Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

Kisheria hukamatwi kwa kosa ambalo wakati unakamatwa hukulitenda.

🫎🫎🫎🫎🫎 Sheria ya wapi
Wewe utakamatwa kwa kosa la kuwauwa Wananchi
Sababu niwewe ndio chanzo cha ule MOTO ✅️

KWASASA Lissu kikubwa anachofanya pale Mahakamani ni kukaa kukaa kuwasha 💥💥💥💥💥💥💥💥 na upande wa Jamhuri Unapambana kuonesha niyeye ndio chanzo cha MOTO wa Mo29 ✍️
 
Hakuna kitu kama hicho. Kama ni hivyo hata yule aliyesema hakutakuwa na nywinywi wala nywinywi alkamatwe maana naye amechochea hasira za watu.

Kivipi yeye katutoa Shaka tu sisi Wananchi

Wkt uyo Tundu Mwenye risasi mwilini katuwashia MOTO Wananchi 💥💥💥💥💥💥 tumezikana wa kutosha✍️
 
Lissu mjanja anamlinda shahidi wake na kunyonga upande wa pili, mpaka hapa amefaulu na shahidi ametulia, hana wenge.

Wenge hapewi na Lissu

ngoja kesho John Mnyika majina yake kama
Ajayasahau nyumbani

Na miaka yake 🤠✍️

Kesho ndio kesho John Mnyika kaingia kwenye Mfumo ✍️
 
Nilijua tu Ajuaye Zengeli alkiendelea na maswali atabagzwa walete masuala ya jinsia kama Katuga mwenyewe aliwaambiwa nilikuambia usiwe mjinga, Mrema akaambiwa nimekuambia kwenye kesi unadhani ni kwenye kesi ya bibi yako? Bora Ajuaje amekimbia
 
Sasa ndugu yangu Econonist
Lissu ndio chanzo baada kutangaza kukinukisha kuzuiya Uchaguzi nk.

Nayeye ni mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha Upinzani tena ni Maarufu sana ndani ya nchi na kimataifa
Wafuasi wake wakatenda kile kawatuma kufanya✍️

Ktk utekelezaji wake kile Mwenyekiti kawaagiza baadhi yao Wakafa kama sisimizi

JAMHURI imeshajua chanzo ni yule mwenye kutembea na risasi nikama Nyati Kajeruhiwa kwasasa hatari kwa usalama wa Wananchi wote!!
Na police wakatekeleza kile samia alichowatuma?
 
Nawewe Umeshiba Migebuka mchana huu!!!

Nani kasema Lissu katangaza hadharani Uhaini

Unajua kwanini walifukuza
watu wa Media

Kisha wakabaki wenyewe

Uyu mh Lissu mwanzo kadhani ni mchezo wa kisiasa kumbe kuusu Kesi yake.

Lkn wenzie wamemshtua Jamhuri itakufunga Maisha weka
Akili sawa tumia
vizuri DOMO ilo✍️
Hebu sema mkiweka vikao vyenu vya ndani huko ccm mnakuwa na wanahabari?
 
28 August 2026

1787938835950.jpeg

28 Aug2026
MAHAKAMANI PAMOTO! MNYIKA ATOA USHAIDI - AFICHUA KILICHOTOKEA KWENYE MKUTANO wa LISSU..

View: https://m.youtube.com/watch?v=MdDaTEGOE8s
 
Zoezi la maswali ya dodoso kutoka kwa Jamhuri kwenda kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, litaendelea asubuhi hii Agosti 28, 2026 huku likitarajiwa kukamilika ili kutoa nafasi kwa shahidi mwingine kutoa utetezi wake.

Kutokana na muda wa shughuli za mahakama kuisha hapo jana Agosti 27, 2026, Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, liliahirisha kesi hiyo.

Katika maswali ya dodoso jana, Jamhuri walimuuliza Lissu maswali katika maeneo mbalimbali ya ushahidi wake ikiwemo katika maeneo ambayo Lissu alidai kwamba Mashahidi wa Jamhuri walioletwa dhidi yake walitoa ushahidi ulio kinzana kimaelezo na kimaandishi.

Pia walimuhoji Lissu aseme kama baada ya yote yaliyomkuta ikiwemo kushambuliwa kwa risasi, kama aliwahi kutoa taarifa polisi, jambo ambalo Lissu alidai kwamba alishalifanya na hakuna hatua yoyote ambayo iliwahi kuchukuliwa.

Tundu Lissu, anashtakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania.

Fuatilia mwenendo wa Kesi zilizopita;
=====

LIVE UPDATES KUTOKA MAHAKAMANI

Maombi yakiongozwa na Askofu Glorious Shoo ndani ya ukumbi wa mahakama baada ya ukumbi kuwa tayari una wahudhuriaji kwa ajili ya kusikiliza mwenendo wa Kesi



Katibu Mkuu wa CHADEMA, John John Mnyika akiwasili Mahakamani. Ikimbukwe John Mnyika ni moja kati ya mashahidi upande wa utetezi na kuna uwezekano mkubwa leo akatoa utetezi wake.

Mweyekiti wa CHADEMA- Taifa, Tundu Lissu amefikishwa kwenye ukumbi wa mahakama kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili.

Agosti 27, 2026 tuliishia sehemu ya 297, kwahiyo leo tunaendelea na;

Sehemu ya 298


Inapigwa Courtttttt harakaharaka na Jaji Karyemaha ametangulia kwa kasi sana.

Anafuatia Jaji Ndunguru na Mzee wa Burudani Jaji Kiwonde yuko nyuma yao.

Wanaingia wanakaaa.

Mwenyekiti Lissu nae anatafuta Vitabu vyake.

Karani anasoma namba ya kesi na kukaaa.

Anasimama Ajuaye Zengeli anasema anasaidia na Katuga, Mrema, Thawabu, Cathbert na Winniwa Kasawa wote ni Mawakili wa Serikali.

Na shauri limekuja kwa mshitakiwa kuulizwa maswali ya Dodoso.

Mhe. Lissu : Niko tayari kuendelea.

Mhe. Lissu anaomba niongee na Mawakili wangu kwanza, anaenda pale Dr. Nshala, Mahinyila, Nashon Nkungu, Dorice Kafuku,

Ajuaye: Nia ya kutenda kosa inathibitishwa na tendo?

Mhe. Lissu: Sio kweli

Ajuaye: Waheshimiwa tulikuwa na swali moja kwa shahidi na tumemaliza maswali ya Dodoso kwa shahidi huyu.

Majaji wanaandika na Mheshimiwa Lissu anapanga makabrasha yake hapa.

Mhe. Lissu anaomba kufanya re-examination baada ya kuwa wamemaliza kufanya cross examination.

Anasimama Katuga kuwa naomba tutoe hoja anasema Re examination ni moja ya examination ya utoaji ushahidi. Kifungu cha 155 Sura ya 6/2023.

Kifungu cha 156(3) cha Sheria ya Ushahidi kinasema Re-Examination itafanyika kwenye mambo gani na utaratibu wa kufuata.

Nimerejea kwenye hivyo vifungu ili tupate tafsiri kuwa yale maswali aliyoulizwa ndio tutaita re examination. Alikataa uwakilisha yeye mwenyewe ni jinsi gani atajifanyia maswali ya ufafanuzi kutokana na majibu yake. Lengo ni kutoa ufafanuzi.

Waheshimiwa Majaji tunaomba mahakama ijiulize. Majibu shahidi katoa mwenyewe, na kujiuliza anajiulizaje mwenyewe.

Huwezi kuwa Jaji kwenye kesi yako. Principle zetu za kisheria ziko hivyo. Unajuaje wengine hawajakuelewa hadi utake kutoa ufafanuzi.

Haya maswali ya re-exanination yanaulizwa na nani? Hili eneo ni gumu na muangalie vifungu vya Sheria unless tutakuwa tunafungua uwanda mwingine wa ku introduce inshu mpya.

Ili kuepuka hili la usijijibu wewe na ukajiuliza wewe. Mahakama inaweza kumuuliza yenyewe. Hiyo right ya re-examination iko kwa party iliyomuita shahidi.

Jaji Ndunguru: Sasa ombi lako ni nini?

Katuga: Mahakama kama itataka kumuuliza imuulize yenyewe lakini pia imuelekeze shahidi nini cha kujibu na naomba Mahakama itoe maelekezo kwenye eneo hilo. Ni hayo tu.

Jaji Ndunguru: Anateta na wenzake. Naona wanachungulia PC kwenye ile ya Karyemaha. Mshitakiwa unasemaje?

Mhe. Lissu: Naomba Wakili wa Serikali aiambie Mahakama kama ameleta pingamizi aseme au ameleta mapendekezo na maelekezo kwa Mahakama.

Amesema anawapa ushauri kama ni ushauri tuachane nao tufanye kazi iliyotuleta na kama ni pingamizi basi nitamjibu.

Jaji Ndunguru: Mnasemaje Serikali

Katuga: Labda kama alikuwa hasikilizi, mimi naomba mwongozo wa Mahakama.

Mhe. Lissu: Hakunaga kuomba mwongozo Mahakamani lakini basi ngoja nijibu huo mwongozo.

1. Re examination ni haki ya shahidi aliyekuwa examined ndio maana kifungu cha 156(1) alichotaja ni haki ya re-examination ni haki yangu basi Wakili wa Serikali alipaswa kunyamaza kimya.

2. Anasema atajiongozaje kama hana Wakili. The fact kwamba shahidi kwamba ndo mshitakiwa haimuondolei haki ya kufanya re exanination. Sasa nitafanyaje? Nitarejea maswali niliyoulizwa nitasema majibu yangu na nitaweka ufafanuzi wangu hapo.

3. Hii inaweza kuwa ni fursa ya ku introduce new facts huwa wana rise objection kwahiyo hofu yake ni unfounded completely. Ni hofu ya bure kabisa.

4. Hamna mwongozo wa kutoa hapa na kesi ndio zinaendeshwa hivyo.

Sehemu ya 299

Jaji Ndunguru anamwambia Mhe. Lissu, sasa hayo uliyosema si ndio mwongozo tunapaswa kumpa?

Mhe, Lissu anasema tutafika tumechoka sana kama mwongozo wenyewe mnaopaswa kuutoa ni huo kila mara.

Yeye mwenyewe wakati anaomba ni kama alikuwa hajielewi anaomba nini hana uhakika kabisa.

Jaji anateta na wenzake kwa dakika kadhaa hapa. Sijui wanateta nini? Hizi kazi ni ngumu sana.

Jaji Ndunguru anawasha MIC sasa pamoja na kwamba umesema kuwa umejibu na suala hili ni dogo lakini Mahakama ni muhimu ikatolea muongozo hili.

Sasa suala ni scope ya hiyo re examination. Sasa tutajikita kwenye scope hiyo na kama kutakuwa na new matters basi serikali wazuie au wataomba kukuuliza maswali. Mahakama pia ina nafasi ya kuuliza na hatuwezi kuzuia Re-Examination. Kazi yetu tunaijua vizuri.

Mhe. Lissu anasema naomba wasaidizi wangu wanipatie swali la mwisho lililoulizwa.

Anapatiwa sasa.

Majaji wanapiga story na kuangalia kompyuta zao sijui kuna nini tena, Mhe. Lissu hajaanza bado re examination.

Anasimama Ajuaye Zengeli anasema Waheshimiwa Majaji naona utaratibu unakiukwa. Shahidi anaomba washauri wake wampe sio utaratibu.

Mhe. Lissu: Kwamba naulizwa maswali lazima niwe naandika na kujibu hapo hapo inawezekana? Hili nalo lina shida kweli mimi kuandikiwa? Watu wameandika maswali na majibu hawa vijana wangu shida iko wapi? Mapingamizi ya bure kabisa.

Jaji Ndunguru: Basi endelea.

Mhe.!Lissu: Niliulizwa kuhusu nia inathibitishwa kwa matendo, nikasema sio kweli. Ufafanuzi wangu ni kwamba sio kila nia inathibitishwa kwa matendo. Nyingine ni kuchapisha.

Jaji Ndunguru: Tuendelee

Mhe. Lissu: Aliniuliza kuhusu Mahakama kutokulazimishwa au haipangiwi na baraza la umoja wa Mataifa. Ufafanuzi wangu ni kwamba Mahakama mapendekezo au maoni hayo ya vyombo vingine ni muhimu pia kuzingatia ushauri wa hizo taasisi zingine.

Katuga: Mambo ya Umuhimu asiyalete.

Mhe. Lissu: Basi niseme Mahakama huwa inaangalia maamuzi ya vyombo vingine.

Katuga: Mimi sitaki aende huko. Asililete sasa hivi.

Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu tuzo na kwamba nimezileta nikasema sijazileta na ni legal principles na kwamba mimi sio mwenye wajibu wa kuthibitisha sina hatia bali mzigo wa uthibitishaji uko upande wa mashitaka. Iko hivyo.

Mhe. Lissu: Niliulizwa vilevile kwamba niliwahi kuwa Rais wa TLS na nikajibu kweli na nikaulizwa wakati unashitakiwa na kesi hii ulikuwa Rais wa TLS na je kunakupa kinga.

Jaji Ndunguru: Naona hilo ni obvious hata usilitoleee ufafanuzi.

Mhe. Lissu: Sawa basi kuna swali la njia za Kidemokrasia nilisema ipo ya Mahakama na maandamano ya kidemokrasia. Nikaulizwa ipo kwenye kifungu gani cha Katiba nikasema kifungu cha 20(1) Cha Katiba. Naomba kutoa ufafanuzi kuwa hizo njia za nje ya mahakama zinatambulika kikatiba na zimethibitishwa hivyo na Mahakama

Sehemu ya 300

Mhe. Lissu anaendelea na Re-examination

Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu Ndyanabo na Mtikila na nikasema Mtikila alienda Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika na hadi sasa serikali haijatekeleza maamuzi ya Mahakama ya Haki za Binadamu za Afrika.

Jaji Ndunguru: Hiyo naona ni the obvious nayo usifafanue kabisa.

Mhe. Lissu: Haina shida. Niliulizwa sana kuhusiana na scope ya kifungu cha 39(2)(d) juu ya neno Or kati ya Overt act or deed. Ufafanuzi wangu ni kwamba act or deed is the same thing. Act something that is done and a deed is something is done.

Katuga: Huu ni ushahidi au submission. Anakoenda ni kutoa tafsiri ya overt act or deed.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa naona Mahakama inisomeee ili tusivutane vutane hapa.

Jaji Karemaha anasoma kilichoandikwa, anasema kwa vile nimeandika kingereza nitasoma.

Mhe. Lissu: Basi naomba niendelee. Kuhusu mihimili mitatu na kazi zake. Nikasema moja ya kazi za Bunge ni kutunga Sheria na serikali kusimamia sheria. Ufafanuzi wangu ni kwamba kutunga sheria sio kazi pekee ya Bunge.

Mhe. Lissu: Kuhusu mashahidi wa mashitaka hawakuja kutoa ushahidi kuhusu namna nilivyokamatwa. Uhalali wa kukamatwa kwangu ni suala tofauti kwasababu sheria zimeweka utaratibu wa namna ya kukamata na ulifuatwa au laaa suala hilo lilipaswa kujibiwa na upande wa mashitaka.

Mhe. Lissu: Nimeulizwa kuhusu waandishi wengi wa habari waliokuja Tar. 03/04 niliulizwa kama waandishi hao walikuwa wanajua nilichokuwa naenda kuwaambia na kama niliwapa hotuba yangu mapema. Nikasema sikuwapa. Nataka kufafanua, waandishi wa habari huwa hawapewi taarifa hizo kabla.

Katuga: Hilo la kwamba huwa hawapewi hizi taarifa hilo sikuuliza.

Mhe. Lissu: Yeye ndo alileta habari za constructive publication

Jaji Ndunguru: Na wewe ukasema kuwa hukuwa na control ya hao watu, nafikiri hata hili majibu yako yalinyooka tu.

Mhe. Lissu: Sawa. Kuhusu maandamano na kuzuia uchaguzi. Nilisema uchaguzi usiokuwa huru sio uchaguzi.

Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu adhabu ya kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code atahukumiwa adhabu ya kifo na Wakili akasema sentenced to death. Mimi nilisisitiza ni adhabu ya kifo.

Jaji Ndunguru: Hivyo vifungu vinatofautiana cha mwaka 2022 na cha mwaka 2023. Kuna sheria moja ina liable to death na nyingi shall be sentenced to death. Kwahiyo ile ya 2022 ni kwamba sio lazima upewe adhabu ya kifo lakini ya 2023 ndio haina hiyo option. Inasema direct sentenced to death.

Mhe. Lissu: Haya tuendelee. Kulikuwa na maswali kuhusiana na mashahidi wa kificho na nasisitiza hawakuwa wanajulikana kwa mtu yeyote isipokuwa aliyewaleta.

Kuna hili lingine la kwamba tuliwatoa nje waandishi na nikasema kwa yale ambayo hatukutaka yachapishwe tuliwatoa ni kwasababu walichoitiwa kilikuwa kimeshakamilika.

Naomba sasa vielelezo D1 hadi D16 kwasababu vilitumika sana kwenye cross examination.

Anasubiria kupatiwa.

Sehemu ya 301

Mhe. Lissu anaendelea na Re-examination

Mhe. Lissu: Kuhusu D1 kile kielelezo cha Kaaya kule chini kabisa kimeendikwa maelezo, ziko hizo sehemu kwahiyo alipaswa kuandika na kuandikwa maelezo.

D2 nacho pia hicho kielelezo Samwel Elibariki nacho niliulizwa maswali kadhaa angalia mwisho utaona. Ipo sehemu ya mtoa maelezo na afisa aliyeandika maelezo, hizo sehemu zote zimesainiwa na mtu mmoja.

D5 ambayo ni maelezo ya PW 6 nayo pia kuna signature moja imepita sehemu zote za aliyeandika maelezo na aliyemuandika maelezo kote ni yule yule.

Exhibit D8 ni maelezo ya PW9 nae pia vilevile. Kuna uthibitisho wa Afisa aliyeandikiwa maelezo. Uthibitisho pia wa chini yake ameandika vile vile yeye pia. Amejionya na kujithibitisha mara mbili.

D11 maelezo ya PW12 inasema Koplo Vicent nae pia alijionya na kujiandika Maelezo yake. Mtu huyo huyo.

D15 ambayo ni maelezo ya Amin Mahamba PW 16 kila page kuna mtoa maelezo na aliyeandika maelezo. Lakini imesainiwa mtoa maelezo pekee lakini aliyeandika maelezo haipo kabisa.

D14 cha PW 15 Koplo Amani kwenye kila page saini ya mtoa maelezo imejazwa na afisa aliyesimamia maelezo ipo Koplo Robert. Ndo nilisema huyu pekee ndio alifuata utaratibu. Detective Corporal Robert ndio niliandika maelezo ya Detective Coporal Amani. Huyu alikuwa sahihi.

Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu wale mashahidi waliokiri kufanya uhalifu. Walikiri Polisi na baadae wakaambiwa wawe mashahidi dhidi yangu na baadae tuhuma zikafutwa. Je unawaita wahalifu walishapelekwa mahakamani hapana lakini ni wahalifu. Ufafanuzi ni kwamba watu ambao ni wamepanga kufanya uhalifu, wakakamatwa kwa kufanya uhalifu, wakakiri wanapanga kufanya uhalifu wakaja mahakamani tumepanga kufanya uhalifu na wakaachiliwa hao ni wahalifu.

Ajuaye: Ameanza kutoa ushahidi hapa tena.

Mhe, Lissu: Nimetoa ufafanuzi Jaji

Jaji Ndunguru: Haya tuendelee hebu

Mhe. Lissu: Naomba niishie hapo. Kwenye hii re examination.

Kesi imeahirishwa hadi saa nane kamili tutarudi Mahakamani.

Kuendelea na Shahidi John Mnyika. DW2.


Mahakama imerejea 🚨🚨 sasa tuendelee na Sehemu ya 302

Majaji wanaingia.

Ajuaye anasema wako tayari kuendelea wao upande wa Jamhuri.

Jaji Ndunguru anamuuliza Mh. Lissu nae anasema yuko tayari kuendelea. Na shahidi wake anaitwa JOHN JOHN MNYIKA.

Katibu Mkuu Mhe. John Mnyika anaitwa na anapanda kizimbani amevaa Shati nyekundu ya Chama.

Anafuatwa na Karani wa Mahakama wanateta na Mnyika anacheka.

Jaji: unaitwa nani?

Mnyika: John John Mnyika,

Jaji: umri wako?

Mnyika: Miaka 46

Jaji: Kazi yako

Mnyika: Katibu Mkuu wa Chadema.

Jaji: Dini yako?

Mnyika: Mkristu

Jaji: haya muapishe.

Mimi John John Mnyika naapa ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu na Mungu anisaidie.

Sasa Mhe. Lissu anaanza.

Mhe. Lissu: Nitakayokuuliza uyajibu kwa utaratibu maana Majaji wanaaandika na mimi nafahamu una sauti nzuri tu.

Sasa waeleze majaji umeshikilia nafasi hii ya Chadema kuanzia lini?

Mnyika JJ: Kuanzia 2019 mimi ni Katibu Mkuu.

Mhe. Lissu: Kabla ya hapo ulikuwa na nafasi yoyote nyingine?

Mnyika JJ: Kabla ya KM nilikuwa Mkurugenzi wa Vijana Chadema Taifa kuanzia 2003 hadi 2011 wakati naishikilia nafasi hiyo mwaka 2007 niliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa habari na uenezi hivyo nilishikilia nafasi mbili kwa wakati mmoja. Nafasi ambayo niliitumikia mwaka 2014.

Na wakati huo huo kati ya mwaka 2009 hadi 2011 nilishikilia nafasi ya Mkurugenzi wa mambo ya nje na uhusiano wa Kimataifa wa CHADEMA.

Na Mwaka 2014 niliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa nafasi ambayo niliishikilia hadi 2019 nilipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu.

Nilipokuwa mbunge pia

Mhe. Lissu: Huko tutakwenda pia bado subiri. Nafasi nyingine je?

Mnyika: Nilikuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni kwa vipindi viwili.

Mhe. Lissu: Nafasi nyingine?

Mnyika JJ: Nilikuwa Katibu wa Wabunge wa Chadema Bungeni kati ya mwaka 2010 mpaka 2015 na nikawa tena Katibu kuanzia mwaka 2016.

Jaji ulikuwa mbunge wa?

Mnyika: Nilikuwa Mbunge wa jimbo la Ubungo 2010 hadi 2015 na baadae Jimbo la Kibamba 2015 hadi 2020.

Mhe. Lissu: Nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema ni nafasi ya aina gani katika uongozi wa Chama.

Mnyika: Ni nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Chama ambae ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Chama na ni msimamizi mkuu wa rasilimali, utawala, uendeshaji wa Chama. Na Katibu Mkuu ndie msimamizi mkuu wa utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya vikao vya juu vya Chama ambavyo ni Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Chama.

Mhe. Lissu: Taratibu tararibu.

Vilevile ni msimamizi mkuu wa wafanyakazi wa Chama na waliopo makao makuu ya Chama ikiwemo pia makatibu wote wa Chama.

Mhe. Lissu: Sasa nisubiri mimi.

Eheee Sasa shahidi naomba waeleze Majaji kama Chama Chako huwa kinafanya vikao au mikutano ya Chama na utaratibu wake ukoje?

Mnyika: Chama huwa kina mikutano ya aina mbili kuu ambazo ni Mikutano ya ndani.

Usiposikia Jaji amesema Mhhhhhhh ndo uendeleee.

Mnyika: Kuna Mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani.

Jaji Ndunguru : Sio lazima niseme mhhhhhh naweza sema endelea.

Mnyika: Kwa mikutano ya ndani ngazi ya utendaji chombo husika ambacho ni sekretarieti kinakaaa kikao cha ngazi ya Kitaifa chini ya Katibu Mkuu na kufanya maandalizi ya kikao hicho. Na majukumu yanagawanywa ya maandalizi yake.

Mhe.Lissu: Hapohapo. Subiri. Sasa waeleze majaji nani ni wajumbe wa hiyo sekretarieti?

Mnyika: Ni Katibu Mkuu wa Chama Taifa ambae ndie Mwenyekiti wa Sekretarieti. Manaibu Katibu wakuu wawili. Mmoja wa Zanzibar na Mwingine wa Bara, Wakurugenzi wa Kurugenzi za Chama Taifa, Wataalamu na Katibu wa Sekretarieti anayeteuliwa na Katibu Mkuu na Makatibu wa Mabaraza ya Chama kwa maana ya Baraza la Wazee, Baraza la Vijana na Wanawake. Anataja na vifupi vyake BAZECHA, BAWACHA na BAVICHA.

Sehemu ya 303

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shaidi wake Mhe. Lissu.

Mhe. Lissu: Katika wajumbe wote hao uliowataja, waeleze Majaji kama Mwenyekiti wa Chama ni sehemu ya hiyo sekretarieti ya Chama Taifa.

Mnyika: Sio sehemu ya sekretarieti. Mwenyekiti hayupo kwenye sekretarieti.

Mhe. Lissu: Tuko Mahakamani leo kwasababu ya kesi ya uhaini inayonikabili mimi.

Shitaka la hiyo kesi linasema kwamba mnamo Tarehe 03/04/2025 niliitisha mkutano wa watiania ya kugombea nafasi mbalimbali na nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma kuvuruga uchaguzi mkuu huo na nataka uwaeleze majaji kama una ufahamu wowote wa huo Mkutano?

Mnyika: Ninaoufahamu huo Mkutano wa Tar. 03/04/2025 wazo lake lilitoka kwangu, niliuandaa kwa maelezo yangu.

Uliandaliwa na sekretarieti ambayo nilisimamia vikao sekretarieti yaani kupanga na kugawanya majukumu na maandalizi ya vikao hivyo.

Pia niliidhinisha fedha za matumizi ya Mkutano huo kama accounting officer na nilishiriki Mkutano wenyewe.

Mhe. Lissu: Sasa Shahidi kwenye ushahidi wako wa mwanzo ulisema kuna aina mbili za mikutano. Ulisema kuna mikutano ya hadhara na ile ya ndani. Sasa huo wa tarehe 03/04/2025 ulikuwa wa aina gani?

Mnyika: Ulikuwa wa ndani wa Chama. Ulikuwa na lengo la kudai mageuzi ya kimfumo wa uchaguzi chini ya kauli mbiu ya NO REFORMS: NO ELECTION. Na kwa tafsiri yetu ya Kiswahili ni kwamba BILA MABADILIKO HAKUNA UCHAGUZI.

Mhe. Lissu: Ukiwahusu akina nani?

Mnyika: Waliokuwa na nia ya kugombea wote, viongozi wa Chama pia

Mhe. Lissu: Mliwaalika akina nani haswa hao viongozi wa Chama?

Mnyika: Mwenyekiti Tundu Lissu, Makamu Bara John Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Mzee Said. Na viongozi wakuu wengine ambao ni sehemu ya Sekretarieti.

Mhe. Lissu: Huo Mkutano unaouita wa ndani ulifanyikia wapi?

Mnyika: Ulifanyikia Mikocheni Makao Makuu ya Chama katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama Makao Makuu.

Mhe. Lissu: Ni waaandishi wa habari gani mliowaalika?

Mnyika: Tuliwaalika kwa ujumla.

Na kazi ya kuandika tulilikabili hilo jukumu kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chama Brenda Rupia na pia nilielekeza itolewe taarifa kwa umma kuhusu mkutano huo. Lilitolewa tangazo hilo la Taarifa kwa Umma kwa waandishi.

Mnyika: Tarehe 27/03/2025 lilitolewa Tangazo likiwa limesainiwa na Brenda Rupia ambayo ilialika waandishi wa habari na pia kuueleza umma kuhusu kuitishwa kwa kikao hicho.

Mhe. Lissu: Wakati wewe na sekretarieti mnafanya yote hayo Mwenyekiti wa Chama alikuwa kwenye ziara kanda ya Nyasa kama sehemu ya Oparesheni NO reforms No Election kwa kutumia njia ya Mikutano ya Hadhara.

Mhe. Lissu: Kanda ya Nyasa maana yake nini ni sehemu gani nchi hii?

Mnyika: Inajumuisha Mkoa wa Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa na Rukwa. Chadema ndio tunaiita hiyo Kanda ya Nyasa.

Mhe. Lissu: Hiyo kanda ilitumia muda gani kama unakumbuka?

Mnyika: Ilianza Tar. 23/03/2026 hadi kabla ya Tar. 03/04

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji wakati mnafanya hayo maandalizi alishiriki kwa namna yoyote maandalizi ya mkutano huo wa tar. 03/04/2025

Job Mrema: Akumbushwe kuwa utaratibu ufuatwe.

Mhe. Lissu: Hakuna pingamizi acheni niendelee.

Eleza ushiriki wa Mwenyekiti wa Chama?

Mnyika: Hakushiriki kwa namna yoyote?

Mhe. Lissu: Kuhusu kualika watia nia au waandishi wa habari?

Mnyika: Hakushiriki kabisa kualika watia nia au waandishi wa Habari.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji waandishi wa habari na vyombo vyao walioshiriki mkutano huo?

Mnyika: Jambo TV, The Chanzo na Mwanzo TV.

Mhe. Lissu: Naomba nipatiwe D16 maelezo ya DW17

Jaji Ndunguru: Mna lolote serikali?

Ajuaye: Hatuna shida kabisa.

Mhe. Lissu: Sasa Shahidi wasomee Majaji kwa mujibu wa kielelezo hicho shahidi wa Jambo TV alipataje taarifa za Mkutano?

Mnyika: Nakumbuka taarifa za Mkutano huu nilizipata na kuziona pia nakumbuka kutoka kwa Mkurugenzi wetu ambae ni John Marwa ambae na yeye alilipata Tangazo hilo kutoka kwa Afisa habari wa Chadema.

Sehemu ya 304

Mhe. Lissu: Sasa endelea hapo?

Mnyika: Niliona pia vyombo vya Habari vya Azam na vingine

Katuga: Anasimama Katuga anasema hicho kielelezo cha Mahakama hajaomba ku refresh memory.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kama anaona hilo ni shida basi naliondoa tu.

Mhe. Lissu anaendelea: Sasa Shahidi hii tuhuma wewe unaionaje?

Mnyika: Hiyo ni tuhuma ya uongo. Ni tuhuma ya kubambikiza tu.

Mhe. Lissu: Wakati mnatuma hizo taarifa kwa hao waandishi wa habari mlituma maelekezo mengine ya waje na nini na waje na vitu gani?

Mnyika: Hatukuwaambia waje ma chochote. Hatukusema waje na Pen na Karatasi wala chochote.

Mhe. Lissu: Imetolewa maelezo kwamba walikuja na camera hapa Mahakami sasa wewe unasemaje?

Ajuaye: Naomba ali rephrase swali.

Mhe. Lissu: Sitapoteza muda. Imesemwa kuwa mimi ndio nilirusha matangazo wewe unasemaje?

Mnyika: Chadema tunaamini katika uhuru wa vyombo vya habari kwahiyo hatuwezi kuwaingilia waandishi wa habari. Walirusha wao na sisi hatuhusiki.

Mhe. Lissu: Kwahiyo ilikuwaje siku ya hilo tukio?

Mnyika: Sehemu ya kwanza vyombo vya habari vitahusika na sehemu ya pili tutabaki viongozi na watia nia kwa muda mfupi.

Mhe. Lissu: Hiyo sehemu ya kwanza ni ipi?

Mnyika: Ni ile hatua ya awali ya maelezo ya Viongozi wakuu. Ambao ni Mwenyekiti, Makam wake na Manaibu wa Katibu mkuu. Anawataja kwa majina wote.

Mhe. Lissu: Sasa waeleze Majaji lengo la kuwaalika Waandishi wa habari ni nini?

Mnyika: Wachukue habari na kufikisha kwa umma suala limalohusu madai yetu ya mabadiliko ya Kikatiba na kisheria ya kuwezesha uchaguzi huru na Haki chini ya Kauli Mbiu ya No reforms No Election. Bila Mabadiliko hakuna Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Unaposema hotuba ya Mwenyekiti ilikuwa ndefu zaidi una maanisha nini?

Mnyika: mazungumzo yalikuwa ni takribani masaa matatu. Na katika muda huo Mwenyekiti alizungumza zaidi ya masaa mawili alizungumza Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Mhe. Lissu: Hayo mazungumzo ya Mwenyekiti ya Masaa mawili yalihusu nini hasa?

Mnyika: Mwenyekiti alizungumzia historia ya madai ya kutaka mageuzi ya Kikatiba kutaka uchaguzi wa huru na haki. Kuanzia Kabla, wakati wa tume ya Rais iliyokusanya maoni ya mfumo wa vyama vingi, almaarufu Tume ya Nyalali kati ya mwaka 1991 na 1992.

Akazungumzia mapendekezo ya tume hiyo kutaka kuandikwa kwa Katiba Mpya na kufanyika mabadiliko ya kikatiba ya kuwezesha Uchaguzi huru na Haki namna yalivyokataliwa na serikali ya Chama kimoja CCM.

Na akaendelea kuelezea juu ya madhara ya kutofanyika kwa mabadiliko hayo toka mwaka 1995.

Akaeleza maoni ya tume zingine na kamati zingine zilizoundwa kuelezea maswala ya Kikatiba kuhusu uchaguzi akataja tume ya Kisanga, Kamati ya Bomani na Tume ya Jaji Warioba ya Mwaka 2014.

Mnyika anateleza tu. Useminari mwingi nidhamu yakutosha na madini yakumwagika.

Mwenyekiti alieleza namna CCM walivyotumia wingi wao kwenye Bunge la Katiba na kutumia wingi wao kujaribu mchakato wa Uchaguzi.

Pia alielezea madhila ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019, Uchafuzi wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 namna ambavyo mawakala wetu walifanyiwa kuondolewa vituoni.

Pia Mwenyekiti alieleza kuhusu hatua ambazo Chama kilichukua baada ya Uchaguzi huo ambao baadhi ya wanachama walifungwa Gerezani lakini ni uchaguzi ambao watu wetu walipigwa sana wakiwa wanadai haki kutendeka.

Sasa chama chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mbowe kilichukua hatua mbalimbali kukabiliana na hali hii ya kipindi hicho na hatimaye baadae Mwenyekiti Mbowe alipewa kesi ya Ugaidi kutokana na msimamo wetu na wa Chama wa kudai Katiba Mpya na alikaa rumande kati ya Mwaka 2021 na mwaka 2022.

Na alipotolewa baada ya kesi yake kufutwa. Yalianza mazungumzo kati ya Chadema upande mmoja na CCM na serikali upande mwingine.

Sehemu ya 305

Mnyika anasema na katika mazungumzo hayo akaeleza kuwa upande wa CHADEMA uliwasilisha kwa mazungumzo na kwa maandishi mapendekezo ya maeneo ya marekebisho na mabadiliko ya Kikatiba ya kuwezesha Uchaguzi huru na Haki. Na namna ambavyo mwaka mmoja wa mazungumzo upande wa CCM na Serikali ulijibu kwa mdomo na maandishi kukataa mapendekezo yote ya CHADEMA na marekebisho ya KATIBA

Mhe. Lissu: Mapendekezo hayo yalikuwa yanahusu nini?

Mnyika: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Kwa kifupi ni mapendekezo ya kubadilisha sheria za Uchaguzi huo.

Mimi nilikuwa sehemu ya timu ya watu 10 iliyokutana na Rais mwezi Mei 22, 2022 na Katika Timu yetu na mazungumzo na Rais mapendekezo ya kukwamua Mchakato wa Katiba Mpya yaliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wakati huo Freeman Mbowe.

Anaendelea Mnyika.

Mapendekezo tuliyokuwa nayo ni pamoja na marekebisho ya kisheria na Kikatiba niliwasilisha mimi uchaguzi wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Iwapo Mchakato.......

Jaji Ndunguru: Shahidi kuna maji kidogo. Wenzako tunaandika kuna muda midadi inakupanda unaongea mfululizo.

Mnyika: Nashukuru ngoja ninywe sasa.

Watu wanatabasamu.

Mapendekezo tuliyoyatoa ni kwamba kutokana na muda uliokuwa umebaki basi tufanye marekebisho katika maeneo mahsusi ili kuwezesha Uchaguzi huru na Haki na tuliziita ni Minimum Reforms.

Mhe. Lissu: Kikao cha Rais alisemaje sasa?

Mnyika: Alisema nimeyapokea na kwa mazungumzo zaidi na akaahidi timu ya watu watano kutoka CCM ambayo iliongozwa na Abrahaman Kinana na sisi Mwenyekiti Mbowe alisema ataunda Timu ya Watu watano ambayo na mimi nilikuwa sehemu ya watu hao.

Mhe. Lissu: Mazungumzo hayo kati ya Timu ya CCM yakiongozwa na Kinana na Timu ya CHADEMA yaliishia wapi na matokeo yake yalikuwa nini?

Mnyika: Yaliendelea kuanzia Mwezi June, 2022 mpaka tarehe 31/05/2023

Hadi kipindi hicho walitujibu mchakato wa Katiba Mpya usubiri hadi uchaguzi mkuu wa 2025 na pili marekebisho yoyote ya Katiba yanayohusu Uchaguzi na yanayogusa Katiba hata kama ni muhimu vipi lakini yasingewezekana kwa kipindi hicho.

Mhe. Lissu: Sasa shahidi waeleze Waheshimiwa Majaji.

Anasimama Ajuaye: Waheshimiwa Majaji muda sio rafiki na tumepokea concern kutoka watu wa usalama kuwa saa 11 imefika.

Jaji Ndunguru: Mshitakiwa unasemaje?

Mhe. Lissu: Wamesema masuala ya Ulinzi na Usalama mimi nitajuaje.

Jaji: Basi tukutane Jumatatu saa tatu kamili asubuhi tukutane hapa. Ahsanteni.

===

John Mnyika ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amepandishwa kizimbani mchana wa Agosti 28, 2026, kama shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, Tundu Lissu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Jumatatu Agosti 31, 2026 ambapo Mnyika ataendelea kutoa ushahidi wake baada ya muda wa Mahakama siku ya leo (Agosti 18, 2026) kuisha.
 

Attachments

  • 1000024076.jpg
    1000024076.jpg
    45.1 KB · Views: 5
Wenge hapewi na Lissu

ngoja kesho John Mnyika majina yake kama
Ajayasahau nyumbani

Na miaka yake 🤠✍️

Kesho ndio kesho John Mnyika kaingia kwenye Mfumo ✍️
Sio kesho mkuu ni jumatatu
 
Back
Top Bottom