TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE BRENDA RUPIA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 10.
Jaji Ndunguru: Turejee mlolongo wa majibu ya Mahakama.
Alisema kwamba “No Reform, No Election” ilianza 2024.
“Sikusema Mshtakiwa alielekeza njia ya kuzuia uchaguzi, kuvuruga uchaguzi.
Sikusema katika ushahidi wangu njia ya kuvuruga uchaguzi.
Pia sikusema Mshtakiwa alielekeza namna, njia za kuvuruga uchaguzi.
Isipokuwa alieleza njia za kuzuia uchaguzi.”
Nipo sahihi?
Nassoro Katuga: Naomba urudie tena.
Lissu: Hicho ndicho nilichokisema.
Nassoro Katuga: Sisi hoja yetu kwamba re-examination kazi yake ni kufanya clarification ya majibu ya shahidi.
Sasa shahidi anakiri kwamba huyu mtu alitoa njia za kuvuruga uchaguzi.
Na ameconfirm kwamba huu ushahidi haukuwepo katika in-chief.
Sasa ukimwambia afafanue vitu ambavyo anakiri hakusema na vilikuwa muhimu kusema, sasa tunapokeaje vitu vya namna hii?
Kifungu cha 157(3) kinazuia, Mheshimiwa.
(Anakisoma.)
Sasa, Mheshimiwa, shahidi ameshaisaidia Mahakama kwamba ulikuwa ushahidi muhimu, alipaswa au ulete sasa kwa kutumia jibu la “ndiyo”, ndiyo au ulete.
Ndiyo maana tunafanya principle of estoppel kuzuia huu ushahidi.
Ingekuwa mtu anaulizwa umeleta nyaraka katika cross-examination, anasema hajaleta, halafu wakati wa re-examination ndiyo ulete?
Maana yake ni kuleta ushahidi ambao unakiri wewe mwenyewe hukuleta wakati wa in-chief.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, inabidi na mimi niseme.
Sheria inasema kwamba re-examination will refer to the matter of cross-examination kwa mujibu wa Kifungu cha 156(3).
Swali limeulizwa, shahidi amejibu, nina haki ya kufanya re-examination.
Hiyo kwamba je, umeleta Mahakamani, ni sehemu tofauti.
Wakili anachanganya majibu yake.
Kama kuna jambo jipya, sheria vilevile imesema.
Jaji Ndunguru: Hebu uliza sasa swali lako.
Lissu: Nataka aeleze hizo njia.
Jaji Ndunguru: Akijibu hizo njia, je, zikawa majibu mapya?
Lissu: Ni Mahakama izuie au upande wa mashitaka wapewe nafasi ya cross-examination.
Jaji Ndunguru: Sawa, tuendelee.
Lissu: Fafanua jibu kwamba Mwenyekiti alielekeza njia ya kuzuia uchaguzi.
Brenda: Alielekeza.
Lissu: Alielekeza njia ya kuvuruga uchaguzi?
Brenda: Alielekeza.
Lissu: Twende wakati unaelekezwa maswali na Wakili Job Mrema.
Alikwambia ueleze kwamba aliposema maneno hayo aliungwa mkono.
Ukasema hufahamu kama aliungwa mkono.
Hebu fafanua jibu lako.
Brenda: Waheshimiwa Majaji, sifahamu kama walimuunga mkono kwa sababu hapakuwa na swali la kama mnaunga mkono.
Lissu: Umeulizwa maswali mengi sana ya sababu za wewe kukamatwa.
Ukasema ni kuhusu post ya David McAllister.
Ukaulizwa kama ulifanya uchunguzi.
Ulikuwa na maana gani uliposema umefanya uchunguzi?
Brenda: Waheshimiwa Majaji, nilimpigia direct David McAllister kumuuliza hilo jambo.
Akaniambia hizo ni taarifa za kweli.
Huo ndiyo uchunguzi wangu.
Lissu: Uliulizwa kama taarifa ni ya uongo, ukasema hiyo taarifa siyo ya uongo.
Hebu fafanua.
Brenda: Waheshimiwa Majaji, nilimpigia Mbunge wa Bunge la Ulaya, David McAllister, direct, akaniambia ni kweli.
Ndiyo maana nilitoa taarifa, siyo ya uongo.
Nassoro Katuga: Hakusema kama alipiga simu.
Tungeweza kuuliza maswali ya cross.
Hakusema kama alipiga simu.
Tunaomba iondolewe.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unasemaje?
Lissu: Nafikiri hiyo sehemu ya kumpigia simu McAllister iondolewe. Haikuulizwa hapo mwanzo na haijapata ruhusa ya Mahakama kuingia.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI