Kesi ya Uhaini: Amani Golugwa, amemaliza kutoa ushahidi kesi ya Lissu

Kesi ya Uhaini: Amani Golugwa, amemaliza kutoa ushahidi kesi ya Lissu

Iki chama Mashahidi wote wa Jehova
Mana Wate Wakristo Chama cha Wakristo kama sitakosea✍️
Cdm imeshavuka upuuzi wa kidini, inaangalia uwezo na mwenyekutaka kuwa nao. Huo upuuzi wa kubalance dini umebaki kwa ccm maana wao ndio wanaona dini kama sehemu nzuri ya kuhadaa watu.
 
Si yule galugwa bado hajamaliza, na ninahisi mawakioi wa serikali warakaa nae muda sana sababu wanaona wanammudy
Mkuu mimi ni layman, tofauti na mnavyodhani Galugwa kashindwa kujieleza kwa mawakili wa serikali, ni kuwa Galugwa kaenda vizuri na kawaingiza choo cha kike akina Katuga,japo Katuga ni mzuri ila ameshindwa kung'amua mapema mtego wa Galugwa, ile ya galugwa kujifanya hajui anakuja kufunguka zaidi wakati amemaliza kabaki anahojiwa na Lissu akiwa kamashahidi hapo ndipo majibu yale ya sijui,sikumbuki aliyokuwa awapa akina Katuga ndipo yatafunguliwa bomba na kuelezwa kwa ufafanuzi mkubwa na huyo huyo aliyekuwa anasema hajui.
 
Shauri la uhaini namba 19605/2025 linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, litaendelea leo Septemba 7, 2026 katika hatua ya maswali ya dodoso kwa shahidi wa tatu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Amani Golugwa.

Maswali hayo ya dodoso yanaulizwa na Jamhuri, ambao Ijumaa Septemba 4, 2026 kutokana na kutamatika kwa muda wa shughuli za Mahakama hawakuhitimisha zoezi hilo huku wakitarajiwa kuhitimisha leo.

Hatua ya Maswali hayo ilifikiwa baada shahidi huyo kuhitimisha zoezi la kumtetea Lissu katika kesi hiyo na ikiwa itatamatishwa leo majaji watatoa nafasi kwa mshtakiwa kuuliza maswali ya ufafanuzi kwa shahidi huyo (Re-examination).

Tundu Lissu, anashtakiwa kwa kosa la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kama ilivyorekebishwa 2023.

===

Kutoka Mahakamani

Tundu Lissu ameingia Mahakamani muda huu amesema wamemzui kuvaa T shirt iliyoandikwa “LISSU — SIXTEEN BULLETS SURVIVOR.” akiingia Mahakanikuvaa, ila ukumbi mzima umevaa ujumbe huo kwa Niaba yake.


Baadhi ya viongozi wa CHADEMA pamoja na baadhi ya wafuasi wa Chama hicho wakiwa katika ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Septemba 7, 2026, kabla ya kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu kuendelea katika hatua ya maswali ya dodoso kwa shahidi wa tatu Amani Golugwa.

Leo, imetimia miaka 9 tangu aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki na sasa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ashambuliwe kwa risasi akiwa anatoka bungeni kwenda nyumbani kwake Area D na katika ukimbi wa Mahakama wanachama wa CHADEMA wamevalia t-shirt zenye ujumbe kuhusu Lissu

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, akiwasili Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Septemba 7, 2026, kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho.

Ijumaa Septemba 4, 2026 tuliishia sehemu ya 356 so leo tunaendelea na sehemu ya 357, Mahakama imeanza na Ukumbi umepambwa kwa Tshirt nyeupe za BAVICHA zimeandikwa kwa Maandishi Mekundu TUNDU LISSU Sixteen Bullets Survivor, Septemba 7;

Mwenyekiti wetu Mhe. Lissu ameingia ukumbini neno lake la kwanza ni T-SHIRT YANGU WAMEIKATALIA lakini hakuna shida tuko vizuri.

Naambiwa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) walimpelekea zawadi ya Tshirt ili aweze kuivaa leo ambapo imetimia miaka tisa tangu apigwe risasi lakini Magereza wamekataa kumpatia kwahiyo hajavaa Tshirt yake leo.

