TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI
Lissu: Majibu ambayo nimeyatoa nilikuwa fairly consistent kwamba maelezo ya Polisi Mashahidi yanatakiwa yatolewe mbele ya Polisi mwingine.
Sasa kwa sababu ni muhimu, nipo tayari nieleze upya, wapewe nafasi ya cross-examination.
Sasa nina haki ya kutumia vielelezo ambavyo wao walivituma.
Hata vielelezo walivyo navyo vinaonyesha hivyo, kwamba kuna askari mwingine wa kusimamia.
Jaji Ndunguru: Ndicho hicho unachotuambia, endelea tu.
Lissu: D1, maelezo ya PW2, kwa fomu yenyewe inaonyesha kuna space ya signature ya afisa anayetoa maelezo na anayeandika.
Kwenye D2 kuna sehemu ya saini ya mtoa maelezo na saini ya afisa aliyeandika maelezo.
Hizo sehemu mbili zimesainiwa na mtu mmoja.
Mtoa maelezo na saini, na mtu aliyeandika maelezo ni mtu mmoja, Inspector Kaaya.
Akasaini sehemu ya mtoa maelezo na afisa aliyeandika maelezo.
Waheshimiwa Majaji, Kielelezo D5, maelezo ya PW6. Kwenye mwisho wa maelezo kuna sahihi ya mtoa maelezo na sahihi ya afisa wa Polisi.
Imesainiwa across signature moja sehemu zote mbili.
Kielelezo D8, maelezo ya PW9. Mwishoni katika hiki Kielelezo kuna sehemu, Waheshimiwa Majaji, na hii ni muhimu sana, Waheshimiwa.
Kuna saini ya mtoa maelezo na kuna saini ya afisa wa Polisi, zote zimesainiwa na mtu mmoja na mbele ya signature kuna cheo chake, ASP.
Halafu, Waheshimiwa Majaji, kuna uthibitisho wa aliyeandikiwa maelezo, PW9 Lutufye.
Chini kuna mwingine, ASP Lutufye, kwamba: “Nathibitisha ni maelezo yangu kwa uaminifu na kwa usahihi.”
Amejithibitisha kama mtoa maelezo na mwandika maelezo.
Kielelezo D1, Waheshimiwa Majaji, saini ya mtoa maelezo na saini ya afisa aliyeandika maelezo katika kila ukurasa.
Mwishoni, Waheshimiwa Majaji, kuna uthibitisho wa afisa aliyeandika maelezo, Detective ..., “Nathibitisha kwa uaminifu nimeandika maelezo ya Detective Coplo Vincent.”
Mtu huyo huyo.
Kielelezo D15, katika kila page kuna sehemu ya saini ya mtoa maelezo na imesainiwa na mtu huyo huyo na PW16.
Kielelezo D14 ni cha PW15, Detective Coplo Amani Michael. Katika kila page saini ya mtoa maelezo imejazwa, saini ya mwandika maelezo imejazwa.
Ndiyo mtu pekee ambaye maelezo yake yameandikwa kwa usahihi.
Afisa aliyeandika maelezo ni Detective Coplo Robert, anasema: “Kwa usahihi nathibitisha nimeandika maelezo ya Detective Amani Michael.”
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI