Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Umeona kwenye ndoto ya saa ngapi
Namimi nikaote kwa muda uho😂
 
Katuga anajaribu kumfunga Brenda kwenye majibu aliyoyatoa jana kuhusu No Reforms, No Election na maana ya uasi,

Ili kuonyesha kwamba baadhi ya conclusions zake zinapingana na maana ya kawaida ya maneno hayo.

Angle ya kisheria ambayo ni muhimu hapa ni distinction kati ya dictionary meaning na legal meaning.

Kamusi inaweza kutoa maana ya kawaida ya neno uasi, lakini haiwezi yenyewe kuthibitisha kwamba matumizi ya neno hilo katika hotuba ya Lissu yalitimiza statutory elements za treason chini ya Penal Code.

Na hapa ndipo prosecution imepazimika kwenda hatua nyingine, yaani kutoka kwenye maana ya neno, kwenda kwenye context, mens rea, actus reus, attribution na causal nexus.

Pia Katuga anatumia contradiction ya No Reforms, No Election na maana ya uasi kama impeachment tool.

Lakini kusema kwamba chama kilitaka mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi hakumaanishi moja kwa moja kwamba kilikuwa kinataka kuuangusha au kuubadilisha mfumo wa kisiasa kwa njia ya jinai.

Hii ndio distinction kati ya political reform advocacy na criminal insurrection ambayo mahakama italazimika kuitazama kwa ushahidi mzima.

Sehemu nyingine muhimu ni namna Katuga anavyojaribu kupima reliability ya memory ya Brenda kupitia maswali ya mavazi ya Lissu, miwani, Tshirt, bendera na video ya Jambo TV.

Haya yanaweza kuonekana kama maswali madogo, lakini kisheria yanaweza kutumika kutest kama shahidi kweli aliona video kwa umakini kiasi anachodai.

Lakini kutokumbuka Tshirt au miwani pekee hakumaanishi testimony yote ni ya uongo, yaani mahakama huangalia materiality ya discrepancy na kama inaathiri facts zinazobishaniwa.

Na hapa kuna jambo lingine muhimu la kuzingatia, Brenda anakiri kuwa aliwasikiliza mashahidi wa Jamhuri waliotangulia.

Hili linaweza kuibua swali la independent recollection, yaani kama ushahidi wake unatokana na kumbukumbu yake binafsi ya tukio au umeathiriwa kwa kiasi fulani na exposure yake kwa testimony iliyotangulia.

Hilo linaweza kuwa relevant kwenye weight and credibility, ingawa sio automatic ground ya kuondoa ushahidi wake.

Kutoka X
Nimekuelewa sana mkuu leo nachokiona ni kujaribu ku test kumbukumbu za shahidi na kufanya ajipinge.
Binafsi leo naona kama shahidi anawekwa kwenye angle mbaya jambo ambalo si zuri. Nilitamani a stick kwenye kile jana amesema. Jambo nililoogopa zaidi ni swala la sumu, hili nisilisema maana nimeona ameenda oof track kwa uelewa wangu, am very sad
 
WASOMAJI WA KESI INAYOENDELEA * ANGALIZO
Ili kuweza kufuatilia mwenendo wa kesi bila kutekwa na ushabiki, wala sarakasi zinazotokea mahakamani. Sikiliza cross examination ya kesi mojawapo nchini Kenya iliyopo ktk lugha ya Kiswahili
Ili kuweza kufuatilia mwenendo wa kesi bila kutekwa na ushabiki, wala sarakasi zinazotokea mahakamani. Sikiliza cross examination ya kesi mojawapo nchini Kenya iliyopo ktk lugha ya Kiswahili

TOKA MAKTABA
MARCH 2026
Nairobi, Kenya


Afisa Police Akubali Mapengo Muhimu Wakati wa cross-examonation (Uchunguzi Mtambuka) Katika Kesi ya Kushambuliwa ya Boniface Mwangi


View: https://m.youtube.com/watch?v=OI3zlLdGBqI
Wakili James Wanjeri alimhoji koplo wa polisi katika kesi inayoendelea inayomhusu mwanaharakati Boniface Mwangi, akifichua kutofautiana kukubwa katika maelezo ya upande wa mashtaka. Afisa huyo, Bw. Yano, aliiambia mahakama kwamba alijibu simu ya dharura saa 3:30 usiku na akafika muda mfupi baadaye, lakini alikiri kwamba hakujitambulisha katika eneo la tukio au kuthibitisha kama tukio hilo la kelele lilikuwa na leseni.

Koplo alikubali zaidi kwamba si kelele zote zinawakilisha kosa la jinai, na alithibitisha kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa kupima viwango vya kelele au kuthibitisha uhalali wa mkutano huo. Kuhusu madai mazito zaidi, afisa huyo alikiri kwamba matamshi ya kukera ya mshtakiwa yalikuwa ya jumla na hayakuelekezwa kwa afisa yeyote maalum.

Ushahidi wake kuhusu shambulio hilo linalodaiwa pia uliibua maswali, kwani alidai glasi ilirushwa kwa afisa—lakini glasi hiyo haikutolewa mahakamani.

Alikiri zaidi kwamba licha ya uwepo wa wahudhuriaji 60–70, hakuna mashahidi huru walioitwa, hakuna taarifa zilizorekodiwa kutoka kwa umma, na hakuna kumbukumbu za simu au ingizo la OB lililotolewa kuhusu malalamiko ya awali—mapengo ambayo upande wa utetezi unasema yanadhoofisha kesi ya upande wa mashtaka kwa kiasi kikubwa.

Officer Concedes Key Gaps During Cross-Examination in Boniface Mwangi Assault Trial

Lawyer James Wanjeri mounted a sharp cross-examination of a police corporal in the ongoing case involving activist Boniface Mwangi, exposing major inconsistencies in the prosecution’s account. The officer, Mr. Yano, told the court he responded to a distress call at 9:30 p.m. and arrived shortly after, but admitted he never introduced himself at the scene or verified whether the alleged noisy event was licensed. He further conceded that not all noise amounts to a criminal offence, and confirmed no steps were taken to measure the noise levels or establish the legality of the gathering

On the more serious allegations, the officer acknowledged that the accused’s alleged offensive remarks were general and not directed at any specific officer. His testimony on the alleged assault also raised questions, as he claimed a glass was thrown at an officer—yet the glass was never produced in court. He further admitted that despite the presence of 60–70 attendees, no independent witnesses were called, no statements were recorded from members of the public, and no call logs or OB entry were made regarding the initial complaint—gaps the defence argues significantly weaken the prosecution’s case.

KUJIONGEZA UWEZO WA KUFUATILIA MTIFUANO WA KISHERIA MAHAKAMANI BILA USHABIKI



Tujufunze jinsi ya kufuatilia mwenendo wa kesi kwa kuangalia kwa umakini ushahidi unaotolewa na pia cross examination kama zimejikita katika kuipa uzito chargesheet, au zimeshindwa kujikita ktk mambo ya msingi katika hati ya mashtaka yaani chargesheet. Hapa chini ni elimu na nyenzo za kukuwezesha kufuatilia mwenendo wa mashauri mahakamani ukiwa na fikra huru:


08 October 2025
Nairobi, Kenya
Lawyer John Maina Grills Cop Who Accused Boniface Mwangi of Assaulting Him

View: https://m.youtube.com/watch?v=-_PjSaxUWuk
Lawyer John Maina on Wednesday intensely cross-examined a police officer who accused activist Boniface Mwangi of assaulting him during an April 2025 altercation at Mwangi’s Sema Ukweli offices in Kilimani. The officer claimed Mwangi attacked him while resisting arrest, but the defense disputed this, alleging the officer was intoxicated and attempted to draw his firearm. Maina questioned inconsistencies in the officer’s account and suggested the police were covering up an assault against Mwangi. The case, which has drawn public attention, continues before the Kibera Law Courts.
Source : Court Helicopter

N.B

A chargesheet is the final investigative report filed by law enforcement to show a magistrate that enough concrete evidence exists to start a criminal trial.

Role of Concrete Evidence :

Foundation: The report relies on gathered proof like witness statements, forensic tests, and digital media.

Not Proof of Guilt: The document reflects the officer's opinion based on findings, not a final conviction.

Court Review: A judge evaluates the listed facts to formally frame charges and begin proceedings



View: https://m.youtube.com/watch?v=NccKrdx5VR8

During an intense cross-examination, defence lawyer Shadrack Wambui cast serious doubt on the credibility and competence of cyber-forensic analyst Juma Mwajirani, whose report forms part of the evidence against political commentator Nuru Okanga.Wambui began by asking Mwajirani to state the specific charges Okanga faced. The analyst initially relied on a DCI request letter that cited publication of false information and cyber harassment, but later retracted his answer, admitting he did not actually know the charges.

Lawyer Shadrack Wambui Dismantles Cyber forensic Analyst in Nuru Okanga’s Case


View: https://m.youtube.com/watch?v=fGvmL6yviqA

key facts, including whether he knew that Rigathi Gachagua is a former District Officer and former Deputy President details he conceded he did not know. When questioned about his understanding of “inflammatory” content, Mwajirani added that he does not know how to use a gun and that “not everyone shot with a gun dies,” a statement that raised concerns over the basis of his analysis.

On the technical front, the analyst confirmed that TikTok and YouTube accounts can be created without Gmail, acknowledged that the videos in question were posted by Diff Media and Riba News, yet admitted he did not access or identify the owners of those accounts. Of the 22 comments under the videos, he included only three in his report prompting Wambui to question whether the investigation was selectively conducted.

Wambui also highlighted a glaring discrepancy: the DCI request letter used by Mwajirani was dated 2023, even though the case pertains to 2024. The defence argued that such inconsistencies reflect a poorly handled and unreliable investigation.

26 November 2025
Lawyer Abner Mango Discredits Cyber Analyst Over Flawed Report in Nuru Okanga’s Case

View: https://m.youtube.com/watch?v=F4HV4Bo0L6w
Defence lawyer Abner Mango, together with other lawyers representing Nuru Okanga, challenged the credibility of analyst Juma Mwajirani’s report, arguing it was incomplete and selectively focused on Riba News while ignoring Diff Media, despite both being linked to the disputed video.

Mango questioned why Mwajirani did not investigate who owns the accounts or whether Okanga had any connection to them.

The defence also raised concerns about the handling of Okanga’s seized phone. Mwajirani admitted he never examined the device, checked for malware, or verified whether other users could access it gaps the defence argued undermine the integrity and reliability of his analysis.


View: https://m.youtube.com/watch?v=CJNiDPTw66E

cyber forensic expert’s report in the case against political commentator Nuru Okanga was severely weakened today after a blistering cross-examination by defence lawyer Hon. Babu Owino.Cyber and digital forensic analyst Juma Mwajirani came under intense scrutiny as Babu methodically poked holes in both his qualifications and his conclusions. The defence questioned the credibility of Mwajirani’s certification, pointing out that the institution he cited does not issue forensic analyst credentials.Babu further discredited the report by highlighting glaring inconsistencies—among them, the use of a 2023 reference letter to support an investigation conducted in 2024

02 July 2026

Deal Ruthlessly With DCI.Orengo Tough Question to Ruto DCI Officer In Court While Representing Bob

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZH5rUg3NSGs

Source : Court Helicopter
 
Nimekuelewa sana mkuu leo nachokiona ni kujaribu ku test kumbukumbu za shahidi na kufanya ajipinge.
Binafsi leo naona kama shahidi anawekwa kwenye angle mbaya jambo ambalo si zuri. Nilitamani a stick kwenye kile jana amesema. Jambo nililoogopa zaidi ni swala la sumu, hili nisilisema maana nimeona ameenda oof track kwa uelewa wangu, am very sad

..suala la jaribio la sumu dhidi ya Tundu Lissu lilikuwa halina msaada wowote kwa Katuga na alipoteza muda kulishadidia.

..Jaji anaposema Wakili muongoze shahidi mara nyingi huwa analenga tukio kama lile.

..Wakili awe wa utetezi au mashtaka anatakiwa asimame ktk mstari na maswali yake yajielekeze ktk shauri lililopo mahakamani.
 
Muda wa John Heche unakaribia sasa mzee wa kazi yaani yeye kazaliwa anajiamini hakuna wa kumtisha apo mawakili wajipange sana

Kwaiyo Shemeji Heche
sasa atazitapika tone tone zetu

MUNGU ni. Mwema uyu ngoja kwanza mh Lissu amalize kucheka na Shemij wake❗️

kesho
Mh Lissu hatukabidhi uyo
Shemeji yake
Tujue pesa kaweka wapi na nguvu ya kuwafukuza Wanachama kaitoa wapi🤠🤠
 
MAHAKAMA IMERUDI TOKA MAPUMZIKO.

MAHAKAMA INAREJEA / MAJAJI WANAINGIA.

Mahakama ipo kimya kwa muda.

Majaji wanateta kidogo.

Mawakili wa Serikali wapo tayari.

Lissu yupo tayari.

Shahidi wa tano yupo tayari.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, kolamu inabaki kama ilivyo. Tupo tayari kumsikiliza shahidi namba 5 wa upande wa utetezi.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa unasemaje?

Lissu: Nipo tayari, Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: Palikuwa na jambo moja sasa. Mara ya mwisho tulireserve kuhusu wale mashahidi wengine.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nakumbuka mlichokielekeza kwamba nianze na hawa mashahidi kwanza, halafu nikikamilisha ndiyo tuendelee na uamuzi.

Kwa hiyo, tuendelee na mashahidi hawa kwanza.

MAJAJI WANATETA.

Jaji Ndunguru: Upande wa mashitaka?

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, tunaungana na alichosema Mshtakiwa. Tuendelee na shahidi, baada ya hapo Mahakama itasoma uamuzi.

MAJAJI WANATETA.

Bado Majaji wanateta. Kuna wingu zito hapa, wacha tusubiri tuone.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1

Jaji Ndunguru: Basi tumekubaliana tutaendelea na shahidi aliyepo.

Na leo, baada ya kusikiliza shahidi aliyepo, tutasoma huo uamuzi, kusudi pande zote mbili zijue status za hao mashahidi.

Lissu na Mawakili wa Serikali: Sawa.

Jaji Ndunguru: Shahidi, jina lako?

Heche: Naitwa John Wegesa Heche.

Jaji Ndunguru: Umri wako?

Heche: Miaka 45.

Jaji Ndunguru: Unaishi wapi?

Heche: Tarime/Mwanza.

Jaji Ndunguru: Unafanya shughuli gani?

Heche: Makamu Mwenyekiti CHADEMA.

Jaji Ndunguru: Dini yako?

Heche: Mkristo/Msabato.

Heche: Mimi, John Wegesa Heche, naapa mbele ya Mahakama hii tukufu kwamba ushahidi nitakaoutoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu. Mungu nisaidie.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Jaji Ndunguru: Utamuongoza?

Lissu: Nitamuongoza.

Lissu: Shahidi, umesema wewe ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Umekuwa kwenye nafasi hiyo tangu lini?

Heche: Nimekuwa Makamu Mwenyekiti Bara (Tanganyika) tangu mwaka jana, mwezi Januari 2025.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anapatikanaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anapatikana kwa kuchaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa chama chako anatumikia nafasi hiyo kwa muda gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anatumikia nafasi hiyo kwa miaka 5.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo nafasi nani alikuwa mtangulizi wako?

Heche: Waheshimiwa Majaji, kabla yangu nafasi hii alikuwa Tundu Antipas Lissu, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Taifa.

Lissu: Kabla ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, ulikuwa kwenye nafasi gani?

Heche: Kabla ya mimi kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, nilikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Kamati Kuu ni chombo cha namna gani?

Heche: Kamati Kuu ndiyo chombo cha utendaji cha Baraza Kuu.

Lissu: Wajumbe wa Kamati Kuu wanapatikanaje?

Heche: Mwenyekiti wa Chama Taifa, Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu ambao ni Bara na Zanzibar, wanaochaguliwa kwa nafasi zao.

Wenyeviti wa Mabaraza:

Mwenyekiti wa BAWACHA,
Mwenyekiti wa BAVICHA,
Mwenyekiti wa BAZECHA.

Wenyeviti wa Kanda.

Kuna Kanda 10, ambazo 8 kutoka Bara na 2 kutoka Zanzibar.

Wajumbe wanaochaguliwa na Baraza Kuu la Chama.

Na wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Lissu: Kwa ufahamu wako, wajumbe wa Kamati Kuu ni wangapi?

Heche: Kuna watano wa Baraza Kuu, watano wa Mwenyekiti.

Kuna 10 wa Kanda.

Kuna wanaoingia kwa nafasi zao 6.

Na wajumbe 3 ambao kwa nafasi zao.

Na kuna Sekretarieti ambao siyo wapiga kura.

Kwa hiyo, wapo jumla 29.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji majukumu ya Kamati Kuu.

Heche:

1. Kusimamia Sekretarieti ya Chama Taifa, ambacho ndiyo chombo cha utendaji wa kila siku.

2. Kufanya vikao na maamuzi ya vikao ya mambo yanayojitokeza mara kwa mara.

3. Kusimamia shughuli za utendaji wa chama.

4. Kupitia mihutasari ya nyuma na kuidhinisha.

5. Kupanga vikao vya Baraza Kuu la Chama.

6. Kupitisha ajenda zinazoenda katika Baraza Kuu la Chama.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, umekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama kwa wakati gani?

Heche: Nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama kwa miaka 15, tangu mwaka 2011.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Leo hakuna jipya
Mh Lissu na Shemeji yake wapo kwenye kama matani yenye ukweli

Ngoma nzito kwanzia Kesho au kesho kutwa pale Heche wakikutana na kina Katuga nk✍️
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nafasi zingine za chama ulizowahi kushikilia.

Heche: Nimekuwa Mwenyekiti wa Tawi wa CHADEMA Students Organization (CHASO).

Lissu: Tawi gani?

Heche: Tawi la SAUTI Mwanza, tangu 2006 hadi 2009.

Lissu: SAUTI ni kitu gani?

Heche: St. Augustine University of Tanzania.

Lissu: Nafasi nyingine?

Heche: Nimekuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa (BAVICHA), mwaka 2011 mpaka 2014, nafasi ambayo ilinipa ujumbe wa Kamati Kuu.

Nimekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, mwaka 2016 mpaka 2019, nafasi ambayo ilifanya niwe Mjumbe wa Kamati Kuu.

Lissu: Kanda ya Serengeti ni kitu gani?

Heche: Ni Kanda yenye mikoa mitatu: Mkoa wa Mara, Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa Simiyu.

Nimekuwa Diwani wa Tarime.

Lissu: Nilikuwa nakuja huko, usinitangulie.

Heche: Sawa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nafasi yako ya uongozi nje ya chama.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nimewahi kuwa Diwani wa kuchaguliwa katika uchaguzi mdogo wa marudio mwaka 2008.

Baada ya Mbunge na Diwani kufariki, niligombea na kuchaguliwa kuwa Diwani wa Tarime Mjini.

For the record, nilichaguliwa nikiwa bado mwanafunzi wa chuo kikuu.

Lissu: Chuo gani? (Usidhani kwamba watu wanafahamu mambo yenu.)

Heche: Nilikuwa bado mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine, Mwanza.

Vilevile, nimekuwa Mbunge kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020.

Lissu: Kuna nafasi zingine za uongozi ambazo ungependa Majaji wazifahamu?

Heche: Nikiwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa, nilikuwa Mjumbe wa Bodi wa International Democratic Union, tangu nikiwa Mwenyekiti wa Vijana mpaka nilipomaliza.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Kitanzi kimekaribia

Uyu anaweza kufungwa Maisha Sababu kosa lake lipo kwenye kukusudia kutenda Uhaini limebaki apo✅️

Kama Jamhuri isingeshindwa kwenye kesi Mahakama y Rufaa kwenye ule mpango wa kuongeza Ushahidi mpya wa Mo29

mh Lissu yumkin angenyongwa kwa %80
 
Uyu anaweza kufungwa Maisha Sababu kosa lake lipo kwenye kukusudia kutenda Uhaini limebaki apo✅️

Kama Jamhuri isingeshindwa kwenye kesi Marekani ya Rufaa kwenye ule mpango wa kuongeza Ushahidi mpya wa Mo29

mh Lissu yumkin Angenyongwa kwa %80

..kivipi?

..kitu gani kinathibitisha kukusudia kutenda uhaini?

..hata Dudu Baya juzi alivyotoka kwa Katambi aliposti anakwenda kukinukisha.
 
Back
Top Bottom