TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI
MAHAKAMA INAANZA
Lissu ameanza kuingia, kisha Majaji wakafuatia.
Ukimya unarejea mahakamani.
Karani wa Mahakama anasoma: Criminal Session; Kesi Namba 19605 ya 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.
Wakili wa Serikali, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha Mawakili wenzake:
1. Nassoro Katuga
2. Tawabu Issa
3. Job Mrema
4. Cathbert Mbilinyi
5. Kasara
Mshtakiwa yupo anajiwakilisha mwenyewe.
Shauri limekuja kwa ajili ya maswali ya dodoso.
Tupo tayari kuendelea.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa...?
Lissu: Mheshimiwa Jaji, nipo tayari kuendelea, isipokuwa naomba dakika tano za consultation na Mawakili wangu.
Wanasogeza kizimbani kwa Shahidi (Lissu) Wakili Dkt. Lugemeleza Nshala, Wakili Nashon Nkungu, Wakili Deogratius Mahinyila, Wakili Dorice Kafuku na Mwanasheria Garatwa.
Majaji na wao wanateta pale juu.
Lissu: Nipo tayari, Waheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Unakumbushwa pia kufuata kiapo chako.
Lissu: Sawasawa.
Wakili wa Serikali, Ajuaye, amesimama.
Ajuaye: Shahidi, jana unakumbuka tulipoishia. Naomba nikuulize swali moja la mwisho.
Shahidi, kweli au si kweli kwamba nia ya kutenda kosa lolote inathibitishwa na tendo husika?
Lissu: Siyo kweli.
Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, tulikuwa tuna swali moja kwa shahidi.
Na tunaomba tutamke rasmi kwamba tumemaliza rasmi maswali ya dodoso kwa shahidi.
Jaji Ndunguru: Mmmmmhhhh...
Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba kufanya re-examination.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, samahani, tuna concern kabla hamjalitolea maamuzi. Tulikuwa tuna hoja.
Jaji Ndunguru: Ndiyo, endelea.
Nassoro Katuga: Upande wa Jamhuri tunajua kuwa re-examination ni moja ya njia ya utoaji wa ushahidi.
Na re-examination imekuwa provided kisheria, ukingalia kifungu cha 155(3) cha Sheria ya Ushahidi.
Anasoma: Kwamba re-examination ya shahidi itakayofanywa na upande ambao umemuita shahidi huyu, uwe Defence au Prosecution, au Mdai au Mdaiwa.
Ila kifungu cha 156(3) kinasema re-examination itakuwa juu ya yale mambo tu ambayo yalijitokeza katika examination.
Kama patatokea suala jipya, Mahakama itatoa nafasi kwa examination tena.
In any matters, kama atakuwa anaeleza masuala ya examination, ndiyo itakuwa re-examination.
Mshitakiwa anajiwakilisha mwenyewe na yeye alikataa kabisa Mawakili.
Atafanyaje re-examination juu ya majibu yake wakati re-examination ni kufafanua majibu yake aliyotoa, kama kifungu cha 156 kinavyosema?
Pale ambapo upande ulioita unaona kwamba utoe ufafanuzi kutokana na majibu yako.
Waheshimiwa Majaji, suala ambalo tunaomba Mahakama hii tukufu ijiulize:
Shahidi anajiwakilisha mwenyewe na ushahidi katoa yeye.
Atajiulizaje maswali na kufafanua?
Kuna possibility kubwa kwamba re-examination inayoenda kufanyika sasa ni kwenda kuwa examination-in-chief.
Wakati purpose ya re-examination ni kufafanua: hivi ulimaanisha nini na kujibu hivi nilimaanisha hivi.
Kujifanyia mwenyewe re-examination ni sawa na kuwa mwamuzi katika suala lako mwenyewe.
Kama angekuwa na Wakili, basi Wakili angemuongoza kufafanua.
Kwa mujibu wa hivi vifungu, kuna haki ya re-examination tunaiona, lakini utaratibu ndiyo haujaeleweka. Ni eneo humu na linahitaji ufafanuzi wa Mahakama yenu.
Tutakuwa tunafungua uwanda mwingine.
Mahakama inaweza kumuuliza kama itaona inahitaji ufafanuzi wa majibu yake.
Lakini Sheria ipo silent kwamba ikiwa huyo party ndiye shahidi.
Ndiyo maana wanasemea during examination-in-chief, leading questions haziruhusiwi.
Lakini during re-examination, leading questions zinaruhusiwa.
Jaji Ndunguru: Hoja yako ni nini kama unasema Sheria ipo silent?
Nassoro Katuga: Nyie Mahakama mtaona utaratibu mzuri, lakini kama itahitajika kufanya hivyo, Mahakama imuelekeze kutoa explanation kwa majibu yenye maana zaidi ya moja.
Re-examination sawa, Sheria ipo kimya, lakini tunaomba Mahakama iweze kum-control kwa yale majibu yenye jibu zaidi ya moja.
Naomba Mahakama itoe mwongozo katika suala hilo kabla shahidi hajaianza.
Ni hayo tu kwa upande wetu.
MAJAJI WANATETA
Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba kabla sijajibu, naomba Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, aseme ameleta kitu gani?
Ni pingamizi au maneno? Na kama ni pingamizi, nitabidi nijibu na mtoe uamuzi.
Au ni maelezo tu kama mapendekezo na maelekezo kwa Mahakama?
Jaji Ndunguru: Upande wa Jamhuri unasemaje?
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, tumeiomba Mahakama itoe uamuzi na mwisho tumeomba Mahakama itoe mwongozo.
Hakuna sehemu tumesema tunapinga na siyo pingamizi.
Lissu: Kwa hiyo siyo pingamizi?
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI