Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Heche Dadake ndio Mke wa Mwenyekiti wa Chadema mh Lissu

Ndiomana kwasasa ndani ya Chadema Mh Heche yupo juu na anaogopwa na wenzake pale Chadema

Si umeona upendeleo yeye kuwekwa baada ya wenzie ili Shemeji Heche ajifunze kwa wenzake ✅️

Ukiwa na Dada mjini ni fursa 😂

Lissu ameoa Mkurya wa Tarime.
Na Heche ni Mkurya wa Tarime.

Kwahiyo ushemeji wao umejengwa
kwa hilo na sio Kishemeji kwamba Dada wa Heche ndio mke wa Lissu.

Ni kama Ww uoe mchaga. Kwahiyo wachaga wote watakuwa mashemeji zako.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 7.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ilikuwa katika Mahakama gani hiyo?

Heche: Ilikuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ikisikilizwa na Hakimu aliyekuwa anaitwa Mashauri, ambaye baadaye akaja kupanda kuwa Jaji.

Lissu: Baada ya kuhukumiwa, kitu gani kilifuata?

Heche: Tulikata rufaa katika Mahakama Kuu na ile hukumu ikatupiliwa mbali.

Na tuliamuliwa kurudishiwa fedha zetu ambazo mpaka sasa sijawahi kurudishiwa.

Nimefanya juhudi zote nirudishiwe milioni 40 zangu, lakini ni kama nimedhulumiwa, japo Mahakama Kuu ilishatoa amri.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ni Jaji gani wa Mahakama Kuu alitoa hiyo hukumu, kama unamkumbuka?

Heche: Jaji Mgeta, Waheshimiwa.

Lissu: Sasa shahidi, unakumbuka ulisema kulikuwa na mauaji ya Akwelina Akwilini. Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo habari ya mauaji ya Akwelina Akwilini iliishia wapi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, iliishia hapo baada ya sisi kufungwa, lakini hakuna Polisi yeyote aliyekamatwa wala kushitakiwa au kufungwa kwa mauaji yaliyofanyika kipindi hicho.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nilikuwa naendelea na mauaji ya wakati wa uchaguzi.

Wakati mimi nagombea Ubunge mwaka 2015, wakati naenda kufanya kampeni kwenye Kijiji cha Nyanungu, Tarime Vijijini, mwaka 2015, tulishambuliwa na akauawa Bwana Bhoke Mwita Weitei.

Lissu: Mlishambuliwa na watu gani?

Heche: Tulishambuliwa na wafuasi wa CCM ambao walikamatwa na baadaye kesi ilifunguliwa, wakaachiwa, na kesho yake ikaharibiwa. Haikuendelea, ikaisha.

Lissu: Ukisema kesi ilifunguliwa na baadaye wakaachiwa, unamaanisha nini?

Heche: Walikamatwa kwa sababu wanafahamika pale kijijini.

Walikaa Magereza na baadaye kuachiwa, na kesi haikuendelea.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwenye uchaguzi huo wa mwaka 2015, kitu gani kilitokea katika uchaguzi wa Busanda?

Heche: Mwaka huo huo 2015, Jimbo la Busanda, aliuawa Kiongozi wetu Alphonce Chemiu Mawazo.

Ambaye alikuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Busanda.

Waheshimiwa Majaji, tukio hilo hata kumzika kwake ilibidi tu-contest Mahakamani ili tuweze kumuaga katika viwanja vya wazi, huku mwili ukiwa hospitalini.

Ndipo baadaye tukaruhusiwa na Jaji kumuaga, na baadaye tukaenda kumuaga kijijini kwao.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, huyo Alphonce Mawazo alikuwa na cheo gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Alphonce Mawazo alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita wa CHADEMA na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika na mauaji ya Alphonce Mawazo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hiyo kesi sikumbuki vizuri mwisho wake, kwa hiyo siwezi kuieleza vizuri.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Wagesa anathibitisha hapa ni kwa kiasi gani amri za mahakama hazitekelezwi wala kuheshimiwa.
Re; amri ya mahakama kuu warudushiwe pesa zao kutoka kwa kesi ya Aqulina.

Isipokua mahakama ndo zinapokea amri kutoka kwa watawala.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 8.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kilitokea jimboni kwako Tarime katika Uchaguzi Mkuu 2020?

Heche: Waheshimiwa Majaji, mwaka 2020 wakati wa kufunga kampeni Nyamongo, Kata ya Matongo, tulivamiwa na kushambuliwa kwa risasi. Waliuawa watu wawili na wengi kujeruhiwa.

Aliuawa Bwana Chacha Isangora na Chacha Ngabya.

Waheshimiwa Majaji, wote waliowashambulia hawa mabwana ni watu wanaofahamika. Walikamatwa na maganda ya risasi za silaha zao yalikutwa pale.

Ni viongozi wa CCM na mwingine alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji.

Maganda ya risasi yakachukuliwa na Polisi.

Wakashikiliwa, lakini baadaye wakaachiwa.

Wote hao waliuawa kutokana na mambo ya kiuchaguzi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo kuna tukio lingine la uchaguzi katika jimbo lako la uchaguzi.

Heche: Matukio ya uchaguzi hapana, lakini kwenye siasa hizi hizi Polisi walimuua mdogo wangu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ilikuwaje.

Heche: Waheshimiwa Majaji, mdogo wangu anaitwa Suguta Heche.

Alikamatwa na Polisi, akafungwa pingu hivi mikononi kwa nyuma.

Alikamatwa eneo la Sirari mwaka 2018, akachomwa kisu akiwa amefungwa pingu kwa nyuma.

Baadaye walifanya attempt ya kwenda kumtupa kama vile mtu aliyepata ajali au ameshambuliwa na watu wasiojulikana.

Walinzi wa usiku eneo walilotaka kumtupa wakawaona.

Walirudi naye kituo cha Polisi.

RPC wa wakati huo alitoa taarifa kwa umma kwamba mdogo wangu aliuawa na Polisi na akaahidi kuwa huyo aliyemuua atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, ambaye ni Polisi.

Baadaye huyu mtu aliachiliwa na akahamishwa kituo, na mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.

Mimi naamini mauaji yale yalifanywa kwa ajili ya kunikomoa.

Na ameuawa kwa sababu ya misimamo yangu ya kisiasa ya kupinga maovu ya Serikali hii, kama sehemu ya kunitisha waziwazi.

Na kama njia ya kuniambia kwamba kama mdogo wako ameuawa, hata wewe tunaweza kukufanyia kitu chochote na hatua zisichukuliwe.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, imeshafika saa 11 na dakika kadhaa hivi. Naomba nikuulize maswali mawili ya mwisho ya leo, halafu tuhairishe.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 nilipokuja kwenye uchaguzi Mkuu jimboni kwako, Nyamongo, Tarime, kitu gani kilitokea?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Tundu Lissu alikuwa ni Mgombea wa Urais 2020.

Siku ya kwanza tulifanya naye mikutano Kata ya Sirari na Tarime Mjini.

Kesho yake tulipaswa kufanya mkutano Kata ya Matongo, Nyamongo.

Tulipofika kwenye junction ya kwenda Nyamongo, Matongo, kwenye eneo linaitwa Kewanja, Polisi walituzuia pale eneo la Matongo kwa kutupiga mabomu ya machozi.

Watu waliumia sana. Vyombo vya usafiri kama magari viliharibiwa sana.

Watu waliumizwa sana na baadaye wananchi walionyesha resistance, wakaturuhusu tuendelee na mkutano ambao ulifanyika kwa amani.

Polisi walikuwa na lengo ya kuwatawanya wananchi wasije kutusikiliza.

Kwa imani yao, baada ya harassment hiyo walitegemea watu watakimbia kwa vitisho.

Bahati nzuri ilikuwa ni Tarime, siyo rahisi watu kutawanyika kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Watu walikuwa determined kuja kumsikiliza Mgombea wa Urais.

Waheshimiwa Majaji, tangu vyama vingi vianzishwe, haijawahi kutokea kwa Mgombea wa CCM kufanyiwa hivyo vya kuvurugiwa mikutano yao.

Lissu: Siku ya Uchaguzi 2020, Jimbo la Rorya, kilitokea kitu gani?

Heche: Siku ya Uchaguzi 2020, Jimbo la Rorya, alipokuwa anagombea Ezekiah Wenje ubunge Jimbo la Rorya kupitia CHADEMA, walivamiwa wakiwa nyumbani kwao Shirati na Polisi, walishambuliwa na ndugu Nyatega Wenje akauawa.

Nyatega Wenje ni ndugu yake Bwana Ezekiah Wenje.

Lissu: Yeye Ezekiah Wenje, Mgombea, kitu gani kilimtokea?

Heche: Waheshimiwa Majaji, katika hilo tukio Bwana Ezekiah Wenje alinusurika kuuawa, akakimbia Kenya na baadaye uhamishisho Canada.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna kumbukumbu zozote juu ya hatua zilizochukuliwa juu ya Nyatega Wenje.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu za hatua zozote zilizochukuliwa juu ya wauaji wa Nyatega Wenje.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Ni mpumbavu tu anaweza shupaza shingo. Kote Duniani sheria zilitungwa kuweza kuilinda state.
Depends on what you mean by "state", but going by your own inclinations that you have vividly shown in these discussions; your "state" utterly different from the real state, that is the collective people of a given nation.
 
Depends on what you mean by "state", but going by your own inclinations that you have vividly shown in these discussions; your "state" utterly different from the real state, that is the collective people of a given nation.
Mzee hayo unaandikwa kwa hisia, huku ukiongozwa na upumbavu. Only idiot yupo na akili kama zako
 
MAHAKAMA INAISHIA HAPA KWA LEO.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nimemaliza ya leo.

Naomba tuhairishe mpaka kesho tuendelee na examination in chief.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnasemaje?

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, ni sawa tuhairishe mpaka kesho.

MAJAJI WANATETA

Jaji Ndunguru: Kwa kuwa muda umeenda, shauri linahairishwa hadi kesho saa 3 asubuhi.

Uamuzi tutausoma kesho asubuhi.

Shahidi, utaendelea kutoa ushahidi. Unakumbushwa upo chini ya kiapo, utatakiwa kuwepo kesho saa 3 asubuhi.

MAJAJI WANATOKA

TUKUTANE KESHO ASUBUHI.
 
Mzee hayo unaandikwa kwa hisia, huku ukiongozwa na upumbavu. Only idiot yupo na akili kama zako
Nilikwambia wewe ni chizi mmoja tu ambaye bangi za utotoni zilikuharibu akili; sasa unakuja hapa JF kudhihirisha hali yako hiyo mbovu.
Hakuna atakayekusaidia wewe, wala huyo Samia unayempigania katika uchizi wako.. She's a cooked goose!
 
Nilikwambia wewe ni chizi mmoja tu ambaye bangi za utotoni zilikuharibu akili; sasa unakuja hapa JF kudhihirisha hali yako hiyo mbovu.
Hakuna atakayekusaidia wewe, wala huyo Samia unayempigania katika uchizi wako.. She's a cooked goose!
Umeandika maneno mengi but ulichoandika ni zero.
Huwezi ukatulazimisha watanzania zaidi ya 70m, tufuate unachoamini. Fuata yako na sisi tutafuata yetu
 
MAHAKAMA INAISHIA HAPA KWA LEO.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nimemaliza ya leo.

Naomba tuhairishe mpaka kesho tuendelee na examination in chief.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnasemaje?

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, ni sawa tuhairishe mpaka kesho.

MAJAJI WANATETA

Jaji Ndunguru: Kwa kuwa muda umeenda, shauri linahairishwa hadi kesho saa 3 asubuhi.

Uamuzi tutausoma kesho asubuhi.

Shahidi, utaendelea kutoa ushahidi. Unakumbushwa upo chini ya kiapo, utatakiwa kuwepo kesho saa 3 asubuhi.

MAJAJI WANATOKA

TUKUTANE KESHO ASUBUHI.
Tunasubiri uamuzi wa kesho asubuhi.

Mara paaah DPP hana nia ya kuendelea na kesi hii.
Unpredictable
 
Back
Top Bottom