Kesi ya Mirathi ya Dkt. Likwelile: Vicky Kamata ashindwa, mahakama yasema ndoa yao haikuwa halali

Nina swali moja, kwenye mwenendo wa kesi inasemekana Dr alioa 1986. Ndoa ya kiserikali. Mwaka 94 akasheherekea ndoa ya kikristo. Je unapewa vyeti viwili? Kama cheti cha kwanza ndicho halali je ndoa ya kiserikali ni ya mke mmoja au wake wengi?
 
Nimesoma hukumu. Kuna sehemu imeandika vicky alifoji mukhtasari wa kikao cha familia na kuupeleka mahakamani kuonesha familia imemteua kuwa msimamizi wa mirathi.

Hilo swala la kufoji litambana hata akikata rufaa
Forgery haina excuse, na wakimkazia sana anaweza funguliwa kesi ya Jinai!!
 
Pole sana Vicky Kamata!! Pole nyingi kwa watoto wa marehemu kwa kipindi chote cha kutafuta haki yenu na hongereni kwa ushindi ..Hongera na mahakama kwa maamuzi walitotoa ila Dada Vicky kama bado una ukakasi na kudai kuna mahali zako ulichangia naamini mahakama zetu haziangalii cheti cha ndoa tu kama ushahidi fata sheria upate haki yako ...kama ipo
 
Pamoja na ubunge wake anakosa pesa za kujenga?
 
Ndoa ilifungwa 2016 wakati mke halali wa ndoa yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…