TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA
SEHEMU 14
Taarifa ya waangalizi wa kimataifa baada ya 1995 walisema katika taarifa yao kuwa pawe na mabadiliko ya Kikatiba kuifanya Tume ya Uchaguzi iwe Tume Huru ya Uchaguzi, ili matatizo ya 1995 yasijirudie tena, kwa mujibu wa ripoti ya Commonwealth, EU na watazamaji wa ndani ambao walikuwa ni TEMCO, wakijumuisha viongozi wa dini na NGOs.
Magufuli amewafutilia mbali.
Serikali ya Rais Mkapa ilikataa na CCM ikakataa.
Mkapa akaunda Tume ya Jaji Kisanga kuchunguza matatizo ya Kikatiba.
Tume ya Jaji Kisanga wakapendekeza mabadiliko ya Katiba ya kurekebisha matatizo ya uchaguzi.
Mkapa akakataa na CCM ikakataa.
Tukaenda uchaguzi wa 2000 na Tume ileile, matokeo yake maafa yakatokea Pemba.
Kwa mara ya kwanza tukawa na wakimbizi Zanzibar.
Kule Zanzibar ikaja Tume ya Kimataifa.
Mwaka 2003, Mkapa akaunda Tume ya Jaji Mark Bomani, ambayo nayo ilipendekeza Katiba mpya na Tume ya Uchaguzi.
Waheshimiwa Majaji, Jaji Mark Bomani alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza.
Mkapa akakataa na CCM ikakataa.
Badala yake, Mkapa akampendekeza kuwa katika Tume ya Uchaguzi. 😂😂😂
Akanogewa. Mwaka 2005, Jaji Mark Bomani, na yeye akiwa Tume ya Uchaguzi, akachukua fomu kugombea Urais ndani ya CCM.
Wenzie wakamwambia, “Eboooooo, wewe si upo Tume ya Uchaguzi?” Ikawa aibu tupu.
Mkapa kaondoka, akaja Kikwete, na Kikwete alipoingia tu, CHADEMA ikaanza kuwa na nguvu.
Tukaenda kwenye uchaguzi wa 2010 na Tume hii na Katiba hii, yakatokea maafa tena Zanzibar.
Kikwete alipoingia 2010 akasema lazima tumalize kelele za Katiba mpya.
Na mimi nilikuwa Bungeni mwaka 2010. Tulikuwa wachache sana, ila tulifanya kazi kubwa sana.
Kikwete akaunda Tume ya Jaji Warioba.
Ndiyo ikafanya kazi kubwa sana.
Mzee Warioba amefanya kazi nzuri sana. Ndiyo maana hawampendi Jaji Warioba; amesimama kidete yule mzee.
Tunaelekea katika uchaguzi, CCM wakavuruga mchakato wa Katiba mpya.
Kikwete akasema twendeni kwanza katika uchaguzi Mkuu.
Kwa hiyo tukaingia mwaka 2015 na Katiba hii hii na Tume hii hii, ndiyo tukampata Magufuli na Samia.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI