Kesi dhidi ya Mbowe: Ushahidi wa Luteni Denis Urio ni muhimu sana

Kesi dhidi ya Mbowe: Ushahidi wa Luteni Denis Urio ni muhimu sana

Kesi nzima ya serikali inaegemea ushahidi wa Urio halafu wanamtesa!!

Na huo ndio ushahidi mkubwa tulioambiwa na Sirro,huyu mzee astaafu tuu sasa.
Mkuu unazijua angalau "a,b,c" za ulinzi na ussalama wa nchi? Huyo Luteni yupo kazini jombaa!!
 
Nadhani wewe ndo unanipa tip nzuri kuliko wote.Ushahidi kwamba walikwenda Morogoro kabla ya kwenda Moshi nani katoa?(Nataka kujua tu,mi si mfuatiliaji mzuri wa hii kesi)

Huo ni ushahidi wa mke wa Adamoo, mtuhumiwa namba moja…. haujapatiwa ufafanuzi.
 
Ndugu zangu!

Kwa wale tunaofuatilia kwa ukaribu hii kesi pendwa, tutakumbuka maelezo muhimu kutoka kwa mashahidi wa pande zote mbili.

Kwenye kesi ya msingi, tulisikia ushahidi wa ACP Kingai akimtaja Luteni Denis Urio kuwa alitumika kama mtego kwa sharti la kuripoti kila hatua.

Kwa maelezo yake, Urio alihusika 'kumtafutia' Mbowe wasaidizi aliowahitaji. Ikawa hivyo.

Hapa tulitegemea kuwa Urio 'amemchoma' kwa kuripoti mipango yake inayoitwa ya ugaidi.

Lakini kwenye ushahidi wa kesi ndogo uliotolewa na Komandoo Ling’wenya (mtuhumiwa), yeye kamtaja Urio kuwepo kwenye moja ya mahabusu za hao wanaoitwa magaidi na amemshuhudia akipitia mateso kama hao wengine.

Hii inatupa mwelekeo gani? Kwanini mtu aliyetajwa kufanikisha ukamatwaji wa magaidi naye anakula kichapo?

Urio yupo upande gani?

Japo si mmoja wa mashahidi katika hii kesi ya msingi, lakini sasa ni rasmi ameingizwa na itabidi apande kizimbani.

Ushahidi wake unaweza kutusogeza hatua nyingi kuelekea kuufahamu ukweli, tunamhitaji Luteni Denis Urio kizimbani bila kukosa.

Ncha Kali.[emoji1614][emoji276]
Ushahidi wake ni "inevitable" ili picha ya kesi hii iwe wazi. Ni vema upande wa utetezi au mashitaka wamuite kuwa shahidi wao.
 
Hii ishu imesukwa na TISI kwa kushirikiriana machoko wa polisi na Magufuli aliwakatalia huu upuuzi, sasa wamempa huu utopolo Samia, hii vita wajipange watakufa wengi mno, tujipe muda within 12 months mtajionea wenyewe.
Ni kweli, kwanza issu ya Moses Lijenje kupotezwa ishakuwa kubwa mno. Nafikiri Komandoo Moses hakukubali ujinga akaamua kupigana hadi tone lake la mwisho. Hii kitu kinaweza kikawa kikaango wa baadhi ya maafisa wa TISS na Police. Hii kesi ishawageukia kina Kingai tayari...mkumbuke hii ilikuwa enzi za mwendazake, connect dots na yule jambazi sugu la Hai.

Nakumbuka miaka za zamani nikiwa mdogo kabla sijamshitaki kaka ama dada yangu kwa baba ni najipanga kwanza, unaweza kupeleka mashitaka then kibao kikakugeukia wewe unakaangwa vibaya saana !! ndo haya ya kina Kingai.
1633083260185.jpeg
 
Tuliza pressure. Hii ni kesi ndogo iliyoibuka ghafla ndani ya kesi kubwa. Kwenye kesi kubwa ni wazi kuwa mashahidi ni wengi lakini raia ni wachache sana.
JPM alipochomekewa hii kesi akasema... "Aiiiiiiiiii baghosha achaneni nayo majameni..."
Tambua tu kuwa hii kesi inaibua vita na visasi vya siku nyingi baina ya PT, TISS na JWTZ.
Ila ukifkikilia vizuri ni dhahiri viongozi wetu wana shida kwenye kuwaza maana kwa mwenye Hekima hiki kitu hawezi fanya .Tena na ajabu Rais nae kaingizwa mkenge na yeye kaingia.Luteni Urio ndo atamaliza Kila kitu je atakua upande wa Polisi kama Shahid wao kwa mjibu wa RPC Kingai au atakua mshitakiwa kwa mjibu wa watuhumiwa?Mbeleni ni aibu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kesi ikiendelea ni aibu kwa serikali na ikifutwa na DPP ni aibu kwa serikali. Aibu haikwepeki kwa serikali kwa njia yoyote ile, yani kunyoa au kusuka hawapendezi.

Pili, swala la Police kuwateka na kuwatesa Makomandoo wa JWTZ, ambao wana Mahakama, Mahabusu na Police wao (Military Police MP, Martial Courts, Martial Lock Ups) zao pindi wanapotenda kosa. Police walipata baraka kutoka wapi??? Kwa CDF Mabeyo au IGP Sirro au Rais???.

NOTE THAT: Luteni Denis Urio ni bado mkufunzi jeshini, yupo active kama mwanajeshi wa JWTZ na hajasimamishwa kazi bado, na ndio police waliosema wameshamtupa baada ya kumalizana nae kumtekenya TAZARA POLICE STATION.

Tatu, swala la usalama wa washtakiwa na mashahidi kwa hatua ya hii kesi ilipofikia, hatua gani zimechukuliwa kuwa hakikishia wana usalama huko mahabusu walipo hifadhiwa na pindi wanapo safirishwa kwenda mahakamani?

Tumeona wakisafirishwa kwa gari bovu lililogoma kuwaka mahakamani, je ikitokea msafara wao nje ya mahakama au barabarani kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumiminiwa mzigo wa risasi ili kuficha aibu, hilo jambo litachukua taswira gani mbele ya dunia?
Swali la kizushi;

CDF wetu angekua ndio yule mwamba wa Guinea, bwana Kanali Mamady Doumbouya angekubaliana na mwenendo huu wa kuvunja katiba, kulinajisi jeshi la nchi kwa kuwateka Makomandoo na kuwafanya waliofanywa (Kupigwa, Kuteswa na Kuchomwa bisibisi za makalioni)?[emoji38][emoji38][emoji38]
Aliyetupwa siyo kanali Linjenje?
 
Wangekuwa wanajeshi sheria na miongozo ya watumishi wa umma hussusani jeshi ingewalinda lakini walikuwa wameshafukuzwa kwa hiyo wameteswa kama wahalifu wengine raia, Ki ukweli hairuhusiwi kabisa kumtesa mtuhumiwa kwa sababu bado hajathibitika ni mhalifu na hata ikithibitika hukumu ya mahakama ndoo adhabu ,

Ki uhalisia kwa Africa yote wanaanza kumtesa mtuhumiwa ili kama anaweza kutoa taarifa za kuwaongoza polisi kupata taarifa nyingi na ushahidi kwa sababu hatuna technolojia na resource hela ya kufanya upelelezi kwa muda mrefu na kupitia chanel nyingi , kwa hiyo shotcut mtese afunguke chap chap
Unafurahia mateso ya binadamu? Wewe ni "sadist".
 
Kufungua threads nyingi kuomboleza kuwa Mbowe Hana hatia nikujichosha bure hizi porojo na blah blah hazimfutii ugaidi

Tanzania bila ugaidi inawezekana
Wewe unaye mwona ana hatia, umetumia kipima gani? Tanzania bila ugaidi itawezekana pale chama cha magaidi (ccm) chenye wana chama magaidi, kina Hamza, kitakapo tokomezwa!
 
