Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Weee kilaza kwel Kwa iyo huku uvccm unataka waone umesema Actus reus na men's rea waone umefanya kazi ya buku 7? Mbona majaj na mawakili wa serikali wamekaa kmya ww mweny gpa ya 2.3 unaongea nn ?
Sio lazima ujibu kwa kashfa. Mimi nimesema ile list ya vyama vilivyopinga case yake itasaidia vipi. Hilo unashindwa kujibu wewe mwerevu?
 
Mmh napata shida kidogo. Hao waliolaani itamsaidia vipi? Na hiyo historia ya kupigania haki itasaidiaje kwenye shtaka lake.
Nilitamani ajikite kwenye elements za uhaini akidili na actus reus na mensrea na kwamba hajafanya chochote kati ya hayo.
Yaani Kuna saa unakaa unaumia serikali kuamua tu kumpa mtu case nzito bila hata aibu.
Una kichwa kizito kwel uliwezaje kusoma Sheria Kwa kichwa hicho? Huon anaweka msingi na alisema kabsa ushahid wake hautaisha Leo ? Hata mwanafunzi wa certificate anaweza kuelewa anaweka faundation ya utetez wake
 
Una kichwa kizito kwel uliwezaje kusoma Sheria Kwa kichwa hicho? Huon anaweka msingi na alisema kabsa ushahid wake hautaisha Leo ? Hata mwanafunzi wa certificate anaweza kuelewa anaweka faundation ya utetez wake
Noted
 
Kuna sababu nyingi zilizomfanya ajitetee mwenyewe;
1. Kuonesha umahiri wake kwenue sheria! Yeye ni mwanasheria na pia ni wakili msomi.
2. Kutuonesha wananchi na dunia kwa ujumla namna bora ya kupigania haki.
3. Kiwaonesha watesi wake namna alivyo jasiri na shupavu kwenye kupigania kile anachokiamini.
4. Kujiongezea umaarufu wa kisiasa kwa maandalizi ya safari yake ya kuufikia uongozi wa juu kabisa nchini (Urais).

Na kwenye hili, hakika amefanikiwa pamoja na mateso yote anayopitia
Huku mtaani kwa sasa habari ni Lissu tu! Lissu ni Shujaa! Lissu ni mpambanaji wa kweli!, Lissu ni mzalendo kwa nchi yake, Lissu ni mwanasiasa wa kweli, nk. Hakuna cha nani wala nani! Habari ya mjini ni Lissu tu.
Uko sahihi kabisa, ingawa kwa kiasi kikubwa watesi wake wamejikuta wana rise political status yake na kushusha za kwao huenda pasipo wao wenyewe kujua hilo
 
okay,
anawataja hata ambao hawamjui na wala hawasaidii chochote kwenye kinachomkabili, dah.

kifo cha nyani ni cha fedheha sana aise, miti yote huteleza 🐒
Kati ya wewe na hao majaji waliotulia wanamsikiliza na wanachukusa notes kabisa, mbumbumbu wa sheria ni nani??
Aliyenikamata wakati huo alikuwa Senior Superintendent of Police Ramadhani Kingai, leo ndiye...

Majaji: Hebu subiri kidogo.

Mahakama inakaa kimya kidogo, wanaandika.
 
Hahaha 😂
Ningekua yeye ningejikita kwenye uhaini. Lakini sijui kwanini Lissu kaamua kujitetea mwenyewe. Hiyo case ni nzito na tena ya uonevu. Angekuwa na wakili wake kwa maoni yangu angejitetea vizuri zaidi.
Mmmh Kwan hii kesi yake Leo ndo umeanza kufuatilia? Hakumbuki alinyimwa haki ya kuonana na mawakili wake ,na akionana nao askari magereza wanakaa pemben ya lissu? Kwa iyo Hajui Kwa nn aliamua kujitetea mwenyew? Na umesema hapo juu upo kwenye tasnia ya Sheria?
 
ANAENDELEA TUNDU LISSU

SEHEMU YA 3.
Tume iliundwa mwaka 1991, ilikuwa inahoji watu, na mimi nilikuwa mmoja ya watu waliohojiwa.

Nilikuwa mmoja ya watu waliotoa ushuhuda mbele ya Profesa Haroub Othman, ambaye alikuwa mwanazuoni maarufu.

Secretary wa Tume alikuwa baadaye Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, January Msofe.

Kwa hiyo, nimepigania mfumo wa mabadiliko kwa namna hiyo.

Kwa kwenda mbele ya Tume ya Rais kutoa ushuhuda.

Na mwaka 1992 niliacha kusoma chuo nchini Uingereza, nikaja kugombea kwa sababu siku zote nimekuwa concerned na masuala ya ustawi wa nchi hii.

Waheshimiwa Majaji, kwa miaka yote iliyofuata mpaka leo, nimepigania demokrasia, Katiba mpya, mfumo huru wa haki na uchaguzi.

Sijawahi kupumzikaaaaa.

Nje ya kupigania demokrasia, Waheshimiwa Majaji, nimepigania haki za wananchi wa kawaida.

Waheshimiwa Majaji, mwaka 1997 Serikali ya Rais Mkapa iligawa eneo karibu lote la Delta ya Mto Rufiji kwa mwekezaji mmoja wa Ki-Irish.

Ili alime kamba (prawns), wale wadudu wa baharini watamu watamu, enheeeee, kamba.

Kamba ni wadudu wa baharini, lakini wanafugwa.

Waheshimiwa Majaji, najua mmesoma kesi ya Reginald, alikuwa anauzia nchi vifaa vya kijeshi chakavu.

Sasa Mkapa na Serikali yake wakampatia hekta elfu 20 za Delta ya Rufiji ili afuge kamba.

Kama hilo lingefanikiwa, pasingekuwa na msitu wa mikoko katika ile Rufiji tunayoiona leo.

Na kwa tafiti za kitaalamu, ingedhuru maisha ya watu laki moja.

Mimi pamoja na wenzangu, akiwemo Dkt. Nshala...

Hawa ni mashujaa, mnatakiwa muwajue.

Mimi na wenzangu tulisakamwa sana na Serikali ya Mkapa, na Mkapa mwenyewe pamoja na Makamu wake, Dkt. Ali Juma.

Tukaitwa wanaharakati wa kimazingira.

Tukamkimbiza yule M-Irish.

Tukaokoa msitu wa mikoko wa Delta ya Rufiji.

Hiyo ilikuwa 1997 na 1998.

Waheshimiwa Majaji, siyo Rufiji tu. Nimekuwa mstari wa mbele kupigania haki za ardhi za wafugaji na wananchi wanaoishi katika hifadhi za wanyamapori kama Ngorongoro, Loliondo, Tarime, Meatu, Bariadi Mashariki, Maswa Mashariki na ukanda wote wa mashariki ya Serengeti.

Mwaka 2023 nilikamatwa Karatu, nikizuiwa nisiende Ngorongoro kuwaona Wamasai niliokuwa nawapigania tangu mwaka 1996.

Nimepigania haki za wananchi wa maeneo ya ukanda wa mashariki wa Ziwa Tanganyika, kama Nkasi, na ukanda wa Pwani wa Mkoa wa Kigoma.

Maeneo ya wavuvi wa ukanda wote wa Ziwa Victoria, kutoka ukanda wa ziwa magharibi mpaka wa Uganda, pamekuwa na ukiukwaji wa kutisha wa haki za raia.

Watu wanauawa na vyombo vya ulinzi. Inatisha sana.
Maanzisha mapambano ya kudai haki, misingi ya demokrasia na utawala wa katiba na sheria
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 8.

Maeneo ya Tegeta wala siyo usiku, akashushwa na watu wenye silaha na watu wenye magari ya Polisi na bunduki wanazotumia Polisi, na kama siyo Polisi ni Usalama wa Taifa.

Kesho yake, Waheshimiwa Majaji, Mzee Ali Mohammed Kibao akaokotwa akiwa ameuawa maeneo ya ufukweni Ununio.

Akiwa ameteswa vibaya mno na amemwagiwa tindikali.

Waheshimiwa Majaji, wakati Marehemu Mzee Ali Kibao anatekwa nyara na kuuawa, palikuwa na matukio mengi ya viongozi wa CHADEMA kutekwa na kupotezwa.

Kilikuwa kipindi kigumu sana.

Kama chama, tukakaa na kuazimia kwamba kama matukio haya ya utekaji nyara yasipochunguzwa na hatua kuchukuliwa, tutaanza kampeni ya kuandamana nchi nzima kushinikiza hatua zichukuliwe. Na maandamano ni ruhusa kwa mujibu wa sheria.

Na maandamano tulitamka yangeanza tarehe 23 September, wiki 2 baada ya Mzee Ali Kibao kuuawa.

Ilipofika tarehe 23 September, nikavamiwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwangu mapema asubuhi.

Nikakamatwa, nikafikiri naletwa Central kama kawaida, ila nikazungushwa siku nzima huku na huku na baadaye nikapelekwa kwenda kufungwa Kituo cha Polisi Mbweni.

Kwa mara ya kwanza sikupelekwa Central.

Nikakaa Mbweni Polisi mpaka usiku, wakanirudisha nyumbani kwangu. Hawakunifungulia mashitaka.

Waheshimiwa Majaji, nilisema mapema mwanzoni nilikamatwa Karatu ili nisiende Ngorongoro. Ilikuwa March 2023 na ni mara ya kwanza chini ya Samia.

Ili nisiende kuonana na wananchi wa Ngorongoro, na nilienda kufungwa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Monduli, kule Monduli Juu kwa Sokoine.

Wakaniweka Monduli Kituoni siku nzima, halafu jioni wakampigia Mzee: “Alute, njoo umchukue mdogo wako tumemweka huku.”

Na hiyo nayo sikushtakiwa, pamoja na kuvurugiwa utaratibu wangu.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kesi hii, kukamatwa kwangu tarehe 09 April mwaka jana na kufunguliwa mashitaka tarehe 10 April mwaka jana, ni mara yangu ya nne chini ya Samia.

This time, Waheshimiwa Majaji, wamenifungulia kesi ya uhaini.

Na tayari, Waheshimiwa Majaji, hapa nilipo nimeshakaa gerezani miezi 16 naelekea mwezi wa 17, yani mwaka naelekea miezi 5.

Nimeshamaliza miezi 4.

Waheshimiwa Majaji, hiki ni kipindi kirefu zaidi kwa mimi kukaa gerezani kuliko kipindi changu chochote kule katika maisha yangu.

Na ni kipindi kirefu ambacho Kiongozi wa CHADEMA amekaa gerezani kuliko kiongozi mwingine yeyote yule.

Na ninaamini kuliko vyama vyote, kwa kiongozi wa upinzani wa zama hizi za mageuzi.

Na ndiyo kesi kubwa kuliko zote ambayo nimefunguliwa kuliko kiongozi yeyote wa vyama vya upinzani.

Hakuna kiongozi amefunguliwa kesi kama hii, na hakuna kiongozi amekaa muda mrefu kama mimi.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, haya ni ambayo yamenitokea mimi peke yangu. Ninaamini hakuna Kiongozi yeyote wa Juu wa CHADEMA ambaye na yeye hajapitishwa katika bonde la uvuli wa mauti kama mimi.

Wengi wamepitishwa kama mimi.

Mimi nina bahati, pamoja na kuchechemea kama mimi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 9

Wengi nimefanya nao kazi wameuawa na wengine wamepotea, hawajulikani.

Kama chama, tumepelekwa kuzimu na kurudishwa.

Tuna maumivu makubwa ajabu na tumeumizwa sana, na siyo mimi tu.

Tumefunguliwa kesi na Mapolisi na Mawakili hawa wa Serikali, za kila aina na za uongo.

