Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Exactly, mimi nilijua hili toka mwanzo kwamba njia pekee waliyobaki nayo ni kutengeza neno atakalolikubari kisha waachane na ushaidi wao wakazie hapo. Mfano waliposema kuhusu combat LISSU akawaelewa wanataka baadae kusema combat hiyo ni ya kijeahi wewe umeipata wapi, hili wapite kwenye hoja kana kwamba walishakuwa na vitendea kazi kutenda uhaini.

All in all uhaini unaitaji ushaidi wa mpango mkakati au mawasiliano kamili sio tafsiri ya maneno binafsi ambayo kila mtu anaweza kutafsiri atakavyo, so mimi nikisema neno "Wachochezi wa Mabadiriko ya Maendeleo ya kijamii", Mmoja ata fasiri kana kwamba ni ni neno la kufanya tendo baya na mwengine anaweza kutafasiri kana kwamba ni neno zuri.

naomba kujazia hapa hili nieleweke, JK Nyerere alishawai kusema "Nia yangu ya kudai uhuru ni kuzalisha vijana waasi dhidi ya ukandamizaji", maneno haya yanaweza kutafasiriwa kama JK Nyerere aliunga mkono Uwasi, maana maneno yanafuata kwenye sentensi hiyo yanavitendo vizuri na vibaya. Mfano neno ukandamizaji, unaweza kuwa kukandamizwa kwa kikunyangwa na mguu wa mtu mwengine au wewe kukandamiza kitu aridhini.

Hivyo sentensi nzima ina tafsiri zaidi ya moja.

On my knowledge, hapa hakuna kesi ya uhaini kwa mujibu wa kinachobishaniwa ni Maneno yenye tafsiri zaidi ya moja, pia kama alikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi usifanyike je 98% zimetoka wapi, je wamefanikiwa na kama wamefanikiwa why 98% ya ushindi wa SSH, hii tu inathibitisha tosha kwmba uchaguzi haukuiliwa kwa namna ya kumzuia mtu kwenda kupiga kula.
 
Hans Pope akifufuka Leo atashangaa jinsi tulivyoshusha hadhi ya uhaini.
 

..hizi update nashauri uwe unaziweka ktk post ya mwanzo.

..kesho kama ikikupendeza kila unapokuwa na update tafadhali uwe unaongezea ktk post ya kwanza.

..hiyo itatusaidia kuwa na mtiririko mzuri, na itatuwezesha michango yetu kuwa ya viwango.

..Natanguliza shukrani.
 
Aisee watu ni balaa

Mnaediti vitu hv tena?

Kuna sehemu amekiri kuwa "alisema atakinukisha"

Humu hamuandiki, mnamfariji nani?
Shida yenu mmekulia uswahilini unafikiri kukinukisha ni neno linalotambulika kisheria huo ndio ujinga wenu, mnatakiwa mpelekwe shule tofauti na hapo wenye akili kama nchimbi watawakimbia ili mbali wajinga wajinga.
 
Hans Pope akifufuka Leo atashangaa jinsi tulivyoshusha hadhi ya uhaini.

..wacha Hans Pope aliyekuwa akishtakiwa.

..kuna muendesha mashtaka mkuu William Sekule nadhani angemshangaa Nasoro Katuga na wenzake. William Sekule ni marehemu sasa hivi.

..mawakili kama Johnson Mwanyika waliokuwa upande wa serikali naamini wanastaajabu yanayofanywa na warithi wao.
 
Lissu ni big fish kwenye sheria not an easy target.

Nadhani sasa hata hao mashahidi wa jamuhuri wakiona haya yanayoendelea watakuwa wanajisemea "kumbe sio peke yetu tuliopitia zahma"

Hii ndio tofauti kati ya kuni na mbao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…