Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 6

Baadaye, miezi minne upelelezi haujakamilika, Hakimu akaifutilia mbali.

Hiyo ilikuwa kesi ya kwanza wakati wa Kikwete.

Waheshimiwa Majaji, mwaka 2012 Polisi waliua watu wetu katika maandamano jijini Arusha.

Mimi na viongozi tukaenda kushinikiza haki itendeke. Mimi na viongozi wenzangu, Dkt. Slaa, Mustapha Akunaye, Mbunge wa Mbulu, na Said Arfi, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, tukakamatwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali.

Hiyo kesi ikakaa na mashahidi hawakupelekwa, nayo kesi ikafutwa.

Mwaka 2013 palikuwa na chaguzi ndogo za madiwani maeneo mbalimbali, ikiwemo Arusha Mjini.

Mwenyekiti wa CHADEMA wakati huo, Freeman Mbowe, akaenda kufanya mkutano wa kampeni.

Watu wakashambuliwa kwa bomu la mkono na watu kadhaa wakauawa katika mkutano wa kampeni.

Tukarudi tena kuandamana kudai haki itendeke.

Tukakamatwa tena, mimi, Dkt. Slaa na wengineo.

Nilikuwa sijawahi kumuona Mwenyekiti wangu Mbowe akiwa na mbio kama siku hiyo. Yeye alichoropoka. 😂😂😂

Sisi tukashitakiwa kwa kusanyiko lisilo halali.

Polisi, kama kawaida yao, wakatupa mafaili, kesi ikafutwa.

Kwa hiyo, kesi za utawala wa Kikwete ni 3.

Akaingia Magufuli na Samia.

Waheshimiwa Majaji, mwaka 2015 kwenye uchaguzi Mkuu upande wa Zanzibar, Marehemu Sheikh Sharif Hamad alishinda Urais na matokeo yakafutwa na Jecha.

Wakasema patakuwa na uchaguzi wa marudio. Nikahojiwa na waandishi kuhusu uchaguzi wa marudio, nikasema kuwa wanataka kuleta maafa.

Nikakamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi.

Hapa nitarudi nyuma kwa sababu ni muhimu kwa kesi hii.

Aliyenikamata wakati huo alikuwa Senior Superintendent of Police Ramadhani Kingai, leo ndiye...

Majaji: Hebu subiri kidogo.

Mahakama inakaa kimya kidogo, wanaandika.

Waheshimiwa Majaji, nimesema nilikamatwa na Senior Superintendent of Police akiwa Deputy ZCO wa Dar es Salaam.

Waliponikamata, Kingai na wenzake wakanipeleka Central Police, na kabla ya kunipeleka ofisini kwa ZCO, ambaye wakati huo alikuwa Camilius Wambura, ambaye leo ndiye IGP, walinipeleka kwa Wambura kwenda kunitisha kwamba, “Wewe Lissu unajifanya mjanja.”

Nik amwambia Wambura, “Tutakutana mahakamani.”

Kwa hiyo, kesi kwa mara ya kwanza walileta mashahidi, na mmoja ya mashahidi alikuwa Ramadhani Kingai.

Nilipomfanyia cross-examination, hawakuleta shahidi tena mpaka nilipopigwa risasi nikaondoka nchini.

Waheshimiwa Majaji, siku tatu baadaye, tarehe 29 Juni na tarehe 1 Julai, nikakamatwa nikiwa jimboni kwangu Ikungi.

Kwamba nilimuita Magufuli “Dikteta Uchwara.”

Nikakamatwa usiku kwa usiku, nikaletwa Dar es Salaam, na usiku ule nililazwa Chamwino. Pale kuna kituo cha Polisi kina mbu kama nini.

Nikaja kushitakiwa kwa uchochezi.

Around September, tena nikakamatwa nje ya Bunge katika vikao vya Bunge, nikasafirishwa kuletwa Dar es Salaam.

Mwaka umeisha, 2016, nimekamatwa mara 4 na Polisi wa Magufuli na kushtakiwa mahakamani, na mahakama yangu ni Kisutu.

Mwaka 2016 umeisha, nina kesi 4 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Wewe sio mwanasheria bila shaka, huyo hapo sio Mshitakiwa, kwa sasa ni shahidi, anaeleza anavyomjua mshitakiwa ambaye ni yeye. 😊
Huo ni ushahidi, wewe huwezi kuuona sababu sio mtaalamu wa sheria.
Atafika huko mvumilieni aweke msingi wa ushahidi wake.
Mkuu umempiga spana ya kichwa huyo chawa lazima azimie kwanza
 
Kuna sababu nyingi zilizomfanya ajitetee mwenyewe;
1. Kuonesha umahiri wake kwenue sheria! Yeye ni mwanasheria na pia ni wakili msomi.
2. Kutuonesha wananchi na dunia kwa ujumla namna bora ya kupigania haki.
3. Kiwaonesha watesi wake namna alivyo jasiri na shupavu kwenye kupigania kile anachokiamini.
4. Kujiongezea umaarufu wa kisiasa kwa maandalizi ya safari yake ya kuufikia uongozi wa juu kabisa nchini (Urais).

Na kwenye hili, hakika amefanikiwa pamoja na mateso yote anayopitia
Huku mtaani kwa sasa habari ni Lissu tu! Lissu ni Shujaa! Lissu ni mpambanaji wa kweli!, Lissu ni mzalendo kwa nchi yake, Lissu ni mwanasiasa wa kweli, nk. Hakuna cha nani wala nani! Habari ya mjini ni Lissu tu.
Kwenye hili nimekubali Lissu ana akili nyingi sana. Mimi nilidhani ataenda Moja kwa Moja kwenye maneno ya nitakinukisha.
 
Kwenye hili nimekubali Lissu ana akili nyingi sana. Mimi nilidhani ataenda Moja kwa Moja kwenye maneno ya nitakinukisha.
Nilichogundua duniani tumezidiana akili na maarifa. Jamaa kichwani yuko vizuri. Hili halina ubishi. Kwa upande wangu natamani sana siku moja kuongozwa na watu wenye akili nyingi kichwani kama huyu mwamba! Badala ya vilaza ambao hata kujenga hoja tu hawawezi..
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 6

Baadaye, miezi minne upelelezi haujakamilika, Hakimu akaifutilia mbali.

Hiyo ilikuwa kesi ya kwanza wakati wa Kikwete.

Waheshimiwa Majaji, mwaka 2012 Polisi waliua watu wetu katika maandamano jijini Arusha.

Mimi na viongozi tukaenda kushinikiza haki itendeke. Mimi na viongozi wenzangu, Dkt. Slaa, Mustapha Akunaye, Mbunge wa Mbulu, na Said Arfi, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, tukakamatwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali.

Hiyo kesi ikakaa na mashahidi hawakupelekwa, nayo kesi ikafutwa.

Mwaka 2013 palikuwa na chaguzi ndogo za madiwani maeneo mbalimbali, ikiwemo Arusha Mjini.

Mwenyekiti wa CHADEMA wakati huo, Freeman Mbowe, akaenda kufanya mkutano wa kampeni.

Watu wakashambuliwa kwa bomu la mkono na watu kadhaa wakauawa katika mkutano wa kampeni.

Tukarudi tena kuandamana kudai haki itendeke.

Tukakamatwa tena, mimi, Dkt. Slaa na wengineo.

Nilikuwa sijawahi kumuona Mwenyekiti wangu Mbowe akiwa na mbio kama siku hiyo. Yeye alichoropoka. 😂😂😂

Sisi tukashitakiwa kwa kusanyiko lisilo halali.

Polisi, kama kawaida yao, wakatupa mafaili, kesi ikafutwa.

Kwa hiyo, kesi za utawala wa Kikwete ni 3.

Akaingia Magufuli na Samia.

Waheshimiwa Majaji, mwaka 2015 kwenye uchaguzi Mkuu upande wa Zanzibar, Marehemu Sheikh Sharif Hamad alishinda Urais na matokeo yakafutwa na Jecha.

Wakasema patakuwa na uchaguzi wa marudio. Nikahojiwa na waandishi kuhusu uchaguzi wa marudio, nikasema kuwa wanataka kuleta maafa.

Nikakamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi.

Hapa nitarudi nyuma kwa sababu ni muhimu kwa kesi hii.

Aliyenikamata wakati huo alikuwa Senior Superintendent of Police Ramadhani Kingai, leo ndiye...

Majaji: Hebu subiri kidogo.

Mahakama inakaa kimya kidogo, wanaandika.

Waheshimiwa Majaji, nimesema nilikamatwa na Senior Superintendent of Police akiwa Deputy ZCO wa Dar es Salaam.

Waliponikamata, Kingai na wenzake wakanipeleka Central Police, na kabla ya kunipeleka ofisini kwa ZCO, ambaye wakati huo alikuwa Camilius Wambura, ambaye leo ndiye IGP, walinipeleka kwa Wambura kwenda kunitisha kwamba, “Wewe Lissu unajifanya mjanja.”

Nik amwambia Wambura, “Tutakutana mahakamani.”

Kwa hiyo, kesi kwa mara ya kwanza walileta mashahidi, na mmoja ya mashahidi alikuwa Ramadhani Kingai.

Nilipomfanyia cross-examination, hawakuleta shahidi tena mpaka nilipopigwa risasi nikaondoka nchini.

Waheshimiwa Majaji, siku tatu baadaye, tarehe 29 Juni na tarehe 1 Julai, nikakamatwa nikiwa jimboni kwangu Ikungi.

Kwamba nilimuita Magufuli “Dikteta Uchwara.”

Nikakamatwa usiku kwa usiku, nikaletwa Dar es Salaam, na usiku ule nililazwa Chamwino. Pale kuna kituo cha Polisi kina mbu kama nini.

Nikaja kushitakiwa kwa uchochezi.

Around September, tena nikakamatwa nje ya Bunge katika vikao vya Bunge, nikasafirishwa kuletwa Dar es Salaam.

Mwaka umeisha, 2016, nimekamatwa mara 4 na Polisi wa Magufuli na kushtakiwa mahakamani, na mahakama yangu ni Kisutu.

Mwaka 2016 umeisha, nina kesi 4 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 7.

Kesi ya 4 ilikuwa around Desemba kwa miezi 6 ya mwaka 2016.

Waheshimiwa Majaji, nimeanza 2017 nikakamatwa tena Dodoma mwezi Februari na kuletwa tena Dar es Salaam.

Mwezi Aprili palikuwa na uchaguzi wa Rais wa Chama cha Mawakili TLS. Magufuli na Waziri wake wa Sheria, Dkt. Mwakyembe, wakasema huwezi kugombea, ila wanachama wa TLS wakasema gombea.

Siku 4 baadaye nikakamatwa ili siku ya uchaguzi nisiwepo.

Nikakaa Gereza la Ukonga siku 4.

Siku ya Ijumaa nikapelekwa kwa Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe. Mwijage.

Akasema kosa hilo lina dhamana, akasema, “Nenda kagombee urais, Mheshimiwa Lissu.”

Nikaenda kugombea Urais wa TLS.

Between June na August nikakamatwa tena mara 2.

Nikakamatwa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kupimwa mkojo. Nikawaambia, “Kwendeni zenu. Uchochezi na mkojo vinahusiana nini?”

Nilikamatwa kwa sababu ya kukamatwa kwa ndege ya Rais Magufuli baada ya kuvunja mkataba tarehe 19 August.

Nilipolizungumza hadharani, nikakamatwa.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, katika kipindi cha June 2016 na August 2017 nilikamatwa mara 8 na kufunguliwa kesi mara 6 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Zote nilifunguliwa pale. Mahali fulani wakasema hivi: “Anatusumbua na mahakama hatumuwezi, mmalizeni.” Ndiyo tarehe 7 September nikaletewa watu waje kuniua.

Wanaoitwa watu wasiojulikana.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, ya tarehe 7 September naomba niipe context kidogo, kama nilivyosema katika ushahidi wangu wa Ijumaa.

Nilikuwa Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani, mtu mkubwa kidogo.

Nilikuwa nakaa na Waziri wa Madini Kalemani na Mbunge Haji Mponda, ambaye ni Waziri wa Afya wa zamani.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, anasimama.

“Kuna jambo linaendelea hapa. Mshtakiwa anauliza majina kwa hadhara ili wamsaidie, siyo sawa. Huo unakuwa siyo ushahidi wake, ni wa hadhara. Hii siyo sawa.”

Lissu: “Sawa, Waheshimiwa, sito-uliza tena.”

Jaji Ndunguru: “Naomba jamani tuwe wasikivu. Tunapoteza muda bila sababu.”

Lissu: “Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, nilitaka kusema kwamba makazi yale ya viongozi wa Serikali yanalindwa siku 7 za wiki na walinzi wenye silaha.

Na block analokaa Mheshimiwa Spika kuna mlinzi anasimama na bunduki masaa 24.

Siku ninayoshambuliwa, walinzi wote waliondolewa na geti lilikuwa wazi.

Nimetoka Bungeni kwenda nyumbani kula chakula cha mchana, ndipo nikashambuliwa. Risasi 16 zikazaa operesheni 25, na risasi moja natembea nayo.

Kwa sababu madaktari wanasema ni salama kuiacha kuliko kuigusa.

Sijawahi kuitwa na Polisi hata siku moja kwamba siku hiyo ilikuwaje.

Siku hiyo ilikuwa nife, lakini sikufa. Mungu si Athumani.

Mimi sikufa, badala yake Magufuli akafa.

Na zile kesi zote 6, baada ya Magufuli kufa, miezi 6 baadaye nazo zikafutwa.

Akaingia Samia.

Zile Four R, katika kutekeleza zile Four R, tarehe 12 August 2024...

Kama Makamu Mwenyekiti wa chama, nikaalikwa kwenye Baraza la Vijana la CHADEMA.

Katika sherehe yao ya kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, siku ya Umoja wa Mataifa, inaadhimishwa duniani kote.

Jeshi la Polisi likapiga marufuku mkutano wa CHADEMA, siyo CCM.

Tukasema Jeshi la Polisi halina mamlaka hayo.

Nikasafiri kwa ndege kwenda Mbeya tarehe 12 August 2024.

Jioni nikapokelewa na viongozi na kupelekwa katika ofisi ya chama, giza limeshaingia tayari.

Ofisi za chama za Kanda.

Samahani, Waheshimiwa Majaji, ilikuwa tarehe 11, siyo 12, kwa sababu tarehe 12 ndiyo sherehe yenyewe.

Mahali niliposema tarehe 12 parekebishwe.

Basi ilipofika jioni, Waheshimiwa Majaji, nikiwa katika ofisi za chama, tukavamiwa na kundi kubwa la Jeshi la Polisi.

Likiongozwa na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, anaitwa Awadhi Juma, kama sikosei.

Mimi na viongozi wenzangu, Waheshimiwa Majaji, tulipigwa sana na tukakamatwa.

Na mimi nilichukuliwa na Polisi, Waheshimiwa Majaji, usiku ule mpaka Vwawa, ambayo ipo Mkoa wa Songwe, kama unaelekea mpaka wa Zambia.

Nikaenda kufungwa huko.

Kesho yake, Waheshimiwa Majaji, nikapakiwa kwenye gari nikasafirishwa kurudishwa Dar es Salaam.

Nikaletwa Central Police Dar es Salaam tena alfajiri siku inayofuata.

Nikakabidhiwa kwa Polisi wa Kituo cha Kati Dar es Salaam. Nikawauliza, “Kosa langu ni nini?”

Wakaniambia, “Ahaaaa, Mheshimiwa Lissu, tunakupeleka nyumbani.”

Kweli wakanipeleka nyumbani kwangu Tegeta alfajiri.

Sikufunguliwa mashitaka pamoja na kupigwa na kuvurugwa.

Hiyo ni mara ya kwanza ya utawala wa Samia.

Waheshimiwa Majaji, mwezi unaofuata, mkesha, September 07, Mkurugenzi wa Hamasa katika Makao Makuu ya CHADEMA, Makao Makuu, akatekwa kwenye basi akiwa anaenda nyumbani kwao Tanga.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Nilichogundua duniani tumezidiana akili na maarifa. Jamaa kichwani yuko vizuri. Hili halina ubishi. Kwa upande wangu natamani sana siku moja kuongozwa na watu wenye akili nyingi kichwani kama huyu mwamba! Badala ya vilaza ambao hata kujenga hoja tu hawawezi..
Kweli kabisa. Kwenye kesi hii Lissu amejionesha uwezo wake wa akili ulivyo. Very smart.
 
Wewe nabii Tito, unaita kuteteta wananchi porojo?. Uliokuwepo 1998? 2002? Wakati Lissu anapigania haki za kimazongira?. Uwe na heshima hata kidogo.
kwa hizo porojo anazo mbwelambwela hapo ndio anawatetea wananchi au anajionyesha kwa mabwenyenye ya magharibi wanaomtumia kama kibaraka kwamba hajawasahau hata kama kanaswa kwenye 18 za alikokusudia kukinukisha?🐒
 
Mmh napata shida kidogo. Hao waliolaani itamsaidia vipi? Na hiyo historia ya kupigania haki itasaidiaje kwenye shtaka lake.
Nilitamani ajikite kwenye elements za uhaini akidili na actus reus na mensrea na kwamba hajafanya chochote kati ya hayo.
Yaani Kuna saa unakaa unaumia serikali kuamua tu kumpa mtu case nzito bila hata aibu.

Ongezea kushushuliwa na Jaji
Kuusu jana kumbe Ijumaah

Lissu Mbishi sana ile Kesi hangewaachia wanzie nayeye angekuwa anachomekea sehemu akiona mambo sio vile kataka!!

Daktari mbona kuna wakati nayeye anakaa foleni kumuona Daktari mwenzie 🫡🫡

Lissu Yeye ndio mwenye tuhuma tena yupo Lupango👈

Niwazi kiakili hawezi kuwa vizuri kama angekuwa yupo
nyumbani kwaamaana anatokea nyumbani 👈

So hangewaachia wenzie wampambanie👈

Lkn Jamaa m'bishi sana
lile kabila la Wanyiramba Wanaume wapo kama Wamasai ni Wabishi
kinoma ✍️
 
Gentleman wewe ni mwanasheria? 😊
Sheria ni taaluma, hapo TL sio Mshitakiwa, yupo kwenye kizimba cha Ushahidi na hapo anajenga msingi wa ushahidi "preliminary evidence building" juu ya mshitakiwa ambaye ni yeye. Ni vizuri lujua yeye ni nani, jipeni subra msikilizeni, mnawahi wapi??😊
hakuna msingi hapo gentleman kwa huyo muungwana,
ni hivyo hivyo atabwabwaja wweee mpaka muda utakwisha.

hivyo alivyo anza mpaka atakavyomaliza ni porojo tupu kwenda mbele, hata anaetegemea kujifunza ataambulia patupu.

ndivyo alivyo akibananishwa kwenye 18 za wanataaluma wenyewe, anakua empty head kabsaaa 🐒
 
Ongezea kushushuliwa na Jaji
Kuusu jana kumbe Ijumaah

Lissu Mbishi sana ile Kesi hangewaachia wanzie nayeye angekuwa anachomekea sehemu akiona mambo sio vile kataka!!

Daktari mbona kuna wakati nayeye anakaa foleni kumuona Daktari mwenzie 🫡🫡

Lissu Yeye ndio mwenye tuhuma tena yupo Lupango👈

Niwazi kiakili hawezi kuwa vizuri kama angekuwa yupo
nyumbani kwaamaana anatokea nyumbani 👈

So hangewaachia wenzie wampambanie👈

Lkn Jamaa m'bishi sana
lile kabila la Wanyiramba Wanaume wapo kama Wamasai ni Wabishi
kinoma ✍️
Nafikiri hivyo angekua na wakili. Case ni nzito na pia kuwa gerezani hayupo sawa sana. All in all ni chagui lake kujiwakilisha.
 
Kesi kama hii inaitaji kwanza utulivu wa Akili

Kitu ambacho Lissu pale alipo hana
Japo anajaribu kujionyesha yupo sawa kikamilifu kiakili 💪‼️

lkn kitendo cha kutokea Lupango chenyewe tu hawe yoyote lazima utakwama kiutulivu kutokea Lupango kunakutoa Mchezoni %60
 
Lissu si kaka yangu, si ndugu yangu, sina ubini nae lakini naungana nae kwa damu ya udugu wa kitaifa, mapambano dhidi ya mabadiliko ya mfumo wa utwala, Demokrasia na Haki za binadamu.

Binafsi naenda mbali zaidi yake kwamba Misingi yote hii ya kitaifa inaitaji mamlaka huru ya uangalizi na hapo ndipo pendekezo langu la mihimili minne ya kitaifa linaingia, yaani.
1. Baraza la usimamizi wa taifa
2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania

Muundo huu wa dola unakamilisha ukuu wa dola kulinda rasilimali zake, haki za wananchi wake, tunu za taifa na Mamlaka za nchi.

Rasimu ya katiba iliyoanzisha muundo huu inapatikana kwenye tobuti ya www.katibampya.com
 
Back
Top Bottom