Kesi ya Mbowe: Umuhimu wa Ushahidi wa Kaaya ni upi?

Umuhimu wake ni maelezo yake na matendo ya Mbowe ambayo aliyafanya. Ni kithibitisho cha alichofanya gaidi kama atabainika kuwa gaidi
 
Mbowe amekiri kuyapokea hayo majina aliyopewa na Kaaya? Na unajua aliyataka kwa sababu gani?
 
Nafikiri Shahidi ana umuhimu wa ku link kwamba Mbowe alikuwa na dhamira ya kumdhuru Sabaya, kuwa alienda kutafuta namba za watu wake wa karibu, ikiwemo walinzi wake..Sisemi kuwa ushahidi wake una mashiko ila lengo la ushahidi wake ndio huo
 
Hawa vijana wa ccm reasoning capacity yao ni ndogo sana mpaka wanatia huruma kwa kweli, sasa kitu kidgo kama hicho ameshindwa kuelewa kweli?
 
Nadhani Kibatala hakuigeuza bali kamsaidia kumfafanulia tu.

Ndiyo maana baadhi ya watajwa wamekwisha hukumiwa.

Kama Mh. Mbowe alivyomwambia kwa maana halisi ya kuwa:

"The rest wasn't his business."
Kwa jicho la kisheria, maelezo ya shahidi #2 kwenye eneo hilo, yametumiwa na Kibatala kwa faida ya Mbowe. Ameyaweka kwa namna ambayo hata shahidi hakujua anaelekezwa kutoa faida kwa Mbowe. Mawakili na Jaji, wameliona hilo na imewekwa kwenye records.

Cc mliberali
 
Ni kweli alikutana. Ni kweli alimpa pesa. Ni kweli alikua na mawasiliano naye kwa simu na kuonana. Ni kweli alipewa majina ya wahalifu wa genge la Sabaya nk.

Baada ya hayo yote, Mbowe alianza kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kureport kwenye vyombo husika kwamba kuna genge linadhuru watu na linataka kumdhuru yeye pia. Hatimaye serikali ilifanyia kazi hizo tuhuma na wahalifu wamehukumiwa miaka 30.
 
Mbowe amekiri kuyapokea hayo majina aliyopewa na Kaaya? Na unajua aliyataka kwa sababu gani?
Hayo majina akiwemo Sabaya, sasahivi wamehukumiwa miaka 30. Bado huoni kwa nini Mbowe aliyahitaji majina hayo? Hasa ukichukilia yeye Mbowe alikua ni Mbunge wa Hai ambako wahalifu hao walikuwepo wakiongozwa na aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai. Mbunge alikua anapewa taarifa na wananchi (akiwemo Kaaya) juu ya uhalifu wa hao wenye majina.
 
Nafikiri Shahidi ana umuhimu wa ku link kwamba Mbowe alikuwa na dhamira ya kumdhuru Sabaya, kuwa alienda kutafuta namba za watu wake wa karibu, ikiwemo walinzi wake..Sisemi kuwa ushahidi wake una mashiko ila lengo la ushahidi wake ndio huo
Kaaya kashindwa kufanya hivyo, kashindwa kujielekeza kama unavyopenda iwe. Hata Jaji anajua kwamba, shahidi huyo alikua wa maana hiyo, lakini kahamishwa muelekeo na Kibatala na kujikuta anamsafisha mtuhumiwa wa ugaidi Mbowe na amekiri kwamba Mbowe hakuwa anafanya vikao vya uhalifu. Jaji kazi yake ni kuandika na mwisho ni kutoa ruling.
 
Waliombambikiza kesi hii ni mazuzu tu
 

Uko sahihi mkuu. Kuomba namba au majina ya watu haijawahi kuwa uhalifu! Kujua namba na jina la mtu bila yeye mwenyewe kujua si uhalifu. Shahidi alipoulizwa kama alisikia uhalifu ukipangwa ktk vikao na akasema hapana, aliua kabisa sababu ya yeye kuwepo pale!! Alipoulizwa kama alitoa taarifa polisi, kwa Sabaya kuhusu hata kuombwa majina akasema hapana, aliua kabisa hata sababu ya yeye kutokea sasa hivi kama shahidi!! Mbaya zaidi ni kuonesha alikutana na Mbowe huku au Mbowe akiwa gerezani au yeye akiwa gerezani!! Na alipokubali kuwa maelezo yamechukuliwa baada ya kuachiwa huru - dhana ya kuwa jambo hili lilipangwa inakuja (japo kisheria sio baya).

Shahidi wa 2 hakuwa na maana iliyokusudiwa na upande wa mashitaka. Mbowe anaweza kukubali alikutana nae na kwa kuwa hakuna ripoti kuwa alitaka kuwadhuru na hawajashurika mpaka sasa - isiwe na madhara kwake.
 
Ni mapema sana ku conclude hivyo hatujui mashahidi wanaofuata watasema nini. Inawezekana wanajenga kesi ili baadae walete ushahidi mwingine ambao uta collaborate na ushahidi wa Kaaya.
 
Nadhani ushahidi muhimu katika kesi hii ni yale maelezo ya watuhumiwa ya kukiri kosa ambayo yaliwekewa pingamizi lakini mwisho wa siku mahakama ikayapokea!
 
Hakika mkuu. Hizo logics umeziweka vizuri. Hoja za mawakili wa utetezi zilifanikiwa kuharibu ushahidi wa Kaaya.
 
Nadhani ushahidi muhimu katika kesi hii ni yale maelezo ya watuhumiwa ya kukiri kosa ambayo yaliwekewa pingamizi lakini mwisho wa siku mahakama ikayapokea!

Huu ni vyema kuuita ushahidi wa Jaji Siyani ambaye hata hivyo hajaweka bayana aliona au kusikia nini kutoka kwa washitakiwa kabla ya kukamatwa kwao.
 
Wewe jamaa akili zako ZA kishenzi kama meko na Sabaya wake.
Mtaishia kubaya

Faida ya roho mbaya unayoishabikia ni maiti .
Na hawa unaowashabikia watakuruka kama walivyomruka Sabaya
 
Hii kesi uzito wake nadhan n yale maelezo ambayo yalikataliwa kwenye kesi ndogo.... kwangu nadhani ndo msala mkubwa kwa washtakiwa... sijui watapangua kwa mbinu ipi
 
Hivyo ndivyo ulivyoona wewe?
Ila kwa upande wangu nimeona kuwa
1. Kaaya kamuunganisha Mbowe na Sabaya
2. Kaaya kamuunganisga Mbowe na Bwire et al
3. Kaaya kaonyesha kuwepo kwa mikutano kwenye maeneo yanayomilikiwa na Mbowe
na hii ndiyo kesi yenyewe
 
Hii kesi uzito wake nadhan n yale maelezo ambayo yalikataliwa kwenye kesi ndogo.... kwangu nadhani ndo msala mkubwa kwa washtakiwa... sijui watapangua kwa mbinu ipi
Subiri utaona. Mawakili kazi yao ni hiyo. Ushahidi wa upande wa jamhuri ukiwa na mashaka kama tunavyoyaona na judgement ikawa fair, hakuna kesi hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…