Ngarob
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,053
- 3,612
Yaani hii kesi Ina maajabu...Brenda kuhusu video alijibu kuwa aliiona lakini alipoulizwa kama mahakamani ililetwa alijibu haikuletwa na prosecution so kupitia ushahidi huo ni wazi kuwa prosecution case has already fallen down long time ago kwasababu ukimuondoa PW 17 wengine wote walieleza kuwa waliona kwenye jambo Tv ambayo video haipo na kwamba hata huyo 17 yeye ndiye aliyeeleza kuwa alichapisha kwenye mtandao wao sasa kwa mazingira hayo ili mahakama ifikie uamuzi ni lazima ijiulize
1. whether the accused published the alleged statement.
2. whether the accused person made statement amounting to treason puersuant to Section 39(2)(d) Penal code cap. 16 R.E. 2023.
Na hapa ndio dhana ya ile video inakuwa muhimu kwani lissu hakatai kutamka maneno hayo lakini anasema yalichukuliwa out of the context kwani maneno yaliyopo kwenye Information ni machache wakati yeye aliongea maneno mengi kwa mukutadha tofauti ndio maana hoja ya lissu ukitaka kujua kuwa yuko smart kila shahidi wake anamuhoji swali kwamba aliongea kwa muda gani ambapo wote wamejibu ni zaidi ya masaa mawili hii ni kumaanisha kwamba video ya Jambo ingekuwepo ndio majaji wangepima dhana mens rea na sio vipande vipande vya kwenye Hati ya mashtaka ambavyo anapowasomea haizidi hata dakika moja wakati yeye aliongea masaa zaidi ya mawili. Mwisho kabisa hata hao mawakili wa Serikali wanapoteza muda tu huku wakijua wameshashindwa kesi na hata ikitokea kwa ujinga akutwa na hatia, hiyo hatia itakuwa kama kesi za akina mbowe ambazo kwenye rufaa ni asubuhi tu kesi anashinda.
NB: Ni kama hivi mtu anasema alinunua shamba na kuandikishana lakini maandishi hajayaleta mahakamani ili kuthibitisha kuwa waliandikishana hivyo hoja ya kwamba alikuwepo kwenye eneo la kuandikishana na alisain inakuwa haina maana yoyote kwasababu maandishi ambayo amesema waliandikishana alipaswa kuyaleta so hata huyo shahidi PW17 aliyerecord na hakuleta recorded video ni sawa na kazi bure maana alipaswa kuileta ili mahakama iamini kuwa kweli kupifanyika publication tofauti na hapo zinabaki story za vijiweni tu.
Ushahidi wote wa Jamuhuri ulikataliwa angalia list
-Video ya Jambo Tv
-Forensic examination ya Video
-Report ya Election violence ya October 29 ya Mahamba
Sasa hii kesi inaendeshwa kwa maneno tuu... Jamuhuri inatoa maneno pamoja na Mashahidi wao
Mshitakiwa na yeye anajitetea hivyo hivyo
Mbaya zaidi kesi inaendeshwa bila kuona viini vya Uhaini