Amesimama Ajuaye kutambulisha mawakili wa Serikali na wamesema wako tayari kuendelea.

Mhe. Lissu nae amesema yuko tayari.

Anasimama Katuga na kuanza kuendelea.

Katuga: Lile suala la Roho mbaya umelifuta?
Golugwa: Una roho mbaya.
Katuga: Mwandishi akichukua habari inakuwa mali yake?
Golugwa: Ndio
Katuga: Ni kwa mujibu wa sheria au maoni yako?
Golugwa: Sio maoni yangu. Mimi sio shahidi wa maoni, najua huo ndio ukweli nafahamu na Sheria inasema.
Katuga: Kifungu cha sheria umetaja au hujataja?
Golugwa: Ni mali yake lakini kifungu sijataja.

Katuga anachekacheka, anamuuliza Golugwa kwahiyo leo umekuja kwa style hii? Ni kweli ulisema kuhamasisha uasi sio kosa ni neno la kisiasa.

Golugwa: Nakumbuka nilisema.
Katuga: Siasa za CHADEMA zinatumia lugha gani?
Golugwa: Lugha ya Kiswahili.
Katuga: Ni kamusi gani inayotumika kutafsiri inaitwaje
Golugwa: Tunatumia lugha ya kiswahili.
Katuga: Kamusi ya kisiasa ipo au haipo?
Golugwa: Sina uhakika.
Katuga: Uchaguzi Mkuu upo Kikatiba?
Golugwa: Ndio
Katuga: Kuvunja Sheria sio sababu ya Uhaini? Ulisema hivyo.
Golugwa: Sikusema
Katuga: kupinga sio kuvunja sheria ulisema?
Golugwa: Tutapinga uchaguzi ni sentensi kamilifu? Tutazuia uchaguzi ni sentensi kamilifu? Ni sentensi zinazoleta maana?.
Katuga: Ulisema Mwenyekiti aliongea muda mrefu?
Golugwa: Zaidi ya lisaa limoja na nusu hadi mawili.
Katuga: Hivi kwenye hotuba ulisikia Mwenyekiti akisema majaji ni ma ccm?
Golugwa: Sikusikia.
Katuga: Ulisikia au hukusikia Mwenyekiti akisema Mahakamani hakuendeki?
Golugwa: Sikumbuki.
Katuga: Mwenyekiti akisema Mapolisi wanaingia na vibegi kwenye vituo vya kura? Ulisikia?
Golugwa: Sikumbuki.
Katuga: Wewe uliyosema umeyasema yote au ulisema baadhi ya yale aliyosema Mwenyekiti?
Golugwa: Niliyoyasema ndio nimesema kama yalivyo. Sina uhakika ndio yote aliyosema
Katuga: Kwahiyo hujui au unajua kama kuna mengine aliyazungumza.
Golugwa: Sifahamu.
Katuga: Maneno kwamba Majaji ni Ma CCM yeye alisema kwamba maneno hayo aliyasema kwenye Mkutano?
Golugwa: Mimi sikusikia.
Katuga: Vikao vya Chama chenu vinakuwa na maazimio?
Golugwa: Vikao vya kawaida vinakuwa na maazimio.
Katuga: Ulisema wewe ni mtu wa minutes? Unaandika zile minutes za vikao?
Golugwa: Ndio
Katuga: Katika uandishi wa minutes na maazimio huwa ni sentensi fupi ?
Golugwa: Ni fupi ndio au inaweza kuwa paragraph lakini zinaeleweka.
Katuga: Kukinukisha ni tendo?
Golugwa: Inaweza kuwa tendo.
Katuga: Ulisema mwenyekiti aliposema tutaenda kukinukisha alisema ni kitendo gani kifanyike ili ndio kuwe kukinukisha?
Golugwa: Sikusema hivyo vitendo.
Katuga: Ukichoma Kitu kikanuka kwahiyo umekinukisha?
Golugwa: Sijazungumzia mambo ya kuchoma.
Katuga: Ukichoma kitu kinatoa harufu au hakitoi mfano tairi?
Golugwa: Ukichoma kitu unakuwa umechoma. Maana ya kukinukisha nimesema.
Katuga: Mwenyekiti siku ya hotuba alielezea mbinu za kukinukisha?
Golugwa: Hakuelezea hizo mbinu.
Katuga: Ni haki au sio haki kwa mtu aliyeona au kusikia akatafsiri yale maneno kwa namna atakayoona?
Golugwa: Inategemea na huyo mtu.

