Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Iwafikie wale machawa, mbogamboga. Waone Ni kwa namna gani, hii nchi imeharibika. Yaani hata maamuzi ya mahakama yanadharaulika.
 
Tatizo hajui Sheria
So tegemea vituko kutoka kwake sio chengine
Pale sio jukwaa la Siasa kukusanya tone tone ✍️
Mkuu kwani Heche anaenda mahakamani kama mwanasheria wa Lissu au shahidi wa Lissu?
Mbona huku Jf kuna vilaza sana aisee??
 
Tatizo lako ni heat period inakusumbua. Unbalazimisha watu wote duniani wawaze kama wewe. Fala kabisa
Hiyo "heat period" ndio kitu gani hicho!
Ninapokwambia wewe ni chizi mvuta bangi usifikiri nakuonea tu bila ya sababu..
Dalili zote zinaonyesha wewe ni mwathirika.
 
Hiyo "heat period" ndio kitu gani hicho!
Ninapokwambia wewe ni chizi mvuta bangi usifikiri nakuonea tu bila ya sababu..
Dalili zote zinaonyesha wewe ni mwathirika.
heat period ni nyege kali zinazofanya uwe na hisia kali na usitumie akili.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 8.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kilitokea jimboni kwako Tarime katika Uchaguzi Mkuu 2020?

Heche: Waheshimiwa Majaji, mwaka 2020 wakati wa kufunga kampeni Nyamongo, Kata ya Matongo, tulivamiwa na kushambuliwa kwa risasi. Waliuawa watu wawili na wengi kujeruhiwa.

Aliuawa Bwana Chacha Isangora na Chacha Ngabya.

Waheshimiwa Majaji, wote waliowashambulia hawa mabwana ni watu wanaofahamika. Walikamatwa na maganda ya risasi za silaha zao yalikutwa pale.

Ni viongozi wa CCM na mwingine alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji.

Maganda ya risasi yakachukuliwa na Polisi.

Wakashikiliwa, lakini baadaye wakaachiwa.

Wote hao waliuawa kutokana na mambo ya kiuchaguzi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo kuna tukio lingine la uchaguzi katika jimbo lako la uchaguzi.

Heche: Matukio ya uchaguzi hapana, lakini kwenye siasa hizi hizi Polisi walimuua mdogo wangu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ilikuwaje.

Heche: Waheshimiwa Majaji, mdogo wangu anaitwa Suguta Heche.

Alikamatwa na Polisi, akafungwa pingu hivi mikononi kwa nyuma.

Alikamatwa eneo la Sirari mwaka 2018, akachomwa kisu akiwa amefungwa pingu kwa nyuma.

Baadaye walifanya attempt ya kwenda kumtupa kama vile mtu aliyepata ajali au ameshambuliwa na watu wasiojulikana.

Walinzi wa usiku eneo walilotaka kumtupa wakawaona.

Walirudi naye kituo cha Polisi.

RPC wa wakati huo alitoa taarifa kwa umma kwamba mdogo wangu aliuawa na Polisi na akaahidi kuwa huyo aliyemuua atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, ambaye ni Polisi.

Baadaye huyu mtu aliachiliwa na akahamishwa kituo, na mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.

Mimi naamini mauaji yale yalifanywa kwa ajili ya kunikomoa.

Na ameuawa kwa sababu ya misimamo yangu ya kisiasa ya kupinga maovu ya Serikali hii, kama sehemu ya kunitisha waziwazi.

Na kama njia ya kuniambia kwamba kama mdogo wako ameuawa, hata wewe tunaweza kukufanyia kitu chochote na hatua zisichukuliwe.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, imeshafika saa 11 na dakika kadhaa hivi. Naomba nikuulize maswali mawili ya mwisho ya leo, halafu tuhairishe.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 nilipokuja kwenye uchaguzi Mkuu jimboni kwako, Nyamongo, Tarime, kitu gani kilitokea?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Tundu Lissu alikuwa ni Mgombea wa Urais 2020.

Siku ya kwanza tulifanya naye mikutano Kata ya Sirari na Tarime Mjini.

Kesho yake tulipaswa kufanya mkutano Kata ya Matongo, Nyamongo.

Tulipofika kwenye junction ya kwenda Nyamongo, Matongo, kwenye eneo linaitwa Kewanja, Polisi walituzuia pale eneo la Matongo kwa kutupiga mabomu ya machozi.

Watu waliumia sana. Vyombo vya usafiri kama magari viliharibiwa sana.

Watu waliumizwa sana na baadaye wananchi walionyesha resistance, wakaturuhusu tuendelee na mkutano ambao ulifanyika kwa amani.

Polisi walikuwa na lengo ya kuwatawanya wananchi wasije kutusikiliza.

Kwa imani yao, baada ya harassment hiyo walitegemea watu watakimbia kwa vitisho.

Bahati nzuri ilikuwa ni Tarime, siyo rahisi watu kutawanyika kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Watu walikuwa determined kuja kumsikiliza Mgombea wa Urais.

Waheshimiwa Majaji, tangu vyama vingi vianzishwe, haijawahi kutokea kwa Mgombea wa CCM kufanyiwa hivyo vya kuvurugiwa mikutano yao.

Lissu: Siku ya Uchaguzi 2020, Jimbo la Rorya, kilitokea kitu gani?

Heche: Siku ya Uchaguzi 2020, Jimbo la Rorya, alipokuwa anagombea Ezekiah Wenje ubunge Jimbo la Rorya kupitia CHADEMA, walivamiwa wakiwa nyumbani kwao Shirati na Polisi, walishambuliwa na ndugu Nyatega Wenje akauawa.

Nyatega Wenje ni ndugu yake Bwana Ezekiah Wenje.

Lissu: Yeye Ezekiah Wenje, Mgombea, kitu gani kilimtokea?

Heche: Waheshimiwa Majaji, katika hilo tukio Bwana Ezekiah Wenje alinusurika kuuawa, akakimbia Kenya na baadaye uhamishisho Canada.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna kumbukumbu zozote juu ya hatua zilizochukuliwa juu ya Nyatega Wenje.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu za hatua zozote zilizochukuliwa juu ya wauaji wa Nyatega Wenje.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Vyombo vya Ulinzi vinatumika kama toilet paper
 
Wamefika wawili, brenda na golugwa wamempiga mwenzao kitanzi....lakini kwa sababu tunapenda mihemko ya uanaharakati basi tutapinga
Mkuu... Ngoja nikupe mwanga kidogo..

Sijui kama unaifuatilia hii kesi,
Unakumbuka mwezi February Jamuhuri ilitaka kuongeza ushahidi Mpya wa mtu anaitwa Mahamba, Mahakama ikakataa

Huyu Mahamba ndiye Moja ya Wapelelezi wakubwa wa October 29 na alikuwa na full report ya mambo yaliyotokea

Sasa Mahakama huangalia ushahidi uliopo mbele ya Majaji na sio vyombo vya habari...

Sasa maswali ya Katuga sijui Kuvuruga Uchaguzi kwa kukata vidole, Kuchoma karatasi za kura.. Brenda alikuwa anajua na timu ya Mawakili wa CHADEMA walikuwa wanajua...wewe jibu NDIO

Sasa Majaji wataangalia haya maswali ya kuchoma kura, kukata vidole yanatokea wapi ? Mbona hatuna ushahidi huo Mahakamani ...na Ushahidi huo ukiwepo lazima uwe na muunganiko kwamba Lissu amefanya

Kama report ya Amin Mahamba ingekubaliwa Mahakamani ...basi haya maswali ya kuvuruga Uchaguzi , kuchoma moto vituo nk yangekuwa na mantiki katika kesi...

La mwisho kesi hii ni Uhaini na mwendelezo wa kesi ni vitu viwili tofauti...
Yaani bado mambo ya Uhaini hayajatokeza labda tusubiri mashahidi wanaokuja..kama wataongezeka
 
Back
Top Bottom