Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

jamaa anakaba miguu yote wengine watapitia wapi sasa kwa uwezo huo alio nao mbona anawapa kazi ya kwenda kujipanga upya maana sioni mwanya wa kumpita mpk dk hii na dk ndo hizi za majerui😅

alivyosema anaenda kuandaa mashahidi dhahiri amewaandaa vyema.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Na siku ya kura, mawakala wa CHADEMA kuondolewa vituoni.

Na kura kuingizwa vituoni zikiwa zimeshapigwa tayari katika masanduku ya kura kwa mitutu ya bunduki.

Akaeleza juu ya hatua ambazo Chama kilichukua kwa Kamati Kuu ya 2020, wakati huo Mwenyekiti wa Chama akiwa ni Freeman Mbowe, za kusaini mabadiliko ya Kikatiba kupitia jina la Tume Huru ya Uchaguzi.

Na matokeo yake Mwenyekiti Freeman Mbowe akabambikiziwa kesi ya ugaidi na kukaa rumande kutoka 2021 mpaka 2022.

Na alipotolewa kwa kesi yake kufutwa, alipokutana na Rais Ikulu, wakati huo Samia Suluhu Hassan, na hatimaye kuanza kwa mazungumzo baina ya CHADEMA kwa upande mmoja na CCM kwa upande mwingine.

Akaeleza kwamba upande wa CHADEMA uliwasilisha kwenye mazungumzo na kwa maandishi mapendekezo na maeneo ya marekebisho na mabadiliko ya Kikatiba ya kuwezesha uchaguzi huru na haki, na namna ambavyo baada ya mwaka mmoja wa mazungumzo upande wa CCM ulijibu kwa maandishi ya kuwezesha uchaguzi wa huru na haki.

Na hatimaye mazungumzo kuvunjika.

Lissu: Hebu simamia hapo.

Mnyika: Mazungumzo ya kuwezesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Ubunge na Urais wa mwaka 2025.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ushiriki wako mwenyewe katika mazungumzo hayo ya CHADEMA.

Mnyika: Mimi nilikuwa sehemu ya timu iliyokutana na Rais tarehe 22 Mei 2022.

Lissu: Subiri kidogo waandike.

Lissu: Endelea ulipoishia.

Mnyika: Nikisema kwamba mimi nilikuwa sehemu ya timu ya watu 10 iliyokutana na Rais tarehe 22 Mei 2022.

Na katika kikao hicho na Rais, mapendekezo ya namna ya kukwamua mchakato wa Katiba Mpya yaliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe.

Na mapendekezo ya hoja nyingine 10, ikiwemo hoja nyingine 10 za mazungumzo, hoja moja wapo ikiwa ni marekebisho ya Kikatiba na kisheria ya kuwezesha uchaguzi huru na haki, niliwasilisha mimi.

Lissu: Uchaguzi huru na haki wa mwaka gani?

Mnyika: Uchaguzi wa 2024 kuhusu uchaguzi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa, na Uchaguzi Mkuu wa 2025 wa Madiwani, Wabunge na Rais.

Lissu: Endelea.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Wakuu,

Narudia TUHIMIZE watoto wetu wapende shule.
Hapa ukiwa na akili za kijinga unateketea hivi hivi.

Mtaji wa CCM ni kutoa elimu mbovu kwa watu wengi iwezekanavyo!
Kitu cha kwanza ambacho CCM ilishafanikiwa ni kunajisi elimu ya kibongo, kuwa elimu mbovu. Wao watoto wao wanawapeleka Ulaya na Marekani wakasome huko. Hawasomi elimu zetu hizi za Kinjekitile Ngwale.
 
Mtaji wa CCM ni kutoa elimu mbovu kwa watu wengi iwezekanavyo!
Kitu cha kwanza ambacho CCM ilishafanikiwa ni kunajisi elimu ya kibongo, kuwa elimu mbovu. Wao watoto wao wanawapeleka Ulaya na Marekani wakasome huko. Hawasomi elimu zetu hizi za Kinjekitile Ngwale.
Mkuu,

Binafsi nikiwa kama kijana nimegundua taifa hili vijana tusome na tusikariri wengi wetu Hatuna uwezo binafsi.
 
Alisababishaje wakati alikuwa ndani?.

Sasa ndugu yangu Econonist
Lissu ndio chanzo baada kutangaza kukinukisha kuzuiya Uchaguzi nk.

Nayeye ni mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha Upinzani tena ni Maarufu sana ndani ya nchi na kimataifa
Wafuasi wake wakatenda kile kawatuma kufanya✍️

Ktk utekelezaji wake kile Mwenyekiti kawaagiza baadhi yao Wakafa kama sisimizi

JAMHURI imeshajua chanzo ni yule mwenye kutembea na risasi nikama Nyati Kajeruhiwa kwasasa hatari kwa usalama wa Wananchi wote!!
 
hapa kuna kesi ya uchechezi sio uhaini
Hata huo uchochezi wenyewe hauna mashiko. Lissu alikamatwa April 9, 2025. Vurugu za uchaguzi zilitokea Oktoba 29, 2025!! Kwenye hizo vurugu siyo Lissu au viongozi wa CHADEMA waliohusika kuziandaa.

Isitoshe kauli zake alizitoa katika mazingira ya kisiasa (kwenye mkutano) na siyo sehemu ya kificho akiwa na kundi la maafisa wa jeshi, nk.
NB: Mimi ni Bushlawyer tu niliyenufaika kidogo na hizi kesi kupitia committal zake mbalimbali.
 
TUNDU LISSU ANAISHIA HAPA KWA LEO KUMHOJI SHAHIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Mnyika: Hayo mapendekezo yalikuwa ni mapendekezo sambamba kwamba, kama upatikanaji wa Katiba Mpya ukichelewa, kufanyike marekebisho mahususi tuliyopendekeza ya Kikatiba ya kuwezesha uchaguzi wa huru na haki, tuliyoyaita Minimum Reforms.

Lissu: Baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Rais, kitu gani kilitokea?

Mnyika: Rais akiahidi mchakato wa mazungumzo utaendelea na akaahidi kuunda timu ya watu watano, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana, na sisi kwa upande wetu aliyekuwa Mwenyekiti wetu wakati huo, Freeman Mbowe, akaahidi kuunda timu ya watu watano, ikiwemo mimi, na akaiunda.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, mazungumzo hayo kati ya timu ya CCM ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao, Abdulrahman Kinana, na huku yakiongozwa na Mbowe, yalidumu muda gani?

Mnyika: Yalidumu kuanzia 31 Juni 2022 mpaka 23 Mei 2023, baada ya CCM kutujibu kwa maandishi kwamba:

1. Mchakato wa Katiba Mpya usubiri mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.

2. Marekebisho yoyote yanayohusu Katiba, hata kama marekebisho ni ya maeneo mahususi (Minimum Reforms) ya kuwezesha uchaguzi huru na haki, kama kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na matokeo ya Urais kuhojiwa Mahakamani.

Maamuzi ya Tume kuhojiwa Mahakamani.

Na Tume kuwa na watumishi wake au kuajiri watumishi wake huru, ili mradi yanahusu marekebisho ya Katiba, yasubiri wakati wa kushughulikia mchakato wa Katiba Mpya baada ya 2025.

Lissu: Shahidi, waeleze Majaji.

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, muda siyo rafiki na tumepokea concern kutoka kwa watu wa Usalama. Tunaomba ahirisho.

MAJAJI WANATETA.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nimesikia kuna masuala ya maombi ya kiulinzi ambayo mimi siyajui na Majaji hawatajua.

Tukubali tu, saa 11, muda umeenda.

MAJAJI WANATETA.

Jaji Ndunguru: Shauri linahirishwa hadi Jumatatu asubuhi saa 3 kamili.

Ushahidi utaendelea.

MAJAJI WANATOKA.

TUKUTANE JUMATATU ASUBUHI.
 
Back
Top Bottom