MONEY IS NOT EVERYTHING
JF-Expert Member
- Sep 11, 2024
- 2,242
- 3,161
SHAHIDI NINA MASHAKA NAYE MPAKA HAPO...!
nani tena huyo kafa....?Huko jamhuri ya ndizi wauwaji nao wamefiwaaaaaawamefiwaaaaaaa
Inakuuma eehKwahiyo mnaenda Mahakamani kupiga makofi🤣🤣🤣
Au mnataka muonekane kwenye ma blog
Hafizi ameir mumu wa samuyaNa
nani tena huyo kafa....?
Hii ndio tathimini mujarab ya kahaba la kizimkaziTATHIMINI YA MPAKA SASA
🔴 Prosecution — 80%
🟢 Defence — 20%
All ears mkuu ManyanzaTUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 1.
Jaji Ndunguru: Maswali ya rejea.
Lissu: Nawashukuru Waheshimiwa Majaji.
Shahidi: Pole.
Golugwa: Asante.
Lissu: Naomba nikuulize maswali ya ufafanuzi kutokana na kile ambacho umekisema wakati wa maswali.
Nianze mwanzo kabisa wa cross-examination iliyofanywa na Wakili wa Serikali Mwinuka.
Alikuhoji sana namna ya kushughulikia malalamiko ya uchaguzi, kama yanapelekwa katika Mahakama.
Wewe ukasema unapeleka katika kamati za rufaa.
Hebu wafafanulie Majaji.
Golugwa: Waheshimiwa Majaji, katika malalamiko ya uchaguzi zipo kamati za rufaa zenye wajibu wa kupokea na kufanyia kazi.
Na ndiyo wagombea wetu walipeleka malalamiko ya kukataliwa fomu au kuenguliwa.
Lissu: Ukaulizwa baada ya kupeleka huko kamati za rufaa, ukaulizwa majibu yalikuwaje.
Ukajibu kwamba sehemu kubwa zilikataliwa kwa ushenzi uleule.
Golugwa: Rufaa tulizopeleka za kukataliwa fomu na kuenguliwa katika uchaguzi...
Lissu: Uliulizwa kama unakumbuka kama baada ya hayo mlichukua hatua zozote za kwenda Mahakamani.
Ukajibu hatukwenda Mahakamani, badala yake mliona njia za kisiasa ndiyo za kuchukuliwa.
Golugwa: Yeah, tuliona njia za kisiasa ni sahihi kwa sababu...
Mwinuka: Hili swali, Waheshimiwa Majaji, halihitaji ufafanuzi.
Alisema hatukufungua kesi.
Lissu: Jibu lake ni hatukufungua kesi, tukiona njia za kisiasa ni sahihi zaidi.
Kwa maoni yangu, hili linahitaji ufafanuzi.
Mwinuka: Amesema kwa rekodi zake, nadhani Mahakama ingetugaidia katika rekodi.
Jaji Ndunguru: Tuendelee. Tumeona kwamba waliamua kwenda katika siasa.
Lissu: Shahidi, nilikuuliza kwamba ulipoulizwa kama mmechukua hatua za kisheria kwenda Mahakamani, ukasema hapana, mliona hatua za kisiasa.
Hebu elezea.
Golugwa: Kwa jinsi wagombea wetu wa vitongoji, vijiji na mitaa kwa nchi nzima, lilikuwa ni swala kubwa la kutatuliwa kisiasa na si kwenda Mahakamani.
Lissu: Vilevile umeulizwa maswali mengi ya uchaguzi wa 2020.
Ukaulizwa kama ulijaza fomu, ukasema hapana.
Kama mlipinga malalamiko ya Ubunge wa uchaguzi huo Mahakamani.
Ukaulizwa kwamba kama hamkupinga matokeo, maana yake Mahakama haikuona shida yoyote.
Fafanua hapo.
Golugwa: Hatukwenda kwa sababu Mahakama haina mamlaka ya kutamka Katiba ni mbovu. Jambo hili ni la wananchi kupitia Bunge.
Mwinuka: Waheshimiwa Majaji, shahidi ameongeza maneno mapya.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, nakubaliana na Wakili wa Serikali. Shahidi kaongeza maneno mapya.
Shahidi, hayo maswala ya kuongeza ongeza maneno ndiyo yamekuweka hapa siku nne.
Golugwa: Hatukwenda Mahakamani, tuliona jambo hili linahitaji kushughulikiwa kisiasa.
Lissu: Uliulizwa kuhusu uchaguzi wa Madiwani.
Uliulizwa vilevile kama mlikwenda Mahakamani kupeleka malalamiko Mahakamani, ukasema hamkwenda.
Wafafanulie Majaji.
Golugwa: Uchaguzi wa Madiwani pia tuliona malalamiko, isipokuwa tuliona kwamba matatizo yale yanahitaji kushughulikiwa kisiasa.
---
Lissu: Nakumbuka aliulizwa maswali mengi kuhusiana na watazamaji wa uchaguzi.
Kuhusiana na ripoti ya Thabo Mbeki, kwamba utaje title za ripoti.
Ukasema hukumbuki.
Wafafanulie Majaji kwa nini ulisema hukumbuki.
Jaji Ndunguru: Ameshasema hakumbuki, sasa afafanue nini na hakumbuki.
Lissu: Okay.
Shahidi, uliulizwa kama umesikiliza hotuba ya Jaji Chande.
Ukasema umesikiliza hotuba ya Jaji Chande ila huiamini.
Hebu fafanua.
Golugwa: Haikuwa na taarifa inayobeba uhalisi kama vile sababu za watu kutekwa na kupotea.
Lissu: Ukaulizwa hata sababu za machafuko huziamini? Ukasema sababu za machafuko ni za kweli, lakini sikubaliani na hotuba kwa ujumla wake.
Hebu fafanua ulikuwa na maana gani.
Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sababu za kutokubaliana na hotuba kwa ujumla wake inajengwa na misingi ya kuundwa kwa tume yenyewe.
Lissu: Ukienda hivyo sehemu mpya wataamka.
Eleza kwa nini hukubaliani nayo.
Golugwa: Idadi ya watu waliouawa ni moja ya jambo linalonifanya nisikubaliane nayo.
---
Lissu: Nilisikia kuhusu kuulizwa na Wakili katika muktadha wa mkutano wa tarehe 03 Aprili mwaka jana, kulikuwa na unyunyu wowote pale.
Ukasema kuwa hapakuwa na unyunyu katika mkutano wa tarehe 03 Aprili.
Mwinuka: Waheshimiwa Majaji, alishajibu kwamba hapakuwa na concept ya unyunyu.
Lissu: Kuna neno linarudiwa rudiwa sana kwamba jibu limejifunga, linajitosheleza.
(Anasoma Kifungu cha 166.)
Hakuna swala hapa la hilo jibu linajitosheleza.
Hii habari wanayotaka kuileta hapa haipo sawa kabisa.
Wakili anasema jibu lilitolewa linaweza kuleta further cross-examination.
Jaji Ndunguru: Shahidi, jibu.
Golugwa: Hapakuwa na chupa za unyunyu zilizokuwa zimepangwa mezani.
Lissu: Ndiyo ufafanuzi wenyewe. (Anacheka.)
MAHAKAMA KICHEKO
---
Lissu: Tuje na maswali ya Nassoro Katuga kwamba ni kweli kama Kamati Kuu mwaka huu mwezi Agosti iliketi.
Ukasema ni kweli. Ukaulizwa kuhusu maazimio ya Kamati Kuu, ulisoma, wewe ukasema ni kweli.
Ukaulizwa kuhusu kauli ya viongozi waelekeze nguvu na muda wao katika kumtetea Mwenyekiti.
Wafafanulie Majaji.
Golugwa: Nilikuwa namaanisha viongozi wakuu ambao ni mashahidi katika kesi hii, Mheshimiwa Heche, Mheshimiwa Katibu Mkuu John Mnyika, Amani Golugwa, kuelekeza nguvu zao na muda wao katika kumtetea Mwenyekiti katika kutoa ushahidi.
---
Lissu: Uliulizwa kuhusu aina ya viongozi.
Ukasema kuna viongozi wa kuteuliwa na viongozi wa kuchaguliwa.
Na kwa nafasi yako wewe, ukasema Naibu Katibu Mkuu wa chama anateuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Baraza Kuu.
Hebu eleza haya majibu yako kuhusu nafasi yako.
Golugwa: Ili niweze kuitwa Naibu Katibu Mkuu, Mwenyekiti atalipeleka jina langu Baraza Kuu.
Nakuwa Naibu baada ya jina kuthibitishwa na Baraza Kuu.
Lissu: Ukaulizwa pia kuhusu nafasi ya Katibu Mkuu. Fafanua na hiyo.
Golugwa: Katibu Mkuu anakuwa Katibu Mkuu pale ambapo uteuzi wake unathibitishwa na Baraza Kuu.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.