Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar

Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar

Kweli mkuu
Wanachofundishwa ni utabiri wa fujo kama tu wapinzani wakifanya mikutano ya siasa na maandamano ya amani nothing else, lakini jinsi ya kutenda haki Zero.
 
Sisi tupo nyuma ya jamii forums tutashinda kwani sauti ya wengi ni sauti ya mungu
 
Kesi ya kipuuzi kabisa isiyo na merit!Mfungua kesi kila kitu 'sijui'
Hawa wanapoteza bure muda na hela za serikali
 
Lisu na wenzie wanafanya kazi ya kuwaokoa wateja wao na adhabu tu na si kusimamia msimamo wa jf kuzuia taarifa. Baada ya kesi na watuhumiwa kuwa wamepunguziwa adhabu, jf itatoa ushirikiano kwa polisi kuliko chombo chochote cha habari.
Hujui kuwa wanatakiwa kupata kibali cha mahakama cha kuomba taarifa hizo za wateja?

Na je,unajua ni lazima ujenge hoja mahakamani ndio upewe hicho kibali?

Huoni kuwa JF walikataa kutoa taarifa hizo kwasababu walijua polisi walikuwa hawana kibali cha mahakama kinachowaruhusu kudai taarifa za mtumiaji wa JF anaelalamikiwa?
 
Lissu yupo vizuri kuuliza maswali. Naona shahidi wa jamuhuri anaweweseka

Kila la kheri JF
 
Lisu na wenzie wanafanya kazi ya kuwaokoa wateja wao na adhabu tu na si kusimamia msimamo wa jf kuzuia taarifa. Baada ya kesi na watuhumiwa kuwa wamepunguziwa adhabu, jf itatoa ushirikiano kwa polisi kuliko chombo chochote cha habari.
kwa misingi ipi labda?
 
Nashauri ukaguzi wa vyeti uwapitie hawa jamaa.
sio kwamba nawaonea wivu ila wanalirudisha taifa nyuma kama ilivyotoea leo mahakamani sasa jamii inajifunza nini kuhusu huyo askari?
 
Hahahaha, hata iweje siwezi nikakubali kufanyiwa Cross Examination na Lissu.
Yule (Mh. Lissu) ni rahisi kummudu wakati wa Cross Examination. Kuna mbinu nyingi za kummiliki kwenye mahojiano ya namna hiyo. Moja ni kufanya delay tactic na legal provocation technique; akiziruka hizo unamletea nyingine(sizitaji)! Lazima ahame kwenye mstari na akose cha kuuliza ama aulize off target!
 
Ndiyo maana biashara na mahakama siitaki, hii miswali si kuishia kujichanganya tu....
 
Unatuchamba au!!
Sikuchambi mkuu, hapa tunaweka siasa pembeni kwa manufaa ya TAIFA na JF ambapo ndio uwanja wenu wa kupiga pesa huko lumumba!

JF ikifutwa nna uhakika hata wewe kazi utakua huna na mwisho wa siku chakula kitakua hakuna kwa shem wetu na familia kwa ujumla!

Tujiunge kwa pamoja tuseme NO kwa wabaka sheria akiwemo mkuu wenu, tujiunge kwa pamoja kumpigania shujaa wa sheria ukanda wote wa kaskazini mwa jangwa la sahara ndugu Mh. wakili msomi na rais wa TLS Tundu Lissu ambaye yeye kaacha kazi zake na kuenda kukutetea wewe na wenzako wa lumumba!!

JF forever JamiiForums AshaDii Maxence Melo Mzee Mwanakijiji
 
Hauwezi kuwa shahidi wakati kila swali unaloulizwa unasema hujui. Prosecution kama hawatawaleta mashahidi makini mahakamani kwenye kesi anayetetea Tundu Lissu ni sawa na Barcelona FC kupambanisha na Mbao FC.
 
Shahidi ameacha doubts za kutosha, na hakuna wa kuja kuzifuta hizo doubts, isipokuwa wa kuziongeza! The extent of Proof in Criminal Cases is 'Beyond any Reasonable Doubt'!
 
Huu uzi watu wa ccm wakiuona inakua kama nyoka aina ya koboko amenusa harufu ya diesel au mafuta ya taa au nailoni lililochomwa!! tafadhali wana CCM tuungane kwa pamoja piteni huku wakuu!! siasa na uchama tuweke pembeni kwa maslahi ya TAIFA na jf kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom