Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar

Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar

Tundu Lissu anamuuliza sasa " ulisema kuwa katika barua hiyo JF ilijibu kuwa ina wajibu wa kulinda faragha za wateja wao. Kwa ufahamu wako kuna haki ya kila mtu kulindiwa faragha ya mawasiliano yake au hakuna?"
Jibu: Inategemea

Tundu Lissu: Haki ipo au haipo??
Jibu: Kwa private person sifahamu...

Tundu Lissu: Kwa ufahamu wako kuna haki ya kulindiwa faragha ya mawasiliano kwa kila mtu including private persons?
Jibu: Sifahamu

Duh, hatari! Huyu hafahamu chochote ndiye mwenyewe cheo kikubwa huko Polisi ya wadanganyika.
 
Kwa mara ya kwanza namuona mheshimiwa Rais anampongeza TL kwa uzalendo anaounyesha.

Classified information kama hii aliyoitoa FUHRER ni wazi mheshimiwa Rais kama aliiona ni lazima aliifanyia kazi na aliipenda.

Ni wazi kuwa Tundu Lissu anatetea masilahi ya Taifa katika hili na kama Mh Rais anaifatilia hii kesi, namuomba awachuze hawa wapelelezi wanaodai kuiwakilisha jamhuri kumbe wanawatetea wezi wa kodi.

Tundu Lissu kwa hili unalolifanya nakuhakikishia Mh Rais ni lazima amekukubali kwa hili japo kuna mengine huwa unaropokaropoka tu wala hayana faida yeyote.
 
Mashahidi ni mabashite wanajua kusoma na kuandika sasa msawali technical ya Lisu watayaweza kweli?
 
Back
Top Bottom