Kesi ya Mbowe: Mbowe na viongozi wa CHADEMA msiposikiliza ushauri wa Godbless Lema anaeshauri muondoe mawakili mahakamani, mtakuja kujiulaumu sana

Serikali siyo wajinga kumfungulia Mbowe kesi ya ugaidi. Mbowe mwenyewe anajuwa namna alivyolikoroga.

Muulizeni kati ya Desemba 2020 na March 2021 mpaka tunamzika Magufuli alikuwa wapi? Muulizeni ni kitu gani aliomba kwenye ubalozi wa Denmark na alijibiwa nini?

Nendeni na ubalozi wa Canada mkaone status ya papers zake kwa alichokiomba. Mmasingizia alikuwa kwenye biashara zake Dubai, ana biashara gani Dubai?

Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?

Mbowe alitaka kuweka nchi kwenye status of instability immediately baada ya uchaguzi kukamilika. Serikali ilipogundua njama ndipo akalazimika kukimbia.

Nani kasikia masekondari ya shule za Kisslami yanachomwa tena baada ya Mbowe kuwa mikono salama pale Ukonga?

Na kwa kiasi kikubwa amshukuru Samia ambaye ameacha Mahakama itende haki kwani ingekuwa hajawahi kukimbia nchi wakati wa Mwendazake, saa hizi Mbowe angekuwa na msaidizi wake Ben Saanane huko kuzimu.

Nashangaa Wana CDM mnamtukana Rais SSH eti mwanamke wakati ameacha uhuru wa habari na utawala wa sheria uendelee.
 

Huu utoto umecopy na kuniletea, wakati aliuleta nimempa vitasa huko saa hii anatapika tu Makande.
 
Uko sahihi
 
Unga umezidi maji au siyo!!

Kama tulivyoipongeza mahakama kwenye hukumu ya kesi ya Sabaya,tutaipongeza pia kwenye hukumu ya Mbowe.

Kurukaruka kwa maharage ndiyo kuiva kwenyewe.
Ipo siku mtakuja juta kufungua hii kesi na mtakuja laumia sana.

Someni matokeo ya kesi za aina hii duniani mtajua nini kinaweza kutokea.

Hata kama mmekosa maarifa, hata historia inashindwa kuwaongoza?!

Anyway, kabla ya nyie kupoteza dola, lazima tuyashuhudie haya na mengineyo siku za usoni(historia inaonyesha hivyo).
 
Jambo la yakini ni hili mbowe akifungwa itatengeneza uhasama Kati ya ccm na wananchi. Popote atakapoonekana mwanaccm na uniform majaliwa yake anajua mungu kwani huku mtaani watu wanaamini ccm inamsumbua mbowe na inataka kumfunga kwani watu wanahoji Kama walitaka kumuua lisu watashindwa kumfunga mbowe?
 
Sijui umekurupuka kutoka wapi ukaja na hii mihemko hapa.

1. Unadai Mbowe ndie alihusika kuchoma shule za kiislamu moto, wakati hati yake ya mashtaka ni kutaka kulipua vituo vya mafuta, hili shtaka lako jipya peleka ushahidi mahakamani usituletee kelele hapa.

2. Unashangaa Mbowe kusafiri kati ya Dec. 2020 na March 2021, kwani hiyo ndio mara yake ya kwanza kutoka nje ya nchi? na kama alikuwa nje ya nchi na serikali wanamtafuta kwanini hawakutumia interpol wawasaidie kumpata? hapa napo wewe ni jinga tu.

3. Unadai kuna matatizo kwenye paper zake ubalozi wa Denmark na Sweden, vyema tuwekee hapa tuyaone hayo matatizo, usituletee umbea wako uliouokota mtaani halafu unataka kutulisha na sisi pumba, hapa tunakwenda na evidence.

4. Kama unaamini Mbowe hana nguvu, kwanini alivyoenda Mwanza kwaajili ya kudai Katiba Mpya ndio serikali ikamkamata, kwani kabla ya kukamatwa kwake hawakujua kama alikuwepo Kilimanjaro na Dsm? sijui umekurupuka toka wapi kuja kujaza server ya watu kwa huu upupu wako wakutunga.
 
Mimi binafsi sina shaka na mawakili! Shaka yangu ni juu ya wale alioshitakiwa naye.Wale siyo kwamba wamechomekwa kwa lengo ambalo hatulijui?
 
Japo ni maamuzi magumu lakini ndio mwenendo unavyoelekea
 
Huo ushahidi ulionao wewe peke yako ambao hata Kingai na Mahita hawana.


Utopolo.
 
Mimi binafsi sina shaka na mawakili! Shaka yangu ni juu ya wale alioshitakiwa naye.Wale siyo kwamba wamechomekwa kwa lengo ambalo hatulijui?
Mwenendo wa kesi. Hiyo ya kuchomekwa wale wengine ni kesi nyingine.
 
Umenena pointi.

Kama alivyomkataa yule jaji wa mwanzo, afanye kuondoa mawakili. Huwezi kutetewa na mawakili wakati hadi rais alishakuhukumu kupitia chombo kikubwa cha habari, ni upotevu wa muda.
Maza sijui alipewa ushahidi gani ambao mpaka sasa wanashindwa kutoa mahakani na sisi tuone huo ukweli wao. Maana mpaka sasa hauhitaji kuwa mwanasheria kujua kuwa kesi hii imeumbwa.
 
Achana na huyo Mpumbavu ana ushahidi ambao hata Kingai na Mahita hawana. Mpuuzi huyo.
 
Napinga hii hoja, kujitoa mapema kwenye hii kesi kwa style ya kususa ndio kutawapa jamhuri sababu ya kupandikiza propaganda zao ambazo mpaka sasa zimefeli, kesi ibaki mahakamani mpaka dakika ya mwisho, na ikibidi kama hukumu itakuwa mbaya wakate rufaa mahakama ya rufani.

- Wacha ulimwengu unaofuatilia hiyo kesi uendelee kujionea kila hatua ya uozo wa mahakama zetu na majaji, wawakilishi wao wapo wanahudhuria hiyo kesi, kitendo chochote cha kujitoa utakuwa ni utoto usiokuwa na maana yoyote.

Kila jambo linalofanywa huacha precedence iwe mbaya au nzuri, kususia kesi mahakamani itaonekana jamaa ni wahalifu kweli na wataitumia karata hiyo kuwajaza ujinga wale wasiojitambua na watawaamini, kwamba Chadema ni chama cha vurugu, hakuna kuitoa kesi mahakamani, wacha waendelee kujivua nguo mpaka dakika ya mwisho, wenye akili zao wanaujua ukweli.
 
Manzoni mlisema Serikali ifute kesi ya Mbowe kukwepa aibu maana haina ushahidi. Sasa mnabadili gia angani Mbowe awaondoe mawakili. Mimi nasema kesi iendelee mpaka mwisho na haki itendeke.
 
Watajuta lini? Tayari wameshaanza. Hii kesi imefunua uozo mwingi sana.
 
Duniani?

Nenda Rwanda hapo jirani tu ujionee PK anavyowafunga wapinzani wake kwa uhaini na kuwasamehe akijisikia and nothing has changed.

Unamfahamu Kenule Beeson "Ken" Saro Wiwa? Naye aliamini kwa ile hukumu ya kunyongwa ingemfanya awe hatari zaidi akiwa mfu kuliko hata akiwa hai.

Kwa aina ya upinzani uliopo na sampuli ya wafuasi wake,tuna miongo si chini ya 6 hizi wishful thinking zikiendelea kuwa ndoto.
 
ninge kuwa mfuasi wa mbowe, ktk kipindi hiki kigumu ningemshauri atubie sana maovu yake aliyo yatenda yanayo julikana na yasiyo julikana, maana huenda hii ni saaa ya malipo kwake kwa uovu alio watendea wengine.
 
Hata Yesu alihukumiwa kusulubiwa kwa hila za wanadamu.

Isitoshe, hata mkimfunga Mbowe, CHADEMA bado iko pale pale na moto wake ule ule.
Ndio maana munataka atoe mawakili na yeye auchune kimya, ili afungwe muchukue uenyekiti sio?
 
Huna akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…