Waheshimiwa Majaji, Tume ya Rais ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai, maarufu kama Tume ya Jaji Chande, hii hapa. (Anaonyesha kitabu.)

Inapendekeza Jeshi la Polisi lifumuliwe kwa sababu ya kuumiza watu na kukandamiza haki za watu.

Siyo tu Polisi peke yao wanaofungulia watu mashitaka ya bure, na Mawakili wa Serikali nao.

Kesi za Polisi peke yake bali mashtaka ya Serikali.

Tumezika watu wengi sana.

Mimi nimezika viongozi wengi sana, Waheshimiwa Majaji, ndani ya hii miaka 3.

Tumeumizwa sana na nimeumizwa sana.

Anasimama Wakili Mkuu wa Serikali, Nassoro Katuga.

Lissu anakaa kwenye kiti.

Nassoro Katuga: Anafungua kitabu cha sheria.

“Waheshimiwa Majaji, ombi letu ni kwa Mahakama tukufu, au kuikumbusha Mahakama tukufu, kinachotolewa hapa ni ushahidi in chief.

Kifungu cha 156(2) kinasema in chief must relate in facts.

Kesi yetu ni uhaini.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 60 cha Sheria ya Ushahidi, kimeruhusu ushahidi wa good character, tukaacha ajieleze good character.

Tunaona anajielekeza kwenye mambo mengine, kusema watu wamekufa.

Kama vile sisi tulitaka kuleta ya October 29, tukakatazwa, na utaratibu ni uleule, asilete mambo mapya.

Mambo ya watu wengine sijui wamekufa au wamefanyeje, asilete hapa.

Haya ya watu wamekufa ni good character? Ni sehemu ya kesi yetu?”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 10

Tukiacha aongelee vitu ambavyo siyo relevant kwa kesi yetu, tunaharibu mwenendo wa kesi yetu.

Labda aseme vitu vinavyohusiana na good character, ndiyo sheria imeruhusu.

Jaji Ndunguru: “Mshtakiwa.”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, utetezi wangu ni utetezi wangu kwamba kesi hii ni ya kutengeneza, kama vile Mawakili wa Serikali na Polisi wanavyofungulia watu mashitaka ya bure.

Mapolisi na Mawakili wa Serikali they abuse their power.

Huwezi kusema siyo relevant.

Nina haki kutoa utetezi wangu.

Wana haki ya kuni-cross-examine, kama ambavyo mashahidi wao walileta ushahidi wao.

Anaposema tunaweza kutumia wiki mbili, inanishangaza sana.

Mimi nimekaa mwaka na nusu kusubiri mashitaka yao, wao wananishangaa kujitetea wiki mbili.

Hawa vipi?

Sipotezi muda, najitetea, Waheshimiwa Majaji.

Lililo jema kwao liwe jema kwa wengine.

Sitokaa mwaka na nusu kama wao, ila wavumilie kama hizi wiki mbili ndiyo utetezi wangu.

Wana haki ya kuja kunihoji, wao wana wasiwasi gani?

Ni hayo tu, Waheshimiwa Majaji.”

MAJAJI: Wanateta kidogo kabla ya kutoa uamuzi.

Mahakama inanong’ona kidogo na watu wanasonya hapa na pale.

Jaji Ndunguru: “Tuendeleeni.”

Lissu: “Asante, Waheshimiwa Majaji. Nataka nimalizie hili, niende katika uchaguzi.”

Jaji Ndunguru: “Lakini zungumza yaliyombele yetu.”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, kesi inahusu uhaini kwa kuvuruga uchaguzi. Nitaeleza kuhusu uchaguzi.

Waheshimiwa Majaji, nataka kuzungumza kuhusu taarifa iliyopelekwa kwa Muendesha Mashtaka Mkuu.”

Anasimama Wakili wa Serikali Mkuu, Job Mrema.

“Waheshimiwa Majaji, tuna hoja kwa Kifungu cha 177 cha Sheria ya Ushahidi.

Waheshimiwa Majaji, kwa upande wa Jamhuri tumekuwa tukiona shahidi anasoma makabrasha yake.

Anasoma.

Kifungu hiki kinaeleza shahidi kueleza kwa kumbukumbu zake anachokijua.

Na kama anataka kujikumbusha, kuna utaratibu anatakiwa afuate.

Tumevumilia, lakini tunashindwa kumvumilia.

Anasoma makaratasi na hatujui ametoa wapi.”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, Kifungu cha 177 kinasema kwamba shahidi anapokuwa anatoa ushahidi wake, anaweza kujikumbusha ushahidi wake kwa kusoma nyaraka zake zinazomhusu.

Kifungu kidogo cha pili kinasema shahidi anapotumia ushahidi ambao siyo nyaraka zake.

Sijaona sehemu ambako kifungu kinasema shahidi anaweza kusoma kwa ruhusa ya Mahakama nyaraka zake.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 5.

Kama mkishawishika na hoja na ushahidi wa Mawakili wa Serikali, ni kifo.

Msisambwe, ooh sijui kuna nini, bali ni kifo. You don't get more serious than this.

Waheshimiwa Majaji, leo nakabiliwa na kesi kubwa kuliko zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hii ni mwendelezo wa kesi nyingi za jinai ambazo nimewekewa na Serikali hii, Polisi na Mawakili wake.

Waheshimiwa Majaji, sina hakika na watu wengine nje ya chama changu CHADEMA.

Lakini ndani ya CHADEMA, mimi ndiye mwanachama na kiongozi ambaye nimeshitakiwa mara nyingi kuliko kiongozi au mwanachama yeyote.

Waheshimiwa Majaji, na kesi zote ambazo nimefunguliwa zimekuwa ni kesi za kisiasa.

Zimetokana na matendo yangu, kauli zangu na misimamo yangu ya kisiasa.

Waheshimiwa Majaji, tuanze na utawala wa Marehemu Rais Mkapa.

Mwaka jana, Waheshimiwa Majaji, wakati wa Christmas, mwanangu mmoja alinitumia ujumbe kwamba:

“Baba, upo gerezani, unatukumbusha kwamba Christmas yetu ya kwanza duniani ulikuwa gerezani.”

Wakati wa Mkapa, nilikamatwa tarehe 23 Desemba 2002, siku mbili kabla ya Christmas, kwa kosa la uchochezi.

Wanazungumza sana uchochezi watu hawa.

Sababu gani?

Kwa kuongoza kampeni ya kudai mauaji ya wananchi wa Bulyanhulu yachunguzwe, baada ya watu zaidi ya 60 kufa.

Kwa kudai mauaji haya yachunguzwe, nikakamatwa nikapelekwa Makao Makuu ya Polisi, Shimoni.

Pale chini kuna gereza linaitwa Shimoni. Pale wanajaza watu, wengine wanakaa miezi.

Kwa bahati nzuri nilikuwa maarufu, wakanipeleka mahakamani siku ya Christmas.

😂😂😂😂😂

Walimpata wapi Hakimu sijui, ila akanisomea mashitaka, akaniambia ondoka hapa.

Uchunguzi ulikuwa miezi 6.

Walioshitakiwa wenzangu walikuwa Augustine Lyatonga Mrema na Dkt. Lugemeleza Nshala, ambaye leo ni Wakili wangu.

Kosa ni kudai uchunguzi wa mauaji ya wananchi.

Miezi 6 wakaifutilia mbali baada ya kukosekana kwa ushahidi. Wakashindwa kuleta mashahidi.

Mwaka 2005 akaingia Jakaya Kikwete.

Waheshimiwa Majaji, nilizungumzia Tarime, ipo karibu sana moyoni mwangu.

Mwaka 2005, Julai, nikiwa Mbunge, Polisi walifanya mauaji eneo la Nyamongo, wakaua watu 3 (wanakijiji).

Nikiwa Bungeni, wananchi wa Nyamongo wakanipigia simu: “Mheshimiwa, inabidi uje. Polisi wameua na wanataka tuzike, tumegome. Njoo.”

Nikaondoka Bungeni, nikaenda Tarime kudai uchunguzi wa mauaji yale ufanyike.

Nilipofika Tarime, tukapata taarifa kwamba Polisi wana mpango wa kutaka kuvunja milango ya chumba cha kuhifadhia maiti ili waibe maiti.

Tukaenda kuweka kambi chumba cha kuhifadhia maiti ili Polisi wasiibe maiti.

Tukapigwa sana. Kuna picha maarufu Polisi wamenichania combat yangu, ila picha ni ya Tarime.

Nikapigwa vibaya sana. Wakanichania combat yangu, tukakamatwa, tukapelekwa kilomita 40 nje ya Tarime. Kesho yake tukashitakiwa kwa criminal trespass.

Nikapelekwa Gereza la Wilaya ya Tarime siku 4. Pale nilipokuwa natoa wenzangu, safari hii nikawa mimi ndiye mfungwa.

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
Mkuu Manyanza Mungu akubariki Sana hili darasa analotoa Lissu ni habari nyingine.

Yaani namna anavyofikiria ,anapangilia maelezo pamoja na kumbukumbu,yaani ubongo wake ni balaa huyu mtu
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 11

Kama nikitakiwa kujikumbusha, nilitakiwa nifungue hili faili langu, na hata sijaanza kusoma faili langu.

Na kama nitatakiwa kuomba ruhusa, nitaomba nikifika, na kifungu hakisemi niombe ruhusa, nitaomba nikifika.

Jaji Ndunguru: “Endelea, shahidi.”

Lissu: “Nimesema haya yote niliyozungumza ni yale yaliyopelekwa kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali.

Ya kwangu na mengi niliyozungumzia yapo katika hiyo communication.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kesi hii kiuhalisia ni mgogoro wa kisiasa unaohusu nchi hii.

Kuhusu uchaguzi na kuhusu chaguzi zetu, na hiyo ndiyo essence ya kesi hii.

Taarifa iliyopo Mahakamani, Waheshimiwa Majaji, inatuhumu kwamba nilitengeneza nia ya kuhamasisha watu kutishia Serikali ili kuvuruga uchaguzi.

Maneno ninayodaiwa kuyasema, kwa kuyaangalia tu, yanahusu uchaguzi.

‘Tutazuia uchaguzi, tutahamasisha watu wazuie uchaguzi.’ It’s all about election.

Mashahidi wote 17 wa upande wa Mashitaka, kila mmoja wao amesema ametoa ushahidi in connection kuhusiana na kauli zinazodaiwa kuwa za kwangu kuhusiana na uchaguzi.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa nyaraka (document evidence) ambao umetolewa kutoka D1 hadi D16.

Exhibit D1 to D16 zina-touch on election, with various degrees of explanation.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, katika sehemu hii ya ushahidi wangu naomba nizungumzie uchaguzi wa Tanzania.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa PW1, PW2, PW3, na kwa kiwango fulani PW16 na PW17,

wameiambia Mahakama hii, Waheshimiwa Majaji, katika ushahidi wao kwamba kauli wanayodai nimeichapisha kwenye Jambo TV YouTube ina urefu takribani saa 3.

PW16 na PW17 wamesema ina takribani saa 2 na kadhaa.

Lakini wote kwa ujumla wao, mashahidi 15 wamesema hiyo picha mjongeo ina urefu huo.

Waheshimiwa Majaji, maneno waliyoleta Mahakamani yanamaliza dakika 1, maneno ambayo yamenifanya niwe gerezani kwa tuhuma hii.

Hayo masaa 3 na dakika zingine walizosema, hawasemi nilizungumza kitu gani.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, nitazungumza nilizungumza kitu gani.

Lakini, Waheshimiwa Majaji, ili muelewe hayo mazungumzo ya masaa 3, ili muelewe kwa nini nilizungumza kuhusu uchaguzi wa nchi hii kwa masaa 3...”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom