Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

tatizo siyo huruma ila ni hofu juu ya uzito wa nyundo(nondo za kisheria) atakazotumia kushindilia msumari aliokwisha piga tokea jana kwenye kujitetea kwake ila ngoja tuendelee kula darasa huru.
 
Mbona kakaa ukonga zaidi ya mwaka sasa. Mkuu Mimi sio mtaalamu wa sheria
Nimesema kuwa hii kesi ni ya Samia hivo ingekua ya uhaini kweli kweli (high treason), maana yake hata mtu wa Jambo Tv aliyechapisha angekua ndani na Lissu, wale waliokua meza kuu na Lissu wangekua ndani.
Hii kesi ni kisiasa kunyanyasana kutesena ili government iendeshe mambo bila noise pollution...
Hii kesi ni Samia , Wambura na Mkunda.
 
Nilisema jana kuhusu hili: Ni haki ya upande wa utetezi kufanya re-exam, na haki iyo anayo TL ambaye ni Shahidi na upande mwingine mshitakiwa.

Kuna maswali ambayo TL kama anaejitetea, anapaswa kuyafafanua, lakini haruhusiwi kuleta jambo jipya. Ni haki yake kufanya hivyo maana ndio utaratibu kama angekuwa na mawakili wake. Jamaa ni smart aisee.

Kuna swali moja, TL aliulizwa kwamba; Mhalifu anaruhusiwa kuja kutoa ushahidi, alijibu Ndiyo. Hakutoa maelezo, naamini atatumia fursa hiyo kueleza ni vipi mashahidi waliokamatwa na kuachiwa (wahalifu), na badae kuombwa kuja kutoa ushahidi wao katika kesi yake wanaweza kuwa "wamepangwa".

TL katika kesi hii; anataka ku "disqualify" mashahidi na ushahidi wao, ndio kete ya kesi hii. Na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama ifuatavyo;

1. Ameonyesha kwamba; katika mashahidi wote 17, ni shahidi mmoja tuu, wa Jambo TV ndie alikuwa eneo la tukio "eyewitness". Mashahidi wengine wote ni mapolisi, walitoa ushahidi wao kupitia Video, ambayo ilikataliwa mahakamani kuwa kama ushahidi.

2. Ameonyesha kwamba; mashahidi wengine ambao hawakuwepo eneo la tukio ambao sio mapolisi, walikamatwa kwanza kwa uhalifu. Wakafutiwa kesi zao (wakaacha huru), na badae wakaombwa kuwa mashahidi katika kesi hii. Anajaribu kuonyesha kwamba hii ni hila "anaonewa" na watesi wake (Mapolisi), ambao ameshaonyesha wana nia ya siku nyingi kumfunga, yaani ana tatizo nao la kibinafsi (akiwemo kingai).
TL anakusudia kuonyesha kundi hilo la mashahidi ushahidi wao sio wa kuaminiwa na na mahakama.
Aliulizwa na wakili; Je, wahalifu hawaruhusiwi kutoa ushahidi mahakamani? Akajibu; wanaruhusiwa.. ila.. akaambiwa. Amwshajibu.

Sasa tusubiri TL, katika re-examination aje aseme; ni vipi au kwa namna gani, ushahidi wa wahalifu hauzingatiwi mahakamani. 😊
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Wakili wa Serikali, Ajuaye, anasimama: Waheshimiwa Majaji, tunaona kama utaratibu unakiukwa. Shahidi anaomba swali la mwisho ambalo hajaandika. Anatakiwa asomewe na Mahakama swali na majibu yake, na siyo kuwaomba wasaidizi wake.

Jaji Ndunguru: Shahidi, unasemaje?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, niliomba hivi: niliomba swali la mwisho kwa jinsi lilivyoandikwa na wasaidizi wangu.

Jaji Ndunguru: Ulishapewa.

Lissu: Ndiyo, nilishapewa...?

Jaji Ndunguru: Ilibidi uombe Mahakama.

Lissu: Mimi nilikuwa najibu na siwezi kujibu huku naandika. Sasa nikiandikiwa na washauri wangu maswali ya cross-examination ni kosa?

Tutafika tukiwa tumechoka sana.

Mheshimiwa Jaji: Tuendelee, Shahidi.

Lissu: Nianze na swali la mwisho kwamba nia inathibitishwa na matendo.

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, mimi napinga hilo swali. Anataka kuelezea, na mimi niliuliza kweli au siyo kweli.

Lissu: Nimeulizwa swali, Waheshimiwa Majaji, nikajibu. Nina haki ya kufafanua kwanini nimesema siyo.

Vinginevyo, anayeamua nijibu nini ni Wakili wa Serikali, siyo mimi.

Jaji Ndunguru: Shahidi, labda tuelewane kitu kimoja. Wote tunajua re-examination inatokana na swali uliloulizwa. Kama unaenda kuzungumzia uhaini, yeye anasema hakusema uhaini.

Lissu: Sawa, tuendelee. Mimi nilisema siyo kweli, nia inathibitishwa kwa matendo. Kuna makosa mengine nia inathibitishwa kwa uchapishaji, na mengine yanathibitishwa kwa matendo.

Sasa, Waheshimiwa, naomba niendelee.

Waheshimiwa Majaji, niliulizwa na Nassoro Katuga kwa ushahidi wangu kwamba hii kesi imeshachunguzwa na Mahakama ya Kimataifa na Afrika.

Katuga akauliza Mahakama yetu ipo, nikasema ipo huru.

Inalazimishwa, nikasema hailazimishwi.

Lakini, Waheshimiwa Majaji, pamoja na hayo, Mahakama hizo zina umuhimu wake pia.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, ndiyo yale yale niliyokataa mimi.

Swali niliuliza mimi na swali jepesi kabisa, halikuuliza umuhimu wake.

Hili tutaomba kufanya cross-examination, analeta ushahidi mpya.

Unless aombe Mahakama alete ushahidi mpya na sisi tufanye cross-examination.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, hili siyo jambo jipya.

Alileta jambo la Baraza la Haki la Umoja wa Mataifa.

Ameleta mwenyewe na nataka kufafanua hilo.

Jaji Ndunguru: Hili suala litatuchukua muda mrefu kama hatutofuata taratibu.

Na katika re-examination siyo lazima uende huko.

KILA MTU AWEKE EMOJI

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Kazi IPO!!!
 
Dah, lissu wa moto mimi hapo nishaanza kufikilia re-examination in chief maana sheria hipo kimya kwenye ushaidi unaotolewa na shaidi ambae ni mshtakiwa hapo hapo. Pia kwenye cross examination yq mawakili wa serikali nimesikia mala zote wakimuuliza shaidi kana kwamba wanamuuliza mstakiwa, hapa lksau i think anaenda kjwatupilia mbali kwamba mlikuwa mnamuuliza mstakiwa badala ya shaidi wa mstakiwa hivyo dodoso lenu ni bure kabisa.
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI


Lissu: Nimeacha maswali kadhaa.

Jaji Ndunguru: Yaani umeshaanza kutumia tena neno β€œumuhimu.”

Lissu: Basi nisitumie tena neno β€œumuhimu.”

Nataka kusema kwamba pamoja na Mahakama zetu kuwa huru, bado kuna Mahakama nyingine za kimataifa zenye sura za kimahakama ambazo zinafuatiliwa na maamuzi yake kutumika na Mahakama zetu.

Nassoro Katuga: Mimi sikuuliza hilo swali kwamba Mahakama inaweza kutumia maamuzi ya hizo Mahakama nyingine.

Sikurelate na hilo suala kabisa, hizo Instruments.

Alipojibu kwamba Mahakama zetu zipo huru, niliacha hivyo hivyo.

Kama swali ambalo halikusema hivyo, atakuwa analeta new fact.

Lissu: Waheshimiwa, tusipoteze na suala hilo.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, niliulizwa kuhusu tuzo mbalimbali ambazo nimepewa.

Nikaulizwa kama hizo tuzo, kama sijazileta Mahakamani, nikasema sina kazi ya kuthibitisha kesi.

Wakasema, kwa kifungu gani? Nikasema ni Legal Principle.

Sasa nataka kufafanua hili jibu.

Waheshimiwa Majaji, niliposema ni Legal Principle za sheria ya ushahidi, nilikuwa namaanisha kwamba katika kesi ya jinai, Mshtakiwa hawajibiki kuthibitisha innocence yake (kwamba hana hatia).

Hana wajibu huo.

Bali mzigo wa kuthibitisha upo kwa upande wa Mashitaka.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, niliulizwa vilevile kwamba kwenye ushahidi wangu nilisema niliwahi kuwa Rais wa Tanganyika Law Society, nikasema ni kweli.

Wakauliza wakati nashitakiwa nilikuwa bado ni Rais wa Tanganyika Law Society, nikasema hapana.

Wakauliza kama kuwa Rais wa Tanganyika Law Society kunanipa kinga, nikasema hapana.

Hapa nataka nifafanue.

Jaji Ndunguru: Mbona hapo hakuna cha kufafanua kwa sababu kinga zipo kwa mujibu wa sheria.

Lissu: Basi tuendelee.

Lissu: Niliulizwa pia kuhusu kupinga uchaguzi ni kwa njia gani.

Nikasema kwa njia za kimahakama.

Wakauliza kwa sheria ipi, nikasema kwa mujibu wa Katiba.

Sasa naomba ku-clarify haya majibu yangu.

Article 20(1) inatambua njia za kutaka mabadiliko na kupinga sheria na Katiba.

Ni kwamba hizo njia za nje ya Mahakama zinatambulika kikatiba, na zimethibitishwa hivyo na Mahakama.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE
 
TUNDU LISSU NA WAKILI WA SERIKALI LEO WATATOANA DAMU MAHAKAMANI

Waheshimiwa Majaji, nikaulizwa maswali kama namfahamu Ishengoma Ndyanabo, wakauliza alifanya nini. Nikasema alienda Mahakamani kupinga sheria ya uchaguzi.

Wakauliza kwamba namfahamu pia Christopher Mtikila. Nikasema namfahamu, alienda Mahakamani kuhusu mgombea binafsi, na mpaka leo Serikali haijatekeleza hukumu ya Mahakama ya Afrika.

Nataka kufafanua.

Jaji Ndunguru: Hakuna haja ya kufafanua, huwezi kufafanua kitu kilicho wazi.

Lissu: Wakauliza pia kuhusu Sheria ya Interpretation kuhusu kutumika maneno β€œor” yanayosomwa pamoja. Nikasema ndiyo.

Mheshimiwa Jaji, maneno yale ya β€œovert act” au β€œdeed”...

Nassoro Katuga: Sikusema hayo maneno. Tulisoma Sheria ya Interpretation. Hakuna sehemu niliuliza tofauti ya maneno ya β€œovert act” na tafsiri ya neno β€œdeed”.

Lissu: Naomba Mahakama itusomee.

Jaji: Tusikilize Mahakama ilichoandika kuhusu hilo.

Jaji anasoma.

Lissu: Sawa, naendelea Waheshimiwa Majaji.

Waheshimiwa Majaji, niliulizwa kama nafahamu kama kuna mihimili mitatu ya dola na nikaambiwa niitaje.

Nikasema ni Serikali, Mahakama na Bunge, na nikaulizwa nitaje mihimili hiyo. Nikaanza na Bunge kwamba moja ya kazi za Bunge ni kutunga sheria.

Nikaulizwa kuhusu Serikali na nikasema jukumu la Serikali ni kusimamia sheria.

Niliposema moja ya kazi za Bunge ni kutunga sheria, nina maana kwamba siyo kazi pekee ya Bunge.

Na nikasema moja ya majukumu ya Serikali ni kusimamia sheria, lakini ni moja tu ya kazi za Serikali.

Waheshimiwa Majaji, kulikuwa na ushahidi kuhusu mashahidi wa upande wa mashtaka wa namna ambavyo hawakuja kutoa ushahidi wa namna nilivyokamatwa.

Nilisema nilikamatwa Mbinga, ila uhalali wa kukamatwa kwangu ni suala tofauti.

Kwa sababu sheria zimeweka utaratibu wa namna ya kukamata watuhumiwa.

Suala la kwamba nilikamatwa ni suala ambalo lilihitaji kujibiwa na upande wa mashtaka.

Waheshimiwa Majaji, kulikuwa na masuala mengi kuhusu waandishi wa habari waliokuja katika mkutano wa tarehe 03 Aprili.

Niliulizwa kama walikuwa wanajua walichoitwa kufanya. Nikasema hawakuwa wanajua.

Kama niliwapa hotuba yangu, nikasema niliwapa.

Naomba nifafanue.

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, tunaomba tupinge.

Nassoro Katuga: Hilo swali niliuliza mimi kwamba uliwapa au hukuwapa.

Suala kwamba huwa hawapewi ni suala jipya.

Kuwapa au kutowapa hakuhitaji ufafanuzi.

Kama walikuwa wanajua au hawajui haliitaji ufafanuzi.

Ajuaye: Ajikite katika majibu yake na akiachwa aende, sivyo Mahakama itashindwa kutafsiri.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unasema?

Lissu: Haya maswali yalifuatiwa na maneno β€œConstructive Publication”.

Hayo yanahitaji ufafanuzi kwa sababu ukiacha ni kwamba ulichapisha wewe.

Jaji Ndunguru: Naona unatingisha kichwa.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, re-examination haihitaji uweke wewe swali lako.

Sasa umeapa au hujawapa? Unataka kufafanua nini?

Hapa ni kwamba anataka kuyakana majibu yake.

Ukisema waandishi wa habari, tutauliza kwa sheria ipi?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, tusipoteze muda.

Lissu: Nafafanua jibu langu kwamba mimi sikuwa na control na waandishi wa habari.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Leo mawakili was serikali wanapoteana tu, nimesanuka kwanini Lissu aliamua ajitetee mwenyewe, kumbe aliona mbali,
Bravo sana Lissu, mwagaa πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯, ongezaa πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯ hadi watoanee bandama.
Watu weweeeeeee, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
ANATOKA LISSU ANAINGIA WAKILI WA SERIKALI ANAINGIA JAJI MAHAKAMA YA MOTO

Nimekurekebishia makosa ya tahajia na sarufi, bila kubadilisha maana ya mazungumzo:

Jaji Ndunguru: Nakumbusha, ulishasema hukuwa na control, kwa hiyo haiwezi kuwa constructive.

Lissu: Kama jibu lipo hivyo, nashukuru Waheshimiwa Majaji.

Waheshimiwa Majaji, niliulizwa pia kuhusu Ibara ya 30(1), kwamba utekelezaji wa haki haupaswi kuingilia haki zingine.

Nikaulizwa kuhusu habari ya kuzuia uchaguzi kwa maandamano, kama ni haki.

Nikasema ndiyo.

Nassoro Katuga: Sasa hapo ufafanuzi ni nini baada ya kujibu ndiyo?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, labda Wakili wa Serikali hakuwa ananisikiliza.

Nimesema uchaguzi ambao siyo huru siyo uchaguzi.

Jaji Ndunguru: Na sisi ndiyo tumerekodi hivyo.

Lissu: Kuna swali niliulizwa kuhusu Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Na kwamba kwa sheria niliyo nayo mimi inasema mtuhumiwa wa uhaini atahukumiwa kifo.

Wakili akasema sheria aliyo nayo yeye inasema hapana.

Jaji Ndunguru: Mimi sioni cha kufafanua hapo. Ni clarification gani hapo?

Lissu: Kama hicho kifungu katika version mbili kina tofautiana, maana yake kilifanyiwa amendment.

Je, kama kimebadilishwa hicho kifungu, kimebadilishwa kwa utaratibu gani?

Jibu langu lilikuwa kwa version ya 2023.

Jibu langu la ufafanuzi ni kwamba version ya 2023 ndiyo latest.

Kwamba nimeshitakiwa mwaka 2025, maana yake hiyo version ya 2023 ilishatoka.

Nassoro Katuga: Wakati anashitakiwa Aprili 2025, version ya 2023 ilikuwa haijatoka.

Lissu: Tuendelee.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, pamekuwa na ushahidi wangu kwamba mashahidi ni wa kificho.

Nikaulizwa kama wanajulikana.

Nikasema hawajulikani.

Ufafanuzi wangu ni kwamba hawajulikani na mtu yeyote isipokuwa ma-Prosecutor. Hawajulikani wanapotokea na anuani zao isipokuwa kwa ma-Prosecutor.

Wa kificho, wamefichwa kwa watu wote isipokuwa kwa watu waliowaleta.

Waheshimiwa Majaji, niliulizwa kwamba wakati wa hotuba yangu waandishi wa habari walitolewa, nikajibu ni kweli tuliwatoa.

Waandishi wa habari tuliwatoa nje kwa sababu tulichowaitia kilishakamilika.

Ndiyo ufafanuzi wangu.

Jaji Ndunguru: Ndiyo ulichojibu mwanzo, kwa hiyo huo siyo ufafanuzi.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba vielelezo vyote kwa sababu vimetumiwa sana.

Anapelekewa karatasi/vielelezo.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, ufafanuzi wangu ni kuhusu maafisa wa Polisi kujiandikia wenyewe maelezo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…