Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

Hilo ndilo linaloendelea kwenye dodoso za huyu shahidi #4. Tusubiri hitimisho la dodoso kwa huyu shahidi.

Kuweka rekodi sawa sawa, dodoso kwa shahidi #4 limekwisha na kesho inshallah anapanda kizimbani moja kwa moja shahidi #5.
 
Tena yamesainiwa kituo kikuu Cha Polisi Moshi siyo hapo Rau ili hesabu ziendane na na saa 7.Au walirudisha mahare wa saa nyuma?
 
Inabidi uwe zuzu ndiyo mtu anaweza kukubaliana na wewe.
 
Mimi huwa kuna kamsemo nakapenda sanaa wkt wa mahojiano...unakuta shahidi kaingia chaka...unaskia tu wakili anamwambia...iambie mahaka au jaji kwamba hapa nmedanganyaa...dizain kama unasnitch kwa jaji....ila ukijua sheria ni raha sanaaa
 
Daaa sikufuatilia maana nilijua leo ni upande wa serikali
Huwa upande wa Jamhuri ni hapo hapo, cross examination kutoka mawakili wa upande wa utetezi ni hapo hapo na hata re-examination kutoka mawakili wa upande wa Jamhuri ni hapo hapo. Leo ambacho hakijafika mwisho ni re-examination ingawa ilifanyika hadi mahakama ilipoahirishwa. Hivyo kesho ni kumalizia re-examination kutoka upande wa mawakili wa upande wa Jamhuri. Lengo la hii re-examination kutoka mawakili wa upande wa Jamhuri ni "ku repair damage" iliyosababishwa na mawakili wa upande wa utetezi kwa shahidi wao wakati wa cross examination.
 
Asante sana mkuu ufafanuzi wa kina.
 
Shahidi ana ugonjwa wa macho pia hakumbuki vizuri lakini ameweza kukumbuka namba ya bunduki haleluya
Hii kesi imejaa maruwe ruwe! Naamini hata Majaji wanaiendeleza hii kesi kwa lengo la kutaka kutoa mafunzo kwa Majaji na Mawakili wengine siku za usoni!

Kinyume na hapo, hii kesi ni ya kufutilia mbali. Maana haina uhalisia hata kidogo.
 

Shahidi #4 imetoka. Kesho straight #5.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…