Nimeazisha uzi wangu baada ya Mods kuunganisha uzi wangu wa updates Mahakamani, mpaka nimeona kero na hasira kupost updates, uzi huu utakuwa unapata updates za majumuisho ya mwisho ya Mh Tundu Lissu
SEHEMU YA 1
WAHESHIMIWA MAJAJI,
Nipo hapa kuwaonyesha kwamba hilo jambo haliwezekani.
Waheshimiwa Majaji, nilikamatwa katika mji wa Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, jioni ya siku ya tarehe 9 Aprili 2025.
Nilichukuliwa nikiwa ninazungumza katika mkutano halali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama ambacho nimekiongoza tangu tarehe 22 Januari 2025.
Waheshimiwa Majaji, baada ya kukamatwa huko, nilisafirishwa usiku huo huo hadi Dar es Salaam.
Mchana wa kesho yake, tarehe 10 Aprili 2025, nilisomewa mashtaka katika kesi mbili zilizofunguliwa dhidi yangu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Waheshimiwa Majaji, katika kesi ya kwanza nilisomewa shtaka la uhaini, kinyume na Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Adhabu, Sura ya 16.
Katika kesi ya pili nilisomewa shtaka la kutoa taarifa za uongo, kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act).
Waheshimiwa Majaji, kesi ambayo imenileta mbele yenu leo inatokana na kesi ya kwanza niliyosomewa mashtaka yake Kisutu, yaani shtaka la uhaini.
Baada ya takribani miezi minne na nusu ya mashauri mawili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) aliwasilisha taarifa katika Mahakama hii kuhusiana na shtaka hilo la uhaini.
Waheshimiwa Majaji, taarifa yenyewe ina tarehe 12 Agosti 2025.
Taarifa hii inanituhumu kwa mambo yafuatayo:
Kwamba, nikiwa na utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma kuwezesha kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025, kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na nilidhihirisha nia hiyo kwa kitendo changu cha kutamka, kusema na kuchapisha maneno yafuatayo:
«“Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi: Msimamo huu unaashiria uasi; ni kweli, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi. Hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha sana sana. Huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga huu uchaguzi kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.”»
Waheshimiwa Majaji, haya ni maneno niliyowasomea ambayo nilisema. Yana kitu kinachoitwa ellipsis (doti doti). Zipo ellipsis nne; kuna ellipsis kabla ya maneno “wanasema” na kuna ellipsis katikati ya maneno haya.
Maana yake ni kwamba kuna maneno ambayo yameondolewa.
Na hilo ni jambo muhimu sana katika hoja zangu za mwisho.
Uthibitisho kwamba kuna maneno yameondolewa ni uwepo wa hizo ellipsis.
Waheshimiwa Majaji, mashtaka tangu mwanzo yanasema kwamba nilifanya kosa hilo katika Wilaya ya Kinondoni mnamo tarehe 3 Aprili 2025.
Wakati wa usikilizwaji wa awali wa kesi hii, mnamo tarehe 22 Septemba mwaka jana, upande wa Mashitaka ulitoa maelezo ya ziada (Additional Information in Support of their Charge).
Waheshimiwa Majaji, kwenye maelezo ya ziada yaliyotolewa wakati wa uwasilishwaji wa awali...
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.