Kimsingi Mbowe kalishwa tango pori. Kama hajatambua hilo hastahili kuwa kiongozi wa chama cha Siasa. Hata jopo la mawakili wake ni zigo katika medani ya kisheria. Wanapaswa kuthibitisha, pasipo shaka, kuwa mashtaka dhidi ya mteja wao ni uwongo mtupu. Hivyo tungetegemea wangeweka pingamizi dhidi ya hiyo "nolle prosequi" (mashtaka kuondolewa) ya Serikali.
Hivyo basi, furaha, nderemo, na shangwe zinazoendelea kuhusu Mbowe kuwa huru (mawakili wake na wanachama wa CHADEMA) ni ushahidi kuwa mashtaka dhidi ya Mbowe na wenzake ni ya kweli.
Kwa hoja zangu hizo mshindi ni viongozi wa dini waliomwomba Rais amwondolee Mbowe mashtaka. Wakati Rais, kama M/kiti wa CCM, chama tawala, na Serikali yake amevuna imani ya WaTz, Mbowe bado anawajibika kuthibitisha kuwa hana hatia kwa mashtaka dhidi yake.