Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

JOHN MNYIKA ANAAPA KUTOA USHAHIDI KESI YA TUNDU LISSU

MAHAKAMA IMEREJE

Majaji wameingia ndani tayari.

Katibu Mkuu John Mnyika ameingia ukumbini tayari.

Mahakama ipo kimya na Majaji wanateta.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, baada ya mapumziko mafupi, shauri linakuja kwa ajili ya utetezi.

Tuendelee na upande wa utetezi.

Jaji Ndunguru: Mshitakiwa.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, na mimi nipo tayari kuendelea.

Jaji Ndunguru: Shahidi.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba kumuita shahidi wa pili wa utetezi, na jina lake ni John John Mnyika.

Mnyika anatoka benchi la mbele na kusogea kupanda juu kizimbani.

Anaelekea upande wa kushoto wa Majaji, ambao ni upande wa kulia wa watazamaji.

Jaji Ndunguru: Shahidi, unaitwa nani?

Mnyika: Naitwa John John Mnyika.

Jaji Ndunguru: Umri wako?

Mnyika: Miaka 46.

Jaji Ndunguru: Unaishi wapi?

Mnyika: Goba, Manispaa ya Ubungo.

Jaji Ndunguru: Kazi gani?

Mnyika: Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Jaji Ndunguru: Dini yako?

Mnyika: Mkristo.

Jaji Ndunguru: Utaapishwa.

Mnyika anaapa: Mimi, John John Mnyika, naapa mbele ya Mahakama hii tukufu kwamba ushahidi nitakaoutoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu. Mungu nisaidie.

Jaji Ndunguru: Utamuongoza.

Lissu: Nitamuongoza.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Asante sana mkuu
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Lissu: Shahidi, nitakuongoza kwa kukuuliza maswali, utajibu kwa sauti Majaji wasikie.

Mnyika: Sawasawa.

Lissu: Umeeleza kwamba ni mkazi wa Goba, Manispaa ya Ubungo, na ni Katibu Mkuu wa CHADEMA. Eleza, umeshikilia nafasi hiyo tangu lini?

Mnyika: Tangu 2019.

Lissu: Kabla ya kuwa Katibu Mkuu, eleza umeshikilia nafasi gani zingine?

Mnyika: Nimekuwa Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA tangu 2003 hadi 2011.

Wakati naishikilia nafasi hiyo, mwaka 2007 niliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Kwa hiyo, nilikuwa nashikilia nafasi zote mbili.

Nafasi ambayo nilitumikia mpaka mwaka 2014.

Na wakati huo huo, kati ya mwaka 2009 mpaka 2011, nilishikilia vilevile nafasi ya Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya CHADEMA.

Na mwaka 2014 niliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa.

Nafasi ambayo nilishikilia mpaka mwaka 2019, nilipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu.

Lissu: Katika kipindi ambacho nilipokuwa Mbunge...

Lissu: Huko sijafika bado, nataka za chama kwanza.

Lissu: Nafasi nyingine za kichama, kama zipo?

Mnyika: Nimeshawahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni kwa vipindi viwili, lakini nitashindwa kukumbuka miaka.

Lissu: Nafasi zingine za chama, kama zipo?

Mnyika: Nilipokuwa Mbunge, nilichaguliwa kuwa Katibu wa Wabunge nilipokuwa Bungeni wa Jimbo la Ubungo kuanzia 2010 hadi 2015. Na baadaye niliporudi tena Bungeni kama Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Dar es Salaam, nikachaguliwa tena kuwa Katibu wa Wabunge kuanzia 2015 mpaka mwaka 2020.

Lissu: Sasa, Shahidi, nafasi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA ni nafasi ya aina gani katika uongozi wa chama?

Mnyika: Nafasi ya Katibu Mkuu ni Mtendaji Mkuu wa chama na Mwenyekiti wa Sekretarieti, ambacho ndiyo chombo cha utendaji wa kila siku cha chama.

Katibu Mkuu ndiyo Msimamizi Mkuu wa utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya vikao vya juu vya chama.

Msimamizi Mkuu wa rasilimali watu, fedha na ofisi za chama.

Mnyika: CHADEMA inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Kanuni za CHADEMA, Miongozo ya CHADEMA, Maadili ya CHADEMA na Itifaki ya CHADEMA.

Lissu bhana! Mashahidi wa upande wake anawauliza maswali ya kawaida tu. Ingekuwa ni mashahidi wa Katuga sasa!
 
Mkielekezwa muewaelewa!
Kesi ya mh Lissu isingewezekana kumalizika ndani ya miezi iyo 6

Sababu zipo

Kesi zile zengine za Uhaini zinawezekana kumalizika ndani ya miezi 6 kwakuwa watenda Uhaini wanakuwa washatenda matukio yao ya msingi 👈

Tofauti na mh Lissu yeye kakamatwa Mwezi wa 4 akiwa na lengo kufanya tukio la Uhaini mwezi wa 10 mwishoni manake mwezi wa 11 tayali miezi mingapi ni 7

Ndiomana Jamhuri ikamuekea Mashahidi wengi 30 lengo kuakikisha Kesi ya mh Lissu inafika mwezi 11
Kutokea apo watajua
Ukweli wa kile mh Lissu kamaanisha
Kivitendo

Mh Lissu alalamika kijinga
Wewe unataka kufanya Uhaini miezi 7 mbele uko❗️

lkn umetutangazia mapema sasa alitaka Jamhuri isimkamate ‼️

Siku iyoiyo unatangaza jambo lako au Jamhuri kusikia jambo lako kupitia uduma za upelelezi 👈

Utakamatwa na watakupitisha kupoteza muda kisheria mpaka muda wako ufike wajue nia lengo lako nini✍️
Unajua maana ya uhaini?
 
Suala la mashahidi wengine kama rais, makamu na waziri mkuu lilikubaliwa au ?
Watajua wenyewe wakubalia au wasikubali. Lissu hana wajibu wakuthibitisha yeye hana hatia bali wao ndio wanatakiwa kuthibitisha ana hatia. Mpaka sasa ni kama Lissu ameshaua ushahidi wote uliotolewa juu yake. Hata akisema leo anafunga ushahidi atashinda bado.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Mnyika: Na vilevile...

Lissu: Subiri kidogo, unakimbia sana. Majaji wanaandika.

Mnyika: Vilevile ni Msimamizi Mkuu wa watumishi wa Makao Makuu ya Chama na makatibu walio chini yake.

Lissu: Naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji kama chama chako huwa kinafanya vikao vya chama na utaratibu wa kuandaa au kuitisha mikutano hiyo.

Mnyika: Chama hicho kina mikutano ya ndani, ikiwemo vikao vya kikatiba, na ikiwemo mikutano ya hadhara.

Lissu: Subiri kidogo, Jaji amesema “Mhhhhhhhh.”

Jaji Ndunguru: Naweza kusema endelea, siyo lazima “Mhhhhhhhh.”

KICHEKO

Mnyika: Kwa mikutano ya ndani, ngazi husika au chombo husika, ambacho ndiyo Sekretarieti, tunakaa kikao chini ya Katibu Mkuu (ngazi ya Taifa), kinafanya maamuzi ya kufanya kikao husika na utaratibu wa maandalizi yake.

Na majukumu yanagawanywa kwa maamuzi yake.

Lissu: Kama nakuelewa sawasawa, kazi ya kuandaa mikutano ya chama ni kazi ya Sekretarieti ya Makao Makuu.

Waeleze Majaji, nani ni wajumbe wa hiyo Sekretarieti.

Mnyika: Wajumbe wa Sekretarieti ni Katibu Mkuu, ambaye ni Mwenyekiti wa Sekretarieti.

Manaibu Katibu Wakuu wawili. Mmoja wa Zanzibar na mwingine wa Tanzania Bara.

Wakurugenzi wa Chama Taifa.

Wataalamu na Katibu wa Sekretarieti anayeteuliwa na Katibu Mkuu.

Na makatibu wa Mabaraza ya Chama; Baraza la Wazee (BAZECHA), Baraza la Wanawake (BAWACHA) na Baraza la Vijana (BAVICHA).

Lissu: Sasa, Shahidi, katika wajumbe wote uliowataja, waeleze Majaji kama Mwenyekiti wa Chama ni sehemu ya Sekretarieti ya Chama Taifa.

Mnyika: Mwenyekiti wa Chama siyo sehemu ya Sekretarieti.

Lissu: Waeleze Majaji kama Mwenyekiti wa Chama anashiriki katika vikao vya Sekretarieti.

Mnyika: Mwenyekiti wa Chama hashiriki vikao vya Sekretarieti ya Makao Makuu, ambayo Mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Haya maswali ukiyafuatilia ni kama Lissu anaondoa Ile dhana ya kwamba ndiye aliye panga mkutano.
 
Back
Top Bottom