Kesi ya Mbowe: Mbowe na viongozi wa CHADEMA msiposikiliza ushauri wa Godbless Lema anaeshauri muondoe mawakili mahakamani, mtakuja kujiulaumu sana

yaani Kibatala amsikilize Lema?![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
kweli ndio maana Halima Mdee na wenzake walikimbia huu upuuzi.
 
Yeye alinusuru maisha yake kwa nini Mbowe asinusuru ya kwake?
 
Mmemuelewa huyu kweli tatizo ukiwa sisiyemu na akili zinatoka

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri wa Lema sio mzuri. Kesi iendelee mpaka mwisho wake hata kama hukumu inajulikana. Kwa kuendelea nayo ndio kutathibitishia ulimwengu kuwa ni ya kupanga. Ni kama vile hilo suala la kususia uchaguzi. Ushiriki wao wa uchaguzi mkuu ndio umewapa ushahidi wa ubovu wa Tume ya Uchaguzi. Hii ni kuliko uchaguzi wa serikali za mitaa waliosusia. Waendelee hivyo hivyo na ikiwezekana siku ya hukumu Mbowe aseme neno. Mandela hakususia kesi ingawa alijua tayari amehukumiwa ila alitumia platform ile kuelezea ubaya wa serikali ya makaburu. Asingeweza kufanya hivyo kama angesusia na kuamua kukaa kimya. Ushauri wa Lema kwenye suala hili unastahili kupingwa.

Amandla...
 
Naungana na Lema. Wajitoe kwa maelekeZo ya Mbowe, then wandike resume kwanini wamejitoa ambayo itasambazwa dunia nzima clearly showing how the judiciary and gov has already made a judgement. kaeni mlijadili hili....
hizo ni akili za wavuta bangi.
Kibatala hawezi kufuata akili za wavuta bangi.
na safari hii ndio mtajua kuwa mahakama huwa haitishiwi nyaau..........
 
Mbowe ashafungwa siku ile BBC
Thirooo akaja kumalizia
Kinachoendelea pale jirani na Udsm ni maigizo ya Bongo movie
Eti jaji anasema kwa mawazo yangu binafsi "naona....." [emoji848][emoji848][emoji848]
,
 
yaani Kibatala amsikilize Lema?![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
kweli ndio maana Halima Mdee na wenzake walikimbia huu upuuzi.

Walikimbia au wameenda kulinda matumbo? Umesikia hata huko bungeni wakiwa moto kama awali? Hapo sio suala la kumsikiliza Lema, bali ndio uhalisia.
 
Katika Hali ya uongozi wa kionevu wa Serikali ya CCM, kuanzia JPM na sasa SSH. Baba Mungu YAHWEH, yapime maneno aliyoyatoa Stuxnet. Kama ni ya Kweli naomba msamaha kwa ajili ya Tanzania. Lakini Kama ni ya Uongo wakati Taifa linaishi kwenye uonevu mkubwa Kiasi hiki! Eeeee Mungu YAHWEH... Amua Leo hii Juu Stuxnet tumechoka na maonevu ndani Tanzania.
 
Naungana na Lema. Wajitoe kwa maelekeZo ya Mbowe, then wandike resume kwanini wamejitoa ambayo itasambazwa dunia nzima clearly showing how the judiciary and gov has already made a judgement. kaeni mlijadili hili....

This sounds good.
 
Hii kesi iendelee haijalishi kuwa Mbowe atafungwa au la tunahitaji kuweka record sawa tupate kujua madhaifu ya mahakama zetu na ubovu wa serikali ktk kuingilia mihimili mingine,ni kesi yenye mvuto mkubwa kuwatoa mawakili eti kwa kuwa rais keshamhukumu mshtakiwa hautasaidia acha tuone mbivu na mbichi.
 
Tuko katika hatua mbaya sana ingawa ndio tunaelekea kupata ukombozi wa kweli. Yote haya lazima yatokee kwanza kabla ya mabadiliko kutokea.
Sikutegema kama Samia anaweza kuwa hivi! na uislamu wote anaou portray mbele za watu anafanya hivi kweli? Mungu atamlaani
 
Salary Slip hoja yako ni ngumu lakini ni nzuri. Naomba niku address maswali yafuatayo.
1. Mawakiri wakishatolewa na mwenyekiti akakaa kimya, na kweli mahakama ikamfunga mwenyekiti miaka 30. Je chama kitafanya nini ili kuhakikisha mwenyekiti anakuwa huru?? Hatua gani itafuata??
2. Mwenyekiti akisema Hana Imani na mfumo WA mahakIama je tutakuwa kwenye position ya kukataa rufaa mahakama ya rufaa??
 
Unga umezidi maji au siyo!!

Kama tulivyoipongeza mahakama kwenye hukumu ya kesi ya Sabaya,tutaipongeza pia kwenye hukumu ya Mbowe.

Kurukaruka kwa maharage ndiyo kuiva kwenyewe.
 
Nimeuliza swali kama hilo! 27 yrs of mandela hatutaki Mbowe aende huko.

Lakini nikuulize, wameshadhamilia kumfunga, sasa hata akimaliza kesi si watamfunga?
 
Walikimbia au wameenda kulinda matumbo? Umesikia hata huko bungeni wakiwa moto kama awali? Hapo sio suala la kumsikiliza Lema, bali ndio uhalisia.
Serikali siyo wajinga kumfungulia Mbowe kesi ya ugaidi. Mbowe mwenyewe anajuwa namna alivyolikoroga.

Muulizeni kati ya Desemba 2020 na March 2021 mpaka tunamzika Magufuli alikuwa wapi? Muulizeni ni kitu gani aliomba kwenye ubalozi wa Denmark na alijibiwa nini?

Nendeni na ubalozi wa Canada mkaone status ya papers zake kwa alichokiomba. Mmasingizia alikuwa kwenye biashara zake Dubai, ana biashara gani Dubai?

Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?

Mbowe alitaka kuweka nchi kwenye status of instability immediately baada ya uchaguzi kukamilika. Serikali ilipogundua njama ndipo akalazimika kukimbia.

Nani kasikia masekondari ya shule za Kisslami yanachomwa tena baada ya Mbowe kuwa mikono salama pale Ukonga?

Na kwa kiasi kikubwa amshukuru Samia ambaye ameacha Mahakama itende haki kwani ingekuwa hajawahi kukimbia nchi wakati wa Mwendazake, saa hizi Mbowe angekuwa na msaidizi wake Ben Saanane huko kuzimu.

Nashangaa Wana CDM mnamtukana Rais SSH eti mwanamke wakati ameacha uhuru wa habari na utawala wa sheria uendelee.
 
Soma historia ya watu waliofungwa na kesi za aina hii katika mataifa mbalimbali kama vile Afrika kusini na kwingineko, utajua nini kitakuja kutokea hapo baadae kama matokeo ya kumfunga Mbowe.

Historia na maandiko matakatifu vinatosha kabisa kutufanya tuwe watabiri wazuri kwani katika dunia ya leo, hakuna jambo jipya zaidi ya teknolojia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…