Kesi ya Uhaini: Amani Golugwa, amemaliza kutoa ushahidi kesi ya Lissu

Kesi ya Uhaini: Amani Golugwa, amemaliza kutoa ushahidi kesi ya Lissu

IMG-20260907-WA0015.jpg

Hii ndio T.shirt ambayo Tundu Lissu amesema wamembania asivae

Ujumbe wenyewe: “LISSU — SIXTEEN BULLETS SURVIVOR.” Itakumbukwa leo ni kumbukumbu ya kupigwa kwake risasi mwaka 2017.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

MAJAJI WAMEINGIA

Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi.

Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya Mwaka 2025.

Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu

Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha mawakili wenzake:

1. Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali Mkuu
2. Tawabu Issa – Wakili wa Serikali Mwandamizi
3. Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali
5. Kasara – Wakili wa Serikali

Wote kwa pamoja tunaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili.

Mshtakiwa, Tundu Antipas Lissu, yupo kizimbani anajiwakilisha mwenyewe.

Shauri limekuja kwa ajili ya utetezi kuuliza maswali ya dodoso.

Amani Sam Golugwa anapanda kizimbani.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, upo tayari?

Lissu: Nipo tayari, Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: Shahidi, unakumbushwa upo chini ya kiapo.

Nassoro Katuga: Shahidi, upo salama?

Golugwa: Tupo salama.

Nassoro Katuga: Wewe upo salama?

Golugwa: Nipo salama.

Nassoro Katuga: Naamini leo swala lako la mimi na roho mbaya umelifuta.

Golugwa: Ni kweli, wewe una roho mbaya.

Nassoro Katuga: Tuendelee.

Nassoro Katuga: Ni kweli ulisema kwamba mwandishi akichukua content inakuwa ni mali yake?

Golugwa: Ni kweli nilisema.

Nassoro Katuga: Ni kwa mujibu wa sheria?

Golugwa: Ni kwa mujibu wa sheria na uelewa wangu. Ukweli wa jambo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba uliposema mwanahabari anapochukua habari inakuwa ni kwa mujibu wa sheria ipi?

Golugwa: Ni mali yake, ila sijataja sheria.

Nassoro Katuga: (Ha ha ha! Leo umekuja hivyo. Itabidi sasa twende kwenye roho mbaya zaidi.)

Nassoro Katuga: Sasa, shahidi, ni kweli kwamba nilikusikia kwamba kuhamasisha uasi siyo kosa, ni neno la kisiasa? Unakumbuka hayo maneno?

Golugwa: Siyo kosa. Nakumbuka kuyasema.

Nassoro Katuga: Hivi siasa zenu za CHADEMA mnazozifanya mnatumia lugha gani?

Golugwa: Ni lugha ya Kiswahili.

Nassoro Katuga: Ni kamusi gani inayotumika kutafsiri hiyo lugha ya Kiswahili?

Golugwa: Tunatumia lugha ya Kiswahili, lakini kama patakuwa na jambo gumu tunatumia kamusi ya Kiswahili.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kuna kamusi inaitwa Kamusi ya Lugha za Kisiasa, kwa ufahamu wako na uzoefu wako.

Golugwa: Sina kumbukumbu.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kuna kamusi inayoitwa Kamusi ya Lugha za Kisiasa.

Golugwa: Hakuna.

---

Nassoro Katuga: Unakumbuka ulisema huoni kosa lolote mtu akisema anaenda kuvuruga uchaguzi?

Golugwa: Nakumbuka, hakuna kosa.

Nassoro Katuga: Ni kwa mujibu wa sheria au maoni yako kwamba maneno hayo hayana kosa?

Golugwa: Ni ukweli, kwa mujibu wa shughuli za kisiasa, maneno hayo hayana kosa.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unafahamu Uchaguzi Mkuu upo kwa mujibu wa Katiba.

Golugwa: Ndiyo, nafahamu.

---

Nassoro Katuga: Nilikusikia pia ukiwaambia Waheshimiwa Majaji kitendo cha kuvunja sheria hakipelekei kosa la uhaini.

Golugwa: Hapana, sikusema hivyo.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, kama wakikuta sehemu umesema kuvunja sheria hakupelekei kosa la uhaini wakuone wewe muongo?

Golugwa: Nitahitaji kurefresh memory.

Nassoro Katuga: Unakumbuka haya maneno kwamba kupinga sheria ni kosa?

Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulitaja hizo sheria zinazosema kupinga siyo kosa.

Golugwa: Nilisema kupinga siyo kosa, ila sikutaja sheria.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama sentensi “tunaenda kuzuia uchaguzi” ni sentensi kamilifu na yenye maana au siyo kamilifu yenye maana.

Golugwa: Ikisomwa vizuri ni sentensi kamilifu yenye maana.

Nassoro Katuga: Unakumbuka ulirejea maneno ya Mwenyekiti aliyoyaongea siku ile, ukataja na muda?

Golugwa: Kati ya saa moja na nusu hadi mawili.

Nassoro Katuga: Ulisema kilicholetwa katika hati ya mashtaka ni sehemu ndogo ya sekunde ngapi?

Golugwa: Sekunde 26.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia Mwenyekiti akisema Majaji ni MaCCM.

Golugwa: Sikumbuki. Aulizwe mwenyewe mhusika.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia au hukusikia maneno ya Mwenyekiti kwamba mahakamani hakuendeki.

Golugwa: Sikumbuki.

---

Nassoro Katuga: Je, ulimsikia akisema polisi wanaingiza kura feki kwenye vibegi mgongoni?

Golugwa: Sikumbuki.

Nassoro Katuga: Shahidi, wewe hayo uliyosema kuhusiana na hotuba ya Mwenyekiti ni maneno yote aliyosema Mwenyekiti au umechagua machache?

Golugwa: Nilisema niliyoweza kuyasema. Sina kiwango cha kupima ni yote au kuna yaliyo baki.

Nassoro Katuga: Unaiambia Mahakama kwamba yale uliyosema yalichukua masaa mawili?

Golugwa: Yamechukua masaa mawili.

Nassoro Katuga: Hujui kama, unajua kuna mengine aliyozungumza ambayo wewe hukuyasema?

Golugwa: Sifahamu.

Nassoro Katuga: Huyo unayemzungumzia amesema hapa Mahakamani kwamba Majaji ni MaCCM. Ulikubali naye?

Golugwa: Sijawahi kuyasikia.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama vikao vya chama chenu huwa vinakuwa na maazimio.

Golugwa: Waheshimiwa Majaji, katika utaratibu wa vikao vya kawaida huwa vinakuwa na maazimio.

---

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama nilikusikia vizuri kwamba wewe kazi yako ni mtunza kumbukumbu/mwanza wa hadidu.

Golugwa: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Ni kweli au si kweli kwamba maazimio ni sentensi fupi zenye kueleweka?

Golugwa: Ni kweli, Waheshimiwa Majaji.

Nassoro Katuga: Kama nilikusikia unasema neno “kukinukisha”, ulilisikia?

Golugwa: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni kweli au si kweli kwamba “kukinikisha” ni kitendo?

Golugwa: Linaweza kubeba muktadha wa kitendo.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako, wewe ulieleza Mahakama hii tukufu kwamba pale Mwenyekiti aliposema “kukinikisha”, mlitakiwa kwenda kufanya hili na hili?

Golugwa: Sikusema kitendo. Nilitoa tafsiri ya “kukinikisha”.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, je, kuchoma kitu kikanuka ni sehemu ya “kukinikisha”?

Golugwa: Hapana.

Nassoro Katuga: Ila tafsiri yako ya “kukinikisha” ni kukifanya kitu kinuke.

Ukichoma matairi yanatoa harufu au hayatoi?

Golugwa: Tafsiri niliyotoa ni kukifanya kitu kitoe harufu. Sijasema uchome tairi.

Nassoro Katuga: Ukichoma kitu, ikiwemo matairi, kinatoa harufu au hakitoi?

Golugwa: Sifahamu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Nassoro Katuga: Huyu Mwenyekiti wako alieleza ni njia gani ya kukinukisha katika uchaguzi Mkuu

Golugwa: Hatukuwa na lengo la kukinukisha zaidi ya kuelimisha Watia nia

Nassoro Katuga: Kwa hiyo Mwenyekiti huenda alisema mkatumie njia kama ya Washabiki wa Simba Sc kufanya panuke

(kuchimba dawa)

Golugwa sijajua unamaanisha nini.

Nassoro Katuga Ni haki au siyo haki kwa mtu aliye sikia hotuba ya Mwenyekiti kutafsiri anavyotaka

Golugwa inategemea

Nassoro Katuga Kwakuwa Mwenyekiti hakusema maana ya Kukinukisha / njia au maelekezo

Itakuwa ni haki au siyo haki ya mtu kwenda kujisaidia katika kituo cha Kupiga kura na kuacha li kitu lake linanuka pale.

Golugwa: siyo haki

Nassoro Katuga Waambie Waheshimiwa Majaji kama ni haki au siyo haki kwa mlaji wa hotuba kwenda Kuchoma Vituo vya Kupiga kura

Golugwa: siyo haki

Nassoro Katuga Ni Ushahidi wako kwamba Jumuiya ya Ulaya walisikitishwa na vurugu siku ya uchaguzi.

Golugwa ni Kweli

Nassoro Katuga Ni Ushahidi wako kwamba Mwenyekiti alisema tunaenda kuuvuruga huu uchaguzi.

Golugwa ni Kweli

Naasoro Katuga Waambie Waheshimiwa Majaji nikweli kwamba siku ya uchaguzi palikuwa na vurugu

Gokugwa Ni kweli palikuwa na uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Shauri la uhaini namba 19605/2025 linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, litaendelea leo Septemba 7, 2026 katika hatua ya maswali ya dodoso kwa shahidi wa tatu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Amani Golugwa.

Maswali hayo ya dodoso yanaulizwa na Jamhuri, ambao Ijumaa Septemba 4, 2026 kutokana na kutamatika kwa muda wa shughuli za Mahakama hawakuhitimisha zoezi hilo huku wakitarajiwa kuhitimisha leo.

Hatua ya Maswali hayo ilifikiwa baada shahidi huyo kuhitimisha zoezi la kumtetea Lissu katika kesi hiyo na ikiwa itatamatishwa leo majaji watatoa nafasi kwa mshtakiwa kuuliza maswali ya ufafanuzi kwa shahidi huyo (Re-examination).

Tundu Lissu, anashtakiwa kwa kosa la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kama ilivyorekebishwa 2023.

===

Kutoka Mahakamani

Tundu Lissu ameingia Mahakamani muda huu amesema wamemzui kuvaa T shirt iliyoandikwa “LISSU — SIXTEEN BULLETS SURVIVOR.” akiingia Mahakanikuvaa, ila ukumbi mzima umevaa ujumbe huo kwa Niaba yake.


Baadhi ya viongozi wa CHADEMA pamoja na baadhi ya wafuasi wa Chama hicho wakiwa katika ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Septemba 7, 2026, kabla ya kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu kuendelea katika hatua ya maswali ya dodoso kwa shahidi wa tatu Amani Golugwa.

Leo, imetimia miaka 9 tangu aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki na sasa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ashambuliwe kwa risasi akiwa anatoka bungeni kwenda nyumbani kwake Area D na katika ukimbi wa Mahakama wanachama wa CHADEMA wamevalia t-shirt zenye ujumbe kuhusu Lissu

MaCCM yana akili za kiquma na kichoko sana. Wanamtungia Lissu kesi ya uwongo ili kumziba mdomo waendelee kula nchi. Wapuuzi wakubwa!
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3

Nassoro Katuga: Sasa kwa vurugu hizo, kwamba kwa maneno ya siku ya uchaguzi ulivurugika?

Golugwa: Si kweli.

Jaji Ndunguru: Hajaelewa hilo swali.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, hajaelewa nini kaulizwa. Swali kasema “si kweli.” Hamjaelewa nini?

Jaji Ndunguru: Tumesema hatujaelewa sisi hilo swali.

Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba siku ya uchaguzi, uchaguzi ulivurugika?

Golugwa: Si kweli.

Nassoro Katuga: Unajua ni aina gani ya uhaini ambayo mshtakiwa unayemtetea hapa ameshitakiwa nayo?

Golugwa: Waheshimiwa Majaji, mimi si Mwanasheria, sifahamu kwa undani. Najua ameshitakiwa kwa uhaini, kifungu cha 39(2)(d).

Nassoro Katuga: Sasa unafahamu au hufahamu aina ya uhaini aliyoshitakiwa?

Golugwa: Nimeshataja.

Nassoro Katuga: Ni aina gani ya kudhihirisha nia ambayo mshtakiwa ameshitakiwa nayo?

Golugwa: Ameshitakiwa kwa nia ya kutaka kutenda uhaini.

Nassoro Katuga: Hiyo nia ni ipi?

Golugwa: Ametaka kutishia Serikali, Bunge na Mahakama.

Nassoro Katuga: Unafahamu au hufahamu mshtakiwa anashitakiwa kwa kutoa na kuchapisha maneno ya kuzuia/kuvuruga uchaguzi?

Golugwa: Nafahamu.

Nassoro Katuga: Ni kweli au si kweli kwamba unathibitisha kuwa mshtakiwa aliyatoa haya maneno?

Golugwa: Ni kweli, alitoa hotuba ndefu yenye hayo maneno.

Nassoro Katuga: Katika mkutano wa 03 April, baada ya maneno mengi ya kulalamikia uchaguzi, alikuja na sentensi chache za maazimio ya siku hiyo kwamba tunaenda kuzuia uchaguzi?

Golugwa: Hatukuwa na kikao chenye maazimio siku hiyo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba msimamo baada ya Mwenyekiti kuamua kwamba Mahakamani hakuendeki, Majaji ni CCM, ni kweli au si kweli? Wasikilizaji wakashangilia.

Golugwa: Sikumbuki.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, kama wakili ana majibu yake, apande akae yeye kizimbani.

Nassoro Katuga: Sijui ni objection au kitu gani.

Jaji: Tuendelee, shahidi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba msimamo baada ya Mwenyekiti kuamua kwamba Mahakamani hakuendeki, Majaji ni CCM, ni kweli au si kweli? Wasikilizaji wakashangilia.

Golugwa: Sikumbuki.

---

Nassoro Katuga: Shahidi, umesema uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria?

Golugwa: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kulikuwa na nia yoyote ya Mwenyekiti kufungua kesi ya kuzuia uchaguzi?

Golugwa: Haikuwepo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji katika ushahidi wako kama ulizungumza Mwenyekiti katika hotuba yake aliwapa njia gani ya kuzuia uchaguzi?

Golugwa: Mwenyekiti alielimisha. Hakuwapa njia ya kuzuia uchaguzi.

Nassoro Katuga: Je, waambie Waheshimiwa Majaji kama Mwenyekiti alitoa njia ya kuvuruga uchaguzi?

Golugwa: Hakutoa njia ya kuvuruga uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
huyu shahidi mbona kama anachomesha wakuu.muuliza maswali anauliza maswali ya mtego sana shahidi hadi sasa ashaapigwa 3.0
 
07 September 2026
High of Tanzania
Kivukoni Front
Dar es Salaam, Tanzania

Treason case no. 19605 / 2025
Republic versus Tundu Lissu

1788768730234.png
 
Back
Top Bottom