Sehemu ya 358

Katuga:
Kwa vile njia ya kukinukisha haikutajwa ni haki ya mtu yeyote kwenda kujisaidia pale kituoni na kufanya mambo yake?
Golugwa: Mimi mambo ya watu wengine siwezi kusema.
Jaji: Naomba ujibu swali.
Katuga: Kwa kuwa kwenye hotuba ya Mwenyekiti hakutoa njia ya Kukinukisha. Swali langu ni rahisi. Ni haki ya mlaji wa hotuba kwenda kujisaidia kwenye kituo cha kura?
Golugwa: Sio haki, halikuwa hata lengo la ule Mkutano.
Katuga: Ni ushahidi wako kwamba Jumuiya ya Ulaya walisikitishwa na vurugu za siku ya uchaguzi?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Ulisema huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga? Alisema hayo maneno Mwenyekiti?
Golugwa: Nilisema.
Katuga: Ni kweli sasa kwamba kwa maneno aliyosema Mwenyekiti yalithibitika kwa vurugu kutokea?
Golugwa: Vurugu hazikuhusiana na Mwenyekiti. Sio kweli hivyo.
Katuga: Ni aina gani ya uhaini ambayo mshitakiwa anashitakiwa nayo?
Golugwa: Sifahamu in details kuwa anashitakiwa kwa uhaini wa aina gani? Nipatiwe charge sheet niisome.
Katuga: Aina gani ya nia anayoshitakiwa nayo?
Golugwa: Nia ya kufanya uhaini. Kuitishia serikali Bunge na Mahakama.
Katuga: Mshitakiwa anashitakiwa kwa kutoa na kuchapisha hayo maneno?
Golugwa: Mshitakiwa alitoa maneno kuhusu huo uchaguzi mfano kukinukisha.
Katuga: Mshitakiwa alikuja na maazimio ya yenye sentensi chache zenye nguvu kwamba tutazuia uchaguzi.
Golugwa: Hatukuwa na maazimio yoyote kwenye kikao kile.
Katuga: Baada ya kusema Majaji ni Maccm akaona hakuna njia nyingine zaidi ya kukinukisha.
Golugwa: Sio kweli
Katuga: Jibu swali sasa
Lissu: Mheshimiwa Jaji kama Wakili wa Serikali anataka majibu yake yaingie apande Kizimbani yeye ili atoe huo ushahidi.
Katuga: Maneno ya kwamba tunakwenda kukinukisha yalishangiliwa sana na watu?
Golugwa: Sikumbuki.
Katuga: Ulisema mtu kumzuia mwingine kushiriki uchaguzi sio haki?
Golugwa: Kama uchaguzi ni wa haki na huru.
Katuga: Katika ushahidi wako mwenyekiti aliwapa njia gani ya kuzuia uchaguzi?
Golugwa: Hakukuwa na lengo lolote la kufanya hivyo.
Katuga: Mwenyekiti alitoa njia ya kuzuia uchaguzi?
Golugwa: Hakusema njia specific
Katuga: kwa ufahamu wako kwenye yale maneno aliyoyasema Lissu 3/4/2025 ni njia gani unaweza kuitumia kuzuia uchaguzi?
Golugwa: Kuelimisha watu
Katuga: Kuna njia gani ya amani inayoweza kutumika kuuvuruga uchaguzi bila kutumia nguvu?
Golugwa: Kuwaelimisha wananchi
Katuga: Unajua au hujui kwa sheria zetu za uchaguzi mshindi anapatikana kwa majority vote?
Golugwa: Kama uchaguzi unakuwa wa haki, huru na wa uwazi ni sawa
Katuga: Tangu Lissu akamtwe ni kweli kuwa Heche aliendeleza Azimio lililotangazwa na Mwenyekiti?
Golugwa: Makamu Mwenyekiti John Heche aliendeleza azimio la chama la no reforms, no election.
Katuga: Makamu mwenyekiti ulikuwa ukitembea nae kwenye hizo ziara?
Golugwa: Hapana
Katuga: Unafahamu kuwa John Heche alisema akiwa East Africa Radio kuwa uchaguzi hautafanyika?
Golugwa: Sikumbuki
Katuga: Ulimsikia Heche akisema tuko determined kuuzuia ucahguzi wa 2025?
Golugwa: Sikusikia
Katuga: ulimsikia Jaji Chande akisema kwamba matukio ya Okt 29 yalilenga kuvuruga uchaguzi
Golugwa: Sikusikia
Katuga: Ulimsikia Jaji Chande akisema vurugu za Okt 29 zilipangwa?
Golugwa: sikusikia
Katuga: Ulimsikia Jaji Chande akisema sababu ilikuwa ni madai ya katiba mpya?
Golugwa: ndio nilisikia
Katuga: Ni msimamo wa chama kuwa nchi ya Tanzania iwe chini ya EU wakati mchakato wa katiba mpya unaendelea?
Golugwa: Hilo swali halimake sense
Katuga: Ulieleza mambo mengi wakati umekamatwa, je ulielezea relevance ya ushahidi huo hapa mahakamani?
Golugwa: Nilielezea madhira tunayopata viongozi wa upinzani
Jaji Nduguru: Uliza maswali wakili
Katuga: Nahakiki tu maswali naelekea mwishoni Mhe. Jaji.

Sehemu 359

Katuga:
Mhe. Jaii sina swali kwa shahidi huyu

Wakili wa Serikali Mwandamizi Ajuaye amesimama kuendelea na maswali kwa shahidi: Ulisema wewe sio mwanasheria na katiba huifahamu kabisa?
Golugwa: Mimi sio mwanasheria ila Katiba naifahamu
Ajuaye: Ni kweli Rais na wabunge hupatikana kwa kuchaguliwa?
Golugwa: Ndio
Ajuaye: Ni kweli uchaguzi ukivurugika viongozi hao hawawezi kupatikana?
Golugwa: Viongozi waliopo wanaendelea
Ajuaye: Shahidi naomba ushike katiba na utuambie ni Ibara ipi
Golugwa: Ibara ya 90(3) ya Katiba
Ajuaye: Watafsirie majaji
Golugwa: It goes without saying, sasa nitafsiri nini hapa? Wakili naona anaelewa polepole
Ajuaye: Rais yupo katika mhimili gani?
Golugwa: Serikali
Ajuaye: Lengo lilikuwa Umma umuunge mkono Mwenyekiti?
Golugwa: Lengo lilikuwa kuuelimisha umma, kwenye kikao lengo lilikuwa kuwaelimisha watia nia
Ajuaye: Nitakuwa sahihi nikisema waandishi wanapokuwa wanarusha habari mbashara hawana nafasi ya kubadilisha chochote?
Golugwa: Waandishi wanajua maana wana kanuni zinazowasimamia
Ajuaye: Unajua maana ya kurusha mbashara?
Golugwa: kurusha moja kwa moja
Ajuaye: Shahidi mliposema mnaenda kuhamasisha uasi mlikuwa mnaenda kuwahamasisha wakina nani?
Golugwa: Waheshimiwa majaji tulilenga watia nia waelewe kuwa kuna kanuni mbovu sana
Ajuaye: Waheshimiwa ni hayo tu kwa upande wa Jamhuri

Lissu anasimama kwaajili ya Re examination, shahidi pole

Golugwa:
Asante Mwenyekiti
Lissu: Wakili wa Serikali Mwinuka alikuhoji sana kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko kwenye uchaguzi wa mitaa, vitongoji na vijiji kama yanaenda Mahakama ya Wilaya ila wewe ulisema ni Kamati za Rufaa za Wilaya, fafanua

Golugwa: Malalamiko ya uchaguzi hushughulikiwa na Kamati za rufaa ambazo zina wajibu wa kuyapokea na kufanyia kazi na ndipo ambapo tulipeleka malalamiko ya wagombea wetu waliokataliwa fomu au kuenguliwa

Lissu: Uliulizwa baada ya kupelekwa huko kamati za rufaa, uliulizwa majibu yake yalikuwaje, ulisema majibu yalikataliwa kwa ushenzi uleule wa mwanzo, ulimaanisha nini?

Golugwa: Rufaa tulizowasilisha kwa sehemu kubwa zilitupiliwa mbali na sehemu kubwa ya wagombea wetu walienguliwa kwenye uchaguzi huo

Lissu: Uliulizwa kama baada ya hayo mlichukua hatua zozote kwenda mahakamani, ulijibu tuliona njia ya kisiasa ndio iliyokuwa sahihi zaidi ulikuwa na maana gani?

Golugwa: Katika mazingira hayo tungefungua kesi ngapi? Mahakama zipi za kutosha kesi zote hizo? Kwasababu wagombea wetu wengi sana walienguliwa nchi nzima hivyo tuliona hakuna haja ya kwenda mahakamani

Mwinuka amesimama: Shahidi alijibu hawakufungua hivyo halihitaji ufafanuzi.

Lissu: Shahidi alisema hatukufungua kwasababu tuliona njia za kisiasa ni sahihi zaidi hivyo niko sahihi kuliuliza

Mwinuka: Naomba record za mahakama zituongoze kwasababu jibu lilitokana na closed question kabisa kwa kumbukumbu zangu

Jaji Ndunguru anajadiliana kwa muda kadhaa na majaji wenzake kabla ya kutoa ufafanuzi

Jaji Ndunguru:
Tumeona shahidi alisema walienda kwenye njia za kisiasa ambazo waliona ni sahihi zaidi
Lissu: Uliulizwa maswali mengi kuhusu uchaguzi wa 2020, uliulizwa kama uligombea kwenye uchaguzi wa 2020 au kama mlipinga matokeo ya 2020 ulisema hapana,

Golugwa: Matatizo ya uchaguzi wa 2020 tulijiridhisha kwamba hayawezi kutatuliwa kwa njia za mahakama kwasababu yalikuwa mengi kwa nchi nzima hivyo nalo hili tuliona litashughulikiwa kisiasa

Lissu: Uliulizwa maswali mengi kuhusu uchaguzi wa madiwani wa 2020 kama mlikwenda mahakamani kupinga matokeo, ukasema hamkufungua kesi mahakamani, ukaulizwa kwahiyo hamkuwa na malalamiko ukasema tulikuwa na malalamiko, ulimaanisha nn?

Golugwa: Tulikuwa na malalamiko kutokana na uchaguzi huo na tuliona yanahitaji kushughulikiwa kisiasa na sio kwenda Mahakamani

Sehemu ya 360

Lissu:
Uliulizwa vilevile kuhusu uchaguzi wa vitongoji, mitaa na vitongoji wa 2024 na ulisema mlipopeleka rufaa zote zilikataliwa kwasababu ya ushenzi na uhuni uliofanywa ndio maana hatukuenda mahakamani, fafanua

Golugwa: kwa idadi ya wingi wa wagombea wetu kufanyiwa huo uhuni na ushenzi tuliona matatizo hayo yanahitaji kushughulikiwa kisiasa
Lissu: uliulizwa kuhusu hotuba ya Jaji Chande ulisema huiamini, eleza kwanini
Golugwa: Baada ya kuisikia kuna mambo hayakuwa halisi kwenye ripoti ile mfano sababu za watu kutekwa na kupotea.
Lissu: Uliulizwa pia kuhusu hotuba ya Jaji Chande kuwa hata sababu za machafuko huziamini, ukasema sababu za machafuko ni za kweli ila sikubaliani na hotuba kwa ujumla wake, fafanua
Golugwa: Sababu za kutokubaliana na hotuba kwa ujumla wake kutokana na taarifa zilizosemwa sio halisi mfano idadi ya watu waliouwawa
Lissu: Uliulizwa katika muktadha wa mkutano wa 3/4/2025 kulikuwa na unyunyu , alisema hakukuwa na unyunyu, fafanua.
Golugwa: Hapakuwa na chupa za unyuunyu zimepangwa isipokuwa ni neno lilitamkwa.
Lissu: Ndio ufafanuzi wenyewe, huku anacheka
Lissu: Unakumbuka uliulizwa kama ni kweli Kamati Kuu ya Chama iliketi 29 August na kuwa wewe ndio ulitangaza maazimio ya kamati kuu, na kuwa kulikuwa na mambo kuhusu kesi hii ukasema ni kweli na ulisema viongozi waelekeze nguvu na muda wao katika kumtetea mwenyekiti, fafanua

Golugwa: Nilimaanisha kuwa viongozi wakuu ambao ni mashahidi kwenye kesi hii John Heche, John Mnyika, Mimi Golugwa badala ya kuendelea na kuandaa Baraza Kuu waelekeze muda wao na nguvu zao katika kumtetea Mwenyekiti kwa maana ya kutokuwa na committment nyingine inayoweza kuwachukulia muda badala ya kujiandaa kumtetea Mwenyekiti.

Lissu: Katuga alikuuliza sana kuhusu hiyo nafasi yako ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama, ulijibu kuwa Naibu Katibu Mkuu anapendekezwa na Mwenyekiti na anateuliwa na Baraza Kuu, akaendelea kukuuliza si uliteuliwa na Mwenyekiti? Ukasema ndio ila Baraza Kuu lilinithibitisha

Golugwa: Naibu Katibu Mkuu anateuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Baraza Kuu
Lissu: Uliulizwa vilevile na nafasi ya Katibu Mkuu, ukasema nae anateuliwa na Mwenyekiti, fafanua
Golugwa: Katibu Mkuu anateuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Baraza Kuu ndipo anakuwa amekuwa Katibu Mkuu kamili.

Lissu: Uliulizwa kuhusiana na kikao cha kamati kuu kilichopitisha azimio la no reforms no election la Desemba 10, 2024 baada ya kuwasilisha ripoti yenye maneno makali, na uliulizwa kuwa kusema hatutashiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike ni kuishinikiza Serikali ulijibu ni kweli, fafanua

Golugwa: Serikali ni mdau muhimu katika kufanya mabadiliko ya kiuchaguzi hivyo tulichokitaka kifanyiwe mabadiliko tulitaka serikali kusikia sauti za wananchi kuhusu mabadiliko hayo kwenye mifumo ya uchaguzi

Lissu: Uliulizwa kwa msimamo wa no reforms no election mlilenga kuzuia mtu yeyote kwenda kushiriki uchaguzi, ulijibu sisi hatukuzuia mtu yeyote kwenda kushiriki uchaguzi, fafanua

Golugwa: Tulilenga kuwaelimisha watu waelewe msimamo wetu kwamba watu wakishaelewa watafanya maamuzi sahihi

Lissu: Uliulizwa maswali mengi kuhusu uchaguzi wa mitaa, vitongoji na vijiji mwaka 2024 na ukaulizwa kama ulitaja majina ya wagombea, wasimamizi waliokimbia kuchukua fomu za wagombea, na majibu yako yalikuwa hapana, elezea haya majibu ya hapana uliyoyatoa

Golugwa: Nilielezea kuhusu vitendo vilivyofanyika
Lissu: Uliulizwa kama CHADEMA ilishiriki uchaguzi wa 2025, ukasema hapana, ukaulizwa kwanini hamkushiriki ukasema tulizuiliwa na Tume ya Uchaguzi

Katuga: Hilo swali shahidi alijibu kwa ukamilifu kuwa walitumia haki yao ya Kikatiba kutokushiriki uchaguzi hivyo ufafanuzi hauhitajiki au vinginevyo rekodi za Mahakama zituongoze.

Sehemu ya 361

Lissu:
Waheshimiwa majaji hiyo hoja kuwa swali halihitaji ufafanuzi haipo kisheria, during re examination maswali yanayofafanuliwa ni yale yaliyoulizwa wakati wa cross examination.
Jaji Ndunguru: Shahidi endelea.

Golugwa: Ni kweli ilikuwa ni haki yetu kutoshiriki uchaguzi ambao sio huru na wa haki tuliamini mabadiliko yangetokea lakini tulizuiliwa na Tume ya Uchaguzi.

Lissu: Unakumbuka ulisema kuhusiana na kuenguliwa kwa wagombea wa CHADEMA na ulisema hujawahi kuona mgombea wa CCM akienguliwa na ukaulizwa kama ulipokea taarifa kutoka CCM ukasema hujawahi kupokea taarifa kutoka CCM

Golugwa: Taarifa za wagombea kuenguliwa zinakuwepo kwenye ofisi za wasimamizi wa uchaguzi na kwa Tume

Lissu: Uliulizwa kuhusu tarehe, mwezi na mwaka wa taarifa za watazamaji wa uchaguzi, ulisema taarifa hizo ziko kwenye public domain na kuwa zilitolewa mwaka 2025 baada ya uchaguzi mkuu, fafanua

Golugwa: Nilimaanisha taarifa hizo zilitolewa mwaka 2025 mara baada ya kile kilichoitwa uchaguzi na nilitaja mwezi Novemba, 2025

Lissu: Uliulizwa kuhusu maandamano kuwa lazima yangeleta bugudha kwa watu wasiohusika na ulisema maandamano lazima yalete bugudha hebu fafanua

Golugwa: Maandamano huleta bugudha kwa waliopo barabarani lakini ni bugudha inayowasha masikio na macho

Lissu: Uliulizwa kama Mahakama inaweza kuelekezwa na EU, ulisema hapana ila mamlaka zingine zinaweza kuzungumzia masuala ya Tanzania, ulimaanisha nini?

Golugwa: Tanzania sio kisiwa kama nchi inawajibika kuzingatia matamko mbalimbali ya kidunia yanayohusiana na haki za binadamu, tunahusiana na watu na kama nchi tuna wajibu wa kuheshimu sheria za kimataifa.

Jaji Nduguru: Hivi sasa ni saa saba na dakika 11 ni muda wa health break kwa mujibu wa utaratibu

Lissu: Waheshimiwa majaji nina chini ya nusu saa nitakuwa nimemaliza

Wakili wa Serikali Ajuaye: Waheshimiwa majaji muda wa health break lakini kama haitamuathiri mshtakiwa amalizie kwa huyu shahidi then ndio twende break.

Lissu: Uliulizwa kuhusu shtaka la uhaini ukasema ni shtaka la uongo, ulimaanisha nini?
Golugwa: nilimaanisha Shtaka ni la uongo kwasababu mtu mmoja hawezi kupanga uhaini, hawezi kujichochea yeye mwenyewe, akatekeleza mwenyewe na akatenda kosa hilo yeye mwenyewe
Lissu: Uliulizwa kuhusu tume ya uchaguzi na uteuzi wake ukasema haiko huru, fafanua
Golugwa: Nilisema haiko huru kwasababu Mwenyekiti na wajumbe wanateuliwa na Rais, Mwenyekiti wa CCM ambaye nae anakuwa mgombea
Lissu: Uliulizwa kuhusu watia nia waliohudhuria kikao cha 3/4/2025 na uliulizwa kama kulikuwa na watia nia kati ya wajumbe wa kamati kuu ambao pia walishiriki kupitisha azimio hilo

Golugwa: Walengwa walikuwa ni watia nia na lengo lilikuwa kuwaelimisha na kuelimishana na kitu endelevu hivyo hata kama walipitisha azimio kwenye vikao bado haja ya kuendelea kuelimishwa ilikuwepo regardless kuwa walishiriki kupitisha.

Lissu: Uliulizwa kuhusu Naibu Katiba Mkuu Zanzibar kuwa ulimualika wakati alikuwepo wakati mnapitisha agenda ya kikao cha 3/4/2025, ukasema ndio ili kuthibitisha ushiriki wake kwasababu anakaa Zanzibar

Golugwa: Ni hayo hayo kuwa anaishi Zanzibar kama sehem ya courtesy tu kuwa anshiriki
Lissu: Uliulizwa kuhusu kukamatwa kwangu na kufunguliwa kesi mbalimbali za uongo, ulijibu ndio , fafanua

Golugwa: Nilimaanisha sababu ya kukamatwa kwake sio ya kweli na ililenga kumuondoa kwenye operation aliyokuwa anaiongoza.
Lissu: Uliulizwa kuhusu mkutano wa 3/4/2025 uliulizwa kama ulijua kilichokuwa kwenye fikra zangu siku hiyo ukasema ndio, ulimaanisha nn

Golugwa: Sekretarieti ndio tuliandaa mkutano huo kwahiyo siku hiyo ya tarehe 03/04/2025 nilijua tunazungumzia kuhusu no reforms no election kwasababu mimi pia ndio nilimpigia simu kuhusu kuhudhuria kikao hicho.

Sehemu ya 362

Lissu: Uliulizwa kuhusu mkutano wetu na shura ya maimamu na sheikh Ponda ulisema kuwa niliyasema, vilevile mkutano na jaji Warioba na ukasema ndio ila ulipoulizwa kuhusu neno kukinukisha kama nilisema kwa sheikh Ponda, ukasema sikusema, ulimaanisha nini?

Golugwa: Nilimaanisha hali ya floor ya kawaida ya mazungumzo haiwezi kutumia maneno yaleyale isipokuwa muktadha ulikuwa ni uleule na kutokuwa na neno moja haina maana kuwa ujumbe wetu wa no reforms no election haukufikishwa kama ulivyokusudiwa.

Lissu: Umeulizwa kuwa ile video inayochukuliwa na chombo cha habari ukasema ni mali ya chombo cha habari kwa mujibu wa Sheria, uliulizwa kuhusu kifungu ukasema sijataja ila hivyo ndivyo ilivyo, fafanua

Golugwa: Kwa ninavyofahama mwandishi anayerekodi pamoja na vifaa vyake vinakuwa ni vya kwake chini ya mamlaka yake na mhusika ndiye anayeweza kuchapisha au kusambaza kile ambacho kipo kwenye mamlaka yake

Lissu: Umeulizwa kama nilisema majaji ni maCCM ukasema hukumbuki, kama nilisema Mahakamani hakuendeki, kama mapolisi wanabeba vibegi vya kura feki, ukajibu nilisema nilichosikia

Golugwa: Nilimaanisha kuwa kile nilichokisema kinatokana na yale yote ambayo niliyasikia

Lissu: Uliulizwa kama kwenye uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa na vurugu, ukasema ni kweli na kuwa EU walisema kulikuwa na vurugu ukasema ni kweli, ulipoulizwa kuhusu Lissu kusema tunaenda kuvuruga uchaguzi ukasema sio kweli kuwa Chadema ilisababisha vurugu sababu chadema ilifungiwa na Lissu alikuwa gerezani

Golugwa: Nilimaanisha kuwa chadema baada ya kufungiwa haikujihusisha na jambo lolote la uchaguzi na Lissu alipokamatwa na kuwekwa gerezani hakuhusika na suala lolote la uchaguzi kwahiyo sio kweli kwamba chadema au Lissu alihusika na vurugu wakati wa uchaguzi.

Lissu: Uliulizwa kuwa uchaguzi ukivurugika au usipofanyika, ukasema waliopo madarakani wanaendelea kuwa madarakani, ulikuwa na maana gani?

Golugwa: nilikuwa na maana mbili maana ya kwanza ni kuwa Katiba yetu inatupa fursa ya uchaguzi kusogezwa mbele lakini pia maana ya pili ni maana iliyokuwa kwenye msimamo wa no reforms no election kuwa tuko tayari hata uchaguzi usogezwe mbele ili tupate mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi.

Lissu: umeulizwa juu ya tafsiri yako ya haya maneno tutahamasisha uasi, ulisema kuwa hayo maneno kuhamasisha uasi yalitakiwa yatafsiriwe kwa muktadha wake na yalilengwa kwa watia nia, ulimaanisha nn

Golugwa: Watia nia waliemishwa kuhusu sheria mbovu zilizopo ambazo zilitakiwa kufanyiwa mabadiliko na kuwa tutakwenda kinyume na hizi sheria mbovu mpaka zikapobadilishwa. Hivyo watia nia walielimishwa na kuwa sasa tunakwenda kinyume na sheria hizi mbovu kabisa.

Lissu: Waheshimiwa majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu, nimemaliza.

Jaji Ndunguru: Shahidi asante kwa kutoa ushahidi sasa uko huru kuendelea na shughuli zako.

Wakili wa Serikali Ajuaye anasimama na kusema ni muda sasa wa break tunaomba ahirisho kuja kuendelea na shahidi mwingine.

Jaji Ndunguru: shauri linaahirishwa hadi sa tisa na nusu

Inapigwa High Couuuuurrrrt

Majaji wanatoka.

Tukutane saa tisa na nusu alasiri ambapo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia Jonas, atasimama Kizimbani kama Shahidi wa 4.


Updates Credit: Hilda Newton
MaCCM ni majitu ta kichoko na kiquma sana. Yanajitekenya na kucheka yenyewe.
 
Back
Top Bottom