Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Sheria ni practice mkuu. Nipo kwenye corporate, criminal sio kihivyo. Nimeelewa dhana hiyo.
P.s. Mimi ni mwanasheria/wakili tangu 2010.

Kuna vitu vya msingi ambavyo kila Mwanasheria lazima avijue ni "Basic". Ni pamoja na sheria ya ushahidi "Evidence law", swali ulilouliza ni sawa na daktari asijue anatomy.
 
Kesi kama hii inaitaji kwanza utulivu wa Akili

Kitu ambacho Lissu pale alipo hana
Japo anajaribu kujionyesha yupo sawa kikamilifu kiakili 💪‼️

lkn kitendo cha kutokea Lupango chenyewe tu hawe yoyote lazima utakwama kiutulivu kutokea Lupango kunakutoa Mchezoni %60
Anaonyesha ukomavu wa kisiasa na kwamba ana hakikisha kwamba mapito ya motoni ni sehemu ya kuandaliwa kwa dharabu hili inyae...
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 8.

Maeneo ya Tegeta wala siyo usiku, akashushwa na watu wenye silaha na watu wenye magari ya Polisi na bunduki wanazotumia Polisi, na kama siyo Polisi ni Usalama wa Taifa.

Kesho yake, Waheshimiwa Majaji, Mzee Ali Mohammed Kibao akaokotwa akiwa ameuawa maeneo ya ufukweni Ununio.

Akiwa ameteswa vibaya mno na amemwagiwa tindikali.

Waheshimiwa Majaji, wakati Marehemu Mzee Ali Kibao anatekwa nyara na kuuawa, palikuwa na matukio mengi ya viongozi wa CHADEMA kutekwa na kupotezwa.

Kilikuwa kipindi kigumu sana.

Kama chama, tukakaa na kuazimia kwamba kama matukio haya ya utekaji nyara yasipochunguzwa na hatua kuchukuliwa, tutaanza kampeni ya kuandamana nchi nzima kushinikiza hatua zichukuliwe. Na maandamano ni ruhusa kwa mujibu wa sheria.

Na maandamano tulitamka yangeanza tarehe 23 September, wiki 2 baada ya Mzee Ali Kibao kuuawa.

Ilipofika tarehe 23 September, nikavamiwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwangu mapema asubuhi.

Nikakamatwa, nikafikiri naletwa Central kama kawaida, ila nikazungushwa siku nzima huku na huku na baadaye nikapelekwa kwenda kufungwa Kituo cha Polisi Mbweni.

Kwa mara ya kwanza sikupelekwa Central.

Nikakaa Mbweni Polisi mpaka usiku, wakanirudisha nyumbani kwangu. Hawakunifungulia mashitaka.

Waheshimiwa Majaji, nilisema mapema mwanzoni nilikamatwa Karatu ili nisiende Ngorongoro. Ilikuwa March 2023 na ni mara ya kwanza chini ya Samia.

Ili nisiende kuonana na wananchi wa Ngorongoro, na nilienda kufungwa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Monduli, kule Monduli Juu kwa Sokoine.

Wakaniweka Monduli Kituoni siku nzima, halafu jioni wakampigia Mzee: “Alute, njoo umchukue mdogo wako tumemweka huku.”

Na hiyo nayo sikushtakiwa, pamoja na kuvurugiwa utaratibu wangu.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kesi hii, kukamatwa kwangu tarehe 09 April mwaka jana na kufunguliwa mashitaka tarehe 10 April mwaka jana, ni mara yangu ya nne chini ya Samia.

This time, Waheshimiwa Majaji, wamenifungulia kesi ya uhaini.

Na tayari, Waheshimiwa Majaji, hapa nilipo nimeshakaa gerezani miezi 16 naelekea mwezi wa 17, yani mwaka naelekea miezi 5.

Nimeshamaliza miezi 4.

Waheshimiwa Majaji, hiki ni kipindi kirefu zaidi kwa mimi kukaa gerezani kuliko kipindi changu chochote kule katika maisha yangu.

Na ni kipindi kirefu ambacho Kiongozi wa CHADEMA amekaa gerezani kuliko kiongozi mwingine yeyote yule.

Na ninaamini kuliko vyama vyote, kwa kiongozi wa upinzani wa zama hizi za mageuzi.

Na ndiyo kesi kubwa kuliko zote ambayo nimefunguliwa kuliko kiongozi yeyote wa vyama vya upinzani.

Hakuna kiongozi amefunguliwa kesi kama hii, na hakuna kiongozi amekaa muda mrefu kama mimi.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, haya ni ambayo yamenitokea mimi peke yangu. Ninaamini hakuna Kiongozi yeyote wa Juu wa CHADEMA ambaye na yeye hajapitishwa katika bonde la uvuli wa mauti kama mimi.

Wengi wamepitishwa kama mimi.

Mimi nina bahati, pamoja na kuchechemea kama mimi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
kwa hizo porojo anazo mbwelambwela hapo ndio anawatetea wananchi au anajionyesha kwa mabwenyenye ya magharibi wanaomtumia kama kibaraka kwamba hajawasahau hata kama kanaswa kwenye 18 za alikokusudia kukinukisha?🐒
Duh! Aiseeh wewe unaumwa. Nadhani hata hufuatilii utetezi wa Lissu. Lissu alikuwa anawatetea wananchi dhidi ya hao mabwenyeynye unaoengelea. Huoni alitoa wananchi 466 kutoka Gerezani Butimba?
 
Kuna vitu vya msingi ambavyo kila Mwanasheria lazima avijue ni "Basic". Ni pamoja na sheria ya ushahidi "Evidence law", swali ulilouliza ni sawa na daktari asijue anatomy.
Asante kwa kunikumbusha, The Law of Evidence can make you win or loss the case.

Umenifanya nikumbuke mbali sana hasa ukisoma criminal laws kitu cha kwanza ni kujua ni nini... ushaidi na ushaidi gani una nguvu mbele ya sheria.
 
Duh! Aiseeh wewe unaumwa. Nadhani hata hufuatilii utetezi wa Lissu. Lissu alikuwa anawatetea wananchi dhidi ya hao mabwenyeynye unaoengelea. Huoni alitoa wananchi 466 kutoka Gerezani Butimba?
to be honest,
siwezi kupoteza muda na wakati wangu kufuatilia porojo nonsense za kibaraka useless kama huyo gentleman 🐒
 
Kesi kama hii inaitaji kwanza utulivu wa Akili

Kitu ambacho Lissu pale alipo hana
Japo anajaribu kujionyesha yupo sawa kikamilifu kiakili 💪‼️

lkn kitendo cha kutokea Lupango chenyewe tu hawe yoyote lazima utakwama kiutulivu kutokea Lupango kunakutoa Mchezoni %60
Usiwe na haraka fautilia mtiririko wake. Kwa Sasa amefika kwenye uhaini. Anajaribu kuonesha kesi ngapi za uonevu amefuguliwa.
 
Hapana mkuu, unaweza kuwa mwanasheria mzuri lakini ukawa huvipi vitu vya msingi kipaumbele. Petty issues kama hizi hazitakiwi kuibuliwa na mtu kama wewe.
Noted mkuu. What do you think about TL representing himself? In my opinion, despite him being a seasoned lawyer, having a defense lawyer would have been best for his case. Being charged for capital offense such as murder, treason and the like sio kazi rahisi kujisimamia.

I wish case hii iishe mwamba arudi uraiani
 
Mmh napata shida kidogo. Hao waliolaani itamsaidia vipi? Na hiyo historia ya kupigania haki itasaidiaje kwenye shtaka lake.
Nilitamani ajikite kwenye elements za uhaini akidili na actus reus na mensrea na kwamba hajafanya chochote kati ya hayo.
Yaani Kuna saa unakaa unaumia serikali kuamua tu kumpa mtu case nzito bila hata aibu.
Wewe hujui malengo ya kisiasa.

Mwenzako hapo anaonesha namna gani ameshatetea raia na mwisho wa siku atakuja kuonesha kwenye hii kesi anavyotetea raia ili hata kama atanyongwa historia yake ibaki inaishi dunia nzima.
 
Mmh napata shida kidogo. Hao waliolaani itamsaidia vipi? Na hiyo historia ya kupigania haki itasaidiaje kwenye shtaka lake.
Nilitamani ajikite kwenye elements za uhaini akidili na actus reus na mensrea na kwamba hajafanya chochote kati ya hayo.
Yaani Kuna saa unakaa unaumia serikali kuamua tu kumpa mtu case nzito bila hata aibu.
Ndiko anakoelekea!
 
Back
Top Bottom