Kwa hisani ya watu wa tweeter!
Freeman Mbowe na wenzake wameletwa tayari. Lakini ulinzi mkali umeimarishwa. Askari wengi. Pia kuna zuio la watu kuingia ndani ya mahakama. Wanasema ni mawakili 20 tu, wanahabari 10 (leo wameruhusiwa), ndugu 5, Viongozi 5, lakini simu marufuku. Tunatafuta alternative, TUWAJUZE!
__________________________
Hadi sasa, tumegoma kuingia ndani ya chumba cha mahakama kwa mafungu ya nyanya na kuingia bila Simu zetu. Sababu ya kugoma, utaratibu wa kuingia unasimimiwa na RPC KINONDONI ambaye bado anaendelea kutoa ushahidi mahakamani kwa kushirikiana na RCO KINONDONI upande wa jamhuri.
______________________________
Tumekubaliana kwamba, viongozi wote kama utakuwa msimamo wao kutokuingia na simu na sisi hatutoingia na TUTATOA MAWAKILI WOTE TUONDOKE NAO..
Kesi isiendelee mpaka pale mahakama itakapoweka utaratibu vizuri, kisheria, badala ya mahakama kuwa controlled na upande mmoja wa kesi
________________________________
Katika mashahidi 24 wanaotegemewa kuletwa na upande wa mashtaka, Mashahidi ambao ni polisi ni 21, kwa kukubaliana polisi kupanga utaratibu mahakamani tafsiri yake wanaingilia mhimili wa Mahakama na mahakama haiwezi kuwa huru kwa taswira hiyo. Tumekataa kuingiza mawakili ndani.
____________________________
Askari magereza wanalalamika kwamba jana tumefanya ujinga sana. Ujinga gani, tunawaukliza, wanasema tulikuwa tunatuma habari nje. Wanamueleza Benson Kigaila, NKM CHADEMA. Tumewaeleza kwamba, anayetakiwa kulalamika ni Jaji sio wao. Mahakama siyo gereza. Wajishikilie vizuri.
____________________
Mahakama imechelewa kwa dakika 40, yote hii ni kutokana na Jamhuri kutaka kuhodhi mamlaka ya mahakama, bila kujua kwamba wote hapa tuna interest na kesi hii, wao ni walalamikaji, sisi ni watuhumiwa. Kwanini watuzuie kuingia mahakamani na simu? Mahakama sio gereza lao. Tumewaeleza
________________________
Watoto wote wa Freeman Mbowe, (Nicole na Dudley) pia wapo nje ya mahakama, pamoja na ndugu zao wengine.
Kama kawaida yao, makarao waliovalia kiraia, wamekaa kwenye siti karibu zote za mahakama, wamechukua nafasi kama kesi ni yao pekee yao.
Mambo ya ajabu yanafanyika
___________________
Lakini kitu cha muhimu hadi sasa ndugu zangu ni kwamba, kwa umoja wetu wote tupo nje ya mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Ubungo-Mawasiliano, tumeshawaelekeza MAWAKILI wetu wasomi kwamba "No ENTRANCE NO CASE"... And it's done, hii ni open court!