GE2025 Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu yaahirishwa hadi Julai 15 2025

GE2025 Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu yaahirishwa hadi Julai 15 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu inatarajiwa kutajwa leo Julai 1, 2025 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Juni 16, 2025 Kesi hiyo iliahirishwa kutokana na Mawakili wa Serikali, kupitia Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga kuomba ahirisho baada ya kuieleza Mahakama kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP analipitia kisha atatoa taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia na kama kesi hiyo iende Mahakama Kuu au hapana.

Ikumbukwe katika shauri hilo ambalo limekuwa likitajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lissu alitangaza kujitetea mwenyewe akidai kuwa hakuwa hakuna mazingira rafiki ambayo yalikuwa yamemuwezesha kukutana na Mawakili wake ambao walikuwa wakienda Gerezani.

Hata hivyo hivi karibuni ilitolewa taarifa kuwa Lissu amepata fursa ya kuonana na Mawakili wake akiwa Gerezani.

Hii kesi itakuwa Mubashara, kwahiyo kila mmoja atajionea Mwenyewe hoja kabambe.
Kumbuka kwamba kwenye kesi hii Tundu Lissu anajitetea Mwenyewe

Tundu Lissu amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu

Hivi ndivyo Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu alivyofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, John Heche amewaongoza Viongozi wa Chama hicho na mamia ya wanachama wa Chadema na Watanzania kwenye Mahakama ya Kisutu leo July Mosi, 2025 kwaajili ya usikilizwaji wa Kesi ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu ambaye leo hii amefikisha siku 83 akiwa Mahabusu. Miongoni mwa Viongozi walioambatana na Heche ni pamoja na John Mnyika na Amani Golugwa.

Hii kesi nahisi mbowe anahusika. Anataka Lissu anyongwe arudie cheo chake.
 
Mkuu P. Swala la kuachiwa huru mh. Lissu lipo wazi. Kesi za maigizo huisha kimaigizo.

Kuhusu kushiriki maigizo ya kitu kinachoitwa uchaguzi, CDM tumesemaaa, NRNE.

Ona, Mahera anagombea ubunge kupitia CCM.

Ona, hapa Mbeya kuna mtu ameambiwa kuwa kazi yake ni moja tu, kwamba ahakikishe HESHIMA ya dada inabaki. Aiseee! NRNE.
 
Hii kesi wangeiweka iwe kila siku iishe mapema maana hao mashahidi wanachekesha kuliko Comedy zenyewe..
Mfano kuna liaskari lile lilijipigiaga zero form 4 lilisema lenyewe kazi yake ni kufanya surveillance mtandaoni ndio likaona huo uhaini 😂😂😂😂😂, Yan only in Tanzania ndio unaweza pata this type of crap and fvckery...
 
Tanzania tuna tatizo kubwa la watu wengi kutokuona mbali,mypia,wengi wenu ni mypic,hanuoni mbali,na wengine ni just too blind to see!。

Ukisusia kitu,uwe na malengo kuwa unasusia jambo fulani ili kupata kitu fulani au kutimiza lengo fulani。

NRNE was a pressure group with a slogan kupresure reforms ili kuwatisha watawala kuwa bila reforms,mtakinukisha mpaka uchaguzi usifanyike!。

Mamlala zetu zilivyo mamlaka jinga,zikatishika,na kuamua kumhifadhi kinara wa kukinukisha pahala salama kwa kumbambikia kesi mbaya ya uhaini ili kuhalalisha kumshikilia hadi uchaguzi upite!。

Nimesema mamlaka zetu ni mamlaka jinga kwa kumzushia kesi ya uhaini,uhaini sio maneno,uhaini ni matendo, actus reus yenye mens rea ya mipango mkakati kupindua serikali!maneno ni sedition tuu!。

Sasa kwa vile Bunge limeishavinjwa,there is no way kutafanyika reforms yoyote,hivyo sasa ni wakati wa Chadema ku disband NRNE, waingie kwenye uchaguzi na kuchukua nchi kama wameokota!。
P
Neno kukinukisha kwenye kamusi ni nini? Tuanzie hapo.
 
Lakini wewe kizazi chako nahmala kitaona mabadiriko ya kweli.

Wewe endele kuishi kizipezipe
 
Yes na Amsterdam
20250508_130957.jpg
 
Kesi ya lisu inawaponza ccm kila siku. Wanajikwaa kwake na kuanguka. Wangekuwa na uwezo wa kuona mbali wangemwachia huru afanye siasa zake kuliko kumshikilia huku wakizidi kujiweka mahali pabaya. Uliona wapi mtu anapanda cheo akiwa gerezani? Halafu wewe unazidi kumshikilia. Ccm mjitafakari kuna vitu mnalazimisha lakini haviwezi kuwa.
Kweli kabisa,wanadhidi kumpa umaarufu
 
Back
Top Bottom