Ndo mnavyojidanganya hapo ufipa? Kweli mmekosa akili nyie watu!

Inaelekea una umri mdogo sana! Uliza komando Tamimu alifanywaje na vyombo vya dola mwaka 1981 baada ya kuongoza jaribio la kutaka kumpindua nyerere?

Tanzania kwenye kudeal na wahalifu haijalishi wewe Nani wanakupa dozi tu!
Wewe ndo unaishi hiyo 1981 ya Tamimu, Hii ni 2021, ambapo haki za binadamu zinazingatiwa!
 
Urio angekuwa ni potential witness upande wa mashitaka angekuwa ni number one witness to testify .... hii maana yake mashahidi Wakuu katika hii kesi ni Kingai, mahita na huyu corporal.... Urio ni story ya kutunga na hawezi kumleta kwakuwa urio akikana maelezo yake basi hii kesi hata ikienda kwenye main case itakuwa imeisha ... kwavile urio awali urio aliteswa na kwakuogopa urio kukana maelezo .... urio hata letwa na jamhuri kama shahidi
 
Sisi wengine tulitoa wito na hamasa kabla hata kesi hii haijaanza, irushwe LIVE COVERAGE kwenye channel maalum, ili wananchi wote wajionee. Kama ilivotokea katika baadhi ya kesi nchini Kenya na South Africa.

Ila mkanyuti wana kijiji cha JF. Mngejionea mauzauza ya ujinga wa Jamhuri kama ingerushwa live.

Kabisa mkuu na hii ndiyo kazi mmojawapo ya TBC badala ya kurusha kipindi cha harusi cha Chereko...
 
Kufungua threads nyingi kuomboleza kuwa Mbowe Hana hatia nikujichosha bure hizi porojo na blah blah hazimfutii ugaidi

Tanzania bila ugaidi inawezekana
Punguza kiherehere na kuwashwa washwa, nani kakutuma uje kwenye huu uzi??
 
Wangekuwa wanajeshi sheria na miongozo ya watumishi wa umma hussusani jeshi ingewalinda lakini walikuwa wameshafukuzwa kwa hiyo wameteswa kama wahalifu wengine raia, Ki ukweli hairuhusiwi kabisa kumtesa mtuhumiwa kwa sababu bado hajathibitika ni mhalifu na hata ikithibitika hukumu ya mahakama ndoo adhabu ,

Ki uhalisia kwa Africa yote wanaanza kumtesa mtuhumiwa ili kama anaweza kutoa taarifa za kuwaongoza polisi kupata taarifa nyingi na ushahidi kwa sababu hatuna technolojia na resource hela ya kufanya upelelezi kwa muda mrefu na kupitia chanel nyingi , kwa hiyo shotcut mtese afunguke chap chap
Urio hajafukuzwa jeshini weweee...
 
..Urio ataletwa na upande wa mashtaka wakati kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

..Ni shahidi muhimu sana wa upande wa mashtaka kwasababu yeye ndiye anayedaiwa kutoa tip kwa polisi kuhusu kuwepo kwa njama za ugaidi.
Sasa ajabu ni pale akina Adamoo wanaposema naye kabinywa sanaaaaa huko Tazara...
 
Ndo mnavyojidanganya hapo ufipa? Kweli mmekosa akili nyie watu!

Inaelekea una umri mdogo sana! Uliza komando Tamimu alifanywaje na vyombo vya dola mwaka 1981 baada ya kuongoza jaribio la kutaka kumpindua nyerere?

Tanzania kwenye kudeal na wahalifu haijalishi wewe Nani wanakupa dozi tu!
Je ni uongo kwamba akina Tamimu, Maganga na wenzake walitaka kumpindua Nyerere? Baada ya mmojawapo kuachiwa (Maganga) kwenye mahojiano mbalimbali alikiri au hakukiri kutaka kumpindua Mwalimu? Ukishajibu hayo maswali rudi hapa tuendelee...
 
Back
Top Bottom