Nayajua yote hayo.
Ndiyo maana nikasemakama kweli alidanganya mambo ya leseni (kama aliendesha bila leseni au alikuwa na leseni feki), wakili mjanja angemwambia kubali kosa la leseni tuliondoe katika mjadala ili tushinde kesi ya mauaji.
Ukishindwa kesi ya mauaji, hukumu yake itafanya kesi ya leseni ifunikwe kabisa.
Wakili wa utetezianaweza kunyumbulisha kesi kwamba mteja wangu si malaika, ana makosa, kaendesha gari bila leseni, lakini kuendesha gari bila leseni si sawa na uuaji, kuna watu kibao wanaendesha magari bila leseni lakini si wauaji, mpeni kifungo au mpigeni faini ya kuendesha gari bila leseni.
Ukiwa muongo katikakuendesha gari bila leseni, unapoteza uaminifu ni kweli, lakini hilo halimaanishi kwamba uongo huounakufanya uwe muuaji.