOTE THAT: Luteni Denis Urio ni bado mkufunzi jeshini, yupo active kama mwanajeshi wa JWTZ na hajasimamishwa kazi bado, na ndio police waliosema wameshamtupa baada ya kumalizana nae kumtekenya TAZARA POLICE STATION.

CDF wetu angekua ndio yule mwamba wa Guinea, bwana Kanali Mamady Doumbouya angekubaliana na mwenendo huu wa kuvunja katiba, kulinajisi jeshi la nchi kwa kuwateka Makomandoo na kuwafanya waliofanywa (Kupigwa, Kuteswa na Kuchomwa bisibisi za makalioni)

Mabeyo ndio chanzo cha yote haya,ni bladifekini sana huyu kumbe, aliamishia nguvu ya Jeshi letu wananchi ”JWTZ ”kwa PoliCCM ili kumfurahisha Msukuma feki wa Chato, na haya ndio matokeo yake, sijuhi ni Msukuma mwenzie . Nimemzarau sana hii takataka inayoitwa Mabeyo.
MaKomandoo wanapona vitani huko, anakuja kuning’inizwa kama popo na ”makada” kufurahisha wahuni tu wa kisiasa, uliona wapi?!
 
Adamoo na mwenzake walienda morogoro kabla ya kuanza safari ya Moshi - Je walikwenda kumwona nani? kwa kusudi lipi? Je yawezekana akawa Luteni Urio na hapo ndipo tatizo likaanziapo?
Mini nafikiri hivyo.

Nadhani wewe ndo unanipa tip nzuri kuliko wote.Ushahidi kwamba walikwenda Morogoro kabla ya kwenda Moshi nani katoa?(Nataka kujua tu,mi si mfuatiliaji mzuri wa hii kesi)
 
Ni nadra sana kuona mtu kama Luteni wa Jeshi aliyeko kazini anateswa hovyo hovyo na hawa ma copro wa Police - nafikiri mama arudishe hadhi ya jeshi letu hili haraka mno - kesi ya Mh. Mbowe imeonyesha wazi wazi.

Kama Mwanajeshi kakiuka basi kuna mamlaka ya kijeshi yamchukulie hatua lakini si kumtoka kambini na kuteswa na raia wakakamavu. Hata leo hii wananchi wakiwaona JWTZ wanapita kwa mazoezi husimama kushangilia huku kina mama kupiga vigelegele - JWTZ ni jeshi letu wananchi lipewe hadhi yake.

Awamu ya tano kuna mambo imefanya hayakuwa sawa kwenye hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
DPP kama ana uelewa mpana sana ni bora akaifuta hii kesi; Just imagine mpaka sasa jamhuri tayari imeshaleta mashahidi watatu kati ya 23 na wote ushahidi wao hauna consistency,sasa wakifika kwa shahidi wa 23 si ndo itakuwa balaa hasa ukizingatia utetezi wana mawakili ambao ni very competent 🤣 🤣 Hii case ishakuwa ni mess kwa upande wa serikali
 
Hii ishu imesukwa na TISI kwa kushirikiriana machoko wa polisi na Magufuli aliwakatalia huu upuuzi, sasa wamempa huu utopolo Samia, hii vita wajipange watakufa wengi mno, tujipe muda within 12 months mtajionea wenyewe.
Achene Mahakama ifanye kazi yake mwisho itoe HAKI. Sasa nyie mnatoa povu kisa Maelezo ya utetezi. Kumbuka katika kujitetea MTU ataeleza lolote analoona litaweza kumnasua. Najua wengi ni Ubinafsi unawasumbua.
 
Nadhani wewe ndo unanipa tip nzuri kuliko wote.Ushahidi kwamba walikwenda Morogoro kabla ya kwenda Moshi nani katoa?(Nataka kujua tu,mi si mfuatiliaji mzuri wa hii kesi)
Mke wa adamoo,juzi mahamani alisema kabla ya hawajaenda Moshi ,wakaenda Morogoro kwanza
 
Fikirishi/Za kunyapia
Hao Komandoo walitengenezwa ili kummumaliza Uhuru lkn imeonekana wategaji hawakuwa makini ni terms au Komando wamekuwa double agents.
Game NZITO

Uhuru! Unaweza kujazia kidogo hizi japo za kunyapia?
 
Back
Top Bottom