Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mahakama imetoa uamuzi kuhusu mapingamizi matano dhidi ya Jamhuri yaliyowekwa na mshtakiwa Tundu Lissu mnamo Novemba 12, 2025, ikiwemo pingamizi kuhusu utaratibu wa usikilizwaji wa shahidi wa siri. Lissu alidai mahakamani kuwa, hata kama sheria ya ulinzi wa mashahidi ingekuwa na uhalali wa kutumika, shahidi huyo alipaswa kuonekana na majaji. Alieleza kuwa hata majaji wanaendesha shauri bila kumuona shahidi huyo, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
Mahakama imekubaliana na pingamizi hilo na kuelekeza kufanyika maboresho ya kizimba maalum ili mashahidi wa siri waweze kuonekana na majaji.
Fuatilia mwenendo wa kesi hapa > Kesi ya uhaini ya Lissu, mahakama kutoa uamuzi wa mapingamizi leo Feb 11, 2026
Mapingamizi mengine manne, ikiwemo kuhusu uhalali wa sheria ya kulinda mashahidi, yametupiliwa mbali kutokana na kile kilichoelezwa kuwa yamekosa mashiko. Baada ya uamuzi huo, kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho, Februari 12, 2026 ambapo upande wa mashtaka utaanza kuwasilisha mashahidi wao, wakiwemo mashahidi wa siri na wale wasio wa siri ambao ni pamoja na askari 19.
Hata hivyo Wakili wa CHADEMA Rugemeleza Nshala amesema, Mahakama kuu imetupilia mbali mapinganizi manne aliyowsilisha Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu na kukubali pingamizi moja kati ya matano la kurekebishwa kizimba cha Mashahidi wa siri.
Soma Pia:

- Shahidi wa Kesi ya Lissu (P7): Nauli ya kuja mahakamani leo nimepewa na mwanamke wangu. Ndiye ananiweka mjini
- Kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 17, 2026, mashahidi wa Jamhuri wasiopungua watatu wangojewa
- Kesi ya uhaini dhidi ya Lissu: Shahidi wa saba kati ya 30 wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa Siri (P6): Lissu alisema tunakwenda kuvuruga uchaguzi na kukinukisha
- Kesi ya Lissu: Hiki ndicho Kizimba cha mashahidi wa kificho, kilichosababisha Kesi kuahirishwa
- Baada ya takribani miezi mitatu, kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 9, 2026
- Kesi ya Lissu: Mahakama yaagiza Kizimba cha Mashahidi wa siri kirekebishwe Majaji wawaone. Kesi kuendelea Feb 12, 2026
- Kesi ya uhaini ya Lissu, mahakama kutoa uamuzi wa mapingamizi leo Feb 11, 2026
- Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu kuendelea Februari 9 hadi Machi 6, 2026
- Shahidi wa kesi ya Lissu (P7) anasema alikamatwa mara tu baada ya kuangalia video ya Lissu iliyokuwa Jambo TV
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa siri (P5): Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha, uchaguzi mkuu hautafanyika
- Mama wa CHADEMA azimia mahakamani baada ya Lissu kudai kunyimwa chakula
- Mahakama kuu, Kanda ya Dar es salaam Tarehe 11 Februari, 2026 kutoa uamuzi mdogo katika kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu