Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

Sasa ndugu yangu Econonist
Lissu ndio chanzo baada kutangaza kukinukisha kuzuiya Uchaguzi nk.

Nayeye ni mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha Upinzani tena ni Maarufu sana ndani ya nchi na kimataifa
Wafuasi wake wakatenda kile kawatuma kufanya✍️

Ktk utekelezaji wake kile Mwenyekiti kawaagiza baadhi yao Wakafa kama sisimizi

JAMHURI imeshajua chanzo ni yule mwenye kutembea na risasi nikama Nyati Kajeruhiwa kwasasa hatari kwa usalama wa Wananchi wote!!
Hakuna kitu kama hicho. Kama ni hivyo hata yule aliyesema hakutakuwa na nywinywi wala nywinywi alkamatwe maana naye amechochea hasira za watu.
 
file_00000000006c81f98a50bf4a97ebdf31.png

Tukutane tena jumatatu panapo majaaliwa 🙏
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Na siku ya kura, mawakala wa CHADEMA kuondolewa vituoni.

Na kura kuingizwa vituoni zikiwa zimeshapigwa tayari katika masanduku ya kura kwa mitutu ya bunduki.

Akaeleza juu ya hatua ambazo Chama kilichukua kwa Kamati Kuu ya 2020, wakati huo Mwenyekiti wa Chama akiwa ni Freeman Mbowe, za kusaini mabadiliko ya Kikatiba kupitia jina la Tume Huru ya Uchaguzi.

Na matokeo yake Mwenyekiti Freeman Mbowe akabambikiziwa kesi ya ugaidi na kukaa rumande kutoka 2021 mpaka 2022.

Na alipotolewa kwa kesi yake kufutwa, alipokutana na Rais Ikulu, wakati huo Samia Suluhu Hassan, na hatimaye kuanza kwa mazungumzo baina ya CHADEMA kwa upande mmoja na CCM kwa upande mwingine.

Akaeleza kwamba upande wa CHADEMA uliwasilisha kwenye mazungumzo na kwa maandishi mapendekezo na maeneo ya marekebisho na mabadiliko ya Kikatiba ya kuwezesha uchaguzi huru na haki, na namna ambavyo baada ya mwaka mmoja wa mazungumzo upande wa CCM ulijibu kwa maandishi ya kuwezesha uchaguzi wa huru na haki.

Na hatimaye mazungumzo kuvunjika.

Lissu: Hebu simamia hapo.

Mnyika: Mazungumzo ya kuwezesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Ubunge na Urais wa mwaka 2025.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ushiriki wako mwenyewe katika mazungumzo hayo ya CHADEMA.

Mnyika: Mimi nilikuwa sehemu ya timu iliyokutana na Rais tarehe 22 Mei 2022.

Lissu: Subiri kidogo waandike.

Lissu: Endelea ulipoishia.

Mnyika: Nikisema kwamba mimi nilikuwa sehemu ya timu ya watu 10 iliyokutana na Rais tarehe 22 Mei 2022.

Na katika kikao hicho na Rais, mapendekezo ya namna ya kukwamua mchakato wa Katiba Mpya yaliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe.

Na mapendekezo ya hoja nyingine 10, ikiwemo hoja nyingine 10 za mazungumzo, hoja moja wapo ikiwa ni marekebisho ya Kikatiba na kisheria ya kuwezesha uchaguzi huru na haki, niliwasilisha mimi.

Lissu: Uchaguzi huru na haki wa mwaka gani?

Mnyika: Uchaguzi wa 2024 kuhusu uchaguzi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa, na Uchaguzi Mkuu wa 2025 wa Madiwani, Wabunge na Rais.

Lissu: Endelea.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Hii ya CCM ya kusema mabadiliko ni mpaka baada ya uchafu WA 2025 ni uhaini na kutaka kupata madaraka Kwa njia haramu
 
Back
Top Bottom