MWENDELEZO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART 4.
[emoji117]SHAHIDI; ikafunguliwa kesi ya kula njama ya kutekeleza Matendo ya kigaidi.
Wakili wa Serikali; ilifunguliwa wapi?
Shahidi; Police Central Dar es salaam. °
JAJI; ulifungua kesi gani?
SHAHIDI; Kula njama ya kutenda vitendo vya kigaidi.
[emoji117]Wakili wa Serikali; ACP kingai, unasema ulimueleleza Inspector Swila kufungua jalada la kesi ya kula njama ya kutekeleza matendo ya Kigaidi, kwanini?
Shahidi; nature ya makosa yenyewe, yangeweza kufanywa yangeweza kuleta madhara kwa watanzania haswa katika kipindi tulichokuwepo.
[emoji117]Wakili wa Serikali; baadae nini kilifuata?
Shahidi; tarehe 04.8.2020 nilienda kukutana na Ltn Denis Urio, aliniambia kwamba alishapata tena vijana wawili na amewaunganisha na Freeman Mbowe
Akanitajia vijana hao ni Adam Kasekwa maarufu Adamoo na Mohammed A. Ng'wenya.
[emoji117]JAJI; Endelea
Wakili wa Serikali; baada ya taarifa nini kiliendelea?
Shahidi; alinieleza tayari vijana wamefika Moshi
JAJI; elezacni vijana wapi, wote wanne au wawili wa mwisho
Shahidi; ahsante Mheshimiwa, aliniambia vijana 3 kati ya hao wa 4
Waikili serikali; tarehe ngapi?
[emoji117]Shahidi; tarehe 04.8.2020
Wakili wa Serikali; akina nani hao Luteni Dennis Urio aliokueleza wamefika tayari Moshi?
Shahidi; ni Mohammed A. Lingwenya, Adam Kasekwa na Moses Lijenge
Wakili wa Serikali; Eleza walikuwa wamefikia kwa madhumuni gani?
[emoji117]Shahidi; Watu hao walikuwa wamefikia wilaya ya Moshi, na walikuwa wamekusudia kumdhuru Lengai Ole Sabaya, ambaye kwa kipindi kile alikuwa Mkuu wa wilaya ya Hai
Wakili wa Serikali; Baada ya kupokea taarifa hiyo ulichukua hatua gani?
[emoji117]Shahidi; Niliwasiliana na DCI nikamfahamisha na baada ya kumfahamisha alielekeza niunde timu itakayofanya ufuatiliaji na hatimaye kuwakamata watu hao. Kabla awajafanya Madhara yoyote kwa wahusika
Nilimtafuta ASP wa Polisi ambaye sasa ni mkuu wa upelelezi Arumeru, Jumanne.
[emoji117]Shahidi; Mwingine Inspector Mahita, Detective koplo Francis, Detective Constable Goodluck na Dereva wangu Constable Azizi. Tulianza Kuweka amiundo Mbinu ya kuwakamata watuhumiwa kabla hawajafanya madhara yoyote.
Wakili wa serikali; Elezea Ulifanya nini baada ya Ufuatiliaji
[emoji117]Shahidi; Siku ya Jumanne nilieleka Moshi, ambapo hao watuhumiwa walikuwa, na kwamba Jioni ile tulianza ufuatiliaji wa hao watuhumiwa kwa ajili ya kuwakamata. Baada ya mawasiliano na wasoro wetu tulihairisha zoezi na usiku ule tukawa tumelala Moshi.
[emoji117]Shahidi; Asubuhi 05.8.2020 tuliamka na kuweka miundombinu na wasiri wetu kwa ajili ya ya ufuatiliaji. Tulipata taarifa kuwa watuhumiwa wapo maeneo ya RAO, Moshi
Wakili wa Serikali; baada ya kupata taarifa hiyo ulichukua hatua gani?
[emoji117]Shahidi; tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 2, Adam kasekwa na Mohammed Ling'wenya. Wakati tumewakamata, tumewaweka chini ya ulinzi nilimuelekeza ACP Jumanne awapekue maungoni. Adama kasekwa alivyopekuliwa alipatikana akiwa na Pisto 1 aina ya Ruvern iliyokuwa na namba 53A 5340
[emoji117]Shahidi; Pia alikutwa na risasi 3. Alikuwa na kete 58 za Heroine, madawa ya kulevya. Mohammed Kingwenya alikuwa na Kete 25 za Madawa ya Kulevya.
Wakili wa Serikali; Eleza upekuzi huu ulifanyika mbele ya nani?
Shahidi; ulifanyika palepale mbele ya mashahidi.
[emoji117]Shahidi; Mmoja namkumbuka anaitwa Anita na mwingine anaitwa Esther. Baada ya kujaza hati ya kuchukua vitu, tuliwachukua watuhumiwa na wale mashahidi hadi kituo cha Polisi mjini kati, eneo la RAU lilikuwa siyo Rafiki kwa kuandika Maelezo yao Pale, ilikuwa la Fujofujo.
[emoji117]JAJI; Spelling za hilo eneo,
Shahidi; Ni RAO
JAJI; Mwanzo tulikuwa tunasikia ni RAU. Kwa hiyo ni RAU au RAO?
Shahidi; ni RAO, Madukani.
Baada ya Kufika ofisi ya mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro nilimuachia Jumanne aendelee kufanya Mahojiano
INAENDELEA PART 5.