⚖️ WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI
📌 SEHEMU YA 3
Nassoro Katuga: Kwa hiyo, katika tafsiri hizo mbili, hakuna uhusiano wowote?
Brenda: Hakuna.
Nassoro Katuga: Unakubaliana na mimi kwamba maana ya neno inaweza kutofautiana kulingana na muktadha linapotumika?
Brenda: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Na katika kuelewa maana ya neno, ni muhimu kuangalia muktadha ambao neno hilo limetumika?
Brenda: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, siyo kila neno linapotumika katika sentensi linakuwa na maana ileile inayopatikana kwenye kamusi?
Brenda: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Unakumbuka jana ulipoulizwa kuhusu maana ya kauli “No Reforms, No Election”?
Brenda: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Na ulieleza kwamba kauli hiyo ilikuwa na lengo la kudai marekebisho ya mfumo wa uchaguzi kabla ya uchaguzi kufanyika?
Brenda: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo, lengo lilikuwa kushinikiza mabadiliko kupitia madai hayo?
Brenda: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Na siyo kwamba kauli hiyo ilikuwa na lengo la kutumia nguvu kubadili mfumo wa kisiasa?
Brenda: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo, unakataa kwamba kauli “No Reforms, No Election” ilikuwa na maana ya uasi?
Brenda: Ndiyo, nakataa.
❤️ WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
🔄 SHARE ZAIDI UJUMBE HUU UFIKE MBALI.