Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 6.

Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba falsafa ya “No Reform, No Election” ililenga CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mpaka mabadiliko?

Brenda: Siyo kweli. Msimamo ni “Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi.”

Nassoro Katuga: Nipo sahihi nikisema kwamba CHADEMA haipo tayari kushiriki uchaguzi?

Ni kweli sasa kwamba CHADEMA ilisema “Hakuna mabadiliko, hakutakuwa na uchaguzi”?

Brenda: Si kweli.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unafahamu uchaguzi ni jambo la kikatiba.

Brenda: Nafahamu.

Nassoro Katuga: Na unajua kwamba Katiba ni mchakato?

Brenda: Nafahamu.

Nassoro Katuga: “No Reform” ilianza lini?

Brenda: 2024.

Brenda: Naomba kurekebisha.

Jaji Ndunguru: Shahidi anaomba kurekebisha.

Nassoro Katuga: Tunaomba kwanza kumuuliza maswali.

Jaji Ndunguru: Shahidi anaweza kurekebisha katika ushahidi wake in chief. Ila katika cross-examination hakuna nafasi ya kurekebisha, labda asubiri re-examination.

Nassoro Katuga: Shahidi, unaweza kueleza kama Mwenyekiti aliwaelekeza namna ipi ya kuzuia uchaguzi?

Brenda: Alielekeza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama alielekeza njia ya kuvuruga uchaguzi.

Brenda: Alielekeza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama alielekeza namna ya kukinukisha.

Brenda: Alielekeza.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako ulisema kwamba kukinukisha ni kupika pilau. Waeleze Waheshimiwa Majaji kama Mwenyekiti alielekeza mpike pilau siku ya uchaguzi.

Brenda: Hakusema tupike pilau.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama katika ushahidi wako wa msingi ulieleza kama alisema aliwaelekeza mkinukishe kwa namna gani.

Brenda: Sikueleza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, katika ushahidi wako uliwaambia Majaji kwamba tutavuruga uchaguzi kwa njia moja, mbili na tatu, kama ulisema?

Brenda: Sikusema.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama Lissu alituambia tufanye ili kuzuia uchaguzi.

Brenda: Sikusema.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Sheria lazima ziheshimiwe. Majambazi wa CHADEMA mkafie mbele
FB_IMG_1732381054839.jpg
20250323_112556.jpg
Screenshot_20250415_093714_X.jpg
Screenshot_20250410_180617_X.jpg
Screenshot_20250411_035715_TikTok.jpg
Screenshot_20250405_004444_X.jpg

Hawa sheria iliheshimiwa na kuchukuliwa hatua kama unavyosema?
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 7.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa umesomewa mara kibao kwamba Lissu alisema kwa umma kwa nia ya kutishia Serikali, ni ushahidi muhimu au siyo ushahidi muhimu?

Nassoro Katuga: “Tutazuia uchaguzi” ni sentensi iliyokamilika yenye maana au siyo sentensi yenye maana?

Brenda: Ni sentensi iliyokamilika yenye kuleta maana.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kuchoma vituo vya kupigia kura au kuchoma karatasi za kupigia kura inaweza kuwa ni kitendo cha kuzuia uchaguzi.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kuharibu mali kunaweza kuvuruga amani na hivyo kusababisha kuzuia uchaguzi.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kukata vidole vya waliopiga kura kunaweza kutishia wengine wasiende kupiga kura na hivyo kuzuia uchaguzi usifanyike.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Kama ulisikia Mwenyekiti akisema kwamba tutafungua kesi Mahakamani kama njia za kisheria?

Brenda: Sikusikia.

Nassoro Katuga: Ulisema CHADEMA inaamini katika demokrasia?

Brenda: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Hivyo, ni haki mtu kushiriki uchaguzi?

Brenda: Ni haki mtu kushiriki uchaguzi huru na wa haki.

Nassoro Katuga: Ni haki kumzuia mtu kushiriki uchaguzi?

Brenda: Siyo haki.

Nassoro Katuga: Ni kosa kisheria na jinai kwa mtu kuhamasisha mtu mwingine kuuzuia uchaguzi?

Brenda: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa mtu yeyote aliyesikiliza hotuba, kutafsiri anavyotaka...

Brenda: Ni haki au siyo haki kwa mtu aliyesikia hotuba ya Mwenyekiti kufanya anavyotaka?

Brenda: Ni haki.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo, ni haki kwa mtu aliyesikia hotuba ya Mwenyekiti kutenda anavyotaka?

Brenda: Ni haki.

Nassoro Katuga: Unaukumbuka ushahidi wa PW3?

Brenda: PW3 ni kati ya mashahidi ambao sikuwasikia.

Nassoro Katuga: Ni kweli au si kweli hawa G55 walikuwa ni wanachama wa CHADEMA wa wakati ule?

Brenda: Ni wanachama.

Nassoro Katuga: Ni kweli au siyo kweli kwamba mara baada ya wao kujitoa (waria nia) katika msimamo, baada ya kuona huu msimamo una ushirika uasi?

Brenda: Walijitoa na wengine wakabaki.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Katuga anajaribu kumfunga Brenda kwenye majibu aliyoyatoa jana kuhusu No Reforms, No Election na maana ya uasi,

Ili kuonyesha kwamba baadhi ya conclusions zake zinapingana na maana ya kawaida ya maneno hayo.

Angle ya kisheria ambayo ni muhimu hapa ni distinction kati ya dictionary meaning na legal meaning.

Kamusi inaweza kutoa maana ya kawaida ya neno uasi, lakini haiwezi yenyewe kuthibitisha kwamba matumizi ya neno hilo katika hotuba ya Lissu yalitimiza statutory elements za treason chini ya Penal Code.

Na hapa ndipo prosecution imepazimika kwenda hatua nyingine, yaani kutoka kwenye maana ya neno, kwenda kwenye context, mens rea, actus reus, attribution na causal nexus.

Pia Katuga anatumia contradiction ya No Reforms, No Election na maana ya uasi kama impeachment tool.

Lakini kusema kwamba chama kilitaka mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi hakumaanishi moja kwa moja kwamba kilikuwa kinataka kuuangusha au kuubadilisha mfumo wa kisiasa kwa njia ya jinai.

Hii ndio distinction kati ya political reform advocacy na criminal insurrection ambayo mahakama italazimika kuitazama kwa ushahidi mzima.

Sehemu nyingine muhimu ni namna Katuga anavyojaribu kupima reliability ya memory ya Brenda kupitia maswali ya mavazi ya Lissu, miwani, Tshirt, bendera na video ya Jambo TV.

Haya yanaweza kuonekana kama maswali madogo, lakini kisheria yanaweza kutumika kutest kama shahidi kweli aliona video kwa umakini kiasi anachodai.

Lakini kutokumbuka Tshirt au miwani pekee hakumaanishi testimony yote ni ya uongo, yaani mahakama huangalia materiality ya discrepancy na kama inaathiri facts zinazobishaniwa.

Na hapa kuna jambo lingine muhimu la kuzingatia, Brenda anakiri kuwa aliwasikiliza mashahidi wa Jamhuri waliotangulia.

Hili linaweza kuibua swali la independent recollection, yaani kama ushahidi wake unatokana na kumbukumbu yake binafsi ya tukio au umeathiriwa kwa kiasi fulani na exposure yake kwa testimony iliyotangulia.

Hilo linaweza kuwa relevant kwenye weight and credibility, ingawa sio automatic ground ya kuondoa ushahidi wake.

Kutoka X
Brenda kuhusu video alijibu kuwa aliiona lakini alipoulizwa kama mahakamani ililetwa alijibu haikuletwa na prosecution so kupitia ushahidi huo ni wazi kuwa prosecution case has already fallen down long time ago kwasababu ukimuondoa PW 17 wengine wote walieleza kuwa waliona kwenye jambo Tv ambayo video haipo na kwamba hata huyo 17 yeye ndiye aliyeeleza kuwa alichapisha kwenye mtandao wao sasa kwa mazingira hayo ili mahakama ifikie uamuzi ni lazima ijiulize
1. whether the accused published the alleged statement.
2. whether the accused person made statement amounting to treason puersuant to Section 39(2)(d) Penal code cap. 16 R.E. 2023.
Na hapa ndio dhana ya ile video inakuwa muhimu kwani lissu hakatai kutamka maneno hayo lakini anasema yalichukuliwa out of the context kwani maneno yaliyopo kwenye Information ni machache wakati yeye aliongea maneno mengi kwa mukutadha tofauti ndio maana hoja ya lissu ukitaka kujua kuwa yuko smart kila shahidi wake anamuhoji swali kwamba aliongea kwa muda gani ambapo wote wamejibu ni zaidi ya masaa mawili hii ni kumaanisha kwamba video ya Jambo ingekuwepo ndio majaji wangepima dhana mens rea na sio vipande vipande vya kwenye Hati ya mashtaka ambavyo anapowasomea haizidi hata dakika moja wakati yeye aliongea masaa zaidi ya mawili. Mwisho kabisa hata hao mawakili wa Serikali wanapoteza muda tu huku wakijua wameshashindwa kesi na hata ikitokea kwa ujinga akutwa na hatia, hiyo hatia itakuwa kama kesi za akina mbowe ambazo kwenye rufaa ni asubuhi tu kesi anashinda.

NB: Ni kama hivi mtu anasema alinunua shamba na kuandikishana lakini maandishi hajayaleta mahakamani ili kuthibitisha kuwa waliandikishana hivyo hoja ya kwamba alikuwepo kwenye eneo la kuandikishana na alisain inakuwa haina maana yoyote kwasababu maandishi ambayo amesema waliandikishana alipaswa kuyaleta so hata huyo shahidi PW17 aliyerecord na hakuleta recorded video ni sawa na kazi bure maana alipaswa kuileta ili mahakama iamini kuwa kweli kupifanyika publication tofauti na hapo zinabaki story za vijiweni tu.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

MAHAKAMA IMEANZA

Lissu anaingia Mahakamani.

Majaji wanaingia Mahakamani.

Jaji Ndunguru: Haya, tuendelee.

Karani wa Mahakama anasoma kesi:

Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya Mwaka 2025

Jamuhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Wakili wa Serikali Mkuu Ajuaye Zegeli anawatambulisha Mawakili wenzake:

1. Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali Mkuu
2. Tawabu Issa – Wakili wa Serikali Mkuu
3. Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali
5. Mwanuka – Wakili wa Serikali Mkuu

Ajuaye Zegeli: Kwa pamoja tunawakilisha Jamhuri.

Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo kizimbani. Shauri linakuja kwa ajili ya utetezi na maswali ya dodoso, tupo tayari kuendelea.

Shahidi namba 4 yupo kizimbani kwa ajili ya kuulizwa maswali ya dodoso.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nipo tayari.

Jaji Ndunguru: Shahidi, ni matumaini yangu kwamba katika session hii ya asubuhi tutamalizana na shahidi.

Tupo sawa, Waheshimiwa?

Nassoro Katuga: Tutajitahidi.

Lissu: Mimi kwa upande wangu mpaka sasa sina maswali ya re-examination. Ni speed yao tu.

Jaji Ndunguru: Tuendelee. Shahidi, nakukumbusha kwamba upo chini ya kiapo.

Nassoro Katuga: Shahidi, waambie Waheshimiwa Majaji kwamba ni ushahidi wako kwamba ulikamatwa tarehe 10 June, baada ya Mwenyekiti kukamatwa.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ni sahihi kwamba ulikamatwa baada ya kuchapisha taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Ulaya?

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Ulivyoichukua hii taarifa kwamba kuna taarifa ya kumpa sumu Lissu, je, wewe binafsi ulifanyia uchunguzi kupata ukweli wake?

Brenda: Kutoa taarifa ilikuwa ni kati ya mipango yangu ya kufanyia uchunguzi.

Nassoro Katuga: Kabla hujachapisha, ulifanyia uchunguzi?

Brenda: Nilifanyia uchunguzi.

Nassoro Katuga: Je, kabla ya kuchapisha ulijua ni ya kweli?

Brenda: Nilifanyia uchunguzi kuwa ni kweli. Imechapishwa na McAllister.

Nassoro Katuga: Baada ya kupata ile taarifa kwa huyo McAllister, je, ulifanyia uchunguzi kupata ukweli wake au hukufanyia uchunguzi?

Brenda: Nilifanyia uchunguzi.

Nassoro Katuga: Ulijiridhisha kama Lissu alitaka kuuawa kwa sumu?

Brenda: Nilijiridhisha.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama uliiambia Mahakama kwamba ulifanyia uchunguzi.

Brenda: Sikuiambia.

Nassoro Katuga: Waambie Majaji kama unajua kumuua mtu kwa sumu ni kosa la jinai.

Brenda: Najua.

Nassoro Katuga: Iambie Mahakama, wewe kama wewe, kabla hujachapisha hiyo taarifa yako, kama uliwahi kutoa hiyo taarifa kituo cha polisi na kujihakikishia kuwa una facts kwamba Lissu anataka kupewa sumu gerezani.

Brenda: Ndiyo, nilikuwa natoa taarifa. Sikutoa taarifa kabla ya hapo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni kosa kisheria kutokutoa taarifa za jinai kama una uhakika nazo?

Brenda: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua uwepo wa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Brenda: Naomba unisomee. Mimi siyo Mwanasheria.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naomba nimpe CPA asome kifungu cha 8.

Brenda: (Anasoma) Kifungu cha 8 cha CPA:

"A Person who..."

Brenda: This is exactly what I did.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba wewe binafsi kama ulitoa taarifa.

Brenda: Kuchapisha ndiyo kutoa taarifa kwa umma na authorities.

Nassoro Katuga: Kile ulichochapisha ulikopi kwa McAllister au umetoa kwako binafsi?

Brenda: Both.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama hicho unachokiita “ulitangazia umma” which is contrary na ulicho kisoma cha kuripoti Polisi.

Waambie Waheshimiwa Majaji kama katika hiyo report (taarifa kwa umma) ulisema kwamba umefanya uchunguzi wako uliothibitisha kuwa kuna mpango wa kumpa sumu Lissu gerezani.

Brenda: Sikueleza katika hiyo taarifa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Rupia ni hela kubwa vile heee.!
 
Back
Top Bottom