Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Nassoro Katuga: Waheshimiwa, hakuulizwa hilo swali. Huku ni utaratibu wa kumpa shahidi ushahidi.

Kama una-refer kitu, kiwe ni kile kilichotoka kwa shahidi.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, hizi objections zinatupotezea muda. Kinachokatazwa ni leading questions tu za "Yes" au "No".

Hizi objections zinatupotezea muda kwa sababu ni baseless.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, hilo ni swali ambalo lina-suggest jibu.

Leading questions zimeelezwa kifungu cha 156, kwamba swali lolote linalopendekeza jibu siyo swali sahihi.

Lissu: Kama ndiyo hivyo anavyosema kwamba nasuggest jibu, kusema aeleze, nasuggest nini?

Anaposema kwamba tumekaririshwa shuleni, mimi nimesoma LLB miaka 34 iliyopita.

Mimi siyo wajuzi, tunapotezeana muda.

Jaji Ndunguru: Sawa, tuendelee.

Lissu: Kwamba nashitakiwa kwa kuwaalika waandishi wa habari.

Mnyika: Hayo ni mashtaka ya uongo.

Mnyika: Mimi nilitangaza katika hotuba ya utangulizi kwamba mkutano utakuwa na awamu mbili, na kwamba awamu ya kwanza vyombo vya habari vitahusika.

Na baadaye vyombo vya habari vitaondoka na kubaki na watia nia wenyewe kwa muda mfupi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo sehemu ya kwanza ambayo waandishi wa habari wangehusika nayo ni ipi?

Mnyika: Kwa kumbukumbu zangu, ni hatua ya awali ya maelezo ya viongozi, ambapo kulitolewa hotuba fupi fupi na Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ali Ibrahim Juma; Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika; Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Mzee Saidi; Makamu Mwenyekiti Bara, John Wegesa Heche; na hatimaye hotuba ndefu iliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antipas Lissu.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba health break ya dakika 5 kwa ajili yangu mwenyewe.

Jaji Ndunguru: Ruhusa.

Lissu: Asante.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Uhaini unapangwa na mtu mmoja sio , yeye we upange baada ya miezi 7 uje ufanye, vurugu za kuzuia ghasia ni tofauti na uhaini...Ukizuia uchaguzi kwa ghasia unapewa kesi ya uchohezi sio uhaini wala ugaidi. Tuwe tunasoma sheria kidogo wazee.
Haya miezi 7 imepita imeenda hadi 10 huo uhaini umefanyika?
Maana kwa mujibu wa Polisi walikamata watu 4 waliopanga kuvuruga uchaguzi polisi wakaomba wawe mashahidi wao , bado mtu yupo gereza ya Oktoba ukayaona.
Jaji Warioba alimshauri Samia tusiende kwenye uchaguzi kukiwa na watu zaidi ya 6 umewaacha hali itakua mbaya, umeona yaliyotokea?

Twende taratibu sasa
Umesema kuzuiya Uchaguzi sio uhaini
Ni Uchochezi

Sasa Uchaguzi utawezaje kuzuiya na isiwe Ugaidi uhaini! tupe mfano utafanyaje kuzuiya????
 
Watajua wenyewe wakubalia au wasikubali. Lissu hana wajibu wakuthibitisha yeye hana hatia bali wao ndio wanatakiwa kuthibitisha ana hatia. Mpaka sasa ni kama Lissu ameshaua ushahidi wote uliotolewa juu yake. Hata akisema leo anafunga ushahidi atashinda bado.
Hata section ya mwisho ya re - exams pale inaonuesha polisi wamendika wenyewe polisi na kusaini mwenyewe. Na ametusanua kuwa polisi mmoja tuu ndiyo kaandikiwa na kusaini na kasaini aliuemwandikia.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI


Lissu: Nimerudi Waheshimiwa.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Waeleze Majaji, lengo la kuwaalika waandishi wa habari katika hiyo sehemu ya kwanza lilikuwa ni nini?

Mnyika: Lengo nilikuwa wao kuchukua habari kupitia uhuru wao wa habari na kufikisha kwa umma swala linalohusu madai yetu ya mabadiliko ya Kikatiba na kisheria ya kuwezesha uchaguzi huru na haki chini ya kauli mbiu ya No Reforms No Election (Bila mabadiliko hakuna uchaguzi).

Lissu: Shahidi, umeieleza Mahakama kwamba katika hotuba zilizotolewa, hotuba ya Mwenyekiti ilikuwa ndefu zaidi. Unamaanisha nini ukisema ndefu zaidi?

Mnyika: Mazungumzo ya awali yalikuwa ya takribani masaa matatu.

Katika muda huo, zaidi ya masaa mawili au zaidi kidogo alizungumza Mwenyekiti wa Taifa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kwamba mazungumzo hayo ya Mwenyekiti ya masaa mawili na zaidi alizungumzia nini?

Mnyika: Alizungumzia historia ya madai ya Katiba ya kuwezesha chaguzi huru na haki.

Tangu ya Tume ya Vyama Vingi maarufu kama Tume ya Nyalali kati ya 1991 na 1992.

Akazungumzia mapendekezo ya tume hiyo ya kutaka kuandikwa kwa Katiba mpya, na kufanyika mabadiliko ya kisheria ya kuwezesha uchaguzi wa huru na haki yalivyokataliwa na Serikali ya chama kimoja wakati huo.

Lissu: Lingine?

Mnyika: Akaendelea kuzungumzia juu ya madhara ya kukataliwa mabadiliko hayo yalivyojitokeza katika chaguzi zilizofuata kuanzia 1995.

Akaeleza jinsi ya maoni ya tume nyingine au kamati zilizoundwa kushughulikia masuala ya Kikatiba au matatizo ya kiuchaguzi.

Akataja kuhusu Tume ya Kisanga, akataja kuhusu Tume ya Bomani.

Akaeleza kuhusu mchakato wa mabadiliko wa kati ya 2011 mpaka 2014 ulioanzishwa na Tume ya Mabadiliko ya Sheria iliyotungwa na Bunge, maarufu kama Tume ya Warioba.

Na namna CCM ilivyotumia wingi wake kwenye Bunge Maalum la Katiba kukwamisha mchakato huo.

Akaeleza madhara ya kukosekana kwa mabadiliko hayo kwa uchaguzi mkuu wa 2015.

Uchaguzi wa Vitongoji na Vijiji wa mwaka 2019 na uamuzi wa CHADEMA kujiondoa katika uchaguzi baada ya wagombea kujiondoa katika uchaguzi.

Na yaliyotokea katika uchaguzi wa 2020, ambapo yeye alikuwa na mgombea urais na baadhi ya waliokuwa pale walikuwa ni wagombea wa ubunge.

Juu ya wagombea kuenguliwa kwa mapingamizi yasiyo ya msingi.

Na waliobakia wengine kuzuiwa kampeni.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom