Kesi ya Mbowe: Haki Haikuonekana Kutendeka

Kesi ya Mbowe: Haki Haikuonekana Kutendeka

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Haki haijawahi kujificha.

Jaji Siyani kwa kujiridhisha kuwa:

1. Mshitakiwa wa pili alikamatwa akawasaidia polisi kumtafuta Mosses Lijenje Moshi, Boma Ng'ombe hadi Arusha,
2. Njiani wakapata mishikaki na Mo Energy,
3. Mshitakiwa wa pili akatoa maelezo kwa ridhaa yake ndani ya masaa 4 yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria,
4. Kwamba madai ya kuteswa kwa washitakiwa yalikuwa ni porojo tu,

Kama ilivyo kwa misahafu kuweza kutumika kufikia hitimisho lolote, ama kwa hakika Jaji Siyani hakubakia nyuma:

1. Jaji hakutaka kujishughulisha kujua walikuwa wapi wahanga wengine wa yaliyosemekana mateso Moses Lijenje au Luteni Urio,
2. Jaji hakutaka kujishughulisha wala kuhitaji uthibitisho wa madaktari kujiridhisha madai ya kuteswa ya washitakiwa.

"Kwa hukumu hii Sirro, Kingai, Mahita na polisi kwa ujumla mmepewa leseni ya kuuwa nzi. Kuwa uweni nzi wote popote mtakapowaona. Jaji Kiongozi mpya kawapa ruksa hiyo."

Haki kuonekana hadharani ikiporwa ni pigo kwa utawala wa sheria.

Kwa hakika leo imekuwa ni siku mbaya kabisa kwa mahakama na utawala wa sheria hapa nchini.
 
Kwa Sabaya mnakenua meno haki imetendeka ,kwa mbowe haki haikutendeka.
Acheni kuingilia uhuru wa mahakama kenge nyinyi.

Kwa SABAYA tumekenua meno kwa sababu haki ilionekana ikitendeka na ndiyo maana mapanya mliojawa na aibu mkarejea mashimoni:

IMG_20211016_132442_593.jpg
 
Haki haijawahi kujificha.

Jaji Siyani kwa kujiridhisha kuwa:

1. Mshitakiwa wa pili alikamatwa akawasaidia polisi kumtafuta Mosses Lijenje Moshi, Boma Ng'ombe hadi Arusha,
2. Njiani wakapata mishikaki na Mo Energy,
Siku mbili tu baada ya Sabaya kufungwa hahahahahhhh
 
Kwani mama alisema jeshi akihojiwa na BBC?
AU UMESAHAU?

ALISEMA "Nafikiri alipoona anatafutwa akajikita kudai katiba ili akikamatwa asingizie ni kwasababu ya madai ya katiba,Na kama unakumbuka mbowe hakuwepo Nchini muda mrefu"

Sasa kwa kauli hiyo ,Jiongeze.Ushakuwa mkubwa.!!!
 
Kinachogomba ni kujaribu kuweka ghiliba kuwa kuna kesi.

Si watoe tu hiyo hukumu waliyonayo hata kwenye radio tu?

Au wewe huwashauri hivyo hawa ambao ni miungu watu?
 
Wapuuzi kweli hawa watu.

Vyombo vyote viwe macho sana na kauli za hawa wanafiki na wahuni.

Kamwe wasitetereshwe na hawa majambazi wauza madawa ya kulevya.
 
Kinachogomba ni kujaribu kuweka ghiliba kuwa kuna kesi.

Si watoe tu hiyo hukumu waliyonayo hata kwenye radio tu?

Au wewe huwashauri hivyo hawa ambao ni miungu watu?
Mama si alishamaliza ? Hukumu ipi wewe ambayo unayosubiria?
 
Jaji Siyani ameamua kuamua kesi kwa hisia, facts na sheria kaona ujinga.

Kingai na Mahita hawajui chochote kilichomo kwenye PGO, ila "jaji wao" kawaona ma genius.

Badala ya jaji aamue kwa kuangalia sheria inasemaje, yeye ameamua kwa kuangalia "maoni yake"

Ameamua kuyatumia "maoni yake" kukwepa kutoa haki kwa anayestahili ili alinde ugali wake mpya alioletewa juzi kwenye sahani, na akuficha ujinga wa kina Kingai.

Kwa hukumu hii ndogo ya leo, nimeuona mkono wa Samia kwenye kuikamilisha, aliamua kuingia kichwani kwa jaji, akakaa, akatulia tuli, jaji akaendeshwa kama mwanasesere.
 
Jaji Siyani ameamua kuamua kesi kwa hisia, facts na sheria kaona ujinga.

Hii ni zaidi ya hisia. Kesi imeamriwa zaidi kulipa fadhila kwa ile mamlaka ya uteuzi.

Kale ka lugha ka "udhaifu" kaliko mfikisha paschal mayalla kwenye tume ya maadili kalikuwa kanamhusu sana huyu mheshimiwa.
 
Kweli biashara ya binadam hasa fikra ya binadam bado ipo. Hiki kipindi mahakama haina meno juu ya vipande vya fedha. Inauma lakn ndy hivyo!!
 
Back
Top Bottom