Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Tulia upate darasa na elimu
 
Huna akili utajuaje haya anayosema
 
Akili za kujua hayo unazo?
 
ndio,
endelea kuifanya kazi yako ndugu mtuhumiwa, ili hatimae na majaji nao waendelea kufanya kazi yao ya kutoa haki bila kuwachelewesha kwa porojo ambazo hazikusaidii 🐒
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA

SEHEMU YA 4.

Lakini, Waheshimiwa Majaji, kipekee kabisa, najulikana ndani na nje ya nchi kwa kupigania maeneo yenye madini kama dhahabu.

Kwa takribani miaka 10, kuanzia mwaka 1996, mimi ndiye nilikuwa nazungumzia masuala ya madini katika nchi hii.

Maeneo ambayo Serikali ya Mkapa iliwapa wawekezaji kutoka nje.

Geita Gold Mining, maelfu ya wananchi waliondolewa kwa nguvu.

Nilikuwapo wakati wanaondolewa.

Bulyanhulu, Agosti mwaka 2002, nilikuwapo wakati palipotokea mauaji, wakati Serikali ya Mkapa inawaondoa wananchi kuwaachia Wakanada.

Ndipo nikapata kesi yangu ya kwanza ya jinai mwaka 2002.

Nilipigania kufanya kampeni ya kudai uchunguzi huru wa kimataifa wa mauaji ya wananchi wa Tanzania nchini Tanzania, Marekani na Canada, everywhere, na nikapata na kesi ya jinai.

Eneo la Dusu, Nzega, palikuwa na mgodi unaitwa Golden Pride Mining wa Australia.

Mimi nilikuwapo kupinga hilo.

Tarime, Nyamongo pia. Na Waheshimiwa Majaji, Tarime ni muhimu sana kwangu, siyo kwa sababu ni kwetu, bali kwa miaka mitatu nilitoa watu 466 gerezani kutoka Gereza la Wilaya Tarime na Gereza la Butimba, Mwanza.

Watu walifungwa bure kwa makosa ya uongo kabisa ili wafungwe watu wapore ardhi yao.

Nilitoa watu 466, akiwemo Marehemu Chacha Wangwe, ambaye baadaye akaja kuwa Mbunge.

Tarime ikanipa kesi ya jinai pia katika wakati wa Serikali ya Jakaya Kikwete.

Baadaye nitaeleza kuhusu hizi kesi.

Buhemba, ambayo sasa ni Wilaya ya Kahama, Butiama, Mererani Wilaya ya Simanjiro, Manyoni, Ikungi Mashariki, Jimboni kwangu.

Kote huko palikuwa na dhahabu, ila ikaja kuwa ni maafa kwa wananchi waliopelekewa hilo mali.

Kila mara panapokuwa na ukandamizaji wa haki za wananchi, nimejitahidi kuwa sehemu ya mapambano ya wananchi hao ya kupinga huo ukandamizaji.

Kauli mbiu yangu, Waheshimiwa Majaji, (my motto): “Upinzani dhidi ya ukandamizaji ni utiifu kwa Mungu” (Resistance to Oppression is obedience to God).

Msimamo wa maisha yangu haya umekuwa na gharama kubwa sana kwangu.

Waheshimiwa Majaji, kesi hii ni kesi ya uhaini, na kama ambavyo nimesema mara nyingi, Waheshimiwa Majaji, kwamba uhaini, kama ulivyotafsiriwa kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu, ndiyo kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 24 ya Katiba yetu).

SHARE UPDATE HIZI ZIFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 5.

Kama mkishawishika na hoja na ushahidi wa Mawakili wa Serikali, ni kifo.

Msisambwe, ooh sijui kuna nini, bali ni kifo. You don't get more serious than this.

Waheshimiwa Majaji, leo nakabiliwa na kesi kubwa kuliko zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hii ni mwendelezo wa kesi nyingi za jinai ambazo nimewekewa na Serikali hii, Polisi na Mawakili wake.

Waheshimiwa Majaji, sina hakika na watu wengine nje ya chama changu CHADEMA.

Lakini ndani ya CHADEMA, mimi ndiye mwanachama na kiongozi ambaye nimeshitakiwa mara nyingi kuliko kiongozi au mwanachama yeyote.

Waheshimiwa Majaji, na kesi zote ambazo nimefunguliwa zimekuwa ni kesi za kisiasa.

Zimetokana na matendo yangu, kauli zangu na misimamo yangu ya kisiasa.

Waheshimiwa Majaji, tuanze na utawala wa Marehemu Rais Mkapa.

Mwaka jana, Waheshimiwa Majaji, wakati wa Christmas, mwanangu mmoja alinitumia ujumbe kwamba:

“Baba, upo gerezani, unatukumbusha kwamba Christmas yetu ya kwanza duniani ulikuwa gerezani.”

Wakati wa Mkapa, nilikamatwa tarehe 23 Desemba 2002, siku mbili kabla ya Christmas, kwa kosa la uchochezi.

Wanazungumza sana uchochezi watu hawa.

Sababu gani?

Kwa kuongoza kampeni ya kudai mauaji ya wananchi wa Bulyanhulu yachunguzwe, baada ya watu zaidi ya 60 kufa.

Kwa kudai mauaji haya yachunguzwe, nikakamatwa nikapelekwa Makao Makuu ya Polisi, Shimoni.

Pale chini kuna gereza linaitwa Shimoni. Pale wanajaza watu, wengine wanakaa miezi.

Kwa bahati nzuri nilikuwa maarufu, wakanipeleka mahakamani siku ya Christmas.

😂😂😂😂😂

Walimpata wapi Hakimu sijui, ila akanisomea mashitaka, akaniambia ondoka hapa.

Uchunguzi ulikuwa miezi 6.

Walioshitakiwa wenzangu walikuwa Augustine Lyatonga Mrema na Dkt. Lugemeleza Nshala, ambaye leo ni Wakili wangu.

Kosa ni kudai uchunguzi wa mauaji ya wananchi.

Miezi 6 wakaifutilia mbali baada ya kukosekana kwa ushahidi. Wakashindwa kuleta mashahidi.

Mwaka 2005 akaingia Jakaya Kikwete.

Waheshimiwa Majaji, nilizungumzia Tarime, ipo karibu sana moyoni mwangu.

Mwaka 2005, Julai, nikiwa Mbunge, Polisi walifanya mauaji eneo la Nyamongo, wakaua watu 3 (wanakijiji).

Nikiwa Bungeni, wananchi wa Nyamongo wakanipigia simu: “Mheshimiwa, inabidi uje. Polisi wameua na wanataka tuzike, tumegome. Njoo.”

Nikaondoka Bungeni, nikaenda Tarime kudai uchunguzi wa mauaji yale ufanyike.

Nilipofika Tarime, tukapata taarifa kwamba Polisi wana mpango wa kutaka kuvunja milango ya chumba cha kuhifadhia maiti ili waibe maiti.

Tukaenda kuweka kambi chumba cha kuhifadhia maiti ili Polisi wasiibe maiti.

Tukapigwa sana. Kuna picha maarufu Polisi wamenichania combat yangu, ila picha ni ya Tarime.

Nikapigwa vibaya sana. Wakanichania combat yangu, tukakamatwa, tukapelekwa kilomita 40 nje ya Tarime. Kesho yake tukashitakiwa kwa criminal trespass.

Nikapelekwa Gereza la Wilaya ya Tarime siku 4. Pale nilipokuwa natoa wenzangu, safari hii nikawa mimi ndiye mfungwa.

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Tulia wewe mdogo wake na nabii tito
okay,
anawataja hata ambao hawamjui na wala hawasaidii chochote kwenye kinachomkabili, dah.

kifo cha nyani ni cha fedheha sana aise, miti yote huteleza 🐒
 

Wewe sio mwanasheria bila shaka, huyo hapo sio Mshitakiwa, kwa sasa ni shahidi, anaeleza anavyomjua mshitakiwa ambaye ni yeye. 😊
Huo ni ushahidi, wewe huwezi kuuona sababu sio mtaalamu wa sheria.
Atafika huko mvumilieni aweke msingi wa ushahidi wake.
 
Mkuu wewe kuwa msomaji tu, ameanza kujitetea kuwa yeye ni mpigania haki tangu zamani, so ni lazima aseme ni haki zipi au harakati zipi aliwahi kuzipigania. Angekuwa ameenda nje ya mada Jaji angemwambia anatoka nje ya mada.

Ishu ya kutaja hivyo vyama ni kujitetea kuwa kisheria hapaswi kuwa pale sababu majopo ya wanasheria nguli mbalimbali na taasisi kubwa za kisheria hazijamuona kuwa yeye ana hatia, so hapaswi kuwa na kesi hadi sasa.

Sasa Mkuu ili tusichoshane embu kuwa msomaji kisha baadae jioni au usiku ndio uanze kuuliza hayo maswali yako.
 
Ni mwanasheria. Yes it make sense. Kuhusu yeye ni nani. Na kwamba ni kawaida yake kubambikiwa kesi.
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…