Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 5.

Lissu: Sasa shahidi, nimekuita uje utoe ushahidi katika kesi ambayo nimeshtakiwa nayo. Nataka uwaeleze Waheshimiwa Majaji, palikuwa na kitu gani tarehe 03 Aprili mwaka jana?

Heche: Waheshimiwa Majaji, tarehe 03 Aprili mwaka jana palikuwa na kikao cha watia nia (aspirants), yaani wanaotaka kugombea kupitia chama chetu.

Lissu: Lengo la huo mkutano wa watia nia lilikuwa ni nini?

Heche: Ilikuwa ni kuwaeleza kuhusu msimamo wa chama kwamba, bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Nia ilikuwa ni kuwaelimisha kwa nini chama kimechukua msimamo huo uliowekwa katika vikao vilivyotangulia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hivyo vikao ambavyo vilikuwa vimetangulia ni vikao gani na tarehe zake, kama unakumbuka?

Heche: Waheshimiwa Majaji, mimi kama nilivyosema nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Nilikwepo katika vikao baada ya uchaguzi wa vitongoji, vijiji na serikali za mitaa wa mwaka 2024 kuharibiwa kwa nchi nzima, kwa wagombea wa CHADEMA kuenguliwa massively kwa nchi nzima.

Karibu asilimia 80.

Kulikuwa na watu kuuawa, kama Manyoni, ambapo mgombea wetu aliuawa, na Dar es Salaam hapa.

Lissu: Kitu gani kilitokea?

Heche: Chama kilikutana chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe, tarehe 03 Desemba 2024.

Tukajadili kilichojitokeza katika uchaguzi, tukaibaini kwamba ule haukuwa uchaguzi bali uchafuzi na mauaji.

Na hapo chama kikakutana na kuazimia, tukapitisha msimamo wa “No Reforms, No Election.”

Lissu: Umesema Kiswahili chake cha “No Reforms, No Election” ni nini?

Heche: Bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ni mabadiliko gani Kamati Kuu ilisema yasipofanyika hakuna uchaguzi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Kamati Kuu iliazimia mabadiliko makubwa ya Kikatiba na kisheria.

Kuondoa mamlaka makubwa ya Rais.

Kuunda Tume ya Uchaguzi ambayo anateua Mwenyekiti, Wajumbe na Wakurugenzi, ambapo yeye ni mgombea na hapo hapo anaunda tume.

Kama vile Simba wanacheza na Yanga, halafu Simba wanatoa refa.

Lissu: Nchi hii ina tume nyingi. Tunazungumzia tume ipi?

Heche: Tume huru ya Uchaguzi ambayo haitakuwa na upendeleo wakati wa uchaguzi kwa mgombea mmoja wapo.

Lissu: Nakukumbusha usinitangulie.

Jaji Ndunguru: Mkumbushe.

MAHAKAMA: Kicheko.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uzoefu wako wewe na matatizo ya nchi hii.

Heche: Waheshimiwa Majaji, kama nilivyoeleza awali, nimegombea na nimekuwa Diwani na nimekuwa Mbunge katika chaguzi za nchi hii.

Na vilevile nimeshiriki kampeni katika maeneo mbalimbali ya nchi, kama uchaguzi mdogo wa Arumeru, uchaguzi wa Busanda/Geita, uchaguzi wa Igunga, uchaguzi wa Kinondoni mwaka 2018.

Nimeshiriki chaguzi za kugombea Ubunge mwaka 2015 na 2020.

Chaguzi zote hizo, Waheshimiwa Majaji, ziliambatana na maumivu makubwa:

  • Mauaji.
  • Kuenguliwa kwa wagombea wetu.
  • Kunyimwa fomu za viapo vya mawakala wetu.
  • Kuondolewa kwenye vituo wakati zoezi linaendelea.
  • Ratiba zetu kuingiliwa na Polisi.
  • Watu kupigwa katika mikutano ya kampeni.
  • Wagombea wetu kunyimwa fomu za matokeo.
  • Kura kuingizwa na Polisi na Migambo vituoni, ambao wanatakiwa kusimamia uchaguzi.
  • Wagombea wetu kuenguliwa kwa sababu za ovyo, kama kuambiwa wameshindwa kusoma na kuandika au kujaza fomu.

Nitaanza moja kwa moja na mauaji ambayo nimeshuhudia katika uchaguzi.

Katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki, alipokuwa anagombea Joshua Nasari—

Lissu: Kitu gani kilitokea?

Heche: Aliuawa Katibu wetu wa Kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo, kwa kukatwa na chain saw shingoni kutokea nyuma. (Anaonyesha kwa mkono.)

Aliuawa na watu waliokuwa wanasadikika kuwa ni wanachama wa CCM.

Na mpaka sasa hakuna mtu aliye kamatwa na Jeshi la Polisi wala aliyefungwa kwa mauaji hayo.

Lissu: Tukio lingine?

Heche: Hapa Kinondoni, aliuawa Katibu wa Kata ya Hananasifu wa CHADEMA anayeitwa Daniel Yona.

Vilevile, hakuna uchunguzi wala mtu aliyewahi kukamatwa.

Vilevile, Waheshimiwa Majaji, kama nilivyosema, tulipokuwa tunafuatilia viapo vya mawakala wetu katika uchaguzi wa Kinondoni, Februari 2018—

Kwa sababu hizohizo za wazi za upendeleo, tulipokuwa tunafuatilia kwa Mkurugenzi Kagulumjuli viapo vyetu—

Lissu: Kinondoni ni nini? Alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni?

Heche: Ndiyo.

Tulipokuwa tunafuatilia, tulishambuliwa na Polisi kwa risasi.

Baadhi ya wanachama wetu walijeruhiwa vibaya.

Katika kushambuliwa huko, aliuawa mwanafunzi anayeitwa Akwilina Akwelini kwa kupigwa risasi.

Baadaye aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mambosasa, alithibitisha hilo.

Hakuna askari Polisi aliyekamatwa wala kushitakiwa.

Tulishtakiwa sisi:

Mimi, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa wakati huo; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu; Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu; Peter Msigwa, aliyekuwa Mbunge wa Iringa.

Lissu: Kuna Jimbo la Iringa?

Heche: Iringa Mjini.

Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Halima Mdee, aliyekuwa Mbunge wa Kawe; Esther Matiko, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Mjini; na Salum Mwalimu, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Heche na Lissu wapo out of context.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 6.

Lissu: Kwa hiyo, shahidi, kama nimekuelewa, Mwenyekiti wa chama na Mbunge ameshtakiwa, Katibu Mkuu ameshtakiwa.

Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge ameshtakiwa, na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ameshtakiwa.

Na Wabunge wanne wameshtakiwa.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, mlishtakiwa kwa kosa gani na kesi iliishia wapi?

Heche: Hao wote walioshtakiwa ni viongozi wakuu wa chama na Wabunge.

Na wote ni Wajumbe wa Kamati Kuu.

Tulishitakiwa kwa makosa tofauti tofauti.

Kuna mtu alikuwa na kaunti nne za mashtaka, na zilitofautiana tofauti.

Uchochezi, kusanyiko lisilo na kibali.

Lissu: Kabla sijaisahau, waeleze Waheshimiwa Majaji hiyo kadhia ilikuwaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, kama mnavyojua—

Lissu: Hawajui.

Heche: Waheshimiwa Majaji, wakati huo Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu wa sasa, alikuwa ameshambuliwa sana Bungeni.

Kwa hiyo, alikuwa anapata matibabu nje ya nchi.

Wakati huo alikuwa ni Makamu Mwenyekiti—mmmhh, no—Mwanasheria Mkuu wa chama.

Kilichosababisha asiwe na sisi ni kwa sababu alikuwa katika matibabu nje ya nchi baada ya kushambuliwa mwaka 2017.

Lissu: Uamuzi wa hiyo kesi ulikuwaje?

Heche: Uamuzi wa hiyo kesi, tulifungwa kwa miezi sita na kulipishwa faini.

Kwa mfano, mimi nililipishwa milioni 40, lakini jumla ya wote ilikuwa zaidi ya milioni 310.

Tuko Live mkuu… kazi nzuri
 
Nafikiri Tanzania kwa mara ya kwanza rais anaweza akajiuzuru, nimesema nafikiri uenda rais akajiuzuru kabla hizi siku 90 hazijaisha
Abdul akisoma hapa atakucheka sana, mwenzako anafanya vikao vya uwekezaji na Museven wewe unafikiria Mama yake ajiuzuru?
Thubutu.

Wenzako wanaandaa mrithi wao wa 2030 ndio sarakasi zote hizi.

Subiri uchaguzi wa ndani wa Ccm 2027 ndio utaelewa somo.
 
Kawaida ya wapumbavu kujiona welevu.
20250722_160219.jpg
20250719_192454.jpg
20250524_222118.jpg
downloadfile-17.jpg

Unaona majinga haya.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 7.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ilikuwa katika Mahakama gani hiyo?

Heche: Ilikuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ikisikilizwa na Hakimu aliyekuwa anaitwa Mashauri, ambaye baadaye akaja kupanda kuwa Jaji.

Lissu: Baada ya kuhukumiwa, kitu gani kilifuata?

Heche: Tulikata rufaa katika Mahakama Kuu na ile hukumu ikatupiliwa mbali.

Na tuliamuliwa kurudishiwa fedha zetu ambazo mpaka sasa sijawahi kurudishiwa.

Nimefanya juhudi zote nirudishiwe milioni 40 zangu, lakini ni kama nimedhulumiwa, japo Mahakama Kuu ilishatoa amri.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ni Jaji gani wa Mahakama Kuu alitoa hiyo hukumu, kama unamkumbuka?

Heche: Jaji Mgeta, Waheshimiwa.

Lissu: Sasa shahidi, unakumbuka ulisema kulikuwa na mauaji ya Akwelina Akwilini. Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo habari ya mauaji ya Akwelina Akwilini iliishia wapi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, iliishia hapo baada ya sisi kufungwa, lakini hakuna Polisi yeyote aliyekamatwa wala kushitakiwa au kufungwa kwa mauaji yaliyofanyika kipindi hicho.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nilikuwa naendelea na mauaji ya wakati wa uchaguzi.

Wakati mimi nagombea Ubunge mwaka 2015, wakati naenda kufanya kampeni kwenye Kijiji cha Nyanungu, Tarime Vijijini, mwaka 2015, tulishambuliwa na akauawa Bwana Bhoke Mwita Weitei.

Lissu: Mlishambuliwa na watu gani?

Heche: Tulishambuliwa na wafuasi wa CCM ambao walikamatwa na baadaye kesi ilifunguliwa, wakaachiwa, na kesho yake ikaharibiwa. Haikuendelea, ikaisha.

Lissu: Ukisema kesi ilifunguliwa na baadaye wakaachiwa, unamaanisha nini?

Heche: Walikamatwa kwa sababu wanafahamika pale kijijini.

Walikaa Magereza na baadaye kuachiwa, na kesi haikuendelea.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwenye uchaguzi huo wa mwaka 2015, kitu gani kilitokea katika uchaguzi wa Busanda?

Heche: Mwaka huo huo 2015, Jimbo la Busanda, aliuawa Kiongozi wetu Alphonce Chemiu Mawazo.

Ambaye alikuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Busanda.

Waheshimiwa Majaji, tukio hilo hata kumzika kwake ilibidi tu-contest Mahakamani ili tuweze kumuaga katika viwanja vya wazi, huku mwili ukiwa hospitalini.

Ndipo baadaye tukaruhusiwa na Jaji kumuaga, na baadaye tukaenda kumuaga kijijini kwao.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, huyo Alphonce Mawazo alikuwa na cheo gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Alphonce Mawazo alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita wa CHADEMA na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika na mauaji ya Alphonce Mawazo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hiyo kesi sikumbuki vizuri mwisho wake, kwa hiyo siwezi kuieleza vizuri.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom