cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 123,324
- 202,767
Wampe chatGPT tu maana hakuna Ajuaye
😂😂😂
Wampe chatGPT tu maana hakuna Ajuaye
Hata kesi za uchochezi pia ni kesi za kijinga zinazotumika kama tool za kuwakandamiza wapinzani, nchi za kijinga jinga ndio zimebaki na kesi za uchochezi. Sheria ya kesi ya uchochezi zilikuwa adapted kutoka tawala za kikoloni.hapa kuna kesi ya uchechezi sio uhaini
We kichwa nazi uhaini unatangazwa kwenye mikutano ya hadhara?Mkielekezwa muewaelewa!
Kesi ya mh Lissu isingewezekana kumalizika ndani ya miezi iyo 6
Sababu zipo
Kesi zile zengine za Uhaini zinawezekana kumalizika ndani ya miezi 6 kwakuwa watenda Uhaini wanakuwa washatenda matukio yao ya msingi 👈
Tofauti na mh Lissu yeye kakamatwa Mwezi wa 4 akiwa na lengo kufanya tukio la Uhaini mwezi wa 10 mwishoni manake mwezi wa 11 tayali miezi mingapi ni 7
Ndiomana Jamhuri ikamuekea Mashahidi wengi 30 lengo kuakikisha Kesi ya mh Lissu inafika mwezi 11
Kutokea apo watajua
Ukweli wa kile mh Lissu kamaanisha
Kivitendo
Mh Lissu alalamika kijinga
Wewe unataka kufanya Uhaini miezi 7 mbele uko❗️
lkn umetutangazia mapema sasa alitaka Jamhuri isimkamate ‼️
Siku iyoiyo unatangaza jambo lako au Jamhuri kusikia jambo lako kupitia uduma za upelelezi 👈
Utakamatwa na watakupitisha kupoteza muda kisheria mpaka muda wako ufike wajue nia lengo lako nini✍️
Hivi ni faida gani wanayoipata hawa watu kumtaabisha hivi huyu Baba?
Kesi ya Lissu, imetupa hasara ya zsidi ya Trillion 3 kama Taifa!
Suala la mashahidi wengine kama rais, makamu na waziri mkuu lilikubaliwa au ?
Hii kesi hairushwi live?Yaani ushahidi wa Mnyika unawavua nguo hawa waliandaa hii kesi, mawakili wa serikali naona na hapa wamepigwa KO, Maana Lissu yeye haandai Mkutano lakini wao kwenye mashitaka yao wamemshitaki Lissu 🤣🤣🤣
Kuna kusomea kitu kukipenda na kukijua sasa TL anavyo vyoote hivyo kongole kwake aisee.Lissu ni mwana sheria na wakili mbobevu.
Ila wewe bana 🤓Utaenda wewe badala yao ❗️
Nenda mahakamani ukaeleze alisababishaje.Na Vifo vingapi kasababisha 🫎✍️
..TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI
Lissu: Waheshimiwa Majaji, shahidi akikuwa anasema anachokumbuka, wala siku mwambia ajikumbushe.
Kama Wakili wa Serikali naona ni shida, naondoa tu, tuokoe muda.
Jaji Ndunguru: Ni sahihi mshtakiwa kuondoa kwa sababu shahidi ameshadoma unachomuuliza.
Lissu: Sasa shahidi, baada ya ushahidi ambao umeutoa mpaka hapa ulipofikia, je, hii tuhuma kwamba mimi ndiyo niliyeandaa mkutano na kualika waandishi wa habari, wewe unaionaje?
Mnyika: Waheshimiwa Majaji, hii ni tuhuma ya uongo na ni tuhuma ya kubambikiza tu.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kama mlipokuwa mnawaalika waandishi wa habari, palikuwa na maelekezo waje na nini na kitu gani?
Mnyika: Hapakuwa na maelekezo yoyote kwamba waje na nini au na kitu gani.
Lissu: Umetolewa ushahidi katika Mahakama hii kuwa waandishi wa habari waliokuja katika mkutano wa JAMBO TV. Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kulikuwa na maelekezo kwamba waje na kamera.
Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, tunachokiona ni mshtakiwa anamlisha ushahidi shahidi wake.
Lissu: Naomba ueleze kama mliwaelekeza waandishi wa habari kuja na kamera.
Jaji Ndunguru: Rudia tena swali, ukishatumia neno "kama" ni kwamba unapendekeza jibu.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, mliwaelekeza waandishi wa habari waje na vifaa gani?
MAHAKAMA: Kicheko.
Jaji Ndunguru: Nafikiri bado hapo kuna maelekezo, neno "vifaa".
Lissu: Wacha niachane na hilo swali, maana linanipotezea muda.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama palikuwa na maelekezo kwa waandishi wa habari juu ya namna ya kutumia vifaa vyao.
Lissu: Sasa wafafanulie Waheshimiwa Majaji utaratibu uliotumika wa waandishi wa habari kurusha huo mkutano.
WEJA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Yaani kwa kifupi unataka kusema hivi...
Jamuhuri ilisubiri kitendo... Kwa kufanya yafuatayo....
Walikamata watuhumiwa wa Uhaini... Kisha wakawahoji na kuwafutia kesi zao ili wawe mashahidi kesi ya Lissu..
Kisha watuhumiwa wanaachiwa wanarudi mitaani ..baadae miezi 7 mbele wanafanya tukio (Lissu yupo ndani) .. Kisha Serikali inasema kweli tukio limetokea..... Tuendelee na kesi...
Tanzania itakuwa ni channel ya vituko Duniani