Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Kitendo cha Lissu kuwakazia kwenye video kimewamaliza nguvu. Halafu kwenye issue ya kukamatwa na uhalali wa kukamatwa amewapiga chini. Ambayo hii ground tu hata mahakama imkute na hatia mahakama ya rufaa anachomoka. Kitu ambacho majaji hawatakubali.
Sikujua kwanini hata wao waliamua ku raise hiyo hoja kwenye cross examination.

Kwasababu kile kidhibiti kukataliwa na mahakama ilikuwa ni ushindi kwa Lissu.

Sasa kwa ukomavu wa kisheria alionao Lissu there's no way asingesanukia huo mtego wao wa kutaka kuingiza hicho kidhibiti kinyemela.

Hata mimi mwenyewe pale hunikamati. Sasa sembuse gwiji kama yule.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Shida yenu mmekulia uswahilini unafikiri kukinukisha ni neno linalotambulika kisheria huo ndio ujinga wenu, mnatakiwa mpelekwe shule tofauti na hapo wenye akili kama nchimbi watawakimbia ili mbali wajinga wajinga.
Ile ukizingua tunazinguana nayo vipi au haijakaa kimkakati?
 
Ni uthibitisho mwingine kwamba watu wengi wanaonewa huko mahakamani kama hujui hizi taratibu zote za kimahakama na sheria husika.

Tundu Lissu anatoa funzo la kipekee sana kwenye kesi hii.
 
Katuga maswali ya wakoloni na mikataba mbona ametemana nayo?
Alianza kutaka kuingiza mambo ya enzi za Magufuli eti ulitetea makinikia yaondoke nchini. Lisu akamwambia akitaka waendelee huko ataenda. Naona Lisu alimwambia hao wakoloni waliingia kwa mikataba kama wanayoingia akina Samia leo. Naona Katuga akaona huko njia imebana. Hakuna kitu wanaogopa mashahidi wa serekali wakisikia Samia anatajwa.
 
Huwa wako excited na ujinga sijui kwanini.

Nakumbuka machawa walivyokuwa excited na yule shahidi wa mwisho, humu walikuwa wanatuambia kuwa tulieni kuna shahidi huyo ni noma, kwamba ndio ataweka kila kitu hadharani blah blah, Siku ya shahidi kutoa ushahidi kukawa hakuna la maana zaidi shahidi aligaragazwa vibaya kwenye cross examination. Ni watu fulani hivi kama hawajui lolote zaidi ya kutega masikio kwenye makorido wanasikilizia ma Boss zao wanachojadili bila kuzingatia context ya kijachojadiliwa, wao wanakibeba kama kilivyo kuja kukata nacho viuno humu.


Kwenye yote haya hakuna hope la msingi la wao kulifurahia zaidi ya kuonesha jinsi wanavyopwaya kila siku, ni heri wangeendelea kusubiri Nyundo ya jaji ya maelekezo, lakini kwa mwenendo wa kesi hakuna kitu.
 
Ahsante mkuu,Tupo pamoja!
 
Mimi ndio maana sipendi kujiingiza kwenye mijadala na hao machawa wajinga wajinga kwasababu najua wapi tutapofikia.

Hii kesi huwa nafuatilia moja kwa moja X, ni leo tu ndio nimeona nije humu kushea maoni yangu kulingana na kilichotokea.

Kuna watu humu wanatabia za kihayawani, ushindi wao ni kuona unajibizana nao so nilishaweka msimamo wa kutowajibu.

Kwangu mimi niliona kuficha white ndio mbinu sahihi ya kudili nao.
 
Dada wa Tundu Lissu akiongoza maombi muda huu mahakamani kabla ya Kesi kuanza
Uncalled for, and at the wrong place and audience.

Mambo haya ya kuonyeshana imani zetu yaacheni huko huko kunakostahili..

Hiyo haina maana kwamba hatuujui utukufu wa huyo tunayemwomba hayo tunayoomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…