Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Hatua ya maswali ya dodoso (Cross Examination) kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, yanatarajiwa kutamatishwa leo Agosti 27, 2026 na kufungua mlango kwa shahidi mwingine wa Lissu kupanda kizimbani kwaajili ya kutoa utetezi wake.

IMG_7971.JPG

Jana Agosti 26, 2026, Tundu Lissu alihitimisha kutoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Jaji, Dunstan Ndunguru, ambapo ambapo baada ya hatua hiyo, upande wa Jamhuri (Washtaki) walipewa nafasi ya kuuliza maswali hayo kwa mshtakiwa.

Katika utetezi wake wa Jana, Lissu alidai kwamba Ushahidi uliotolewa na Askari Polisi wa upande wa Jamhuri, ulikuwa unatofautiana kwa maelezo waliyoyaandikaa Polisi na yale waliyoyawasilisha mahakamani.

Mwenendo wa Kesi ya Uhaini Mahakamani sehemu ya 289

Majaji wameingia muda huu na Mwenyekiti ameingia Mahakamani.

Anasimama Karani wa Mahakama anasema Criminal Session No. 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.

Iwapendeze Majaji Naitwa Ajuye Zengeli, Nassoro Katuga, Job Mrema, Cathbert Mbiringe, Winiwa wote tunaiwakilisha Jamhuri na Mtuhumiwa yupo hapa. Tuko tayari kuendelea na maswali ya Dodoso.

Mh. Lissu naomba nipate nafasi ya kuconsult mawakili wangu kidogo.

Anasimama Dr. Nshala anashauriana nae hapo kizimbani kwa dakika kama tano.

Sasa niko Tayari.

Katuga: Kaka angu Shikamoo?

Mhe. Lissu: Marahaba

Katuga: Kama nilikuelewa unasema kuna tuzo ulipewa ilitokana na kupigania haki kwa nchi za Afrika. Je ulitaja hizo nchi za Afrika ulizopogania?

Mhe. Lissu: Sikutaja

Katuga: Ulisema heshima imeongezeka ulifanya sensa wapi?

Mhe, Lissu: Heshima haipatikani kwa sensa. Inatokana na watu wanaoheshimika wakakuheshimu.

Katuga: Kwahiyo imeongezeka ni kwasababu wazungu wamesema?

Mhe. Lissu: sijasema wazungu nimesema Jumuiya za Kimataifa na zinaheshimika kweli.

Katuga: Ulisema mgombea wa Mlimba alirudisha fomu akakuta ofisi imefungwa? Je ulikuwepo?

Mhe. Lissu: Hizo ni taarifa rasmi sio lazima niwepo, nilisoma kwenye taarifa rasmi.

Katuga: Ukitoa mashahidi kutoa Jeshi la Polisi hawa waliolindwa hawajulikani na mtu yeyote?

Mhe:Lissu: Ndio

Katuga: Haya maneno umesema kuonesha ukweli wako?

Mhe. Lissu: Kweli

Katuga: Uamuzi wa Majaji ulisemaje kuhusu mashahidi wa siri?

Mhe. Lissu: wawaone wao.

Katuga: Uliwaambia kuwa hawawajui majina na kila kitu?

Mhe. Lissu: ni ushahidi wangu hawawajui ndio

Katuga: kwahiyo hawawajui majina?

Mhezx Lissu: Sasa mtu gani anaitwa P2, Sijui P

Katuga: Kwahiyo hayo ya P1, P2 sio majina?

Mhe. Lissu: Sio majina hayo nimesema.

Katuga: Hizo si ni synonim?

Mhe, Lissu: Synonim sasa ni majina? Hayo sio majina.

Katuga: Umesema ni sheria gani shahidi anapaswa kutoa jina?

Mhe, Lissu: CPA na sheria ya Ushahidi zote zinasema jambo hilo.

Katuga: Naomba Kifungu?

Mhe, Lissu: Kifungu cha 192 cha CPA

Katuga: kisome sasa wapi wanasema wataje majina?

Mhe, Lissu: kisome uone kinasemaje ngoja nikusomeee kinapotaja hitaji la jina?

Katuga: sitaki ukisome.

Mhe. Lissu: Hutaki tena nisome.

Katuga: Kwahiyo neno la kuwa lazima watoe jina lipo?

Mhe: Lissu: Unadhani kwanini mashahidi huwa wanaulizwa majina yao Mahakamani?

Katuga: Hilo sijakuuliza.

Mhe, Lissu: Hiyo sasa utajua mwenyewe kama hujaniuliza.

Katuga: Pw 17 alisema kuna muda waandishi wa habari walitolewa mkabaki wenyewe na kikao cha ndani? Uliwahi kukanusha hilo?

Mhe. Lissu: Nikanushe la nini? Ndio ukweli

Katuga: Una volunteer sana information.

Mhe.Lissu: Ndio kazi yangu.

Katuga: Majibu yako yana vutia sana.

Mhe. Lissu: then, you should be happy.

Katuga: Kwahiyo nichekecheke

Mhe. Lissu: Fanya hivyo

Katuga: Kwahiyo mliwatoa waandishi nje, wewe na wenzako?

Mhe. Lissu: Tuliwatoa.

Katuga: Mliwatoa kwasababu hayo mengine hayakuwa sehemu ya mliyowaitia. Kwahiyo yale ambayo mlitaka wayachapishe ndio mliruhusu wawepo?

Mhe. Lissu: Ndio.

Katuga: Ambayo hukutaka yachapishwe mliwatoa waandishi?

Mhe. Lissu: Yote tuliyotaka watu wajue waliyajua.

Katuga: Je kwenye ushahidi wako ulisema sheria mahsusi kwamba ukigundua kosa la uhaini unapaswa kuwasiliana na DPP?

Mhe.Lissu: Nikitaje cha nini? Haina maana hakipo kama sikukitaja.

Katuga: Mimi lazima nikuulize maswali nisipofanya nitakuwa sifanyi kazi yangu

Mhe. Lissu: Fanya kazi yako.

Katuga: Ulisema kuna mgogoro binafsi na Wambura na Kingai?

Mhe. Lissu: nimesema kuna chuki kubwa dhidi yangu. Nimekuwa persecuted maliciously 24yrs.

Katuga: Umewahi kufungua malicious prosecution

Mhe. Lissu: Haina maana yoyote sijawahi kuwafungulia lakini haiondoi ukweli wowote.

Sehemu ya 290

Katuga: Ulisema Mashahidi waliolindwa walifanyaje?

Mhe. Lissu: Walikuwa ni washitakiwa na watuhumiwa wa makosa

Katuga: Sheria inawazuia wasiwe mashahidi

Mhe. Lissu: Haiwazuiii.

Katuga: Mashahidi wa Jeshi la Polisi walieleza kuwa walikamata wote?

Mhe. Lissu: Walisema wamewakamata waliowatambua.

Katuga: Kwahiyo kuna wengine hawakukamatwa?

Mhe. Lissu: Ntajuaje sasa?

Katuga: Ile kauli yako ya tutavuruga uchaguzi ulisema mtu yeyote anaweza kutafsiri anavyoona?

Mhe, Lissu: Sahihi

Katuga: Walisema hawa mashahidi kuwa waliyopanga yalitokana na maneno yako?

Mhe. Lissu: Najuaje sasa watu siwajui na siwafahamu. Nasemaje watakuwa wanasema ukweli.

Katuga: Katika ushahidi wako umeiambia mahakama hii tukufu kuwa hawa mashahidi hawasemi kweli?

Mhe. Lissu: Nimeiambia mahakama kuwa huu ushahidi ni wa wahalifu na ni waongo.

Katuga: Katika utetezi wako ulisema kuwa wewe uliwachochea?

Mhe. Lissu: Wapi nimesema hivyo? Sijasema mimi.

Katuga: Wanasema maneno yako ndio yaliwachochea sasa wewe uliwaambia majaji kuwa maneno haya hayawezi kuwachochea.

Mhe. Lissu: Nimewaambia Majaji maneno haya hayawezi kuwa uchochezi sio kosa pia. Labda kama ulikuwa umelala.

Katuga: Waheshimiwa naogopa kurudia maswali. Amekaa kimya anatafuta tafuta. Sasa wale mashahidi waliolindwa

Mhe, Lissu: mimi nimekwambia mashahidi waliofichwa hiyo kulindwa umetoa wapi?

Katuga: Witness protection ni nini kiswahili?

Mhe, Lissu: Mashahidi waliolindwa. Lakini sasa mimi nimesema kwangu ni mashahidi waliofichwa. Hiyo ya kulindwa ni yakwako.

Katuga: Je wale mashahidi walifichwa kweli?

Mhe. Lissu: ni ushahidi wangu kuwa hao mashahidi hawajulikani

Katuga: Huo ni ushahidi wa kuona au kusikia.

Mhe. Lissu: Ni ushahidi wa inference hakuna anayewajua isipokuwa mapolisi.

Katuga: Hizo ni speculations au ushahidi wa direct.

Mhe. Lissu: Huo ni ushahidi.

Katuga ameenda kunong'ona na wenzake.

Anauliza sasa swali: Nimehama kwenye inference. Maneno unawezekana maneno ya mashahidi wakulindwa inawezekana walikuwemo humu ndani wakati kesi inaendelea.

Mhe. Lissu: Nimeshasema hawajulikani na mtu yeyote.

Katuga: Ni kweli au sio kweli?

Mhe. Lissu: Ni ushahidi wa inference. Huelewi nini? Kwasababu mnawajua nyie peke yenu.

Katuga: Mimi sitoki hapa

Mhe. Lissu: Hata mimi sitoki.

Katuga: Mahakama inakunote

Mhe. Lissu: Kwanini wewe haikunote?

Katuga: kwahiyo ni kuona au kusikia?

Katuga: Shahidi shule si ulikuwa unafundishwa multiple choice?

Mhe. Lissu: Mimi sijafundishwa multiple choice. Mimi nimefundishwa critical thinking. Sheria unafundishwaje multipe choice? Ndio maana unakuwa mjinga.

Katuga: Hii kauli hawa mashahidi inawezekana walikuwepo mahakamani ni maoni au ushahidi?

Mhe. Lissu: Ni ushahidi wangu maoni kivipi.

Katuga: Kwenye ile video kuwa Majaji ni Maccm ulisema hukumbuki?

Mhe. Lissu: Nilisema nakumbuka. Huwa sikatai maneno yangu.

Katuga: Una kesi nyingine ya jinai ya kuchapisha taarifa za uongo?

Mhe. Lissu: Ipo Kisutu anawatajia hadi namba nyingine ya kesi.

Katuga: Ulisomewa hoja za awali na imeanza kusikilizwa?

Mhe. Lissu: Imesomwa lakini sikumbuki.

Katuga: Uliposomewa hoja za awali na kwamba ulitoa maneno kuwa majaji ni Ma CCM? Ulijibuje?

Mhe. Lissu: Sikumbuki. Sasa unaniulizaje hayo mengine.

Katuga: Mwenyekiti wa CHADEMA ni kweli ulitangaza kutogombea uchaguzi wa Mwaka jana?

Mhe. Lissu: Sikumbuki.

Katuga: Chama chako kilishiriki Uchaguzi mwaka jana?

Mhe. Lissu: Uchaguzi gani sasa? Hakikushiriki.

Sehemu ya 291

Katuga: Kutokulipiwa na matibabu na umeeleza vitu vingi kuhusu uchaguzi. Imani yako uliposema imani yako na mahakama haipo kwahiyo huna imani?

Mhe. Lissu: Hilo ni la kuuliza kweli. Kwenye maswala haya sina IMANI KABISA NA MAHAKAMA.

Katuga: Maswala yapi?

Mhe. Lissu: Si ya Uchaguzi tunazungumzia.

Katuga: Kwahiyo hukupanga kuiomba Mahakama kutengua vifungu fulani vya Katiba?

Mhe. Lissu: Sikupanga.

Katuga: Uliamua kutafuta njia nyingine mbadala?

Mhe. Lissu: Njia ya mbadala ya Kidemokrasia.

Katuga: Jana nilikuulizia kuzuia uchaguzi ni njia ya kidemokrasia.

Mhe. Lissu: Haswaa.

Katuga: Kukinukisha ni njia ya kidemokrasia?

Mhe. Lissu: Haswaa ni njia ya kidemokrasia.

Katuga: Kuhamasisha uasi je?

Mhe. Lissu: Njia ya kidemokrasia kabisa. Mwalimu Nyerere alisema uasi dhidi ya mifumo kandamizi ni halali kabisa.

Katuga: Kifungu cha 52 cha Media Service Act iko sawa na kifungu cha 55?

Mhe. Lissu: Iko sawa.

Katuga: Sheria ya Huduma za Habari iliundwa ku regulate huduma ya habari?

Mhe. Lissu: Ndio

Katuga: Kuzuia uchaguzi uliopo kwa mujibu wa sheria ni kuipinga serikali?

Mhe. Lissu: ni kuzuia uchaguzi. Kuipingaje tena serikali?

Katuga: Kuhamasisha uasi, kukinukisha. Ni kuipinga serikali au kuipindua serikali.

Mhe: Lissu: Hatukuwa tunazungumza habari za serikali.

Katuga: Mbona nakuuliza swali kwa heshima tu

Mhe. Lissu: Huna heshima hata kidogo. Uitoe wapi?

Katuga: Unakumbuka ulisema kuipinga serikali sio kosa?

Mhe. Lissu: Nimesema.

Katuga: Sasa ulikuwa unamaanisha nini?

Mhe. Lissu: Nassoro Katuga nimesema kifungu cha 55 hakijasema serikali peke yake

Katuga: Mimi mdogo ndio maana unanionea.

Mhe. Lissu: Wewe mdogo ungekuwa hapa? Una udogo gani wakili mkuu wa serikali?

Katuga: Ulisema mapolisi kujiandika maelezo ni kinyume cha sheria na je uliwatajia sheria.

Mhe. Lissu: Sikuwaambia lakini kifungu kipo na kinajulikana.

Katuga: Sasa mbona unaniambia sina adabu halafu wewe hujibu maswali.

Mhe. Lissu: Unataka niseme yakwako?

Katuga: Ulisema vielelezo vilivyoingia mahakamani uliviingiza wewe?

Mhe. Lissu: Viliingizwa na Mahakama.

Katuga: Kwahiyo umeridhika na content za hivyo vielelezo?

Mhe. Lissu: nimeridhika vitumike kuonesha sina hatia.

Katuga: Naomba D1 hadi D16.

WANAMTAFUTIA WAMPATIE VIELELEZO.

Katuga: Unakumbuka D1 ni kielelezo cha Kaaya ambae ni PW2 na uliomba yatumike kwa nia ya kudodosa shahidi kwa mujibu wa kifungu cha 163?

Mhe. Lissu: Kweli

Katuga: ni kweli tulisema kuhusu ommission na contradiction?

Mhe. Lissu: Nilisema.

Katuga: Ulisoma kifungu cha 163 hapa Mahakamani? Na ukasema hakuna neno omission kwenye kifungu hicho na neno pekee lililopo ni contradiction?

Mhe. Lissu: Nakumbuka.

Katuga: Ulimuuliza Kaaya ameajiriwa mwaka 2009 na ameenda Zanzibar au hajaenda? Na akajibu hayamo? Unakumbuka?

Mhe. Lissu: Nakumbuka.

Katuga: kutokuwepo kwenye maelezo yake ni contradiction au ommission?

Mhe. Lissu: Omission.

Katuga: Kwenye hiki kielelezo ni contradiction gani ipo hapo?

Mhe..Lissu: Mahakamani alisema ni Uhaini lakini kwenye maelezo amesema ni makosa ya jinai.

Katuga: Uhaini ni madai au jinai?

Mhe. Lissu: Jinai ziko ngapi sasa? Alitakiwa kueleza kuwa jinai ni ipi?

Katuga: Ni bado unasema kwenye hiyo nyaraka kuna contradiction

Mhe. Lissu: Nimeshaonesha.

Katuga: D2 unakumbuka ulimuhoji kwamba yeye ni mtaalamu wa picha aliyetangazwa kwenye GN 725 akajibu maneno hayo hayamo.

Mhe. Lissu: Ndio.

Katuga: Je hiyo ni Contradiction?

Mhe. Lissu: Ni comtradiction ndio kwasababu zilitajwa GN. mbili tofauti. Ni contradiction ya akichokisema kwenye maelezo yake ya maandishi.

Katuga: Yale majibu yote aliyosema hayamo yalikuwa ni contradiction au ommission?

Mhe. Lissu: Ni omission

Katuga: Ulisema hiyo omission inaenda kwenye root ya kesi

Lissu: Tutasema hayo mengine kwenye final submission mimi ni shahidi wa facts.

Sehemu ya 292

Katuga: Naomba twende kwenye D3 Lissu anasema ngoja nitafute. Ametafuta kwa muda mrefu ameipata sasa.

Katuga: D3 kielelezo alisema ananunua Ilala Boma Sokoni. Hiyo ni omission au contradiction?

Mhe. Lissu: Ni omission na ni contradiction pia.

Katuga: maneno kwamba hayamo kwenye maelezo yake kwa mujibu wa jibu hili yanakanganyana na nini?

Mhe. Lissu: Yanakanganyana na kariakoo na Posta Mpya. Wakati huku amesema Ilala Boma.

Katuga: Swali kwa PW4 kwamba alikuwa na smartphone sony Galaxy yapo au hayamo kwenye kielelezo. Alisema hayamo.

Mhe. Lissu: Ndio. Na ni Omission.

Katuga: Kuhusu kuwa na account facebook hajaandika kwenye maelezo? Unasemaje.?

Mhe. Lissu: Hakuandika ni Omission.

Katuga: Alisema amemuona Tundu Lissu kuhusu na hiyo ni Contradiction au Omission?

Mhe. Lissu: Ni Omission

Katuga: huku alisema mzozo huku amesema mabishano. Kwani utofauti ni nini?

Mhe. Lissu: Mzozo ina element za ugomvi hakuna ustaarabu mabishano ni kutofautiana mawazo. Hata marafiki wanabishana.

Wameomba break ya dakika kumi

Sehemu ya 293

Katuga: Tuahirishe kidogo kutoka kwenye D4 hivyo vielelezo tuhamie eneo lingine. Ulisema hawajaleta video kwahiyo wameshindwa kuthibitisha mashitaka yao wenyewe ulisema hivyo?

Mhe. Lissu: Ndio.

Katuga: Wakati unayasema hayo ulikuwa unayajua mashitaka yanayokukabili?

Mhe. Lissu: Ndio

Katuga: Ulikuwa umeyaelewa?

Mhe. Lissu: Sana tu.

Katuga: Mashitaka unayokabiliana nayo kuna sehemu yoyote inayosema unashitakiwa kwa kuchapisha video?

Mhe. Lissu: nachapisha maneno kwenye video iliyosambazwa na jambo Tv.

Katuga: Kwa mujibu wa ushahidi video kiushahidi ina kitu ambacho unaona na kusikia?

Mhe. Lissu: Sawa.

Katuga: Maneno yanaonwa au yanasikiwa?

Mhe. Lissu: Maneno yanasikiwa na kuonwa kwenye kesi hii. Kwa mujibu wa sheria ya ushahidi kitu chakuonwa kinaonwa na chakusikiwa kinasikiwa.

Katuga: Kwenye hiyo video maneno unaona au unasikia?

Mhe. Lissu: Iko wapi sasa hiyo video. Ninayo hapa??

Katuga: Kwahiyo walichokileta ndio walichokisia?

Mhe. Lissu: Huwezi kutenganisha video na maneno. Kivipi sasa? Maneno yapo kwenye video.

Katuga: Kila shahidi anapaswa kuaminiwa?

Mhe. Lissu: Washahidi wa kweli ndio huaminiwa. Waongo hawaaminiwi.

Katuga: Je katika mashahidi wa Jamhuri ni kifungu gani cha Sheria kinasema lazima ulete video ndio tuseme maneno yalisemwa?

Mhe. Lissu: Hiyo ni common sense tu.

Katuga: Akija shahidi akasema niliona radi imepiga na kuua watoto lazima alete video ndio tumuamini?

Mhe. Lissu: Sasa radi na video vinahusiana. Video ilirekodiwa. Sasa radi nani ameruhusu itokeee hadi useme irekodiwe.

Katuga: kama video ikifutwa mtu aliyeona hawezi kutoa ushahidi na kuthibitisha?

Mhe. Lissu: Unakuja kuthibitisha video ipi sasa wakati huna?

Katuga: Kati ya maneno au video ameleta nini?

Mhe. Lissu: Hajaleta chochote. Maneno ya kwenye video yapo kwenye video. Hayawezi kutenganishwa.

Katuga: PW17 alikuwepo Live kwenye Mkutano wako na alisema anayoyakumbuka kwamba mtazuia uchaguzi.

Mhe. Lissu: Hakusema hivyo.

Katuga: Shahidi aliyekuwepo eneo la tukio PW17 ni lazima alete video?

Mhe. Lissu: Ni lazima kwasababu aliyaleta mambo ya video mwenyewe inabidi iwepo.

Katuga: PW 17 kuna mahali alisema alikuwa anaiona na kuisikia?

Mhe. Lissu: Alikuwa anarusha matangazo live sasa atarushaje bila kuiangalia?

Katuga: Mashahidi mapolisi hawaaminiki kwasababu waliandika maelezo yao wenyewe?

Mhe. Lissu: Hawaaminiki kwasababu hawakufuata taratibu za kuandika maelezo.

Katuga: Kila shahidi anaaminika

Mhe. Lissu: Anaaminika shahidi kwasababu ya ushahidi wake sio sura yake.

Katuga: Mimi sina nia mbaya.

Mhe. Lissu: Umenishtaki kwa uhaini halafu uwe hauna nia mbaya.

Katuga: Kifungu gani cha Sheria kinakataza Mapolisi kutoa ushahidi

Mhe. Lissu: Mashahidi ambao hawakufuata utaratibu ndio ushahidi wao hauwezi kuchukuliwa kwa uzito wowote.

Mahakama imeahirishwa mpaka saa nane na nusu


​
Mahakama imerejea......Sehemu ya 294

Mwenyekiti Lissu, ameingia tayari baada ya kumaliza kuongea na mawakili wake na break pia kwa ajili ya Chakula cha Mchana.

Alipata nusu saa pia ya kukaa na Mawakili wake na mashahidi wake wengine. Mh. Heche, Mnyika, Amani na Brenda walikuwepo nae.

Jaji Ndunguru: Mshitakiwa uko tayari tuendelee.

Mhe. Lissu: Niko tayari.

Katuga: Mh. Jaji naomba Exhibit D15. Makarani wanaitafuta. Ni maelezo ya PW 16. Ulisema wapelelezi hawakukuuliza maana ya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka?

Mhe. Lissu: Ndio

Katuga: PW 1 alisema alikuhoji kuhusu maana ya maneno yako?

Mhe. Lissu: Hakunihoji hilo.

Katuga: PW 1 alisema alikupa nafasi kuhusiana na haya maneno kwanini yasiwe ya uhaini?

Mhe. Lissu: Nilimjibu mmeshanikamata na mmeshanishitaki tutakutana mahakamani ndio nilimjibu.

Katuga: PW 1 alikupa nafasi au hakukupa nafasi?

Mhe. Lissu: Alishanishtaki kwa uhaini.

Katuga: Ulizuiwa nini ulipoambiwa utoe maelezo yako?

Mhe. Lissu: Tutakutana mahakamani

Katuga: Ndio maana hukutaka kutoa maana ya maneno?

Mhe. Lissu: Sikuulizwa kuhusu maneno alisema kuhusu uhaini, nikamwambia twende mahakamani.

Katuga: Ungeweza kutoa maana ya maneno au usingeweza pale angekuuliza?

Mhe. Lissu: Sasa halikuulizwa hilo nitoleee nini? Ningejibu angeniambia.

Katuga: Ulirejea Maelezo D15 ni maneno ambayo umeyaamini na yapo kwenye kielelezo chako?

Mhe. Lissu: Maneno yapi? Unauliza mambo jumla jumla. Eleweka.

Katuga: Baada ya kuunda timu mimi na timu tulisikia

Mhe. Lissu: Tulisikiliza sio tulisikia soma vizuri wewe

Katuga: Nina miwani siku hizi sioni vizuri.

Mhe. Lissu: Ukiwa na miwani ndio unasoma vizuri acha uongo.

Katuga: Yangu ni ya bei halisi

Lissu: Sasa unalipwa nini? Au unajitutumua bure tu hapa?

Katuga: Je haya maneno nimesoma ulirejea?

Mhe. Lissu: In relation na ushahidi wa PW1 ndio niliyarejea. Kuhusianisha na PW 16 alichosema.

Katuga: Kwahiyo ulikiamini kielelezo?

Mhe. Lissu: Nilikiamini kivipi? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.

Katuga: Kwahiyo ulikiamini?

Mhe. Lissu: Mimi niwaamini Mapolisi hawa? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.

Katuga: Sasa nijibu unayaamini yaliyomo humo?

Mhe. Lissu: Niamini nini?

Katuga: Uko sawa kweli?

Mhe. Lissu: Wee unanionaje?

Katuga: Naona uko sawa.

Mhe. Lissu: Sasa unaniuliza nini kama unasema niko sawa?

Jaji: Sasa wakili toka hapo. Tumeshapata majibu.

Katuga: Ulisema haya maelezo yote kuanzia D1 hadi D16 ulitaka yatumike kwa ajili yako?

Mhe. Lissu: Nilishajibu toka zamani. Kwa ajili ya kuonesha utofauti wa ushahidi. Contradiction ya ushahidi na ommission zilizofanyika.

Katuga: Kuna sehemu ulisema mahakama i exclude baadhi ya maneno yaliyopo humu?

Mhe. Lissu: Hiyo ni kazi ya submission.

Katuga: Narudia tena ulisema au hukusema?

Mhe. Lissu: Nimekwambia hiyo ni kazi ya submission.

Jaji Ndunguru: jibu tu swali shahidi umeiambia mahakama au hujaiambia.

Mhe. Lissu: Narudia tena nitawaambia wakati wa final submission nimemaliza.

Jaji Ndunguru: Haya sasa wakili wa serikali endelea mbele. Jibu ndio limeshatoka hilo na halitabadilika.

Katuga: Mheshimiwa Jaji naomba nirudishe kielelezo.

Anaendelea kupekua makaratasi yake. Kamaliza maswali ila anatupotezea muda tu hana lolote mshenzi huyu.

Sehemu ya 295

Katuga: Naomba niishie hapa nisiulize maswali mengine niishie hapa. Niwaachie wenzangu.

Anasimama Job Mrema. Nae kuuliza maswali.

Job Mrema: wewe ni mwanaharakati ulisema?

Mhe. Lissu: Ndio

Job: Ulianza lini?

Mhe. Lissu: Nilisema habari za nilipokuwa sekondari, jeshini na kadhalika nilielezea.

Job: Uwanaharakati ni nini?

Mhe. Lissu: Uanaharakati ni mtu anayefanya jitihada za kupigania jambo au mambo fulani.

Job: Wewe pia ni mwanasheria?

Mhe. Lissu: Ndio

Job: Huu uanaharakati unatambulika kwa mujibu wa sheria za nchi?

Mhe. Lissu: Ndio

Job: kifungu gani?

Mhe. Lissu: Kuanzia ibara ya 12 hadi 29 ya Katiba vinatoa uwanja mpana wa kufanya jitihada za kupigania mambo mbalimbali.

Job: sasa ibara ya ngapi imesema harakati ni nini?

Mhe. Lissu: Hujielewi wewe. Nimeshakwambia hizo ibara zinasema watu ni huru, ukipigania uhuru wa watu maana yake unafanya harakati. Katiba inasema haki ya Uhai na kuishi ukipigania kupinga adhabu ya kifo maana yake unafanya harakati za kupigania haki ya kuishi.

Huyu Job Mrema yeye huwa ni kilaza wa aina yake.

Job Mrema: Ni sahihi maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka na walioyasikia waliyatafsiri kadri yalivyo?

Mhe. Lissu: Hawakutafsiri kadri yalivyo.

Job Mrema: Hakuna mahali popote kwa sheria za nchi hairuhusiwi watu kujichukulia sheria mkononi?

Mhe. Lissu: Hakuna sheria inayoruhusu watu kuvunja sheria. Kuhusu Sheria za Uchaguzi nasema kwamba uchaguzi usio huru na haki basi ni haki yao wananchi kuuzuia.

Job: Ukiwa mwanaharakati una kinga ya kufuata sheria?

Mhe. Lissu: Nilishajibu hauna kinga. Kama huna maswali ukakae.

Job: Ukiwa mwanasiasa je?

Mhe. Lissu: Huna kinga.

Job: Ulisema kesi hii ya kisiasa. Je wewe umeshitakiwa kama Tundu Lissu au mwanasiasa.

Mhe. Lissu: Nimeshitakiwa kama Tundu Lissu ambae ni mwanasiasa. Nisingekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA nisingekuwa hapa.

Job Mrema: Kwa mujibu wa hati ya mashitaka kuna mahali wamesema wewe ni mwanasiasa?

Mhe. Lissu: Mashahidi wote wanasema mimi ni Mwenyekiti wa CHADEMA. PH imesema mimi ni Mwenyekiti wa Chadema. Kwahiyo hati haisemi lakini huko kwingine kote ni Mwenyekiti wa Chadema.

Job Mrema: Ulisema umewahi kushitakiwa na ushahidi uliotoa hapa hujaeleza ulishitakiwa kwa kesi gani? Kesi namba ngapi ya Mahakama gani?

Mhe. Lissu: Nilielezea taarifa zakutosha kuhusu kesi hizo mahakama inajua.

Job: Ulisema huwezi kuwa Rais wa TLS halafu ukawa mtu wa hovyohovyo?

Mhe. Lissu: Hilo nilijibu zamani sana. Nilitumikia hiyo nafasi miezi mitano nikapigwa risasi.

Job: Ni sahihi ukitoka kuwa Rais wa TLS unaweza kuwa mtu wa hovyo hovyo?

Mhe. Lissu: Huyu sio mtu wa hovyohovyo. Na nina heshima zakutosha huko Duniani

Job: Umewahi kulalamika kokote kuhusu risasi ulizopigwa?

Mhe. Lissu: Anasimama sasa. Nimelalamika sana. Na wamekataa kuandika maelezo toka nikiwa hospitali Nairobi. Hawajawahi kuandika.

Job Mrema: Umejinasibu kama Mwanasheria

Mhe. Lissu: Kwani wewe hujui kama mimi ni mwanasheria? Utanifananisha na wewe?

Job Mrema: Kifungu cha 10(1) (2)cha CPA. Kinasemaje

Mhe. Lissu: Anakisoma kinahusu kuandikwa kwa maelezo.

Job Mrema: Unakielewaje?

Mhe. Lissu: Taarifa za kosa zinatolewa kwa maandishi au mdomo kwa afisa husika kwenye eneo husika.

Job Mrema: Ulikwenda kutoa taarifa?

Mhe. Lissu: Sikwenda kwasababu nilikuwa nusu mfu. Ulitaka niende lini? Nisingeweza kutoa hayo maelezo nilikuwa napigania uhai wangu.

Job Mrema: Jinai inakufa?

Mhe. Lissu: Ndio maana nilivyorudi nilienda kwa RPC Mroto Dodoma. Nikamwambia mlikuwa mnasema sikuwepo sasa nimerudi haya nihojini sasa kuhusu haya mambo. Hawakuwahi kunihoji kokote.

Job Mrema: Unapopata taarifa ya vitisho ni sahihi upeleke polisi hizo taarifa?

Mhe. Lissu: Ni sahihi kama hivyo vitisho havitoki kwa polisi wenyewe. Kama wanakutisha polisi unaenda tena polisi kutoa taarifa hizo kuwa wanakutisha. Utakuwa mwehu sio bure.

Sehemu ya 296

Wakili wa Serikali Job Mrema: Kama kuna mgogoro si unatakiwa kwenda Mahakamani?

Mhe. Lissu: Ukiwa ni mgogoro wa kiimani unaenda kanisani na msikitini kutatua. Yakisheria ndio unaenda Mahakamani.

Job Mrema: Unakubaliana na mimi kuwa ulisema majaji hawatendi haki?

Mhe. Lissu: Hilo sio geni amelisema jaji Nyalali, Tume ya Warioba imesema. Hata na kikosi kazi pia kimesema. Hakuna jipya hapo.

Job Mrema: Ulisema Majaji ni Ma CCM na Huko Mahakamani hakuendeki?

Mhe. Lissu: Ndio.

Job Mrema: Kupandikiza wananchi chuki katika mfumo wa utoaji haki ni kosa? This is general question.

Mhe. Lissu: hiyo chuki maana yake nini sasa? Niambie kwanza.

Job Mrema: Kifungu cha 52 cha Media service Act. Kinasemaje na unakionaje?

Mhe. Lissu: Kama ukisababisha chuki, dharau au kutokuridhika na mfumo wa utoaji haki ni nia ya kichochezi.

Job Mrema: ukiwa na nia unakiuka kifungu hicho

Mhe. Lissu: Kwa maana ya kifungu cha 52(2) hukiuki lakini 51(1) C ni sawa.

Job Mrema: Kuhusu Majaji ni ma ccm na mahakamani hakuendeki hiyo statement inakiuka kifungu cha 52(1)

Mhe. Lissu: Sikubaliani na wewe kabisa.

Job Mrema: Kulikuwa na amri ya kuficha mashahidi?

Mhe. Lissu: Ndio

Job Mrema: Hukuchukua hatua.

Mhe. Lissu: Niko gerezani unataka nichukue hatua gani?

Job Mrema: Unawakumbuka mashahidi wa siri?

Mhe. Lissu: Nawakumbukaje wakati nimekwambia siwafahamu? Unawafahamu wewe. Majaji na mimi.

Job Mrema: Ni sahihi kwamba uamuzi wa mashahidi wa vificho hauwezi kuzungumziwa kwenye kesi hii?

Mhe. Lissu: ingekuwa haiwezekani hivyo vizimba hapo visingefumuliwa kipindi kile. Kwani nilipinga kwenye kesi gani ya Bibi yako?

Jaji: Haya tuendelee swali lingine.

Job Mrema: Mheshimiwa tunaendelea.

Jaji Ndunguru: Sasa nyie si mpo wengi hapo Mawakili wa Serikali mwingine aingie haraka aanze kuuliza wakati huyu anatafuta maswali yake.

Job Mrema: Uliwasilisha chochote kuhusu kupigwa Tar. 11/08/2024 kule Mbeya?

Mhe. Lissu: Nimesema kwa mdomo na ndio maana niliapa kabla ya kutoa ushahidi.

Job mrema: Tar. 23/09/2024 ulivamiwa nyumbani kwako na polisi na hakuna ushahidi wowote ulioleta?

Mhe. Lissu: Nilisema nivamiwa na kukamatwa wakanipeleka mbweni na usiku walinirudisha nyumbani. Ulitaka nilete nini kwenye hayo maneno?

Job Mrema: Ulisema watu 466 ulisema case no zao wale wa Tarime.

Mhe. Lissu: Sikueleza.

Job Mrema: PW1 ulisema alifungua jalada tarehe 04 April

Mhe. Lissu: Nilivyosema mimi au PW 1 mwenyewe ndio alisema.

Job Mrema: PW 1 Kwahiyo umesema ilikuwa ni lazima amwambie DPP kuhusu mashitaka haya?

Mhe. Lissu: Soma kifungu cha 16 na 24 cha National Prosecution Act kinasema makosa ya jinai ni DPP ndio anapaswa ku coordinate ushahidi. Sasa yeye hakufanya hivyo. Hakuwahi kumpa taarifa na alisema hivyo.

Job Mrema: Ni chombo kipi kimepewa mamlaka ya huyu ana hatia na huyu hana hatia?

Mhe. Lissu: Ilikuwaje nyie polisi mseme huyu ni mkosaji wa uhaini hata kabla ya ushauri wa DPP?

Job Mrema: Sasa kama mashitaka yalikosewa unafanya nini?

Mhe. Lissu: Najitetea kwa makosa ya kubambikizwa.

Job Mrema: Mahakama hii imetoa uamuzi kuhusiana na makosa yako?

Mhe. Lissu: Haijatoa.

Job Mrema. Amerudi kwa wenzake wanaongea kama dakika tano hivi. Jaji Ndunguru anawaangalia kwa hasira sana.

Anasimama anasema naomba kuishia hapa nimkaribishe Ajuaye Zengeli.

Ajuaye: Ni sahihi kwamba wakati mnafanya mkutano huo hamkuwa na kibali chochote?

Mhe, Lissu: Hakuna mkutano wa ndani unahitaji kibali. Pia hakuna mkutano wowote wa vyama vya siasa unahitaji kibali unatakiwa kutoa taarifa tu.

Ajuaye: PGO 403

Mhe. Lissu: Soma wewe inasemaje nikujibu swali.

Ajuaye: Basi soma PGO 402

Mhe. Lissu: Inahusu mikutano ya kampeni

Ajuaye: Umekielewaje?

Mhe. Lissu: Mambo ya uchaguzi na taratibu za kampeni za uchaguzi

Sehemu ya 297

Ajuaye: Ulitoa taarifa sasa wewe polisi?

Mhe. Lissu: Ilikuwa ni miezi sita kabla ya uchaguzi. Natoaje taarifa polisi wakati siku kwenye mkutano wa kampeni na nilishakwambia sikuwa nafanya public meeting.

Ajuaye: Soma kifungu cha 23 cha Political parties act

Mhe. Lissu: Soma wewe uliza swali.

Ajuaye: anakisoma je ulitoa taarifa

Mhe. Lissu: Siwezi kutoa taarifa mikutano ya ndani. NEXT?

Ajuaye: Kifungu kinasema public place or any other area

Mhe. Lissu: Hujui wewe hata kusoma kingereza kifungu kinasema public meeting conducted at any area. Sasa wewe umesoma shule gani Dada angu?

Ajuaye: Tulia kwanza. Una kifungu chochote kinachosema unaweza kufanya mkutano wa ndani bila kibali?

Mhe. Lissu: Hicho hicho kifungu cha 23 cha Sheria ya Vyama vya siasa.

Ajuaye: Maneno ya kukinukisha uliyakubali hata kama video hatujaleta?

Mhe. Lissu: Sikuongea maneno ya Uhaini mimi.

Ajuaye: Ni ukweli kwamba hata kama video haikuletwa lakini uliongea maneno ambayo yapo kwenye hati ya mashitaka?

Mhe. Lissu: Maneno niliyoshitakiwa kwamba yalikuwepo kwenye video yalikuwa ya masaa matatu hayakuwa ya uhaini.

Ajuaye: Video ni kifaa kilichobeba maandishi?

Mhe. Lissu: Kumbe iko hivyo? Mimi sijui.

Ajuaye: subiri nikiwa mshitakiwa au shahidi utaniuliza. Nitakuomba uwe Wakili wangu?

Mhe. Lissu: Siwezi kuwa na mteja kama wewe ambae anasingizia singizia watu makosa.

Ajuaye: ni kweli mahakama ndio inaweza kusema mtu fulani amefanya kosa fulani?

Mhe. Lissu: Itasema kama mtu huyu atakuwa amepelekwa mahakamani.

Ajuaye: Nani anasema walikamatwa kwasababu walikuwa na makosa?

Mhe, Lissu: Walikamatwa bila kuwa na makosa.

Ajuaye: Ulisema kama ukamataji wako ulikosewa?

Mhe. Lissu: Nilisema na Kiswaga aligoma kuandika na hapa nilisema kwenye mahakama hii.

Ajuaye: Ni very serious allegation hizo

Mhe. Lissu: Ndio ndio maana nilileta mahakamani na wewe ulikuwepo siku ile. Uliona.

Ajuaye: Wanaosimamia sheria ya uchaguzi ni serikali?

Mhe. Lissu: Sheria ya Uchaguzi inasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Na tume ya Uchaguzi sio Serikali.

NB. Leo nimeshuhudia ni kwa kiwango gani TAIFA lina Mawakili wa Serikali ni VILAZA.

Ajuaye: Kupinga uchaguzi ni takwa la kisheria?

Mhe. Lissu: Sisi tulikuwa tunataka uchaguzi usifanyike kabisa. Mambo ya kupinga hata kwenye uchaguzi halali kuna kupinga matokeo ya uchaguzi.

Anakuja askari wa Magereza huwa ni mnaa mnaa sana. Mnoko sana. Amewafuata mawakili wa serikali kwasababu imefika saa 11 na nusu kwa sasa.

Wanajadili mawakili wa Serikali muda huu.

Mhe. Lissu: Ule utaratibu wa kuishia saa 11 kamili vipi tumeubadilisha.

Jaji Ndunguru: Tulidhani wanamaliza maswali yao ndio maana tukawa tunawaangalia tu. Sasa ngoja tuwaulize. Upande wa serikali mnasemaje?

Ajuaye: Basi tuahirishe hadi kesho.

Jaji Ndunguru anateta na wenzake.

Live Tweet: Hilda Newton

Kesi imehairishwa mpaka Agosti 28, 2026 | Saa 3:00 Asubuhi


 
Hao majaji wamepangwa, hii kesi mwisho wake ni kukosekana kwa ushahidi kumtia hatiani TL. Lengo ni kumtesa tuu.
Hii ndio itakuwa hukumu ya hovyo ya mashitaka ya uhaini, kusikilizwa na majaji wa hovyo, na kuamuliwa kihivyo hovyo. Rekodi zitabaki zitakuwa za hovyo.
 
Hatua ya maswali ya dodoso (Cross Examination) kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, yanatarajiwa kutamatishwa leo Agosti 27, 2026 na kufungua mlango kwa shahidi mwingine wa Lissu kupanda kizimbani kwaajili ya kutoa utetezi wake.


Jana Agosti 26, 2026, Tundu Lissu alihitimisha kutoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Jaji, Dunstan Ndunguru, ambapo ambapo baada ya hatua hiyo, upande wa Jamhuri (Washtaki) walipewa nafasi ya kuuliza maswali hayo kwa mshtakiwa.

Katika utetezi wake wa Jana, Lissu alidai kwamba Ushahidi uliotolewa na Askari Polisi wa upande wa Jamhuri, ulikuwa unatofautiana kwa maelezo waliyoyaandikaa Polisi na yale waliyoyawasilisha mahakamani.
Waufukweni tunaomba muendelezo basi. Kama mambo ni magumu umkaribishe Manyanza na yeye aweke mkono wake.
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO

Jamani, tunaanza kesi soon.

Majaji wameingia.

Na Lissu ameingia tayari.

Lissu anapanga documents zake.

Majaji wapo kimya kidogo.

Kesi inasomwa na karani wa Mahakama.

Kesi ya Jinai, kesi namba 19605, Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.

Wakili wa Serikali, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha mawakili wenzake:

1. Nassoro Katuga
2. Tawabu Issa
3. Job Mrema
4. Ignasi Mwinuka
5. Mbilinyi
6. Kasara

Kwa pamoja tunawakilisha Serikali, na mshtakiwa yupo tayari.

Kesi inakuja kwa ajili ya dodoso.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nipo tayari, ila kama inawezekana naomba only five minutes za consultation.

Jaji Ndunguru: Sawa.

Wakili Dkt. Lugemeleza Nshala anasogea kizimbani. Wanazungumza na Tundu Lissu.

MAHAKAMA IPO KIMYA KIDOGO.

Lissu: Tupo tayari, Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: Tuendelee na cross-examination.

Nassoro Katuga: Asante, Waheshimiwa Majaji. Naomba tuendelee na dodoso.

Nassoro Katuga: Kaka yangu, shikamoo.

Lissu: Marahaba.

Nassoro Katuga: Unajionaje na hali?

Lissu: Alhamdulillah.

Nassoro Katuga: Unakumbuka ushahidi wako kwamba ulipewa tuzo ya utawala bora?

Lissu: Nakumbuka.

Nassoro Katuga: Ulitaja hizo nchi?

Lissu: Sikuzitaja.

Nassoro Katuga: Uliiambia Mahakama kwamba kukaa kwako gerezani heshima yako imeongezeka. Je, ni lini umefanya hiyo sensa?

Lissu: Heshima haitokani na sensa.

Nassoro Katuga: Heshima inatokana na wingi wa watu wanaokuheshimu?

Lissu: Heshima haitokani na wingi.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo wazungu wakikuheshimu, ndiyo heshima imeongezeka?

Lissu: Sijataja wazungu, bali Jumuiya za Kimataifa.

Zikikaa zikasema, “Muachieni huyu, ni mtu wa heshima,” hiyo ni heshima.

Nassoro Katuga: Mimi sijakuuliza hayo, umeshajibu.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako ulizungumzia mgombea wa Mlimba kwamba alirudisha fomu, akakuta mtu hayupo. Wakati anarudisha fomu ulikuwepo au uliambiwa?

Lissu: Sikuwapo, ila nimesoma katika taarifa rasmi ya uchaguzi.

Nassoro Katuga: Umeshasema hukuwepo.

Lissu: Lakini nimesoma katika taarifa rasmi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ni kweli uliwaambia hawa wengine wawili wa kificho hawajulikani hapa Mahakamani isipokuwa waendesha mashtaka.

Lissu: Ndiyo, nimesema.

Nassoro Katuga: Waambie pia Waheshimiwa Majaji kwamba haya maneno umesema kuonyesha ukweli wako.

Lissu: Kweli.

Nassoro Katuga: Ulileta kipingamizi kwa jinsi kizimba cha mashahidi kilivyokaa?

Lissu: Ndiyo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO

Jamani, tunaanza kesi soon.

Majaji wameingia.

Na Lissu ameingia tayari.

Lissu anapanga documents zake.

Majaji wapo kimya kidogo.

Kesi inasomwa na karani wa Mahakama.

Kesi ya Jinai, kesi namba 19605, Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.

Wakili wa Serikali, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha mawakili wenzake:

1. Nassoro Katuga
2. Tawabu Issa
3. Job Mrema
4. Ignasi Mwinuka
5. Mbilinyi
6. Kasara

Kwa pamoja tunawakilisha Serikali, na mshtakiwa yupo tayari.

Kesi inakuja kwa ajili ya dodoso.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nipo tayari, ila kama inawezekana naomba only five minutes za consultation.

Jaji Ndunguru: Sawa.

Wakili Dkt. Lugemeleza Nshala anasogea kizimbani. Wanazungumza na Tundu Lissu.

MAHAKAMA IPO KIMYA KIDOGO.

Lissu: Tupo tayari, Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: Tuendelee na cross-examination.

Nassoro Katuga: Asante, Waheshimiwa Majaji. Naomba tuendelee na dodoso.

Nassoro Katuga: Kaka yangu, shikamoo.

Lissu: Marahaba.

Nassoro Katuga: Unajionaje na hali?

Lissu: Alhamdulillah.

Nassoro Katuga: Unakumbuka ushahidi wako kwamba ulipewa tuzo ya utawala bora?

Lissu: Nakumbuka.

Nassoro Katuga: Ulitaja hizo nchi?

Lissu: Sikuzitaja.

Nassoro Katuga: Uliiambia Mahakama kwamba kukaa kwako gerezani heshima yako imeongezeka. Je, ni lini umefanya hiyo sensa?

Lissu: Heshima haitokani na sensa.

Nassoro Katuga: Heshima inatokana na wingi wa watu wanaokuheshimu?

Lissu: Heshima haitokani na wingi.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo wazungu wakikuheshimu, ndiyo heshima imeongezeka?

Lissu: Sijataja wazungu, bali Jumuiya za Kimataifa.

Zikikaa zikasema, “Muachieni huyu, ni mtu wa heshima,” hiyo ni heshima.

Nassoro Katuga: Mimi sijakuuliza hayo, umeshajibu.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako ulizungumzia mgombea wa Mlimba kwamba alirudisha fomu, akakuta mtu hayupo. Wakati anarudisha fomu ulikuwepo au uliambiwa?

Lissu: Sikuwapo, ila nimesoma katika taarifa rasmi ya uchaguzi.

Nassoro Katuga: Umeshasema hukuwepo.

Lissu: Lakini nimesoma katika taarifa rasmi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ni kweli uliwaambia hawa wengine wawili wa kificho hawajulikani hapa Mahakamani isipokuwa waendesha mashtaka.

Lissu: Ndiyo, nimesema.

Nassoro Katuga: Waambie pia Waheshimiwa Majaji kwamba haya maneno umesema kuonyesha ukweli wako.

Lissu: Kweli.

Nassoro Katuga: Ulileta kipingamizi kwa jinsi kizimba cha mashahidi kilivyokaa?

Lissu: Ndiyo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Moto unawashwa kidogo kidogo
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba baada ya kurekebishwa, Majaji walikuwa wanawaona.

Lissu: Wanawaona, ila hawawajui majina wala chochote kuhusu wao.

Nassoro Katuga: Iambie Mahakama ulikuwa unarefer mashahidi wa P1 na P2.

Lissu: P siyo jina la mtu, ni jina bandia. Hakuna mtu anaitwa P2. (Mahakama kicheko.)

Nassoro Katuga: Ni sheria gani inayoiambia Mahakama ni lazima ijue jina la shahidi na lisiwe jina la bandia anapotoa ushahidi?

Lissu: Ni CPA na Sheria ya Ushahidi.

Nassoro Katuga: Ndizo zinasema shahidi hatatoa ushahidi mpaka jina lake lijulikane?

Lissu: Shahidi hawezi kutoa ushahidi Mahakama haimjui na mshtakiwa hamjui.

Nassoro Katuga: Ni kifungu gani cha CPA kinasema shahidi atajulikana jina wakati wa kutoa ushahidi?

Lissu: Ukitaka kifungu, lazima niende katika CPA.

Nassoro Katuga: Waambie Majaji.

Lissu: Anafungua CPA yale kizimbani, anasema kifungu cha 192.

Nassoro Katuga: Swali langu ni kuhusu jina halisi na jina bandia. Je, kifungu gani kinasema shahidi hatatoa ushahidi unless jina lake limetajwa?

Lissu: Kifungu cha 192 kinasema shahidi ataulizwa majina yake.

Nassoro Katuga: Ndicho kifungu kinasema shahidi hatatoa ushahidi wake mpaka ajulikane jina?

Lissu: Sheria in general ndiyo inasema hivyo, isipokuwa kwa kesi za watoto na sexual abuse, Mahakama itakaa in camera.

Nassoro Katuga: Nisomee kifungu sasa kinasema lazima ataje jina.

Lissu: Hakuna kifungu cha namna hiyo. Hiyo ni sheria ya wapi?

Nassoro Katuga: Unakumbuka katika ushahidi wake P17 akisema kuna muda katika mkutano wenu mliwatoa waandishi wa habari mkawa na kikao cha ndani?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Je, kuna sehemu umekanusha kuwa hamkuwatoa waandishi wa habari?

Lissu: Sikuona sababu ya kukanusha.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo unakiri kwamba kuna muda mliwatoa waandishi wa habari?

Lissu: Hawakuwa wanahitajika tena. Tulishamaliza tuliyowaitia, siyo kwamba tuliwatoa na kuwarudisha.

Nassoro Katuga: Majibu yako yanavutia sana.

Lissu: Unapaswa kufurahi kama yanavutia. Nashangaa kuona unashangaa.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo nichekecheke?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo mliwatoa waandishi wa habari?

Lissu: Ndiyo, tuliwatoa.

Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba umesema kwamba mliwatoa kwa sababu hayo mengine hayakuwa sehemu ya mlichowaitia?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Mtu akisema kwamba yake ambayo hamkutaka yachapishwe, mliwatoa waandishi wa habari?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo sasa hivi unawaambia Waheshimiwa Majaji kwamba ni kweli yale yaliyochapishwa ulitaka yachapishwe?

Lissu: Yale yote yaliyochapishwa ni yale yaliyokuwa yanawahusu waandishi wa habari.

Nassoro Katuga: Si ndiyo ulitaka yachapishwe?

Lissu: Yalikuwa yanawahusu waandishi wa habari.

Nassoro Katuga: Uliambia Mahakama hii kwamba PW1 katika ushahidi wake alipogundua kosa la uhaini hakuwasiliana na IGP, ZPC, DGIS, DCI wala Afisa Usalama wa Taifa?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Ukitaja kifungu mahususi kwamba kinamtaka mpelelezi awasiliane na hao kabla ya kufungua kesi.

Lissu: Sikutaja, ila haina maana hakipo.

Nassoro Katuga: Unakumbuka ukisema kuna mgongano baina yako na IGP na DCI?

Lissu: Siku sema mgongano binafsi. Nimesema wana chuki kubwa dhidi yangu kwa miaka 24.

Nassoro Katuga: Je, ulishawahi kuwafungulia Malicious Prosecution dhidi ya hawa wawili?

Lissu: Sijawahi, lakini haina maana hawajawahi kunishitaki.

Nassoro Katuga: Ulisema kuhusu mashahidi ambao ni washitakiwa.

Lissu: Nilisema kuhusu waliopanga uhalifu kuachiwa na kuja kutoa ushahidi hapa.

Nassoro Katuga: Kuna sheria inazuia wahalifu kutoa ushahidi?

Lissu: Hakuna, ila...

Nassoro Katuga: Ila ni ya kwako, umeshanijibu.

Nassoro Katuga: Ukisema kwamba Polisi waliwakamata wote waliopanga kuzuia uchaguzi.

Lissu: Waliokamatwa ni waliotambuliwa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom