Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kilichojiri Septemba 8, 2026: Mwendelezo wa Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, shahidi wa nne wa utetezi, Brenda Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, alisema hotuba ya Lissu ya Aprili 3, 2025 ilihusu mageuzi ya mfumo wa Uchaguzi, Marekebisho ya Sheria na msimamo wa "No Reforms, No Election".

Kabla ya kuahirishwa, Brenda alikuwa akiulizwa maswali ya dodoso kutoka kwa mawakili wa Serikali, hatua hiyo ya maswali ya dodoso inaendelea tena hapo leo.

Tundu Lissu, anashtakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na Kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kama ilivyorekebishwa mwaka 2023.

Kinachojiri Mahakamani

Tundu Lissu amewasili Mahakamani muda huu, kwa ajili ya kuendelea na Kesi yake inayomkabili ya Uhaini


Leo Septemba 9, 2026, Shahidi Na. 4 Brenda Rupia anaendelea kuulizwa maswali ya dodoso katika kesi hiyo. Mahakama imeanza na Majaji wameingia, huku Lissu akipokelewa kwa makofi mengi.

Jaji Ndunguru amewaagiza Mawakili wa Serikali kuendelea na dodoso, baada ya Karani kusoma namba ya kesi na Ajuaye Zegeli kuwatambulisha Mawakili wenzake. Mshitakiwa amesema yupo tayari kuendelea na dodoso.

Jaji Ndunguru: Haya Mshitakiwa unasemaje?
Lissu: Niko tayari pia.
Jaji: Shahidi yuko wapi? Haya tunakukumbusha bado uko chini ya kiapo. Muuliza maswali endelea.
Jaji Ndunguru: Sasa mi nataka hii session ya asubuhi tumalizane na huyu shahidi tafadhali.
Lissu: Mimi sina shida. Sina swali la re examination hadi sasa.
Katuga: Haya ulisema ulikamatwa Mwezi wa 7 tar. 12 mwaka jana?
Brenda: Sahihi
Katuga: Ulisema ulitoa taarifa ya Macalister?
Brenda: Sahihi
Katuga: ulisema kuna mpango wa kumpa mwenyekiti sumu kule Gerezani?
Brenda: Ndio
Katuga: Uliifanyia Uchunguzi hiyo taarifa?
Brenda: Nilifanyia uchunguzi nikagundua ni kweli imetoka kwa Macalister
Katuga: Ulijiridhisha kuwa Lissu anataka kupewa sumu au hataki kupewa sumu?
Brenda: Nilijiridhisha ndio.
Katuga: Wambie Majaji ulieleza kuwa ulifanya upelelezi ukagundua kuwa anataka kupewa Sumu?
Brenda: Sikueleza.
Katuga: Ulisema nani anataka kumpa sumu?
Brenda: Sikumtaja ndio.
Katuga: Kumuua mtu kwa sumu ni kosa?
Brenda: Ni kosa ndio.
Katuga: Uliwahi kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi kuwa Lissu anataka kupewa sumu gerezani?
Brenda: Ndio nilikuwa natoa taarifa
Katuga: Unajua au hujui kuwa kutokutoa taarifa za jinai ni kosa kisheria
Brenda: Sijui
Katuga: Unajua uwepo wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
Brenda: Naomba nipewe sheria niisome maana mimi sio mwanasheria
Katuga: Waheshimiwa majaji Naomba nimpe sheria asome
Brenda: Anasoma sheria na kusema nilitoa taarifa kwa umma na Polisi ili wachunguze
Katuga: Ulimtaja mtu aliyetaka kumpa sumu?
Brenda: Taarifa inasema kulikuwa na mpango wa kumpa sumu sio kwamba ilitaja mtu
Katuga: Je taarifa uliyoitoa kwa umma, waambie majaji kama ulieleza kuwa baada ya uchunguzi wako kuwa kuna mpango wa kumpa sumu Lissu akiwa gerezani
Brenda: Sikueleza kwenye hiyo taarifa
Katuga: Kutoa taarifa za uongo mtandaoni ni kosa la jinai?
Brenda: Najua
Katuga: Kukamatwa kwa Mwenyekiti kuna kupa wewe kinga ya kutokukamatwa au kushtakiwa
Brenda: Hainipi kinga mimi ni mfanyakazi.
Katuga: Unajua kuwa kutoa ushahidi wa uongo ni kosa la jinai?
Brenda: Najua
Katuga: Unajua ni jukumu la mtu yeyote mwenye kutaka mahakama imuamini ni jukumu lake kuthibitisha?
Brenda: Sijui
Katuga: Waambie majaji unajua au hujui kwamba hicho ulichokitoa kuwa ulifanya upelelezi na kugundua kuwa kuna watu walitaka kumpa sumu Lissu akiwa gerezani umesema ukiwa chini ya kiapo?
Lissu: Waheshimiwa majaji wakili wa Serikali anamlisha shahidi maneno, shahidi hakusema upelelezi alisema uchunguzi
Katuga: Basi sawa natumia neno uchunguzi
Brenda: Najua kuwa natoa ushahidi wangu chini ya kiapo

Sehemu ya 377

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu, Brenda Rupia.

Katuga: Hiyo account ya huyo mtu wa nje ulikotoa taarifa inaitwaje?
Brenda: Sikumbuki ila taarifa kwa umma ninayo hapa naweza kuirejea
Katuga: Wewe ulitoa taarifa kwenye social media gani?
Brenda: X na Instagram
Katuga: Unawajua au huwajui waliotaka kumpa sumu Mwenyekiti?
Brenda: Sijui ila ni wasiojulikana
Katuga: Katika uchunguzi wako ni kweli kwamba hukupata mtu au watu waliotaka kumpa sumu Lissu?
Brenda ameonyesha utata sana kujibu maswali kizembe ya Katuga. Lissu ameingilia kati na kusema Shahidi jibu maswali tuokoe muda

Brenda: Sikupata
Katuga: Huyo mtu kutoka nje ulikotoa taarifa anaishi Tanzania?
Brenda: David McAllister haishi Tanzania
Katuga: Huyo mtu ameishi na Lissu Ukonga?
Brenda: Hapana
Katuga: Ni kosa gani utatuhumiwa kwa kutoa taarifa za uongo?
Katuga: Kwa mujibu wa kamusi neno linaweza kuwa na maana zaidi ya moja?
Brenda: Ni kweli
Katuga: Ni kweli kwenye kamusi kuna maana saidizi za neno?
Brenda: Sijui
Katuga: Kwenye lugha ya kiswahili unajua maana ya neno kisawe?
Brenda: Sijui
Katuga: Kisawe ni synonym sasa waambie majaji maana ya synonym
Brenda: Synonym means something alike
Katuga: Waheshimiwa majaji naomba nimpe kamusi ili asome maana ya uasi
Brenda: amepokea Kamusi na kuanza kusoma maana ya uasi kuwa ni kitendo cha kupinga wenye mamlaka au taasisi
Katuga: Ni sahihi kuwa uasi ni kupinga sheria kwenye taasisi au chama na ni sawa na kufanya uhalifu ni sahihi au sio sahihi?
Brenda: Sio sahihi
Katuga: umewasomea majaji maana ya uasi kwenye kamusi na maana ya kwanza kuwa ni kitendo cha kuvunja sheria kwa lengo la kubadili mfumo wa kisiasa, sasa jana ulisema no reforms no election jana ulisema mlilenga kubadili mfumo wa kisiasa,

Kabla ya hapo Chadema ni kikundi cha watu au sio kikundi cha watu?

Brenda: Ni chama
Katuga: Chadema inakusanya watu au haikusanyi watu?
Brenda: Inakusanya watu
Katuga: Sasa jibu swali; jana ulisema ile No reforms, No election ililenga kubadili mfumo wa kisiasa. Leo nimekusomesha maana ya uasi kwenye kamusi kuwa ni kitendo cha kupinga Sheria ili kubadili mfumo wa kisiasa, tafsiri hii na jibu lako la jana zinafanana au hazifanani?
Brenda: Hazifanani.
Katuga: Ni kweli ulimtaja John Kitoka?
Brenda: Ni kweli nilimtaja jana
Katuga: Yuko wapi?
Brenda: Simuoni hapa sifahamu alipo
Katuga: Gervas Lyende unamfahamu?
Brenda: Simfahamu
Katuga: Apolinary Boniface unamfahamu?
Brenda: Namfahamu
Katuga: John Kitoka yupo chini ya nani?
Brenda: Katibu Mkuu
Katuga: Kichadema mtu anaweza kufanya kazi za chama akiwa nje ya nchi??
Brenda: Anaweza
Katuga: Mwenyekiti pia anaweza kufanya kazi akiwa nje ya nchi?
Brenda: Mwenyekiti akiwa nje anaendelea na majukumu yake ya uenyekiti
Katuga: Ni kweli kuwa wewe na hao niliowataja mwaka jana mwezi wa kumi mlikuwa nje ya nchi?
Brenda: Sio kweli
Katuga: Ni kweli kuwa jana ulisema kuwa baada ya mkutano wa 3/4/2025 uliona video ya Lissu kwenye Jambo TV?
Brenda: Niliiona
Katuga: Mshtakiwa alikuwa amevaa nini?
Brenda: Alivaa kombati
Katuga: wewe umevaa kombati au sio kombati
Brenda: Kombati
Katuga: Ni kweli alikuwa amevaa miwani?
Brenda: Anaweza akavua au akavaa
Katuga: Ni kweli ndani ya kombati ya kaki alikuwa amevaa T-shirt nyeusi?
Brenda: Sikumbuki
Katuga: Ni kweli nyuma yake kulikuwa na bendera?
Brenda: Ndio
Katuga: Bendera ya Chadema ina rangi gani?
Brenda: Blue, Nyeusi, Nyekundu na Nyeupe
Katuga: Ni sahihi ulisema kuwa mashahidi wa Jamhuri uliwasikiliza wakati wanatoa ushahidi?
Brenda: Ni kweli

Sehemu ya 378

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu, Brenda Rupia.

Katuga: Waeleze majaji kuwa hao mashahidi wa Jamhuri walisema humu kuwa walimuona Lissu akiwa amevaa kombati na miwani, nyuma yake kulikuwa na bendera ya Taifa na Chadema, hao watu watakuwa wanasema ukweli au uongo
Brenda: Sikumbuki kama mashahidi walisema hivyo.
Katuga: Ulisikia Mshtakiwa akisema kuwa majaji ni MaCCM?
Brenda: Sikusikia
Katuga: Ulisikia Lissu akisema Mahakamani hakuendeki
Brenda: Sikumbuki
Katuga: Ulisikia Lissu akisema kwani tukikinukisha watatuua? Si mimi watanikamata na kunifungulia kesi ya uhaini?
Brenda: Nakumbuka
Katuga: Ni wewe ulisema kuwa hii kesi ni ya uongo?
Brenda: Ni ushahidi wangu
Katuga: Wakati unamsikia Lissu anasema atafunguliwa kesi ya uhaini, wewe ni nani wa kusema kesi hii ni ya uongo?
Brenda: Mimi ni Brenda.
Katuga: Wewe una mamlaka gani kisheria kusema hii kesi ni ya uongo?
Brenda: Mahakama ndio ina mamlaka kisheria
Katuga: Ulisikia Lissu akisema mapolisi wanaingia na vibegi vya kura feki?
Brenda: Nafahamu
Katuga: Unafahamu kuwa Lissu anakesi ya kutoa taarifa za uongo mtandaoni Kisutu?
Brenda: Sikumbuki
Katuga: Ulishawahi kusoma hati ya mashtaka?
Brenda: Naomba nipe niisome maana mashtaka ni mengi sana
Katuga: Unajua kuwa Lissu alitaka hotuba yake iende kwa umma?
Brenda: Sijui kama alitaka iende kwa umma
Katuga: Unajua Lissu anavyombo vyake binafsi vya kutoa taarifa zake?
Brenda: Sijui
Katuga: Mwenyekiti akitaka taarifa zake zifike kwa umma unajua hutumia vyombo gani?
Brenda: Atatumia vyombo vya habari
Katuga: Njia pekee Mshtakiwa akitaka kutoa taarifa kwa umma au kwa wananchi ni vyombo vya habari?
Brenda: Sio sahihi
Katuga: Waambie majaji neno uasi kwa jinsi ulivyosoma kwenye kamusi ni lazima uelekeze dhidi ya watu fulani au authority fulani?
Brenda: Ni sahihi
Katuga: Neno tutahamasisha uasi, waambie majaji ilikuwa kuhamasisha uasi dhidi ya nani?
Brenda: Dhidi ya Sheria Kandamizi
Katuga: Anamuonyesha kitabu cha sheria, anauliza uasi ilikuwa dhidi ya sheria hizi?
Brenda: Dhidi ya Sheria Kandamizi
Katuga: Ulizitaja sheria?
Brenda: Sijazitaja
Katuga: Kinachobadili mfumo wa kisiasa ni sheria au ni watu wenye mamlaka?
Brenda: Ni watu
Katuga: Uasi ni dhidi ya Sheria au Watu wenye mamlaka?
Brenda: Dhidi ya sheria kandamizi
Katuga: Aliposema tutahamasisha uasi, tutazuia uchaguzi alimaanisha kuzuia sheria au watu wanaoenda kufanya uchaguzi?
Brenda: Yalilenga sheria kandamizi kubadilishwa
Katuga: Waambie majaji sheria ndio zinazoshiriki uchaguzi
Brenda: Sio sheria
Katuga: Ni nani wanaoshiriki uchaguzi?
Brenda: Watu ndio wanashiriki
Katuga: Unapoenda kuzuia uchaguzi, unazuia watu au sheria isifanye uchaguzi?
Brenda: Maana yake unazuia the whole process maana yake uchaguzi usifanyike kabisa
Katuga: Unajua Chadema inaamini katika demokrasia?
Brenda: Najua
Katuga: Unajua Tanzania ipo katika mfumo wa vyama vingi?
Brenda: Nafahamu
Katuga: No reforms no election ilikuwa falsafa ya vyama vyote?
Brenda: Ni msimamo wa chadema
Katuga: Ni sahihi ulitaja vyama 19?
Brenda: Ni sahihi
Katuga: Kuna ushahidi hapa kuwa No reforms, No election ni msimamo uliolenga kwamba chama hakitashiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike?
Brenda: Sio kweli
Katuga: Kwa majibu hayo niko sahihi kuwa Chadema ilimaanisha kuwa kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi?
Brenda: Msimamo ni kuwa bila mabadiliko hakuna uchaguzi
Katuga: Unafahamu kuwa uchaguzi upo kwa mujibu wa kikatiba?
Brenda: Nafahamu
Katuga: Unafahamu kuwa kubadilisha katiba ni mchakato?
Brenda: Ni mchakato
Katuga: Mchakato wa No reforms, No election ulianza mwaka gani???
Brenda: 2024

Katuga anacheka

Lissu anasema shahidi ameshajibu mbona unamchekea shahidi wewe Katuga?

Sehemu ya 379

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu, Brenda Rupia.

Katuga: Shahidi ameshajua kuwa ni 2024

Brenda: Naomba kubadilisha

Jaji Ndunguru: Shahidi anaweza kubadilisha wakati wa re examination na sio wakati wa cross examination. Kwahiyo twendelee

Katuga: Mwenyekiti katika hotuba yake, aliwaelekeza umma ni vipi wafanye ili kuzuia uchaguzi?

Brenda: alielekeza njia za kuzuia uchaguzi

Katuga: Alielekeza njia ya kuuvuruga uchaguzi?

Brenda: Alielekeza

Katuga: Alielekeza njia ya kukinukisha?

Brenda: Alielekeza

Katuga: Ulisema masuala ya kupika pilau wakati wa ushahdii wako, je waeleze majaji kama Lissu aliwaambia mpike pilau siku ya Uchaguzi

Brenda: Hakusema

Katuga: Je katika ushahidi wako ulisema kuwa ni njia gani mtatumia kuvuruga au kuzuia uchaguzi?

Brenda: Sikusema

Katuga: Waambie majaji katika ushahidi wako endapo ulisema kuwa Mwenyekiti aliwaelekeza njia za kuzuia uchaguzi

Brenda: Sijasema

Katuga: ushahidi wa njia za kuuzuia uchaguzi, kukinukisha ni muhimu au sio muhimu?

Brenda: Ni ushahidi muhimu

Katuga: Tutazuia uchaguzi ni sentensi iliyokamilika na yenye maana?

Brenda: Imekamilika na inaleta maana

Katuga: Tutavuruga uchaguzi je ni sentensi iliyokamilika na inaleta maaba?

Brenda: Imekamilika na inaleta maana

Katuga: waheshimiwa majaji naona watu wanafungua pipi yaani kama wameambizana maana wanafungua kwa pamoja chakachaka inaleta kelele

Watu kicheko😂😂😂😂😂

Jaji Ndunguru: Wakafungulie nje

Katuga: Kitendo cha kuchana karatasi za kupigia kura ni kitendo cha kuvuruga uchaguzi

Brenda: Ni sahihi

Katuga: kitendo cha kuchoma miundo mbinu wakati wa uchaguzi ni kitendo kinachovunja amani

Brenda: Ni Sahihi

Katuga: Kuwakata vidole waliopiga kura inaweza kutishia wengine wasipige kura?

Brenda: Ni sahihi

Katuga: waambie majaji kama ulimsikia Mwenyekiti akisema tutazuia huu uchaguzi kwa kufungua kesi

Brenda: Sikumsikia

Katuga: Ulisema chadema inaamini katika demokrasia

Brenda: Ndio

Katuga: Kama mnaamini demokrasia ni haki vyama vingine vikashiriki uchaguzi ?

Brenda: Ndio

Katuka: hii ni haki ya kikatiba?

Brenda: Ni haki

Katuga: Ni sahihi kuwa sio haki kumzuia mtu kushiriki uchaguzi?

Brenda: Sio haki

Katuga: Ni haki au sio haki kumzuia mtu kushiriki uchaguzi?

Brenda: Ni kosa

Katuga: Unajua kuwa ni kosa la jinai kisheria kumhamasisha mtu kuzuia uchaguzi?

Brenda: sijui kama ni kosa la jinai

Katuga: Ni haki mtu aliyemsikiliza Lissu kuitafsiri hiyo hotuba yeye anavyoona inafaa?

Brenda: Ni haki

Katuga: ni haki mtu aliyeisikiliza na kuielewa kuifanyia hotuba vile anavyoona inafaa?

Brenda: Ni haki

Katuga: Ni haki kutumia njia yoyote kuzuia uchaguzi kutokana na kile alichokisikia?

Brenda: Ni haki

Katuga: Kwahiyo ni haki PW3 alivyosema kwamba yeye alijiandaa kupiga watu siku ya uchaguzi

Brenda: Katika mashahidi ambao sikuwasikiliza ni PW3

Katuga: Ni kweli G-55 walikuwa wanachama wa chadema wakati wa hotuba?

Brenda: Walikuwa wanachama wa chadema

Katuga: ni kweli kuwa hawa G-55 walipingana na msimamo wa chadema na kusema huo ni uasi?

Brenda: Ni kweli

Katuga: Ni kweli kuwa walipoona msimamo wa kuzuia uchaguzi unaashiria uasi walijitoa kwenye chadema?

Brenda: Waliendelea kubaki ila walijiondoa kwenye chama kwa hatua za baadae

Katuga: Ni kweli kwamba baada ya wao kusema huo msimamo unaashiria uasi nsio Mwenyekiti alisema ni kweli kuwa huo msimamo unaashiria uasi?

Brenda: Ni sahihi

Sehemu ya 380
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu, Brenda Rupia.

Katuga: Unajua ni chombo gani hapa Tanzania chenye kulinda amani ya nchi?

Brenda: Jeshi la Polisi na Serikali

Katuga: Katika ushahidi wako uliwaambia majaji ni njia gani iliyopo kisheria inayoweza kuzuia uchaguzi?

Brenda: Sijaeleza

Mhe. Lissu: Naomba break ya dakika 5

Jaji Ndunguru: Ni sawa

Watu tumebreak dakika 5

Haya tumerejea

Katuga: Ulisema Lissu amenyimwa mafao yake bungeni, wewe uliwahi kufuatilia?

Brenda: Sijawahi kufuatilia?

Katuga: Kwakuwa umesema hujafatilia, nitakuwa sahihi kuwa Mwenyekiti anachuki dhidi ya Serikali?

Brenda: Sijui kama anachuki au hana

Ajuaye wakili wa Serikali amesimama, sisi hatuna maswali tena na kwavile nilimsikia Mshtakiwa anasema hana maswali ya re examination, naomba tupate muda wa break ili amuandae shahidi anayefuata then saa saba na nusu turejee

Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji nilisema at that point ila up to this point nina maswali kadhaa

Jaji Ndunguru: Shahidi utaulizwa maswali ya re examination

Mhe. Lissu: Shahidi pole huku anacheka kama kawaida ya tabasamu lake, anasema pole kwa kupitishwa katika tanuru la moto

Brenda: Asante

Mhe. Lissu: kwenye hotuba yangu uliulizwa kama nilisema kuna njia za kuzuia uchaguzi ukasema ndio. Je ulikuwa unamaanisha nini ?

Brenda : Nilimaanisha kuwa ulisema njia mojawapo ni kutokushiriki huo uchaguzi na hapo tutakuwa tumekinukisha kwelikweli

Mhe. Lissu: Katuga alikuuliza kama nilisema tutavuruga uchaguzi ukasema ndio, sasa fafanua

Katuga: Waheshimiwa majaji mimi niliuliza njia kama alizitaja wakati wa inchief kasema ulikuwa ushahidi muhimu na akasema ulikuwa muhimu. Hii ni after thought ili kujisahihisha. Re examination ni njia ya kufafanua kile ulichojibu wakati wa re examination sio kufafanua kile ambacho hukuleta during re examination

Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji nimebishana na wakili wa Serikali Katuga zaidi ya mwaka sasa na sitaki kuendelea kubishana nae sana, naomba rekodi za Mahakama zituongoze. Pingamizi halina msingi wowote, anachosema Katuga kuwa eti kisa tu shahidi wangu alisema ndio kwahiyo nisiulize maswali ya re examination that is nonsense with all due respect. Wasingetaka niyaulize wasingeyauliza during cross examination the fact kwamba wameyauliza lazima niulize for clarification

Hapa Lissu amekuwa mkali kisheria

Ukimya umetawala mahali hapa na majaji wanajadiliana kwa muda kidogo ili waje watoe ufafanuzi. Tunasubili

Jaji Ndunguru: Anarejea kumbukumbu za mahakama na anasoma, ni kweli hayo maswali yaliulizwa.

Katuga: waheshimiwa majaji ni kweli yaliulizwa lakini hoja yetu ni kwamba kwasababu njia za kuzuia au kukinukisha hakuzisema shahidi inchief hawezi kuzileta during re examination kwa mujibu wa kifungu cha 156 cha Sheria ya Ushahidi.

Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji ni mtu mmoja tu anaruhusiwa kuongea hapa mahakamani siku ya leo?

Jaji: Ndunguru: tunasubili amalize

Katuga: Kwasasa kanuni ya estoppel itumike na sio kuleta ushahidi mpya, kwa mfano zingekuwa ni karatasi angeulizwa anagesema anazo na aanza kusoma?

Mhe. Lissu: Kigungu cha 156(3) kinataka ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa during cross examination. Kama kuna jambo jipya sheria haikatazi abdolutely

Jaji Ndunguru: Hebu uliza sasa swali lako. Mfano shahidi akisema sasa hizo njia?

Mhe. Lissu: Kuna mawili mahakama ikatae au ikubali then Jamhuri wafanye cross.

Mhe. Lissu: Ulipoulizwa kuhusu njia za kuvuruga au kuzuia uchaguzi, ulijibu ndio, fafanua

Brenda: Waheshimiwa majaji ni kweli Mwenyekiti alielekeza njia za kuzuia au kuvuruga uchaguzi.

Sehemu ya 381
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re- examination Shahidi wake no. 4

Mhe. Lissu: Uliulizwa kama watu waliniunga mkono wakati wa hotuba ulisema haujui, fafanua.

Brenda: Hakukuwa na swali kwa washiriki kama wanaunga mkono au hawaungi mkono hotuba hiyox

Mhe. Lissu: Umeulizwa mengi sana kuhusu taarifa ya David McAllister, ulipoulizwa kama ulifanya uchunguzi ukasema ndio, fafanua

Brenda: Waheshimiwa majaji nilimpigia simu David McAllister mwenyewe na kuongea nae akasema hizo taarifa ni za kweli ndio uchunguzi nilioufanya.

Mhe. Lissu: uliulizwa na kuambiwa kuwa taarifa hiyo ni ya uongo, ukasema ni ya kweli

Brenda: Nilimpigia David McAllister na akaniambia kuwa taarifa ni ya ukweli kwahiyo taarifa niliyoitoa kwa umma ilikuwa nj ya ukweli.

Katuga: Waheshimiwa majaji taarifa kuwa alipiga simu haikuwepo kwenye inchief wala kwenye cross examination

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa unasemaje?

Mhe. Lissu: Nafikiri hiyo ya kupiga simu ni new matter naomba muikate

Jaji Ndunguru: Sawa

Mhe. Lissu: Shahidi uliulizwa usome tafsiri ya neno uasi, na ukaulizwa hilo neno uasi lina tafsiri zaidi ya moja ukasema ndio, fafanua

Brenda: Waheshimiwa majaji kwavile lina maana zaidi ya moja, unaweza kutumia maana mojawapo na mimi nilimaanisha tafsiri ya pili yenye maana ya kupinga mifumo kandamizi

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu Gervas Liende, kwanini ulisema humfahamu?

Katuga: hilo swali la kwanini ulisema humjui linaleta majibu mapya

Mhe. Lissu: Basically nataka tu wakili wa Serikali ajue kuwa hakuna mtu anaitwa Gervas Liende Chadema

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu wafanyakazi wenzako John Kitoka, ukaulizwa mtu anaweza kufanya kazi ya chama akiwa nje ya nchi? Ukasema inawezekana

Brenda: Waheshimiwa majaji hakuna restrictions kwa sehemu ya kufanyia kazi majukumu yako ya kichama.

Mhe. Lissu: Na hilo linaleta mambo mapya bwana wakili wa Serikali Katuga?

Watu kicheko😂😂😂 hapa Katuga ameinama tu hana cha kusema masikini

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu uasi, ukaulizwa nchi yetu ina mfumo gani wa utawala? Ulisema nchi ina utawala wa kiimla

Brenda: Nilikuwa na maana kuwa Rais ana absolute say, sheria hazifuatwi katika nchi hii.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kama ni kosa kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi ulisema sijui, ulimaanisha nini?

Brenda: Waheshimiwa majaji kisheria mimi sijui kuhamasisha uasi kama ni kosa.

Mhe. Lissu: uliulizwa kama ni haki watu kutafsiri maneno kwenye hotuba kwa wao wanavyoona inafaa, ukasema ni kweli

Brenda: Waheshimiwa majaji ni kweli kila mtu anahaki kutafisiri hiyo hotuba anavyoona yeye

Mhe. Lissu: uliulizwa kama ni haki au si haki kwa watu kufanya wanavyoona inafaa wao, ukasema ndio, fafanua

Brenda: Kwasababu hotuba ililenga watu kuzuia hotuba kwa mfano watu wasingeenda kwenye uchaguzi tayari wangezuia uchaguzi

Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji mimi sina maswali zaidi

Jaji Ndunguru: Shahidi mpaka hapa umemaliza kutoa ushahidi wako kwahiyo mahakama ina ku discharge.

Wakili wa Serikali Ajuaye anasimama: Waheshimiwa mjaji hivi sasa ni saa saba kasoro dakika 9 naomba tutumie muda huu kuahirisha na Mshtakiwa amuandae shahidi wake.

Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi saa nane na nusu

Inapigwa High Cooooouuuurrrrt

Majaji wanatoka.

Tukutane hapa saa nane na nusu mchana.

Kesi itaendelea Saa Nane na Nusu mchana ambapo Makamu Mwenyekiti John Heche ambaye ni shahidi wa 5 wa Lissu ataanza kutoa ushahidi wake.....
Via: Hilda Newton
 
kwa halii mkuu unafanya jamii ikutafsiri tofauti pamoja na maangalizo yote uliyopewa na baadhi ya watu. hakika kunatatizo sehemu anyway ngoja ninyamaze kuepusha shari isiyo na maana jukwaani tukijiandaa na darasa huru😷


🪑🗒🖊
 
Tayari Shahidi Brenda Jonas Rupia ameshafika Mahakamani kuendelea kutoa ushahidi wake .

Mheshimiwa Tundu Lissu anawasili Mahakamani


Kaa tayari kwa updates
 
7C425A95-5D30-4515-A88F-2DDBB04E2163.jpeg
Aibu naona mimi😂😂
 
Ulete na updates sasa. Siyo unakimbilia tu kuanzisha uzi halafu unatokomea kusikojulikana.
 
Mkuu kwani una shida gani na Manyanza ? Mbona huwa unaanzisha Uzi alafu hutoi update? Au ndo Ile kutaka nyuzi yako ifatiliwe wakati wewe hutoi muendelezo?

Anyway sihitaji kufatilia ugomvi wenu ulianziaga wapi ndo maana unamfanyia hivi ila kama Manyanza atakuwa muelewa Leo aistoe update yoyote Ile ya mahakamani Hadi pale mod watakapojirekebisha
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

MAHAKAMA IMEANZA

Lissu anaingia Mahakamani.

Majaji wanaingia Mahakamani.

Jaji Ndunguru: Haya, tuendelee.

Karani wa Mahakama anasoma kesi:

Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya Mwaka 2025

Jamuhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Wakili wa Serikali Mkuu Ajuaye Zegeli anawatambulisha Mawakili wenzake:

1. Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali Mkuu
2. Tawabu Issa – Wakili wa Serikali Mkuu
3. Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali
5. Mwanuka – Wakili wa Serikali Mkuu

Ajuaye Zegeli: Kwa pamoja tunawakilisha Jamhuri.

Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo kizimbani. Shauri linakuja kwa ajili ya utetezi na maswali ya dodoso, tupo tayari kuendelea.

Shahidi namba 4 yupo kizimbani kwa ajili ya kuulizwa maswali ya dodoso.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nipo tayari.

Jaji Ndunguru: Shahidi, ni matumaini yangu kwamba katika session hii ya asubuhi tutamalizana na shahidi.

Tupo sawa, Waheshimiwa?

Nassoro Katuga: Tutajitahidi.

Lissu: Mimi kwa upande wangu mpaka sasa sina maswali ya re-examination. Ni speed yao tu.

Jaji Ndunguru: Tuendelee. Shahidi, nakukumbusha kwamba upo chini ya kiapo.

Nassoro Katuga: Shahidi, waambie Waheshimiwa Majaji kwamba ni ushahidi wako kwamba ulikamatwa tarehe 10 June, baada ya Mwenyekiti kukamatwa.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ni sahihi kwamba ulikamatwa baada ya kuchapisha taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Ulaya?

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ulivyoichukua hii taarifa kwamba kuna taarifa ya kumpa sumu Lissu, je, wewe binafsi ulifanyia uchunguzi kupata ukweli wake?

Brenda: Kutoa taarifa ilikuwa ni kati ya mipango yangu ya kufanyia uchunguzi.

Nassoro Katuga: Kabla hujachapisha, ulifanyia uchunguzi?

Brenda: Nilifanyia uchunguzi.

Nassoro Katuga: Je, kabla ya kuchapisha ulijua ni ya kweli?

Brenda: Nilifanyia uchunguzi kuwa ni kweli. Imechapishwa na McAllister.

Nassoro Katuga: Baada ya kupata ile taarifa kwa huyo McAllister, je, ulifanyia uchunguzi kupata ukweli wake au hukufanyia uchunguzi?

Brenda: Nilifanyia uchunguzi.

Nassoro Katuga: Ulijiridhisha kama Lissu alitaka kuuawa kwa sumu?

Brenda: Nilijiridhisha.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama uliiambia Mahakama kwamba ulifanyia uchunguzi.

Brenda: Sikuiambia.

Nassoro Katuga: Waambie Majaji kama unajua kumuua mtu kwa sumu ni kosa la jinai.

Brenda: Najua.

Nassoro Katuga: Iambie Mahakama, wewe kama wewe, kabla hujachapisha hiyo taarifa yako, kama uliwahi kutoa hiyo taarifa kituo cha polisi na kujihakikishia kuwa una facts kwamba Lissu anataka kupewa sumu gerezani.

Brenda: Ndiyo, nilikuwa natoa taarifa. Sikutoa taarifa kabla ya hapo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni kosa kisheria kutokutoa taarifa za jinai kama una uhakika nazo?

Brenda: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua uwepo wa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Brenda: Naomba unisomee. Mimi siyo Mwanasheria.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naomba nimpe CPA asome kifungu cha 8.

Brenda: (Anasoma) Kifungu cha 8 cha CPA:

"A Person who..."

Brenda: This is exactly what I did.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba wewe binafsi kama ulitoa taarifa.

Brenda: Kuchapisha ndiyo kutoa taarifa kwa umma na authorities.

Nassoro Katuga: Kile ulichochapisha ulikopi kwa McAllister au umetoa kwako binafsi?

Brenda: Both.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama hicho unachokiita “ulitangazia umma” which is contrary na ulicho kisoma cha kuripoti Polisi.

Waambie Waheshimiwa Majaji kama katika hiyo report (taarifa kwa umma) ulisema kwamba umefanya uchunguzi wako uliothibitisha kuwa kuna mpango wa kumpa sumu Lissu gerezani.

Brenda: Sikueleza katika hiyo taarifa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom